Tundu Lissu umebakiza kutubu kwenye kaburi la Hayati Magufuli

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
3,510
7,755
Binafsi nilikuwa nahisi kwamba Tundu Lissu anamchukia sana Hayati Magufuli hasa baada ya kile kisicho na ushahidi kuhusishwa kwake na Tukio la kushambuliwa Tundu Lissu.

Alichokifanya Tundu Lissu katika mazungumzo ya ufisadi wa bandari ya Dares salaam kuhusu JPM ni dhahiri kwanza hamchukii JPM pili ni mzalendo wa kweli, kitendo cha Lissu kusema Hayati Magufuli hahusiki na mikataba ya hovyo ya nchi yetu imeonyesha anamkubali linapokuja swala la uzalendo usiotia shaka katika kulinda rasilimali za nchi.

Tundu Lissu amebakiza kwenda Chato kulia kwenye kaburi la Magufuli na watanzania watamwamini na kumfanya awe Rais wao wa awamu ya 7.
 
Hivi JPM alipokuwa hai, TL hajawahi kusema hana tatizo na JPM kama JPM ila ana tatizo na raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambaye ni JPM?

Sasa kama ugomvi wake ni cheo alichokuwa nacho JPM na si JPM mwenyewe huko makaburini hana sababu ya kwenda maana cheo kipo hai na kule yapo mabaki ya mwili wa JPM.
 
,Binafsi nilikuwa nahisi kwamba Tundu lissu anamchukia sana Hayati Magufuli hasa baada ya kile kisicho na ushahidi kuhusishwa kwake na Tukio la Kushambuliwa Tundu lissu...
Wale wa Masasi wamuwahi mwamba kabla haijafika wakati wa kutafuta kaburi lake ili wakaombe radhi🤔
 
Back
Top Bottom