Uongozi Shirika la Posta na TTCL mkiweka kando utendaji wa kimazoea Mtatoa huduma bora zaidi badala ya kero kwa maslahi ya Nchi yetu

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
19,760
35,205
Wakurugenzi wa haya mashirika mawili mnajidhalilisha sana na kudhalilisha nafasi mlizopewa pamoja na taaluma. Yaani mashirika yanafanya kazi kwa style ya kizamani mnoooooo.

Kuna wakati inabidi mjikagaue msome alama za nyakati, anagalieni basi japo wengine wa nchi nyingine wanaofanya mnayofanya nyie wanafanyaje hadi wanafanikiwa kukua na kuvuka mipaka?

Nyie watu wa posta mnakera kweli. Yaani posta leo ukituma barua ya kawaida ulaya unamaliza miezi 2 haijafika? Halafu mkiulizwa mnajibu kirahisi ati "ukitaka barua yako ifike haraka lipia elfu 80 upewe tarcking number"

Niwaulize kitu kimoja, kama mnajua bila tracking number barua hazifiki kwanini mnawaambia watu watume?

Hivi mnajua mnapoteza mapato kiasi gani kwa urasimu wenu usio na maana? Hizo ndege zinazosafirisha barua na parcel za dhl Sio hizohizo zinasafirisha parcel na barua zenu?

Huduma za posta ni Nero jamani. Jiongezeni japo kidogo basi, fanyeni research mjue wenzenu waliowekeza kwenye hiyo sector wanafanyaje halafu mu improve kidogo. Vinginevyo mumshauri Rais abinafsishe au afunge hayo mashirika tuwaachie wageni watupatie huduma.

Kuna wakati kuliko ukubali kuwa kiongozi wa shirika au taasisi inayoenda kukufia mkononi mwako ni heri kuiacha hiyo office ukafanya mambo mengine

Nimeandika kidogo tuu Wacha kuendelea kutunza swaumu yangu kwanza.

Hii kitu nadhani tatizo ni mfumo. Na mfumo wenyewe umesababishwa na matatizo yetu wenyewe. Nitatoa mfano mmoja hasa kuhusu TTCL. TTCL wanafunga Fibre na kwa bahati nzuri wateja tulijitokeza wengi lakini kila siku kutufungia fibre imekuwa ni wimbo.

Nilipouliza nikaambiwa kuwa tatizo ni machine ya kuchomelea walikuwa na mbili, moja imeharibika kwa hiyo wana moja tu. Wateja ni wengi zaidi ya 300. Lakini kuna wakati, zilipatikana machine mbili ambazo ni used kwa gharama ndogo almost 21% ya mpya lakini kikwazo kikawa ni 'Sheria za manunuzi haziruhusu kununua USED'.

Unaweza kudhani ni mpuuzi ambaye aliweka hii sheria, la hasha, hii sheria iliwekwa baada ya kujua watu wanapiga kupitia njia hii. Mfano ukarabati wa kivuko cha kigamboni.

Pamoja na kulaumu, ambayo ni haki yetu, ila tujilaumu kwa kutokuwa WAUNGWANA katika kila tulifanyalo. Wengi ubinafsi umetuzidi. Wizi imekuwa ni dili etc. Angalia jinsi ambavyo katika Daladala makonda wanavyohangaika kucheki tiketi, na mtu anajitahidi sana kukwepa kulipa, na akikwepa anajiona mjanja. Nenda ujerumani, hakuna konda katika mabasi yao ila kila mtu analipa. Kwao hata mtu akifanya maamuzi ya kununua kitu used hatapata shida kwa vile anajitahidi kufanikisha ila sie hapa, UPIGAJI. Kwa mtaji huu, TTCL haliwezi kushindana na makampuni ya binafsi, hata awekwe nani.

Pamoja na kulaumu, ambayo ni haki yetu, ila tujilaumu kwa kutokuwa WAUNGWANA katika kila tulifanyalo. Wengi ubinafsi umetuzidi. Wizi imekuwa ni dili etc. Angalia jinsi ambavyo katika Daladala makonda wanavyohangaika kucheki tiketi, na mtu anajitahidi sana kukwepa kulipa, na akikwepa anajiona mjanja.

Nenda ujerumani, hakuna konda katika mabasi yao ila kila mtu analipa. Kwao hata mtu akifanya maamuzi ya kununua kitu used hatapata shida kwa vile anajitahidi kufanikisha ila sie hapa, UPIGAJI. Kwa mtaji huu, TTCL haliwezi kushindana na makampuni ya binafsi, hata awekwe nani.

Ref njinjo🙏
 
Ifike mahala mheshimiwa rais avunje zile board zao na kufanya Management Restructuring
Haya mashirika yanatakiwa kusimamiwa na watu wenye akili ya biashara na huduma bora kwa wateja, sio watu wenye akili ya kupata mishahara huku shirika linadorora
Uozo kuanzia juu hadi chini. Nilienda hapo Ubungo Plaza TTCL kwa issue ya kuwekewa internet nyumbani. Aisee.
 
Mashirika mengi ya umma ni janga na mzigo kwa walipa kodi ndani ya nchi hii hakuna uwajibikaji na weledi zaidi kumejaa urasimu wa kijinga sana.

Ifikie hatua iwe mwiko kabisa kwa serikali kufanya biashara nakumbuka ripoti ya CAG prof. Assad ilibaini kuwa ndani ya miaka 5 bodi ya ATCL ilikuwa haina mtaalamu wa biashara ya anga sasa huu si uwendawazimu wa watawala wa kiafrika.

"Lipa kodi kwa maendeleo ya nchi"
 
Mfumo mzima wa uanzishwaji wa mashirika ya umma inatakiwa kufanyiwa marekebisho makubwa, watendaji hadi menejimenti

Na viongozi wanaotakiwa kufanya marekebisho wapo. Kuanzia bodi ya shirika hadi wakurugenzi ila wanahesabu siku za kupata mishahara tuu
 
Wengi wao akili za kizamani wakati dunia ime advance kiteknolojia, tatizo la viongozi wetu hawana exposure na kubebena siyo kuchagua mtu wenye uwezo.
Laiti tungekuwa tunatangaza kazi kuanzia mwenyekiti wa bodi hadi watendaji na sio kwa kuteuliwa labda mashirika yangebadilika
 
Ifike mahala mheshimiwa rais avunje zile board zao na kufanya Management Restructuring
Haya mashirika yanatakiwa kusimamiwa na watu wenye akili ya biashara na huduma bora kwa wateja, sio watu wenye akili ya kupata mishahara huku shirika linadorora
Wapewe wawekezaji ama wazungu Mana mweusi akishapa kahela kidogo kazi inayibakia Ni starehe kwake , michepuko Kama yote,wizi hawawazi kuumiza kichwa apate halali nadhani,atataka viwanja na nchi zote atembee. Sijawahi msikia Warren Buffet ametembelea mbuga za wanyama akaja afrika kuli refresh yupo zake na Berkshire and Hathaway yake. Kazi kusoma kurasa 500 per day, yaani hana Mambo mengi pamoja na kuwa tajiri wa tano duniani. Bado anaishi nyumba aliyoinunua mwaka 1959 kwa $31500 huko Nebraska, sijui ,gari aliyokuwa anatembelea Ni ya zamani mpaka binti yake akamaindi akamwambia baba badili hii gari unatuabisha Kama familia na utajiri wote huo so akamheshimu bintiye.

Sie blacks tukiwa na hela betting Kama Michael Jordan akaliwa hela hapa juzi na kijana wake akapoteza $50k kwa kubeti,utasikia Mayweather Floyd akamfanyia kijana wake bathidei ya 100M tzs ,Mara Tyson akanunua nyumba ya kuishi ya dola million kadhaa Mara akafilisika. Umemsikia Usain bolt naye alipigwa hela zake katika uwekezaji sijui hakuwa na maarifa ama wajanja wamemlia hela.

Yaani weusi Kuja kuendelea Ni kazi mno yanai mno. Huyo ceo hawazi tz iakawekeze hata huko Asia Kama benki ya postal ama hao ttcl tukawekeze huko mabara mengine. Yeye ameingia social networks akachati na mchepuko akapiga biti wafanyakazi Basi anasubiria kuendeshwa na v8 akae pale Serena naye avimbe Basi Hakuna jingine labda anawaza namna ya kumuachia mwanae icho kiti kama yoweeri anamuachia kijana wake kiti
 
Ukisema wapewe wawekezaji wazungu mimi nitasema anakosea sababu wapo weusi tena watanzania asilia wenye uwezo wa kufanya kazi vizuri mno

Na hapo shida sio uzungu au uafrika shida ni utendaji. Mtu anayepewa dhamana lazima afungwe na sheria zitakazompima na kumuwakilisha.

Wazungu tunafanya nao kazi tunawajua, hawana akili za ziada ila wamejengwa kwenye nidhamu ya utendaji na wana mifumo sahihi inayosimamiwa kwa umakini
 
Wengi wao akili za kizamani wakati dunia ime advance kiteknolojia, tatizo la viongozi wetu hawana exposure na kubebena siyo kuchagua mtu wenye uwezo.
Laiti tungekuwa tunatangaza kazi kuanzia mwenyekiti wa bodi hadi watendaji na sio kwa kuteuliwa labda mashirika yangebadilika

Tutafika huko siku moja
 
Haya Mashirika yanafanya kazi kwa mazoea, wangekuwa serious yangekuwa ni mashirika yanayoingiza fedha nyingi sana kwa kuwa tayari yana wateja wengi.

Ukiangalia miaka ya JPM iliamuliwa (indirectly) kila kiongozi wa Umma lazima awe na SimCard ya TTCL kwahiyo tayari wateja wanao ni kuboresha huduma zao tu kuvutia wengine zaidi.

Hao wa Posta ikiamuliwa kila barua za Maombi ya kazi pale Utumishi zitumwe kwanjia ya Posta ina maanisha wangepata Mapato kuliko sasa. Ni suala la kuboresha huduma kwa kuangalia mrejesho wa wateja wao wanavyo recommend baada ya kupokea huduma zao.
 
Ifike mahala mheshimiwa rais avunje zile board zao na kufanya Management Restructuring
Haya mashirika yanatakiwa kusimamiwa na watu wenye akili ya biashara na huduma bora kwa wateja, sio watu wenye akili ya kupata mishahara huku shirika linadorora
Hii kitu nadhani tatizo ni mfumo. Na mfumo wenyewe umesababishwa na matatizo yetu wenyewe. Nitatoa mfano mmoja hasa kuhusu TTCL (maana mama D yeye kasemea posta tu ingawa kichwa cha habari ni pamoja na TTCL). TTCL wanafunga Fibre na kwa bahati nzuri wateja tulijitokeza wengi lakini kila siku kutufungia fibre imekuwa ni wimbo.

Nilipouliza nikaambiwa kuwa tatizo ni machine ya kuchomelea walikuwa na mbili, moja imeharibika kwa hiyo wana moja tu. Wateja ni wengi zaidi ya 300. Lakini kuna wakati, zilipatikana machine mbili ambazo ni used kwa gharama ndogo almost 21% ya mpya lakini kikwazo kikawa ni 'Sheria za manunuzi haziruhusu kununua USED'.

Unaweza kudhani ni mpuuzi ambaye aliweka hii sheria, la hasha, hii sheria iliwekwa baada ya kujua watu wanapiga kupitia njia hii. Mfano ukarabati wa kivuko cha kigamboni.

Pamoja na kulaumu, ambayo ni haki yetu, ila tujilaumu kwa kutokuwa WAUNGWANA katika kila tulifanyalo. Wengi ubinafsi umetuzidi. Wizi imekuwa ni dili etc. Angalia jinsi ambavyo katika Daladala makonda wanavyohangaika kucheki tiketi, na mtu anajitahidi sana kukwepa kulipa, na akikwepa anajiona mjanja. Nenda ujerumani, hakuna konda katika mabasi yao ila kila mtu analipa. Kwao hata mtu akifanya maamuzi ya kununua kitu used hatapata shida kwa vile anajitahidi kufanikisha ila sie hapa, UPIGAJI. Kwa mtaji huu, TTCL haliwezi kushindana na makampuni ya binafsi, hata awekwe nani.
 
Hii kitu nadhani tatizo ni mfumo. Na mfumo wenyewe umesababishwa na matatizo yetu wenyewe. Nitatoa mfano mmoja hasa kuhusu TTCL (maana mama D yeye kasemea posta tu ingawa kichwa cha habari ni pamoja na TTCL). TTCL wanafunga Fibre na kwa bahati nzuri wateja tulijitokeza wengi lakini kila siku kutufungia fibre imekuwa ni wimbo.

Nilipouliza nikaambiwa kuwa tatizo ni machine ya kuchomelea walikuwa na mbili, moja imeharibika kwa hiyo wana moja tu. Wateja ni wengi zaidi ya 300. Lakini kuna wakati, zilipatikana machine mbili ambazo ni used kwa gharama ndogo almost 21% ya mpya lakini kikwazo kikawa ni 'Sheria za manunuzi haziruhusu kununua USED'.

Unaweza kudhani ni mpuuzi ambaye aliweka hii sheria, la hasha, hii sheria iliwekwa baada ya kujua watu wanapiga kupitia njia hii. Mfano ukarabati wa kivuko cha kigamboni.

Pamoja na kulaumu, ambayo ni haki yetu, ila tujilaumu kwa kutokuwa WAUNGWANA katika kila tulifanyalo. Wengi ubinafsi umetuzidi. Wizi imekuwa ni dili etc. Angalia jinsi ambavyo katika Daladala makonda wanavyohangaika kucheki tiketi, na mtu anajitahidi sana kukwepa kulipa, na akikwepa anajiona mjanja. Nenda ujerumani, hakuna konda katika mabasi yao ila kila mtu analipa. Kwao hata mtu akifanya maamuzi ya kununua kitu used hatapata shida kwa vile anajitahidi kufanikisha ila sie hapa, UPIGAJI. Kwa mtaji huu, TTCL haliwezi kushindana na makampuni ya binafsi, hata awekwe nani.

Mchango mzuri mkuu
Nilichoka na swaumu
 
Wakurugenzi wa haya mashirika mawili mnajidhalilisha sana na kudhalilisha nafasi mlizopewa pamoja na taaluma. Yaani mashirika yanafanya kazi kwa style ya kizamani mnoooooo.

Kuna wakati inabidi mjikagaue msome alama za nyakati, anagalieni basi japo wengine wa nchi nyingine wanaofanya mnayofanya nyie wanafanyaje hadi wanafanikiwa kukua na kuvuka mipaka?

Nyie watu wa posta mnakera kweli
Yaani posta leo ukituma barua ya kawaida ulaya unamaliza miezi 2 haijafika? Halafu mkiulizwa mnajibu kirahisi ati "ukitaka barua yako ifike haraka lipia elfu 80 upewe tarcking number"

Niwaulize kitu kimoja, kama mnajua bila tracking number barua hazifiki kwanini mnawaambia watu watume?

Hivi mnajua mnapoteza mapato kiasi gani kwa urasimu wenu usio na maana? Hizo ndege zinazosafirisha barua na parcel za dhl Sio hizohizo zinasafirisha parcel na barua zenu?

Huduma za posta ni Nero jamani.

Jiongezeni japo kidogo basi, fanyeni research mjue wenzenu waliowekeza kwenye hiyo sector wanafanyaje halafu mu improve kidogo. Vinginevyo mumshauri Rais abinafsishe au afunge hayo mashirika tuwaachie wageni watupatie huduma.

Kuna wakati kuliko ukubali kuwa kiongozi wa shirika au taasisi inayoenda kukufia mkononi mwako ni heri kuiacha hiyo office ukafanya mambo mengine

Nimeandika kidogo tuu Wacha kuendelea kutunza swaumu yangu kwanza.
Shukrani sana kwa andiko zuri! Hakika haya ni mashirika hovyo kuwahi kutokea.

Mimi mwezi huu nimetumiwa EMS kutoka Dodoma kuja Sumbawanga, imechukua siku 8 kuipata! Mbaya zaidi hata jiografia ya nchi hii hawaijui, badala ya kuileta Sumbawanga wanapeleka Mpanda! Kutoka Mpanda kuja Sumbawanga imechukua siku 5, kilomita 240! Just imagine!

Hawa TTCL nao ni kituko kingine! Mtandao wao ni udhaifu mno! Kazi ya dakika 3 itakuchukua nusu saa nzima. Hopeless kabisa!
 
Back
Top Bottom