Nani mkali kati ya Diblo Dibala na Dally Kimoko


Heshima Kakuruvi,

Kweli hawa jamaa walikuwa moto wa kuotea mbali.Diblo Dibala,Dally Kimoko na Neneh Chakuchaku walitawala vyema mpini wa solo kwa upande wa bass alikuwepo ngouma lokito na rhyzm alikuwepo Lokasa ya mbongo.

Kwenye anga za muziki hawa jamaa hawasikiki kabisa sijui kimewasibu nini.
Ngouma lokito alikuwa na mbembwe tu...hamna kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sitaongelea Nani zaidi kati yao, but i just want to contribute kwamba kwa wale wanaJF ambao walipata kusikiliza vizuri nyimbo zilizochezwa na hawa watu, kweli watakubali kwamba walikuwa ni vinara wa fani hii na kuwafikia ni kazi ngumu!..Namkumbuka Dally Kimoko katika nyimbo nzuri sana za Aurlus Mabele, ambapo nakumbuka mwaka 1990 nilikuwa natembea umbali wa karibia km 2 kwaajili ya kufuata video pale Corner Bar jirani na External Mabibo.
Yes jamaa walikuwa ni extraordinary

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dally ni mzuri kuliko Diblo kutokana na kazi alizo fanya.Nikipata muda nitaziorodhesha.
Lakini japo kua nitakua nje ya topic nadhani hawa ndio wapiga solo bora
1-Prince Alain Makaba
2-Dally Kimoko
3-Diblo Dibala
4-Kinanga Boeing 737
5-Rolls Papiloni
6-Burkina faso
7-Volvo 840
8-Pipa Noel
9-Papa Felly
10-Dino Vangu
11-Rigo Star
Heshima kwa Ficarré Mwamba huyu nampa heshima kutokana na Solo alio icharaza kwenye wimbo bora wa muda wote toka DRC- Kala yi Boeing! Wa Wenge BCBG 4×4.
 

Heshima Kakuruvi,

Kweli hawa jamaa walikuwa moto wa kuotea mbali.Diblo Dibala,Dally Kimoko na Neneh Chakuchaku walitawala vyema mpini wa solo kwa upande wa bass alikuwepo ngouma lokito na rhyzm alikuwepo Lokasa ya mbongo.

Kwenye anga za muziki hawa jamaa hawasikiki kabisa sijui kimewasibu nini.
Hawa jamaa waliweza kuichakata rhumba na kupata kitu safi cha soukous..... Kwa kweli hawana mpinzani waliweza kucheza na mpini sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye album ya Pepe Kalle ya Pon Mon Paka Bouge Diblo na Dally Kimoko wameshirikiana kupiga magitaa. Katika nyimbo ambazo Diblo kapiga solo basi Dally kapiga rhythm na zile ambazo solo limepigwa na Dally rhythm kapiga Diblo.

Kumbe hawakuwa rivals?? RESPECT!!
 
Dally kimoko na Diblo Dibala wakipiga gitaa basi lazima utamani kutikisa kichwa, au miguu au hata kuinuka kucheza. Gitaa linapigwa hadi mizizi ya moyo inashtuka.


Dally Kimoko
 

Attachments

  • Soukous_Stars_-_Daly_Swing_(audio)(128kbps).mp3
    5.4 MB · Views: 28
Back
Top Bottom