laini

  1. Trainee

    Kusajili laini mnaniletea wakala ananifuata mpaka vichochoroni lakini kufuta usajili mnaniambia nifike dukani kwenu! Hii siyo sawa!

    Halafu kuna mitandao ukipiga ile mia na sita ukaenda angalia usajili inasoma namba na jina lililosajili namba hiyo bila kuambiwa uweke nida! Hii nayo si sawa
  2. Joanne Joel

    Naomba msaada wa ushauri jinsi ya kupata laini za uwakala

    Nahitaji laini za wakala Tigo. (TigoPesa) Halotel (halopesa) Vodacom (m pesa) Airtel (Airtel money) Kwa atakayeweza kunisaidia Nipo Dar es salaam
  3. Candela

    Tahadhari: Mbinu mpya wizi wa pesa vijana wanaosajili laini za simu

    Kama unasoma uzi huu basi u buheri, pole kwa wenye changamoto. Hawa vijana wanaosajili laini za simu mitaani wamekuja na mbinu mpya kukuibia pesa. Wanatumia app za kampuni husika, TIGO PESA APP AU MPESA APP n.k. Wanawahadaa wateja kuwaunga 5G wapate intaneti yenye kasi bure kama ofa...
  4. Uzalendo wa Kitanzania

    Leo nimekula mihogo mitamu na laini kama keki maeneo ya Mbuyuni

    Wadau hamjamboni nyote Huu ni ushuhuda wa kweli kabisa uliothibitisha kuwa nilichokuwa nakifikiria kuhusu mihogo siyo kweli! Leo Jumatano majira ya mchana hapa maeneo ya Mbuyuni nimekula mihogo ya kukaanga ambayo ni mitamu na laini sana utadhani ni keki Nimpongeze sana huyu mama mpishi...
  5. Roving Journalist

    Zaidi ya Sh Bilioni 510 kujenga laini ya kusafirisha umeme kutoka Chalinze Substation hadi Dodoma

    Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeikabidhi Kampuni ya TBEA ya nchini China kandarasi ya kuanza ujenzi wa laini ya kusafirisha umeme kutokea Kituo cha kupozea umeme 'Chalinze Substation' mkoani Pwani hadi Dodoma ikigharimu Sh Bilioni 510. Akizungumzia kandarasi hiyo Aprili 17, 2024 akiwa...
  6. Melki the Storyteller

    Msaada: Laini yangu ya Halotel imepata matatizo ya kiintaneti

    Nimesajili laini ya Halotel mpya, hii ni baada ya kupoteza laini niliyokuwa nikitumia ambayo haikuwa na matatizo yoyote, ni vile tu nilisajiliwa na mtu ambaye niko mbali naye kwa sasa (Ex) Laini hii niliyosajili leo haina ufanisi kabisa kwenye suala zima la kimtandao. Yaani ipo very slow...
  7. Mtemi mpambalioto

    Mbunge Shabiby ataka fedha za bima kwa wote zikatwe kwenye laini za simu

    MY TAKE: huyu mbunge kwanza hana njaa! magari yake mpaka nauli Tsh 49,000 kutoka Dar kwenda dodoma yaan kila sku yeye anaingiza mamilioni ya hela Anachukulia poa kuwakamua maskini ili wasaidie maskini wenzao! yeye anapata mshahara 17Milioni kwa mwezi - Mwalimu anapata laki 3 kwa mwezi! halafu...
  8. Lady Whistledown

    Mbunge wa Gairo, Shabiby ataka fedha za bima kwa wote zikatwe kwenye laini za simu

    Mbunge wa Gairo (CCM), Ahmed Shabiby ameishauri Serikali kukata Sh2,000 kila mwezi kwenye laini za simu huku wabunge, wafanyabiashara na wafanyakazi wakikatwa Sh10,000 ili fedha hizo ziwe chanzo cha mapato kwa Bima ya Afya kwa wote. Amesema kuna wamiliki wa laini za simu milioni 72 nchini ambao...
  9. Mr Why

    Je, ni haki kwa mteja wa Vodacom kukataliwa kufutiwa Usajili wa laini kwasababu ya kuwa na namba moja tu?

    Kampuni ya Vodacom inakatalia wateja wake kufuta usajili wa laini zao kwasababu wanakuwa na laini moja tu. Vodacom wanadai kwamba hawawezi kufuta usajili wa laini moja tu labda ziwe zaidi ya moja. Kwanini wanafanya hivi kwasababu kitendo hiki ni sawa na kumlazimisha mteja atumie mtandao wenu?
  10. JanguKamaJangu

    TCRA yazifungia Laini 21,000 zilizohusika kufanya utapeli

    ZAIDI ya laini 21,788 za mawasiliano ya simu zimefungiwa kupokea na kutoa mawasiliano kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo kutumika kufanya uhalifu mtandaoni kwa kipindi cha miezi mitatu iliopita. Kwa mujibu wa ripoti ya mwenendo wa sekta ya mawasiliano iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa...
  11. DR Mambo Jambo

    Godbless Lema: Makonda tulia wewe ni mtoto laini sana kuliko hata maini

    Aliyekuwa Mbunge Wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema Amemtoa kauli hiyo kwa Katibu mkuu wa itikadi na Uenezi CCM taifa Mh Paulo Makonda huko Jamhuri ya watu wa X.. Baada ya kudai kwamba ataenda bungeni kuomba na kuuliza kuhusu aina ya uenezi wanayotka awe nayo.. Lema Ameendelea kusema kuwa...
  12. Influenza

    Rukwa kinara kwa majaribio ya Utapeli kupitia simu. Dar inaoongoza kwa usajili wa laini yawa ya 3

    Ripoti ya Takwimu za Mawasiliano Tanzania iliyotolewa na TCRA mwezi Septemba, imeonesha Mkoa wa Rukwa umekuwa Kinara wa Majaribio ya Utapeli kupitia simu ikiwa na Majaribio 8,450 kwa kipindi cha Julai hadi Septemba Hata hivyo kwa mujibu wa Ripoti hiyo, Rukwa inashika nafasi ya 25 kwenye orodha...
  13. Kabelwa

    Msaada, laini ya tigo haisomi data

    Habari ndugu, ninaomba msaada wa jambo hili,nime-renew namba yangu ya zantel ktk laini ya tigo kama invyofahamika makampuni haya ni mamoja ,tatizo linakuja kwenye data ni kwamba haisomi kabisa nimejaribu data setting za tigo na hata zantel hazionyeshi mtandao kama ni 2g,h+ au 4g ,naomba msaada...
  14. Vincenzo Jr

    Baadhi ya mitandao ya simu nchini wana vifurushi kausha damu

    Husika na kichwa cha habari hapo juu, Kwanza ningependa ujue mitandao yote ya simu Tanzania ina vifurushi vinavyofanana na kingine kila mtandao na spidi yake. Sasa kumezuka baadhi ya mitandao ya Haloteli, Airtel, Tigo kuwa na vufurushi vya data ambavyo ni data kausha damu, yaani ukinunua...
  15. Exile

    Nadhani airtel waache kutumie neno 4G kwenye laini zao 4G ya airtel sawa na 3G ya halotel

    Nadhani hii kero ya mtandao wa AIRTEL sio kwangu tu kuna wakati unanunua MB ufatilie habari unakutana na changamoto ya mtandao hadi MB zimeisha na huelewi zimeishaje maana taarifa uliyo unaifatilia kama ni video unakuta imeisha na umesikia kwa kukatika katika tu.
  16. Replica

    Vodacom yaendelea kuwa kinara idadi kubwa ya laini zilizosajiliwa, Airtel na Tigo mpambano wa kimya kimya!

    TCRA imetoa takwimu mpaka mwezi Juni 2023 ambapo jumla ya laini za simu zilizosajiliwa zimefikia 64,088,651 huku mtandao wa Vodacom ukiwa kinara. ORODHA 1. Vodacom - 19,116,166 2. Airtel - 17,505,139 3. Tigo - 17,484,387 4. Halotel - 8,410,029 5. TTCL - 1,559,090 6. Smile - 13,840
  17. Decency13

    Hivi kuna usalama kiasi gani kununua laini za uwakala mkononi mwa mtu?

    Kwa wenye uzoefu, Hivi kuna usalama kiasi gani kununua laini za uwakala kwa mkononi mwa mtu?
  18. Replica

    Habari Picha: Dkt. Bashiru akisalimiana na Waziri Mkuu Majaliwa wakiwa na bashasha laini Bungeni, Dodoma

    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Kuteuliwa, Dkt Bashiru Ally Kakurwa kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, leo Jumatano Juni 21, 2023.
  19. K

    Nani anayeihujumu TTCL? Kuna tatizo la kuadimika kwa laini, zinauzwa mpaka 7000

    Nani anayeihujumu TTCL kwa kiwango hiki? Kuna mmbo fulani yanaendelea kwenye TTCL kiasi kwamba tunaona kama ni hujuma kwa TTCL: Kwanza, kipindi kirefu sasa ukitafuta laini za TTCL kwa mawakala wanakuambia hamna. Ni kweli shirika likose laini ambazo kimsingi ndio mteja na ndio zitachochea...
  20. S

    Kwa kauli hizi nashawishika kuamini kuwa sijamuelewa Rais Samia kama ni Dikteta ama Mwanademokrasia

    Kuna mambo yanayothibitisha mkanganyiko ktk kumtafsiri rais Samia. Ukimsikiliza ktk hotuba zake na matamanio yake juu ya wapi anataka kuipeleka nchi yetu rais Samia anaonekana anapenda haki na utangamano. Ukianzia namna alivyorekebisha mtanziko wa kisiasa uliokuwepo kwa kuruhusu mikutano ya...
Back
Top Bottom