Tanesco na tenda kwa kampuni binafsi; TTCL na kampuni binafsi za simu kuanzishwa TCRA

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
TANESCO NA TENDA KWA KAMPUNI BINAFSI;TTCL NA KAMPUNI BINAFSI ZA SIMU KUANZISHWA TCRA.

Leo 12:15pm 03/05/2022

Tanesco wameazimia kuongeza ufanisi na kasi katika kuunganisha umeme kwa wateja,Tanesco itaanza kutoa tenda kwa kampuni binafsi kufanya kazi hiyo huku wao wakijikita kwenye uzalishaji na usambazaji,bila shaka italeta tija na kupunguza muda wa kusubiria,naamini patawekwa utaratibu wa kufuatilia kampuni hizi binafsi bila hivyo gharama za connection zitapanda. Lakini kuanzia nyaya, nguzo na vipuli vingine viwe na viwango,kama mteja akilalamika baada ya miezi michache kwamba mitambo haifanyi kazi vizuri mteja aweze kulalamika moja kwa moja Tanesco na kusiwe na visingizio kwamba haa sio sisi ni kampuni A, B,C tutapitia Ulinganisho wa TTCL na TANESCO.

Kama sijakosea wakati wa TTCL ilipokuwa peke yake hakukuwa na TCRA lakini baada ya kuruhusiwa makampuni binafsi ndipo ikaundwa regulatory authority (TCRA),hivyo hivyo kwenye eneo hilo naamini lazima kutaundwa regulatory authority ambayo hata shirika la umma litakuwa subjected,mlaji atakuwa huru kuchagua mtoa huduma atakaeridhishwa nae hivyo italazimisha watoa huduma kuboresha huduma zao ili waingie kwenye ushindani wa soko huku Wananchi wakifaidika,nadhani ni muhimu sana nafasi za utendaji wa kitaalamu kwenye mashirika ya umma ziwe za kuomba na ziwe za ushindani ili wapatikane watu sahihi na ikitokea underperformance wawajibike,

Kampuni ziko nyingi tuu,zipo kampuni zinazosambaza na kujenga substations za umeme? Standards za vipuri watapewa na supplier wa vifaa wanaweza kuwa Tanesco wenyewe au waka site kampuni ambako contractors wanatakiwa kununua hivyo vifaa na ni kampuni zile zile ambazo Tanesco walikuwa wananunua siku zote,Ukaguzi utafanyika kama unavyofanyika kila siku,mfano pale Yapi Merkez wanapojenga mitambo ya umeme nani wanakagua? Naamini watapewa timeline,lengo hapo hizo meter wanazofungia wateja na vifaa vingine vitanunuliwa na contractors wenyewe kwa specifications walizopewa na Tanesco tena wataambiwa sehemu za kununua,kazi yao ni kuunganisha wateja then wasubirie malipo kutoka Serikalini,inalipwa kulingana na idadi ya watu ukiowaunganisha,Changamoto ni kuunganisha wateja hewa Ili pesa iwe kubwa,hapa ndipo inatakiwa uadilifu maana bila hivyo watu watalipwa pesa za bure kama ilivyokuwaga kwenye bima ya Afya.

Hakuna haja ya kuogopa, ni kuweka utaratibu mzuri tuu na kuzuia loophole zote zinazoweza kuleta hayo matatizo, sio kitu kigumu kabisa ila ni swala la kutumia wataalam kutengeneza huo utaratibu bila siasa au longolongo,makampuni madogo madogo yapate kazi nayo, ila waweke standard nzuri ya kuzingatia ubora wa kazi na bila kuweka ugumu usio na maana yeyote kwa wanaotakiwa kufanya hizo kazi na insurance ni lazima kwa contractor yeyote maana itapunguza ulipuaji wa kazi na za viwango vya chini, contractor ukiharibu kazi bima yako inalipa na ukiendelea kuharibu kazi bima wanafuta insurance yako na kampuni imekufa maana hamna wa kukupa kazi kama huna insurance,

Kama gharama za kuunganishiwa zinapungua hapo sawa ila kama gharama ni hizi au zitapanda zaidi ya hizi kwa kweli sola ndo jibu sahihi kwa wanyonge sema kule kwenye biashara ya sola ukanjanja ni mwingi vifaa bei ghali na vingi sio imara,Majenerator nayo yamepanda bei,tunarudo kule kule ambako JPM alikuwa anatutoa kwa kutujengea Bwawa la Umeme la Rufiji ili umeme upatikane muda wote na ikiwezekana upungue bei,Kiukweli sijawahi kuona injinia wa TANESCO akihusika kwa namba yoyote ile katika kuunganisha umeme majumbani au hata viwanda vidogo,niliwahi kupigiwa simu na dereva wa gari ya Tanesco akiniambia anakuja kwangu kufanya survey,(Nimeunganishiwa umeme sehemu nyingi)
Wanaokuja site ni kijana mmoja aliyepitia VETA na wabeeba nguzo wenye matusi mengi na wanao omba hela kwa mteja kila wamalizapo kufunga mita.

-Muingiliano wa Kimaslahi (Conflict of interest) kati ya Tanesco na kampuni binafsi.

Nashauri tu hizi kazi zinahitaji utaalamu maalumu sasa kampuni zenye wataalamu wa umeme ziko wapi? Utaratibu gani wa ukaguzi, standard za material ni zipi, materials nani ana agiza kampuni au tanesco? kabla ya kukurupuka na kujitafutia njia za kupata pesa,nashauri viongozi wa Tanesco watoe mpangilio ambao unaeleweka,isije kuwa kampuni binafsi zitakuwa za watumishi wa TANESCO,vifaa visichukuliwe TANESCO na kutumika mtaani kama madaktari na maduka ya dawa,muda wa kazi za serikali ndiyo utakuwa muda wa kazi binafsi hii si sawa,kutakuwa na conflict of interest ya hatari,kuna loophole ya kuchota fedha inatengenezwa hapo.

Naamini contracts zitakuwa managed na professionals! Hao watakuwa wakaguzi kabla ya malipo kwa kandarasi kulipwa!! najua umuhimu wa kuwa na in-house expertise?? isijekuwa badala ya kulipia kuingiza Umeme laki 320,000 meter isijekupanda ikawa laki 375,000 ongezeko hilo likawa kuwalipa kampuni mpya,isijekuwa wakandarasi binafsi wakiisha pewa tenda hiyo ikaanza shida kufunga meter kuanza kuwazungusha wateja mara meter zimeisha mara upo kwenye foleni hadi wateja wa 27,000 waishe yote ili utoe pesa maana utakuwa huna pa kushitaki hapo ndipo,tutasaga meno,isije kuwa tenda wapewe watoto wa wakubwa au viongozi wa Serikali,hiyo itakuwa ni kulamba asali na kula masega.

Nimalizie kwa tafakuri ifuatayo;-Hebu tuchukue uzoefu kwenye TTCL na kuruhusiwa makampuni binafsi ya simu je huduma zilikuwaje ukilinganisha na wakati ilipokuwa TTCL peke yake?

-Je kwa zama hizi tunaweza kuepuka biashara za ushindani?

-Je biashara za ushindani zina faida au hasara kwa mlaji /mwananchi?

-Kuna tofauti kubwa kati ya TTCL NA TANESCO.

-Role in Our National Economy.

-Huwezi kuwa na Control ya Bidhaa ikiwa uzalishaji unaotegemea Nishati ya Umeme kama sio Reliable and Affordable

-Stigglers itafanya nishati ya umeme iwe Affordable and Reliable,

Niishauri Serikali yangu ya Tanzania bora iachwe miradi yoote lakini STIGGLERS GORGE,BWAWA LA UMEME LA RUFIJI,BWAWA LA UMEME LA JULIUS NYERERE likamilike, hili mkilifanya hata kama watanzania hatutashukuru,Inshaallah Serikali mkikutana na Mwalimu Nyerere atawaambia wanangu mmeniheshimisha,Rais John Pombe Magufuli aliyeanzisha ujenzi huo nae atakuwepo pembeni akitabasamu.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Mkuu Mpaka leo hujui EWURA kazi yake ni ipi? Kama TCRA inavyofanya kwenye Mawasiliano vile vile EWURA inafanya kwenye Umeme au LATRA kwenye Usafirishaji. So hakuna hajja ya kuwa na Taasisi simamizi iliyopo EWURA itapiga kazi kama kawa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom