SoC03 Malalamiko ya Bando na Huduma nyingine za Mawasiliano, tatizo kuu ni Kutofuata Misingi ya Utawala Bora, na suluhisho ni hili

Stories of Change - 2023 Competition

P Didy Wa Tanzania

JF-Expert Member
May 6, 2022
2,376
3,891
 UTANGULIZI


TCRA NI NINI ?


Ni mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ni taasisi ya Serikali inayosimamia sekta ya mawasiliano katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. TCRA ilianzishwa chini ya Sheria ya Mamlaka Mawasiliano Tanzania namba 12 ya mwaka 2003 baada ya kuunganishwa Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC) na Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC). TCRA inasimamia sekta ndogo za mawasiliano ya simu, intaneti, maudhui ya utangazaji (katika redio na televisheni) na huduma za posta.


Kufuatia maendeleo ya teknolojia, ilionekana haja ya kuunganisha Taasisi mbili za TCC na TBC na kuunda Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania-TCRA mnamo mwaka 2003 kwa lengo la kupunguza urasimu, kuongeza ufanisi na kukuza ubora zinazosimamiwa.

mnamo tarehe 1 Novemba, 2003 TCRA ilianza majukumu . Hatua hii ilitekelezwa chini na kifungu cha 4 (1) hadi (7) cha Sheria ya TCRA, 2003.

Dira kuu ; Kuwa na jamii iliyowezeshwa kwa huduma za Mawasiliano ya kielektroniki na posta zenye hadhi ya kimataifa.

Dhamira; Kusimamia huduma za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kwa kuhimiza ushindani wenye tija, ufanisi wa kiuchumi na upatikanaji wa huduma bora kwa wote; pamoja na kulinda maslahi ya wadau kwa ustawi wa jamii ya Kitanzania

Lengo; Kuboresha maisha ya Watanzania kupitia udhibiti wenye ufanisi, unaochochea na kukuza ubunifu na ambao unahakikisha kupatikana kwa huduma bora na imara za mawasiliano kwa wote na ambazo zinatolewa kwa gharama nafuu.

Baada ya yote tunatakiwa kujua kuwa maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia yanasaidia kukuza ubunifu , kupata taarifa, kujifunza na kutengeneza kipato kwa taifa na wananchi wake .

Lakini maendeleo yote aya hayawezi kuja bila utekeleza ipasavyo kwa misingi ya utawala bora kama vile ; UWAJIBIKAJI, UWAZI, UTAWALA WA SHERIA , USHIRIKISHWAJI , USAWA ,UFANISI WA TIJA ,MWITIKIO, MARIDHIANO NA UADILIFU

kutotekeleza ipasavyo kwa misingi ya utawala bora. kuna pelekea maendeleo kwenye upande wa habari na mawasiliano kutokuwa kwa kasi.

 CHANGAMOTO

Zifuatazo ni miongoni mwa changamoto zinazopelekea malalamiko mengi kwenye sekta ya habari na mawasiliano;

I. KUKOSEKA KWA UWAJIBIKAJI (majibu na maelezo).

"Kwa mujibu wa ibara ya 8(1) (c) ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania, 1997 Serikali ( Viongozi na Watendaji) itawajibika kwa Wananchi".

Maana ya uwajibikaji inataka kiongozi au mtendaji kutoa majibu , kubeba dhamana na kutoa maelezo kwa wananchi juu ya matendo aliyofanya katika kutekeleza dhamana aliyopewa na anaowaongoza au kuwapa huduma.

kukosekana kwa maelezo na majibu kwa kama sehemu ya uwajibikaji katika utoaji wa huduma za mitandao husababisha watu kutokuwa na imani na huduma wanazopata.


II. KUKOSEKANA UWAZI (Upandishwaji wa bei za vifurushi bila taarifa kwa wateja).


Katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, katika kipengele cha uwazi kinasema " kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wowote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za Wananchi , pia juu ya maswala muhimu ya kijamii " Ibara 18).

Hivi karibuni kumejitokeza malalamiko mengi sana juu ya mabadiliko ya bei za vifurushi vya ( MB's , Dakika & Messages) na ukubwa kubadilika bila taaarifa yoyote.

inapelekea idadi ya watumiaji wa huduma kupungua au kuachana na huduma hiyo.

1683883568871.jpg


mamlaka inapaswa kuwa na uwazi na kutoa taarifa kwa wakati, kwa sababu imekuwa ni kilio cha wengi kwamba vifurushi vinaminywa kila uchao na ukimya wa mamlaka husika unadhua maswali mengi.

Itambulike kuwa wingi wa malalamiko ni kiashiria tosha kwamba kuna tatizo sehemu.

III. UKOSEFU MARIDHIANO NA MWITIKIO ( Kwenye huduma za marekebisho ya vifurushi mteja anapokosea kujiunga).
Ukosefu wa umakini na makosa ya kibinadamu inapelekea mteja kujiunga kifurushi ambacho hakuwa hanakiitaji. mfano alikuwa anataka kujinga na kifurushi cha dakika bahati mbaya akajiunga na kifurushi cha Data.

kwa bahati mbaya makampuni ya simu hayana huduma ya kumsaidia mteja wao katika swala la kubadili kifurushi.

Kuna haja ya kutengeneza mfumo utakaokuwa unaweza kubadili kifurushi kimoja kwenda kingine.

Kwa mujibu wa katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania 1977 Raia ana haki ya uhuru wa kushiriki kikamilifu katika mambo yanayomuhusu yeye, maisha yake au taifa lake " ( Ibara ya 21).

IV. KUKOSEKANA KWA UADILIFU NA UTAWALA WA SHERIA. (Unaopelekea wizi na udanganyifu mitandaoni).

Kuna ukosefu mkubwa sana wa elimu ya kutumia mitandao na kumiliki SIM card .
Kuna uwezekano watu wanasajili laini bila kujua sheria za nchi na matumizi ya mitandao na inapelekea wizi , matusi na udanganyifu mwingi.

Ilipaswa mwananchi ajue na akubali sheria za mawasiliano kabla hajasajili SIM card. Usajili wa SIM card kwa njia ya alama za vidole unaonesha umepunguza kiasi tatizo lakini haujamaliza tatizo.

Pia, kumekuwa na malalamiko ya wateja kuungwa na huduma bila ruksa ya mteja na kupelekea kutumika kwa salio bila ridhaa ya mteja .

1683883651170.jpg


TCRA kushirikiana na Makampuni ya simu yanapaswa kufungia SIM card zinazotumika kufanya vitendo vya uharifu.

Wananchi wanataka kuona hatua zikichukiwa baada ya kutoa taarifa.

Katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania inatiria mkazo kipengele cha utawala wa sheria ( Ibara 13 & 24).

V. UKOSEFU WA UFANISI TIJA KWA WATEJA (Juu ya matumizi ya mitandao na vifaa vya internet).

Ikiwa miongoni wa malengo makuu ya TCRA ni " Kulinda maslahi ya wadau na kukuza uelewa wa haki na wajibu wao" ( Rejea Malengo Makuu Namba 4).

Basi inapaswa kutumia nguvu kubwa kuwaelemisha wananchi kuhusu matumizi sahihi ya mitandao, ili wananchi wanufaike na mitandao.

Pia, kumekuwa na malalamiko mengi sana. kuhusu Bando za wateja kuisha mapema tofauti na matumizi yao. hiki ni kiashiria kimoja kuna ukosefu wa elimu wa mipangilio ya vifaa vya internet ambavyo wananchi hawana elimu navyo .

1683910882842.jpg



 SULUHISHO

 Mmoja, Kutekeleza kikamilifu kwa misingi ya utawala bora : Wananchi wanatapoongozwa kwa kufuata misingi ya Utawala bora. Itasaidia kukua kwa nguvu za uzalishaji wa mapato na imani yao juu ya makampuni na serikali yao.

Pili, Uboreshaji wa huduma : Zinapaswa mamlaka kuja na mfumo utakaomwezesha mtumiaji wa simu kuweza kuona kiasi gani cha bando au data ametumia pasina kusumbuka.

Mfano; Kuwa na risiti za data zitakomfikia mteja kwa njia ya message.

zitakazo onesha manunuzi na matumizi ya data. ( sio kutumiwa message bando lako limeisha tu bila maelezo ya matumizi)

Tatu, Kupokea maoni ya wadau hasa watumiaji wa mitandao na kuyafanyia kazi kwa wakati.

Nne, elimu ya matumizi ya mitandao na kuwachukilia hatua watu na mashirika yanayofanya utapeli na udanganyifu.

Imani yangu kwa makampuni ya simu kwa kushurikiana na TCRA yatafanikiwa kuja na suluhisho.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom