Nataka kuhama Dsm, nishauri niende Mkoa gani?

Nataka kuhama Dsm, nishauri niende Mkoa gani?

Salaam wanajamvi,

Naombeni ushauri wa kina, nataka kuhama jiji la Dsm je niende mkoa gani?

Wenye maisha rahisi, vyakula vya kutosha, niweze kufanya biashara pia kwa maana ya mzunguko wa pesa upo,

Tafadhalini mnishauri kwa upendo, nina vidonda vya tumbo.
Njoo MWANZA
 
Ni mama wa nyumbani anayetaka kuanza maisha mkoa mwengine tofauti na Dsm, anayeweza kufanya biashara ndogo ndogo kujiingizia kipato
Sema kabisa kwamba ni singo madha! Yaani biashara ndogo ndogo uikose Dar uende ukaikute mikoani? Unaumwa wewe siyo bure!
 
Kama maisha ya dsm yamekushinda I don't think kama kuna mkoa utakuwa rahisi though is possible
 
Kama maisha ya dsm yamekushinda I don't think kama kuna mkoa utakuwa rahisi though is possible
Na hili ni tatizo la Watanzania wengi, akili zenu mmezifunga mahala pamoja hamtaki kutoka na kujionea sehemu zingine maisha yanaendaje, kubadili mazingira ni ibada pia.
 
Dar Kuna maisha yote unayoyataka wewe. Ukitaka maisha magumu yapo, ukitaka maisha mepesi yapo. Ni wewe tu mikoani inaenda kufanya nn?
Asilimia 80 dar watu wana maisha magumu usiangalie tu kula,kunywa bia na kuwa na kagari maisha ni vile unasonga mbele,una akiba benk n.k...dar mtu unaweza kumuona ana maisha mazuri kama ni muajiriwa akfukuzwa kazi leo mpe mwezi tu anaanza kuuza tugari take nenda mbeya
 
Kahama naiwazia sanaaa, ahsante kwa hili, je unaweza ukanipa dondoo zaidi juu ya Kahama au Geita?
BIashara ipi inafaa, (bado najitafuta sina mijipesa)
Tamaduni zao,
Gharama za maisha,
N.k
Kama unaweza kupika chakula kizuri biashara ya restaurant utapiga hela sana wale raia hua hawaulizi bei wanaagiza tu.

Pia kwenye biashara ya nguo na viatu naona kuna gap unaweza kufanya research yako

Cash point ila hii lazima uwe na kibunda hii ilikua relevance miaka minne iliyopita sijui kwa sasa unaweza kuta ishakua saturated
 
Back
Top Bottom