Nataka kuhama Dsm, nishauri niende Mkoa gani?

Nataka kuhama Dsm, nishauri niende Mkoa gani?

Umezaliwa Dar na kila kitu. 😊
Nenda(Njoo) Dodoma.
 
Nadhani wewe una kichaa, unayeiona Dar ndio kila kitu, nyie ndo mmetujazia mji wetu, umekua mchafu kwa kukosa kwenu ustaarabu.
Mimi siyo kichaa ila wewe sasa! Sema labda umeyabananga hapa mjini ndiyo maana unakimbia! Hebu niambie biashara gani ndogo ndogo hazitoki hapa Dar? Usilogwe kwenda Kahama, huwajui Wasukuma na Waha wewe, labda ukaishie kuuza maku!
 
Asilimia 80 dar watu wana maisha magumu usiangalie tu kula,kunywa bia na kuwa na kagari maisha ni vile unasonga mbele,una akiba benk n.k...dar mtu unaweza kumuona ana maisha mazuri kama ni muajiriwa akfukuzwa kazi leo mpe mwezi tu anaanza kuuza tugari take nenda mbeya
Jamani huu sasa ni uongo wa kufungulia mwaka, yaani kati ya watu 10, wa8 choke mbaya? Siyo kweli!
 
Njoo Kinole Morogoro Ama Mkuyuni Utakula Mema
 
Kama unaweza kupika chakula kizuri biashara ya restaurant utapiga hela sana wale raia hua hawaulizi bei wanaagiza tu.

Pia kwenye biashara ya nguo na viatu naona kuna gap unaweza kufanya research yako

Cash point ila hii lazima uwe na kibunda hii ilikua relevance miaka minne iliyopita sijui kwa sasa unaweza kuta ishakua saturated
Darubini ya Mbao ubarikiwe sana hadi ushangae, Kahama nimeipitisha✅️

In shaa Allah, nikifika nitarudi hapa kusema.
 
Maisha rahisi vyakula vya kutosha njoo huku karibu na Mbuga ya Selou Kila siku tunakula nyama pori asubuhi na jioni, huku hakuna bucha ya Ng'ombe, ni nyama pori tu yaani nimevua kofia
 
Tanga, maisha yapo nafuu, la muhimu zaidi ni biashara gani uataka kufanya?
 
Yaani umezaliwa Dar na umekulia hapa hapa maanake uko kwenu, sasa unakimbiaje Dar kama uko kwenu? Dar wingi wa watu unafanya mzunguko wa pesa uwepo. Haitakaa itokee hata siku moja kwamba mahitaji muhimu yatoshelezwe! Dar watu wanakula mpaka utumbo wa kuku ambao mikoani tunautupa! Sasa hebu fikria hizi biashara ndogo unazowaza kwenda kuzifanyia mikoani ukaamua kuzifanyia hapahapa, fuga hata kuku wa nyama ambao kwa Dar sasa hivi wanauza mpaka wa wiki 4, hapo bado utalialia tu? Jamani mikoani kiugumu nyie! Pasikieni tu!
 
Back
Top Bottom