Nani mkali kati ya Diblo Dibala na Dally Kimoko

Mkuu! Diblo ni habari nyingine sana. Jamaa alikuwa anabadili key zaidi ya 8 kwenye wimbo mmoja. Na kila key anayohamia anaitendea haki. Yaani wafalme wa gitaa (solo) ni Diblo, na rhythm (Locasa)
 
wote wakali ila diblo anatisha kwenye keys,kwenye extra ball ya loketo hakurudia mpigo hata mmoja,kila akibadilisha pigo ni jipya,wataalam wanakwambia alibadili nyuzi mara 32,matchatcha kulikuwa na nyekese,mle gita linalia over limo mumayi
Dah, upo sawa mkuu. Ile Diblo Matchatcha, mtiririko wa key haukuwa wa kawaida!
 
Mkuu kama hujui muziki bora uwe kimya,kuna nyimbo zilikuwa kali kuluko hata za yondo,kuna wasanii kana FEDE LAWU,ALAIN KOUNKOU,FREDE MAJUNGA,JEAN BARON,TCHIKOTCKAYA,SHIMITA,AUROUS MABELE,SOUKOUS STARS,n.k ,kwa uchache tu hao,na wote wamepigiwa solo na diblo dibala,acha kukariri mambo
Nasemaje, DIBLO ndiye mfalme wa solo Guitar duniani. Hao wanamziki wote uliowataja vibao vyote ni vikali mno. Mpaka leo vipo juu, sababu ni solo gitaa la Diblo
 
Nashauri mkasikilize Albums zifuatazo alizoshirikishwa Diblo Dibala, halafu mlete majibu:-

1. Mondory
2. Laissez Passer
3. Extra Ball

4. Amour Madidina - hii album Dali Kimoko aliwekwa pembeni anapiga rhythm Guitar.

5. Boune Tonnerre

6. Ok Madame

Naishia hapo kwanza.
Mkuu hizo sio albums bali ni nyimbo tu,ila kwenye boom tonnere napenda pale mwanzo inavoanza na mondory napenda inavoanza na extra ball napenda inavoanza..raisserpasser ni nzuri sana ila inanikera ina sauti kubwa sana
 
Dah, upo sawa mkuu. Ile Diblo Matchatcha, mtiririko wa key haukuwa wa kawaida!
Huyu diblo hakuwa na mpinzani kwenye solo,gitaa ilikuwa inaongea,kama kwenye hii mtchatcha gitaa inaongea kabisa,anabadili keys mwanzo mwisho,halafu solo yake ilikuwa na fleva
 
Diblo alianza kuwa maarufu kabla ya Dally Kimoko na pia tofauti na mwenziye,Diblo Dibala alisomea kupiga gitaa shuleni na gitaa lake analipiga kisopmi zaidi kuliko Dally Kimoko ambaye yeye anapiga kwa kipaji tu.....

Ukisikiliza solo zao utagundua kuwa zinatofautiana sana na kuna moja imejaa na nyingine inaonekana kama nyepesi hivi,solo ya Diblo imejaa tofauti na ya Dally Kimoko...

Unapotaka kujua nani mkali miongoni mwao hapo kura itamuangukia Diblo Dibala maana yeye na shule imo lakini kama unazungumzia kipaji basi Dally Kimoko yupo juu sana maana hapo alipo anapiga gitaa lake kwa kipaji tu na kama angekwenda na shule nadhani ingekuwa hatari kabisa....

Dally Kimoko anamzidi Diblo kwa umaarufu kwasababu baada ya Diblo Dibala kupata jina alianza kuleta dharau na kudai malipo makubwa sana na ndipo hapo Dally Kimoko alipoinukia na kupata dili nyingi zaidi na kumfanya kuwa maarufu na mwenye pesa zaidi ya mwenzie.Dally Kimoko hakuwa na maringo na wala hakudai malipo makubwa na ndiyo maana alipigia wanamuziki wengi sana hadi wanamuziki wa Afrika ya magharibi akina Oliver Ngoma,sikiliza wimbo wa Oliver Ngoma unaitwa Lussa au Mayumba na utasikia solo ya Dally Kimoko ndani....

Jamaa hakuwa na maringo kabisa na ndicho kilichomzamisha kabisa mpinzani wake...
Umejadili kiweledi mkuu. Mwaka 95 nilikuwa napiga guitar. Models wangu wakiwa Dally na Diblo. Solo za Diblo zilikuwa ngumu kuiga kuliko Dally. Pia ndipo nilipata hiyo habari ya kwamba Diblo alikuwa anaringa akipewa dili. Na alikuwa anadai malipo makubwa. Ila ilikuwa ni heshima kubwa ukifanikiwa kupigiwa solo na Diblo
 
Mkuu hizo sio albums bali ni nyimbo tu,ila kwenye boom tonnere napenda pale mwanzo inavoanza na mondory napenda inavoanza na extra ball napenda inavoanza..raisserpasser ni nzuri sana ila inanikera ina sauti kubwa sana
Mkuu

Hizo ni album zilizoitwa majina ya hizo nyimbo.
 
Aisee nirudie mara ngapi? Hii haimfanyi Tosh kuwa mpiga solo. Wanamuziki (wapiga ala) wengi wanaweza kugusa chombo zaidi ya kimoja. Hii ni kawaida kwenye muziki wa dansi. Na nimekuambia sina haja ya You Tube. Nimeishi kabla na baada ya kundi original la The Wailers (Bob, Tosh na Bunny); kwa hiyo ninaijua historia.

eaqalrights= equal rights
Kubali kuelekezwa, ubishi utakugharimu.

Peter Tosh alikuwa mkali mpaka kwenye kung-fu, alikuwa na mkanda mweusi.

Alikuwa anapiga solo makini sana.
Tafuta wimbo wake wa Bush doctor. usikilize.
 
Mumie Lolo solo kacharaza Dally Kimoko kijana,sikiliza vizuri....

Dally Kimoko anaonekana hapo anacharaza solo....


Hapo waimbaji ni

1. Aurlus Mabele (wengi tulimchanganya tukawa tunamuita Loketo).

2. Jean Barron - mwenyewe, mwenye album

3. Ballow Canta, na

4. Lucien Bokiro

Tumba alisimama Awilo Longomba
 
Kubali kuelekezwa, ubishi utakugharimu.

Peter Tosh alikuwa mkali mpaka kwenye kung-fu, alikuwa na mkanda mweusi.

Alikuwa anapiga solo makini sana.
Tafuta wimbo wake wa Bush doctor. usikilize.
Unaonyesha ujinga na umbumbumbu wako (samahani kwa kutumia lugha kali). Aliyepiga lead guitar (solo) kwenye Bush Doctor ni Donald Kinsey. Peter Tosh alipiga rhythm & acoustic guitars, clavinet, na audio harp, licha ya kuimba.
 
Unaonyesha ujinga na umbumbumbu wako. Aliyepiga lead guitar kwenye Bush Doctor ni Donald Kinsey. Peter Tosh alipiga rhythm & acoustic guitars, clavinet, na audio harp.
Lead guitar kwenye reggae ni BASS guitar.
Usikosee kuelewa.
Usijitwike ujuvi wakati una kichwa cha panzi.
 
Lead guitar kwenye reggae ni BASS guitar.
Usikosee kuelewa.
Usijitwike ujuvi wakati una kichwa cha panzi.
Ha ha ha, eti lead guitar kwenye reggae ni BASS guitar. Unaelewa unachoongea lakini? Hebu kwenda zako huko na ubashite wako. Aliyepiga bass katika huo wimbo ni Robbie Shakespeare.
 
Unaonyesha ujinga na umbumbumbu wako (samahani kwa kutumia lugha kali). Aliyepiga lead guitar (solo) kwenye Bush Doctor ni Donald Kinsey. Peter Tosh alipiga rhythm & acoustic guitars, clavinet, na audio harp, licha ya kuimba.
Mkuu kwa ufahamu wangu lead guitar ni Rhythm siyo solo....
 
Baada ya album ya Extra ball kundi la Loketo lilianza kumtumia Dalli Kimoko kwenye upande wa soro Guitar, na kuachana na Diblo
Mkuu kuwa makini unapoandika mambo haya maana ukileta matatizo ya uandishi yaliyotamalaki hapa nchini kwa sasa kwenye lugha za watu utajikuta unaandika vitu vingine kabisa...

Hakuna guitar linaloitwa soro kula Solo na neno hilo siyo la Kiswahili,kuwa makili mkuu....

Usije kuwa kama jamaa mmoja badala ya kuandika "Global" akaandika "Grobal"...
 
Hapo waimbaji ni

1. Aurlus Mabele (wengi tulimchanganya tukawa tunamuita Loketo).

2. Jean Barron - mwenyewe, mwenye album

3. Ballow Canta, na

4. Lucien Bokiro

Tumba alisimama Awilo Longomba
Lucien Bokilo siyo Bokiro...
 
Umejadili kiweledi mkuu. Mwaka 95 nilikuwa napiga guitar. Models wangu wakiwa Dally na Diblo. Solo za Diblo zilikuwa ngumu kuiga kuliko Dally. Pia ndipo nilipata hiyo habari ya kwamba Diblo alikuwa anaringa akipewa dili. Na alikuwa anadai malipo makubwa. Ila ilikuwa ni heshima kubwa ukifanikiwa kupigiwa solo na Diblo
ni kweli kabisa kwamba kuweza kuiiga solo ya Diblo ni kazi ngumu sana kuliko ya Dally Kimoko,lakini kwangu mimi solo ya Dally Kimoko ni tam kuliko ya Diblo,sikiliza huu wimbo hapa chini wa Mack Mackaire,kuna sehemu Cayern Madoka ameiga kipande cha solo cha kwenye wimbo wa Pardon wa Jean Baron,ukisikiliza kuna tofauti ya namna ya solo inavyosikika lakini kunautam tofauti kabisa....

 
Mkuu hivi ile bendi ya Nouvelle generation au Zipompapompa iliishia wapii
Jamaa wapo lakini nadhani bendi hii haipo tena maana watakuwa wameshakuwa watun wazima sana sasa hivi.Kiongozi wao Luciana Demingongo yupo...

Nakumbuka miaka ya 90 walizusha walipata ajali wakafa wote,kitu ambacho wazushi hawakujua ni kwamba mtu mzima Awilo Longomba [Albert William Longomba] alikuwa ni mmoja wa wanamuziki wa kundi hili na walikuja kuumbuka baada ya watu kujua hili baadaye....

Burudika na wimbo wao huu hapa...

 
Back
Top Bottom