Nani mkali kati ya Diblo Dibala na Dally Kimoko

Nani mkali kati ya Diblo Dibala na Dally Kimoko

Hapo kwa Jean Baron aliyepiga solo album nzima ni Dally Ndala Kimoko na sio Diblo, labda kuna wimbo wa jean baron aliutunga kipindi diblo akiwa bado loketo na kutoka katika album ya Extra Ball
Yeah,nadhani anaongelea Malou wa Jean Baron iliyopo katika Album album hio
 
Mumie Lolo solo kacharaza Dally Kimoko kijana,sikiliza vizuri....

Dally Kimoko anaonekana hapo anacharaza solo....


Aliyecharaza solo ni Benico Popolipo. Dally kapiga kwenye nyimbo chache sana
 
..Siutani mazee..kwani ile mipini ya hawa jamaa mnaionaje?? Hamza Kalala, John Maida, Abel Bartazar, Joseph Mulenga, Saidi Mabela, Kasim Rashid " Kizunga",Kasim Mponda na wengineo iko juu kishenzi nadhani walikosa exposure tu kiasi kwamba hawakuvumia mbali sana!!! Big up Bujibuji..

Mbona mmemsahau marehemu MICHAEL ENOCK na mpini wake enzi zake na Dar Jazz?
 
Sikumbuki kama kuna wimbo wa Pepe Kalle ambao solo ilipigwa na Diblo Dibala lakini nakumbuka wimbo kama Hidaya wa huyo huyo Kabasele Yampanya a.k.a Pepe Kalle solo ilipigwa na Dally Kimoko....

Dally Kimkoko amepigia wengi sana kwasababu hakuwa na maringo wala bei kubwa na hili lilimuinua sana na kumfanya kuonesha kipaji chake cha hatari kabisa kwa watu wengi.....
Wimbo wa pepe kalle wa Pon mon Paka Bouge kapiga Diblo Dibala
 
Daaah kweli umri wangu umeenda sasa , kupitia nyingi hizi za diblo dibala, nimetambua sasa umri umeenda,
 
Diblo kaaribu Sana kwenye albam ya sokous Star huyu jamaa mpaka walifikir labda gitaa Lake linakinanda ndani pia namuheshim Sana kimoko si mchezo ila shikamoo diblo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu GENTAMYCINE pita hapa utoe neno

Nadhani nilishalijibu hili Swali huko nyuma nashangaa hukuona Mkuu. Diblo Dibala ni ( Lionel Messi ) nikimaanisha amezaliwa Kupiga Gitaa la Solo kwakuwa ana Kipaji na Dally Kimoko ni ( Christiano Ronaldo ) nikimaanisha kwamba ana uwezo mzuri wa Kupiga Gitaa la Solo ila ni wa Kujifunza mara kwa mara tofauti na huyo Mwenzake.

Gitaa la Dally Kimoko a.k.a Dalikike au Gitare Enzanga Likwanza huwa linawafurahisha tu Binadamu pekee ila Gitaa la Diblo Kimoko a.k.a Solo Guitar Professeur haliishii tu kuwafurahisha Binadamu bali hata Ndege na Wanyama wote pamoja na Marehemu waliopumzika wakilisikia tu ' wanaburdika ' nalo.

Faida kubwa aliyonayo Dally Kimoko anayomzidi Diblo Dibala ni kwamba ukiachilia mbali Kupiga Gitaa la Solo hilo ila pia Dally Kimoko anaweza kupiga Gitaa la Kiungo ( linaitwa Rhythm Gitaa ) na hata Bass Guitar na alifanya hivi katika ' Album ' ile ya Soukouss Star na hata ile ya Stop Alertez yake Aurlus Mabele.

Kwanini Diblo Dibala atabaki kuwa Mwamba / Mahiri katika ukung'utaji wa Gitaa la Solo ni kwamba Wapiga Solo wengi huko Congo DR uwezo wao ni kupiga Gitaa la Solo lenye Nyuzi kuanzia 8 hadi 12 tu pekee lakini ' Mwanamume ' Diblo Dibala hadi hivi sasa ndiyo Mpiga Solo pekee ambaye anapiga Gitaa lenye Nyuzi 32 na hapo hapo ana uwezo mkubwa wa ' Kuzitekenya ' zile Nyuzi na ukizisikia utadhani anapigia akiwa ndani ya Maji yenye Mawimbi kitu ambacho hulete ladha zaidi katika Wimbo.

Wote hao nawakubali na nawapenda mno japo kwa sasa Congo DR Wapiga Magitaa wa Solo wanaokubalika na kutishiana amani kwa umahiri Wao ni hawa wafuatao:

1. Shevchenko Patou Solo ( Wenge Musica BCBG yake JB Mpiana japo amejiweka Kando na Bendi kwa sasa kwa Ugomvi na Mpenzi wake ambaye pia ni Mnenguaji mahiri wa Bendi hiyo aitwae Yeti Muyeti au Igret Montreal )

2. Ramazani Fulutuni ( Quarter Latin yake Koffi Olomide )

3. Flam Mwenie Kapaya ( Wenge Maison Mere yake Ngiama Makanda Werrason )

4. Pitchou Concorde ( anayepiga na Bendi ya Mwalimu wa Muziki wa Koffi aitwae Felix Wazekwa

5. Burkinafaso Mboka Liya ( mpiga Solo Deiwaka / Ndondo Congo DR nzima ambaye huwa anakodiwa na Wanamuziki wengi )

Ni hayo tu Mkuu na nadhani nimejaribu kidogo kukupa kila ambacho nina ufahamu nacho na hadi Kukuongezea vingine.
 
Back
Top Bottom