Spika Tulia: Wabunge hawasemi uongo, Ripoti ya CAG inaonesha kuna ubadhirifu

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson amesema kutokana na mjadala wa Wabunge kuonesha Halmashauri nyingi zina Ubadhirifu mkubwa, anapata wakati mgumu kusikia kauli za Mawaziri wakisema Wabunge wanasema uongo wakati taarifa za Kamati zinaonesha kuna ubadhirifu katika Halmashauri hizo.

Akitolea ufafanuzi kauli ya Waziri wa Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo aliyedai baadhi ya Wabunge wanasema uongo kwasababu Halmashauri nyingi zimepata Hati Safi, Spika Tulia ametolea mfano Halmashauri ya Bunda ambayo imetajwa katika maeneo 70 tofauti ya Ubadhirifu katika Ripoti ya CAG.

Dkt. Tulia amesema "Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ina Hati inayoridhisha lakini imehusishwa katika kuzima Mfumo wa POS na Wizi wa Saruji hivyo katika mazingira hayo inaniwia vigumu kusema Mbunge amesema uongo kwasababu taarifa inaonesha hali hiyo"
 
Kuanzia serikali kuu hadi serikali za mitaa kuna wizi na ubadhirifu wa hali ya juu. Hapo najua kuna kafara inaandaliwa, mmoja atafungwa kengele na kutupwa kwenye shimo refu ili yao yaendelee.
 
Back
Top Bottom