Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,447
- 7,832
Waziri wa habari, Nape Nnauye amewataka wabunge kuacha kutuhumu wizi kwenye mitandao ya simu kwa ujumla.
Nape amesema bando ni huduma ya ziada ambayo ina masharti ya muda, mtu akitaka lisiishe uko utaratibu wa kutumia 'Main Tarrif' akitolea mfano tiketi za kusafiria za mwezi ambayo hauwezi ukadai hata ukitumia mara moja.
Nape amesema hofu yake ni kutumia Bunge kushutumu uwekezaji mkubwa kuna wizi inakwenda kuharibu huduma ya mawasiliano.
Spika Tulia akifafanua swali la mbunge, alimtaka Nape aeleze kama ni sheria au utaratibu na kama Bunge linao uwezo wa kubadilisha au haliwezekani.
Nape amesema ni utaratibu wa kibiashara ndio maana bei yake ni ndogo kulinganisha na kutumia salio na sio suala la sheria.
====
Akitoa hoja, mbunge Franscis Mtinga ametaka bando ziwe kisheria na Nape kama ambavyo alileta muswada wa kulinda habari binafsi, alete muswada wa kulinda haki kwani mashirika ya simu yanaibia wananchi sana. Mbunge ametaka kutopangiwa jinsi ya kutumia bando alilonunua.