Naibu Spika Tulia Ackson athibitisha Mbunge mmoja kupata maambukizi ya COVID-19

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
559
1,000
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amesema kuwa mmoja wa Wabunge wa Bunge hilo amethibitika kuwa ana maambukizi ya Virusi vya Corona.

Amesema mbunge huyo anaendelea vizuri na Serikali inaendelea kumuangalia na kumpatia matibabu stahiki. Kwa mujibu wa maelezo ya mbunge huyo ni kwamba alisafiri kwenda Dar es Salaam siku za karibuni, na aliporejea Bungeni siku ya Jumatano alianza kujisikia dalili kama zilizotangazwa na wataalamu kuhusu Virusi vya Corona na baadaye alithibitishwa kupata maambukizi ya Corona.

bungelatanzania.png
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom