Nani anayeihujumu TTCL? Kuna tatizo la kuadimika kwa laini, zinauzwa mpaka 7000

Hivi dpworld hawana mwenzao au ndugu yake anaye deal na sekta ya mawasiliano aichukue ttcl

Ova
 
Nani anayeihujumu TTCL kwa kiwango hiki?

Kuna mmbo fulani yanaendelea kwenye TTCL kiasi kwamba tunaona kama ni hujuma kwa TTCL:

Kwanza, Kipindi kirefu sasa ukitafuta laini za TTCL kwa mawakala wanakuambia hamna. Ni kweli shirika likose laini ambazo kimsingi ndio mteja na ndio zitachochea usambaaji wa huduma kwa watu wengi?

Pili, laini ya TTCL kupatikana kwake ni mpaka uinunue kwa gharama ya shilingi 5000 mpaka 7000 na hii ni gharama ya maeneo mengi ya Dar es salaam sijajua upatikanaji na gharama zake mikoani na huku laini za mitandao mengine ni bure kabisa na hadi kifurushi Cha kuanzia unawekewa tena bure. Kwa nini zipatikane kwa gharama hivi?

Tunasikia kila siku TTCL kupata hasara lakini kama mambo yenyewe ndio yako hivi basi hasara ni lazima.

Mitandao mingine ikitumia kila mbinu za kibiashara kuhakikisha zinakuwa na wateja wengi kwa kusambaza laini kwa wingi TTCL wako nyuma kwenye ushindani. Kiuhalisia kabisa, watu wengi sio rahisi kununua laini kwa gharama hiyo. Kama ni kuuza, ingeuzwa hata shilingi 1000.

Mhe. Samia na Waziri Nape tazameni hujuma hizi zinzofanywa dhidi ya TTCL na ikiwezekana libinafishwe tu ili liendeshwe kibiashara zaidi.
Hilo shirika kwenye kila kitu kuna commission za watu! Hizi ndio zinapandisha bei

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka 3-4 nyuma lain za TTCL zilikuwepo mtaani, nakumbuka ata vocha zake hazikuwa ngumu kupata, vifurushi vyake pia vilikuwa nafuu kuliko mitandao mingine.

Nasikitika kusema kwasasa si Lain ila ata vifurushi vyake viko juu kuliko mitandao yote nchini!
Line za ttcl zinaongoza kwa kutumiwa na wale wa nitumie kwenye namba hii mimi baba mwenye nyumba wako jina itasoma bandari dubai world🤣🤣🤣
 
Nadhani ilitakiwa minala yote iwe chini yao na kukodisha kwa makampuni ya simu ili kuhakikisha huduma inapatikana kote bila shida.
Umeona eeh!
Sasa wameingia kwenye ushindani kindezi ndezi!
Kila ripoti ya CAG ikitoka wameangukia pua!
 
Nani anayeihujumu TTCL kwa kiwango hiki?

Kuna mmbo fulani yanaendelea kwenye TTCL kiasi kwamba tunaona kama ni hujuma kwa TTCL:

Kwanza, kipindi kirefu sasa ukitafuta laini za TTCL kwa mawakala wanakuambia hamna. Ni kweli shirika likose laini ambazo kimsingi ndio mteja na ndio zitachochea usambaaji wa huduma kwa watu wengi?

Pili, laini ya TTCL kupatikana kwake ni mpaka uinunue kwa gharama ya shilingi 5000 mpaka 7000 na hii ni gharama ya maeneo mengi ya Dar es Salaam sijajua upatikanaji na gharama zake mikoani na huku laini za mitandao mengine ni bure kabisa na hadi kifurushi Cha kuanzia unawekewa tena bure. Kwa nini zipatikane kwa gharama hivi?

Tunasikia kila siku TTCL kupata hasara lakini kama mambo yenyewe ndio yako hivi basi hasara ni lazima.

Mitandao mingine ikitumia kila mbinu za kibiashara kuhakikisha zinakuwa na wateja wengi kwa kusambaza laini kwa wingi TTCL wako nyuma kwenye ushindani. Kiuhalisia kabisa, watu wengi sio rahisi kununua laini kwa gharama hiyo. Kama ni kuuza, ingeuzwa hata shilingi 1000.

Mhe. Samia na Waziri Nape tazameni hujuma hizi zinzofanywa dhidi ya TTCL na ikiwezekana libinafishwe tu ili liendeshwe kibiashara zaidi.
TTCL ilishauawa tangu RAIS alipotamka kuwa, ttcl wajihusishe na usimamizi wa mkonga wa tafaifa TU. Huduma zingine iachie wengine. Ila inaumiza sana hasa ukifikiria uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali ya awamu ya Tano kwenye shilika hili. Inakera sana
 
Back
Top Bottom