Mrigariga
JF-Expert Member
- Jun 7, 2011
- 1,761
- 1,634
Kweli kabisa MkuuDiblo ndiye mfalme na kama angezaliwa ulaya au marekani angekua idolized kama jimy hendrix.
Kweli kabisa MkuuDiblo ndiye mfalme na kama angezaliwa ulaya au marekani angekua idolized kama jimy hendrix.
Mosi,Hakuna wimbo hata m,moja wa Allan Konkou ambao solo ilipigwa na Didlo Dibala...Mkuu kama hujui muziki bora uwe kimya,kuna nyimbo zilikuwa kali kuluko hata za yondo,kuna wasanii kana FEDE LAWU,ALAIN KOUNKOU,FREDE MAJUNGA,JEAN BARON,TCHIKOTCKAYA,SHIMITA,AUROUS MABELE,SOUKOUS STARS,n.k ,kwa uchache tu hao,na wote wamepigiwa solo na diblo dibala,acha kukariri mambo
Mkuu umenitendea haki.Mosi,Hakuna wimbo hata m,moja wa Allan Konkou ambao solo ilipigwa na Didlo Dibala...
Pili,Jean Baron alipigiwa nyimbo chache sana na Diblo Dibala na wimbo maarufu wa Pardon kapiga solo Diblo Dibala lakini nyimbo kali zaidi na zilizovuma kama PANTALON MORIBA na KOUDIA NDAMBOU,solo kapiga Dally Kimoko....
Ishu hii iko pia kwa Aurus Mabele na kundi lake la Loketo ambalo Jean Baron alikuwa ni mmoja wa wanamuziki wa kundi hilo akiwemo Awilo Longomba na akina balou Kanta na Lucien Bokilo ambako zipo nyimbo chache ambazo solo alipiga Diblo Dibala lakini nyimbo nyingi alipiga Dally Kimoko na baadaye alikuja mtu mmoja anayeitwa Cayen Madoka ambaye alimpigia pia Mack Makaire ambaye naye aliwahi kuwa mwanamuziki wa Loketo ya Aurus Mabele....
Kwenye Soukous Stars sijui unaizungumzia ipi,lakini ile ya mwaka 1996 ambayo ilikuwa na wanamuziki Ngouma Lokito,Yondo "baby" Sister,Shimita,Balou Kanta,Lucien Bokilo,Saladin Wizoo na Lokasa ya Mbongo,solo ya kwenye nyimbo zote hakupiga huyo Diblo maana walikuwa na mpiga solo hatari anayekwenda kwa jina la Saladin Ferreira "Wizoo" na ukitaka kusikia solo yake sikiliza wimbo unaitwa "Abba Guimo" ambao yeye mwenyewe ni mtunzi au sikiliza wimbo wa Yondo Sister unaitwa Derniere Minute....
Kwa ujumla wa hoja yako na wanamuziki uliowataja siyo kweli solo kapiga Diblo Dibala kwa ujumla wake bali kapiga baadhi tu....
daah hayati Jean Baron, mami lolo huu wimbo niliupenda sanaNi album ya Jean baron inayoitwa come on ma huh,huko aliichapa sana solo
kulikuwa na nene tchakou ingawa yeye hajawika sana kama kimoko na dibalawote naona wapo vizuri
Ngoja niusake huo wimbo na nikisikia tu solo nitajua mkuu na nitakuambia....Mkuu umenitendea haki.
Wimbo wa Madi wa Yondo Babe, aliyecharaza Gitaa ni nani?
Leo nataka kujua marapa hawa nani mkali, wako wapi na wanafanya nini.
1.Tutu Kaludji
2.Bill Clinton
3.Rapa Wa General Defao(Ngkoz wa Ngkozi)
4.Rapa wa Bozi Boziana yule wa Nzawiseee
5.Genta Wenge BCBG(Kama ana fuzu kuwa nae rapa)
Hahahahaaaaa mkuu hiyo kadhi ni hatari.....Dally Kimoko balaa,cheki wimbo Lusa wa Oliver Ng'oma na pia Kadhi wa Kanda Bongoman jamaa kacharaza Gita balaa.
alikuwa mwimbaji sio mpiga gitaa huyu mkuuShimita
Kama hakuelewi basi autafute wimbo wa Tosh unaitwa "mistry Babylon"Fanya research yako vizuri......sio unabisha kizembe...kama ww ni mvivu tembelea hata google....Peter Tosh was an accoplished guitarist...take that fact if u dont know that
Mumie Lolo solo kacharaza Dally Kimoko kijana,sikiliza vizuri....Lassier Passie wa Diblo, Extra Ball wa Aurlus Mabele(Groupe Lokheto) Mummie Lolo wa Jean Baron(R.I.P) ft Aurlus Mabele hizo zote Diblo alicharaza Gitaa balaa.
Madi, Derniere Minute, Maweke, Wapi Yo, Africa zote za Yondo Sister Dally Kimoko alicharaza Gitaa balaa. Hivyo hawa wawili wote ni noma.
True that,wewe sasa unawajua sana hawaDiblo alianza kuwa maarufu kabla ya Dally Kimoko na pia tofauti na mwenziye,Diblo Dibala alisomea kupiga gitaa shuleni na gitaa lake analipiga kisopmi zaidi kuliko Dally Kimoko ambaye yeye anapiga kwa kipaji tu.....
Ukisikiliza solo zao utagundua kuwa zinatofautiana sana na kuna moja imejaa na nyingine inaonekana kama nyepesi hivi,solo ya Diblo imejaa tofauti na ya Dally Kimoko...
Unapotaka kujua nani mkali miongoni mwao hapo kura itamuangukia Diblo Dibala maana yeye na shule imo lakini kama unazungumzia kipaji basi Dally Kimoko yupo juu sana maana hapo alipo anapiga gitaa lake kwa kipaji tu na kama angekwenda na shule nadhani ingekuwa hatari kabisa....
Dally Kimoko anamzidi Diblo kwa umaarufu kwasababu baada ya Diblo Dibala kupata jina alianza kuleta dharau na kudai malipo makubwa sana na ndipo hapo Dally Kimoko alipoinukia na kupata dili nyingi zaidi na kumfanya kuwa maarufu na mwenye pesa zaidi ya mwenzie.Dally Kimoko hakuwa na maringo na wala hakudai malipo makubwa na ndiyo maana alipigia wanamuziki wengi sana hadi wanamuziki wa Afrika ya magharibi akina Oliver Ngoma,sikiliza wimbo wa Oliver Ngoma unaitwa Lussa au Mayumba na utasikia solo ya Dally Kimoko ndani....
Jamaa hakuwa na maringo kabisa na ndicho kilichomzamisha kabisa mpinzani wake...
Mi nazipenda LUTTER LUTTER,NABELELI na KODIA NDAMBOdaah hayati Jean Baron, mami lolo huu wimbo niliupenda sana