Nawashukuruni Wana JmiiForum wote-KakaKiiza

Pole sana. Mwenyezi Mungu akupe nguvu na moyo wa subira.
 
Pole sana Kaka Kiiza,

Ni jambo jema kwamba umepata nguvu ya kuja hapa, walau kuongea na wadau.. Nakupongeza kwa kuzidi kuimarika na kuendelea na safari ngumu ya kuukabiri ukweli...

Ukweli kwamba, kweli mkeo kipenzi Subira hauko naye tena...
na kwamba mama watoto wako hautamwona tena...
Na kwamba from 31st August, umwekuwa single parent...

Ni Mungu pekee anayeweza kukusaidia kuikabiri hali hiyo...Na kweli nguvu ya Mkono wake haiwezi kushindwa kitu.

Kwa wale wenye imani, tunaamini kwamba Bwana atakusamamia hadi siku ile wewe na wapendwa wengine mtakapoungana tena na mpezi wenu Subira!

Be strong man.....Na Mungu hatakutupa kamwe!

Raha ya milele umpe Subira ee Bwana, na mwanga wa milele umwangazie...apumzike kwa amani..AMINA!

Tuko pomoja Kaka Kiiza,



Babu DC!!
 
KakaKiiza, karibu sana!! Tuko pmaoja sana, utuwie sana radhi kwa wale ambao hatukuweza kufika msibani kutokana na kuwa mbali kikazi!

Stay strong for the Hand of Might God is with U!
 
Pole baba. Ndio ulimwengu ulivyo. twazaliwa kwa formula tusiyoijua twafa kwa formula hiyohiyo. Imani yako ikutie nguvu usonge mbele na maisha ya hapa duniani.
 
pole sana kiongozi,tuko pamoja tutaendelea kuwa pamoja,niko njiani nakuja dar nitapenda kukuona KakaKiiza,namba yako ninayo hope yangu ulisevu,nitakutafuta
 
Pole sana mkuu wangu. Mungu akupe moyo wa uvumilivu.

Bishanga, hakuwepo msibani? Mbona kama nilimwona?
Yawezekana alikuwepo lakini nilishatoa angalizo kuwa kwayeyote ambae ameshiriki kwanjia moja au nyingine na sijabata uwezo wakumuandika basi aniwie radhi pale nitakapokumbuka nitamuweka!!!Hivyo kama Bishanga alikuwepo sina maana nimemubagua bali muweza ajaniwezesha kuwa nakumbukumbu naye!! Bishanga naomba unisamehe kwa hilo!!
 
Last edited by a moderator:
Mungu akufanyie wepesi ktk kipindi hiki inshaallah!!!
Asalam aleykum Jamii,
Nimatumaini yangu amjambo wote ningeomba kuchua wasaa huu kuelezea machache yaliyopo moyoni mwangu!
Ni majuzi tangu nilipoondokewa na mke wangu kipenzi , Subira Alfred Mwamasso mnamo wa saa 09:27hrs tarehe 31.Katika Hosptali ya Taifa Muhimbili
Napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa wote ambao walikuwa na mimi katika kipindi hiki kigumu na bado wanaoendelea kushirikiana na mimi kwa njia moja au nyingine ningewaomba ni wambie sina chakuwalipa kwa wema mkubwa waliouonyesha kwangu!!Ninawaomba wapokee hii shukurani yangu ya dhati kutoka kwangu kwani nimefarijika kwakiasi kikubwa kwa wale walio bahatika kufika msibani waliona nilikutana na mtu na kujitambulishas yeye ni mwana JF kwa jinsi nilivyo badrika na kuwa nafuraha naye kwakusema ukweli hii ilinifariji sana!!.
Kwakweli nikitu ambacho sikukitegemea mimi binafsi kuwa nitakuja kuwa na marafiki ambo siwakuwai kuwafahamu!Nilidhani rafiki niyule unayekutana naye barabarani,mgahawani,kwenye basi,Baa na sehemu za maofisini na hata kwenye misiba na harusi!!Kumbe la hasha!!
Hata nyuma ya keyboard kuna dunia nyingine inayoishi na inayoweza kuwa msaada mkubwa kwako bila wewe kujitambua!! hasa wewe mhusika utaitumia keyboard kwa uangalifu na kwa umakinai zaidi!!
Ninamengi sana ya kueleza lakini naona siwezi kuyamaliza!!
Hivyo ngoja nifupishe maneno nirudi kule nilikokusudia hapo awali!

********************************************************************************
Napenda niongozwe na utashi wa mwenyezi mungu kwakuwa ndiye amenipa huu uwezo nilionao kwa sasa.
Napenda kutoa shukurani njia moja au nyingine kwa wale wote ambao mliweza kunipa faraja kwenye hiki kipindi kigumu kwangu kwa walenitakao wa sahau nitawaombeni mniwie radhi sana kwani na mimi ni binadamu naweza kughafirika ila na wahaidi kuwa nitakuwa nana UPDATE pale nitakapo kuwa nimekumbuka!

Napenda kutoa shukurani kwa JF Management.

Napenda kutoa shukurani kwa mmoja mmoja kama ifuatavyo:-
(Special Thanks),


Maxence Melo Invisible Kiresua Mtambuzi mamamia YNNAH The Finest Preta Caroline Danzi RR Nicas Mtei TANMO BelindaJacob Dark City Gedeli Mr Rocky FirstLady1 Gaijin Liverpool Chauro Swts The secretary AshaDii afrodenzi tete'a'tete

Kwa wale ambao sijawataja naomba waniwie radhi nikikumbuka nitawaweka hapa!Nimesahau kwa bahati mbaya!

Kila siku ninawaombea wote mlioshirikiana na mimi katika kipindi hiki kizito kwangu napenda kusema

“SINA CHA KUWALIPA MUNGU AWAZIDISHIE BARAKA NA HEKIMA”


Asanteni wote muendelee na moyo huo!na mungu awabariki awahepushe nakila lilobaya awanyoshee njia.AMAN.
 
Pole sana KakaKiiza,
Mungu atampumzisha kwa Amani yake Mkeo Kipenzi/Wifi yetu Subira Alfred Mwamasso.
Najua hutaweza kutukumbuka wote tuliokuja msibani kutokana na wingi wetu,
Ila Tunashukuru kwa Ukarimu wako kwa Wana Jf tuliohudhuria.
Bwana Ametoa,
Na Bwana Ametwaa,
Jina Lake Lihimidiwe.
Ameeen.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom