Nataka Kuacha Ukristo na Kujiunga na Buddhism – Nianzie wapi Dar?

Nataka Kuacha Ukristo na Kujiunga na Buddhism – Nianzie wapi Dar?

Na hii ndiyo sababu inayofanya maombi kutokuwa uthibitisho wa chochote kuhusu mungu.
Yeye atakaye kunifuata na ajikane nafsi yake, auchukue msalaba wake kisha anifuate!!!

Ni maneno ya YESU, Yanayoonyesha una takiwa ujitoe kweli kweli kumfuata, na sio blah blah!!!
 
Kila la Kheri mkuu/

Nenda mtaa wa MINDU pale Upanga kuna tempo lao
Asante sana mkuu. Hii ndiyo information niliyokuwa natafuta. Nitaanza kwa kufika Mindu na kuongea na viongozi wa temple. Nikifanikiwa kupata maelekezo mazuri nitashare hapa.
 
Usisahau kabla ya kufa waachie ndugu zako pesa ya kuchoma mwili wako.

Kuchoma mwili kuna gharama kubwa tofauti na kuchimba shimo na kufukia.
😂😂😂😂Hapo umenipa homework nyingine. Kuhusu kuchomwa , bado sijafika huko mkuu.

Kwa sasa nataka kwanza nijue Buddhism ni nini, meditation, teachings na namna Buddhist anaishi. Mambo ya mwisho wa safari tutayajadili baadaye.😅
 
Ubudha una make sense kuliko Ukristo na Uislamu
Quran 29:17

" Hakika nyinyi mnaabudu masanamu badala ya Mwenyezi Mungu, na mnazua uzushi. Hakika hao mnao waabudu badala ya Mwenyezi Mungu hawakumilikiini riziki yoyote. Takeni riziki kwa Mwenyezi Mungu, na mumuabudu Yeye, na mumshukuru Yeye. Kwake Yeye ndio mtarudishwa"
 
Jipe muda pia kuusoma uislam,ndiyo dini pekee iliyonyooka na ndiyo kimbilio pekee la watu wengi Duniani.
Soma mafundisho halisi ya uislam usiwasome waislam.
Ukristo na Uislamu navijua toka mtoto. Ukristo nimeuishi, ila kuna vitu nilivyozidi kukua nikaanza kutokuendana navyo.

Uislamu pia nimewahi kuujua, lakini ukweli sijawahi kuvutiwa na baadhi ya mafundisho yake wala lifestyle ya Muhammad. Ndiyo maana kwa sasa nimevutiwa na Buddhism na nataka kuifahamu kwa kina.
 
Ukifanikiwa na mimi nishtue hiyo ndio huwa naona ni dini ya ukweli sana na haki, tuachane na upuuzi wa kikristo na uislamu.
Quran 29:25

" Na (Ibrahim) alisema: Hakika nyinyi mmeyashika masanamu badala ya Mwenyezi Mungu kwa mapenzi yaliyo baina yenu katika uhai wa duniani. Kisha Siku ya Kiyama mtakataana nyinyi kwa nyinyi, na mtalaaniana nyinyi kwa nyinyi. Na makaazi yenu ni Motoni. Wala hamtapata wa kukunusuruni."
 
Quran 29:25

" Na (Ibrahim) alisema: Hakika nyinyi mmeyashika masanamu badala ya Mwenyezi Mungu kwa mapenzi yaliyo baina yenu katika uhai wa duniani. Kisha Siku ya Kiyama mtakataana nyinyi kwa nyinyi, na mtalaaniana nyinyi kwa nyinyi. Na makaazi yenu ni Motoni. Wala hamtapata wa kukunusuruni."
"Usiwe.....na miungu......mingine ila.....MIMI"
KUTOKA 20:3.
 
Back
Top Bottom