Nape: Bando ni huduma ya ziada, ukitaka lisiishe tumia salio la kawaida. Mbunge ataka liwe kisheria

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,441
7,778
Waziri wa habari, Nape Nnauye amewataka wabunge kuacha kutuhumu wizi kwenye mitandao ya simu kwa ujumla.

Nape amesema bando ni huduma ya ziada ambayo ina masharti ya muda, mtu akitaka lisiishe uko utaratibu wa kutumia 'Main Tarrif' akitolea mfano tiketi za kusafiria za mwezi ambayo hauwezi ukadai hata ukitumia mara moja.

Nape amesema hofu yake ni kutumia Bunge kushutumu uwekezaji mkubwa kuna wizi inakwenda kuharibu huduma ya mawasiliano.

Spika Tulia akifafanua swali la mbunge, alimtaka Nape aeleze kama ni sheria au utaratibu na kama Bunge linao uwezo wa kubadilisha au haliwezekani.

Nape amesema ni utaratibu wa kibiashara ndio maana bei yake ni ndogo kulinganisha na kutumia salio na sio suala la sheria.

====

Akitoa hoja, mbunge Franscis Mtinga ametaka bando ziwe kisheria na Nape kama ambavyo alileta muswada wa kulinda habari binafsi, alete muswada wa kulinda haki kwani mashirika ya simu yanaibia wananchi sana. Mbunge ametaka kutopangiwa jinsi ya kutumia bando alilonunua.

Nape anapaswa kuwa upande wa wananchi .

Kwanini anawasemea waendesha makampuni ya mawasiliano? Sisi tunalalamika kwamba huduma za internet zimekuwa ju Sana, hata vile vifulushi tulivyo kuwa tunatumia awali kwa bei inayo endana na uchumi wa wananchi wengi vimebadilishwa na kuwa ghari.

Sasa iweje awajibie hao anawao waita wawekezaji? Ndiyo kusema wamepandishiwa gharama za uendeshaji karibu marambili kama walivyo ongeza gharama hizo kwa wananchi?
 
Waziri wa habari, Nape Nnauye amewataka wabunge kuacha kutuhumu wizi kwenye mitandao ya simu kwa ujumla.

Nape amesema bando ni huduma ya ziada ambayo ina masharti ya muda, mtu akitaka lisiishe uko utaratibu wa kutumia 'Main Tarrif' akitolea mfano tiketi za kusafiria za mwezi ambayo hauwezi ukadai hata ukitumia mara moja.

Nape amesema hofu yake ni kutumia Bunge kushutumu uwekezaji mkubwa kuna wizi inakwenda kuharibu huduma ya mawasiliano.

Spika Tulia akifafanua swali la mbunge, alimtaka Nape aeleze kama ni sheria au utaratibu na kama Bunge linao uwezo wa kubadilisha au haliwezekani.

Nape amesema ni utaratibu wa kibiashara ndio maana bei yake ni ndogo kulinganisha na kutumia salio na sio suala la sheria.

====

Mbunge Franscis Mtinga ametaka bando ziwe kisheria na Nape kama ambavyo alileta muswada wa kulinda habari binafsi, alete muswada wa kulinda haki kwani mashirika ya simu yanaibia wananchi sana. Mbunge ametaka kutopangiwa jinsi ya kutumia bando alilonunua.

View attachment 2412504
Nape amevimbiwa hadi kitambi kinaota kifuani badala ya tumboni!
 
Mbunge Franscis Mtinga ametaka bando ziwe kisheria na Nape kama ambavyo alileta muswada wa kulinda habari binafsi, alete muswada wa kulinda haki kwani mashirika ya simu yanaibia wananchi sana. Mbunge ametaka kutopangiwa jinsi ya kutumia bando alilonunua.
Aisee sijui hii nchi wanataka nini? Kila siku wanapiga kelele za soko huria alafu wenyewe ndio wanaharibu....

Hii kitu rahisi sana tuna shirika letu TTCL tuna Shares nyingi Airtel..., Kwanini wasipunguze huko to the minimum...., watu si watahamia huko hence hawa wengine kushusha bei ili wateja waje?

Wanashindwa kutengenezq Sera na kuweka mambo sawa wanaleta porojo na cheap politics ili waonekane ni watetezi...

Hivi katika hizo bundle serikali inakula Kodi kiasi gani? (Wachawi mara nyingi ni hao hao lakini always passing the blame to the next guy)

Sometimes najiuliza hata kama tunahitaji hii Serikali it seems inaharibu kuliko kutengeneza...
 
Kuna uwezekano mkubwa Serikali inajua inachofanya kwa haya makampuni kila mwezi, hasa Mwigulu Nchemba.

Huenda kila mwezi wanapandishiwa kodi/tozo halafu wanapewa ruhusa ya kuihamishia kwa wananchi, manake wameona kuweka tozo direct kelele zimekuwa nyingi.
 
Kwanini anawasemea waendesha makampuni ya mawasiliano?
Vijana wanashindana kukusanya pesa za campaign 2025;
1. January anakamua kwenye miradi ya umeme na Gas
2. Madilu anakusanya kwenye kusamehe kodi.
3. Nape yeye kwenye kugandamiza wananchi kwenye bundles

Kwa kifupi wananchi hatuna hela za kuwahonga, thamani yetu ipo kwenye box la kura!!

Tukutane 2025!!
 
Nape yuko sahihi katika hili japo ni kweli lina maumivu kwa watumiaji wa bando. Lakini ni maumivu yasiyo na uhalisia. Bando ni mfumo wa promotion katika biashara, sasa vipi promotion uiwekee sheria au umlazimishe mtoa promotion au offer iwe endelevu au ya kudumu? Tuwe objective wakati mwingine.
 
Back
Top Bottom