Kama tujuavyo kuwa mheshimiwa sana upande ule, ndugu Tundu Lissu, aliitangazia nchi kuwa anaenda Chato kuhiji kaburi la JPM. Hilo lilitokea juzi kama sio majuzi. Alisema 'lazima' afike.
Baadae tukasikia UVCCM imepiga marufuku 'madange' hayo na kutoa tamko kwa chadema kuwa 'mdako' huo au 'kidali po' hicho wakachezee huko kwao kwenye ile ofisi iliyopakwa rangi kwa bil. 2 ila sio ardhi ya Chato ambako umelala mwili wa aliyewahi kuwa mtu mkubwa nchi na mwenyekiti wa chama chao. Baada ya tamko hilo la UVCCM, tukasikia tena 'hakikisho' la chadema kuwa LAZIMA lissu atafika; UVCCM watake au wasitake.
Leo, tumeamka na threads kadhaa humu za wafuasi wenye uegemeo wa chadema wakiwadhihaki UVCCM kuwa 'kiko wapi'; mbona mheshimiwa tundu lissu ametimiza azma yake ya kufika kaburini kwa jpm 'kuhiji' kama alivyodai?
Sasa sisi wengine ni wadogo tu hatuelewi mambo haya yanavyoenda. Kwa sababu hiyo basi, na kwa heshima au unyenyekevu mkuu, naomba mwenye picha ya tundu lissu akihiji katika kaburi la marehemu JPM (sawa na uhakika alioutoa kwa 100%). Ahsanteni sana.