Nani mkali kati ya Diblo Dibala na Dally Kimoko

kakuruvi

JF-Expert Member
Sep 2, 2009
770
256
Nawasalimu Great Thinkers,

Kama kuna watu waliojaliwa vipaji na wamevitumia ni hawa jamaa wawili Diblo Dibala na Dally Kimoko, hawana utani wanapokamata mpini, mfano Diblo Dibala (Extra Boy), Dally Kimoko (Liza), si mchezo achilia mbali bendi zao za kazi ila wamekuwa wakitumiwa na bendi nyingine kurecord, kama kuna mwenye nyimbo walizopiga mpini leteni humu tusikie mambo, nani zaidi kati ya hawa magwiji wa mpini?
 
kakuruvi umenikumbusha mbali saaaaaaaaaaaaaana yaani sitakuja kuzisahau kazi za uhakika za hawa wanaume wa shoka diblo dibala na dalyyyyyy kimoko,hasa ile albam ya diblo ya matchacha nakumbuka ninayo ngoja niisake nikuwekee kama nitafanikiwa kuipta,kwa kweli leo umenikumbusha enzi zangu.
 
daly kimoko alipiga gitaa ktk albam moja ya aurlus mabele ya extra ball yaani mpaka leo kazi zao za zamani zinawika utazani zimeingia jana sokoni hazichuji ni kama ragae za bob marley hazichuji milele na kazi za hawa watu 2 ni mpya kila siku.
 
kakuruvi,

Sitaongelea Nani zaidi kati yao, but i just want to contribute kwamba kwa wale wanaJF ambao walipata kusikiliza vizuri nyimbo zilizochezwa na hawa watu, kweli watakubali kwamba walikuwa ni vinara wa fani hii na kuwafikia ni kazi ngumu!..Namkumbuka Dally Kimoko katika nyimbo nzuri sana za Aurlus Mabele, ambapo nakumbuka mwaka 1990 nilikuwa natembea umbali wa karibia km 2 kwaajili ya kufuata video pale Corner Bar jirani na External Mabibo.
 
kakuruvi,

Heshima Kakuruvi,

Kweli hawa jamaa walikuwa moto wa kuotea mbali.Diblo Dibala,Dally Kimoko na Neneh Chakuchaku walitawala vyema mpini wa solo kwa upande wa bass alikuwepo ngouma lokito na rhyzm alikuwepo Lokasa ya mbongo.

Kwenye anga za muziki hawa jamaa hawasikiki kabisa sijui kimewasibu nini.
 
Ngongo,

Ngongo nimefurahi sana kumbe na wewe uko njema, kweli hao wengine uliowataja ni moto, tuko pamoja!
 
Mombasa Vata vipi yule wa Lipua lipua? Sikia Temperature anavyonyanyasa! Naambiwa analala usingizi Ubelgiji.

Leka
 
raha ya gita njoo kwetu afrika
..Siutani mazee..kwani ile mipini ya hawa jamaa mnaionaje?? Hamza Kalala, John Maida, Abel Bartazar, Joseph Mulenga, Saidi Mabela, Kasim Rashid " Kizunga",Kasim Mponda na wengineo iko juu kishenzi nadhani walikosa exposure tu kiasi kwamba hawakuvumia mbali sana!!! Big up Bujibuji..
 
..Siutani mazee..kwani ile mipini ya hawa jamaa mnaionaje?? Hamza Kalala, John Maida, Abel Bartazar, Joseph Mulenga, Saidi Mabela, Kasim Rashid " Kizunga",Kasim Mponda na wengineo iko juu kishenzi nadhani walikosa exposure tu kiasi kwamba hawakuvumia mbali sana!!! Big up Bujibuji..

Laligeni unaikumbuka hii, ''Mabe, mabe, mabe, Mabelaa''
 
I liked Franco's string arrangement...six guitars in all....First solo(Gerry Dialungama,Papa Noel),Second solo(Djezzy Madjeku,Feluzi) midsolo(Franco himself),Rhythme1(Aime Kiwakana,Matalanza)Rhytme2(Gege,Simaro)Bass(Deca) acha mchezo...anagalia hii kitu live in Abidjan 1980 utunzi wake Lukoki Diato (wa pili kulia)lead vocals by Djo Mpoyi(far right , passed away in 1996) Wuta Mayi (Second left) and Dalienst Zitani ya Ntessa (died 1994 na kaka wa Kiesse Diambu ya Ntessa 'Wanted' alieimba Eve Sukali,famously with Afrisa International na alipohama akawa decalred 'wanted' ndio na sisi wabongo tukakopi tukamapata 'wanted' wetu Shaaban Yohana of the defunct Vijana Jazz)

Nimeipenda hii shoo ya wimbo huu...imagine in 1980

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=DmLqiyJo8Zc[/ame]
 
Back
Top Bottom