Nahitaji mwenza

Niko serious sana wala sio kidogo, unaposema wote, wote wa wapi, mimi sipo kote mkuu.

Nipo hapa nilipo ambapo hawapo hao.
Inshallah nitakaribia Tanga.
 
Mara nyingi mwanaume wa hivi ana low self esteem.
Mfilisiti hakuna jinai kwa hiki ninachokifanya hapa, kwa namna maelezo yako yalivyo ni wazi umekwazika pasi na sababu ya msingi.

Mwanamke mwenye sifa hizo atakuja pm na bila shaka tutafika tutakapo.

Kwa pamoja mimi na wewe ndgu Mfilisiti tuseme Inshallah.
 
Tembea uone jinsi watu walivyo bize na kazi mpaka wanaishia kutafuta wenza kwenye social media na wanawapata, tatizo lenu ushamba🚮
Jamaa anadhani jinsi anavyoishi yeye basi Tz nzima tunaishi hivyohivyo.
Badili mindset mkuu, sio wote tupo kama wewe, tunaishi kama wewe uishivyo, una ndgu kijijini na wajomba mjini.

Una majirani utitiri na marafiki kisado, badili hiyo kitu, na ukipunguza ego utajifunza mengi.
 
Dahh mkuu huyu mtoto kabisa napeleka wapi mimi, nina watoto watano, wengine wamefika chuo, katakimbia haka😅

Shem Seran . 🤣🤣🤣
Huyu inabidi umpate ili umfundishe mapenzi.

Ila atapata hitaji la moyo wake.

Alaf kigezo ni kimoja tu.
Kutokuwa na mtoto.
Jamaa amenyooka.
Kama yuko serious kweli. Basi namshaur aongeze vigezo.
 
Sio domo zege, maeneo tunayoshinda na ninaokutana nao tunatofautiana mitazamo.
Sawa, achana na mambo ya udomo zege ila washirikishe wazee/familia yako kuhusu hilo wape sifa unazohitaji wataletwa kama wote, haya mambo ya mitandaoni ndio maana malalamiko kwa vijana ni mengi, watu mnabebana bebana tu bila kujua backgrounds za koo zenu.
 
Asante kwa ushauri wako, zama zimebadilika, zamani mtu mpaka anafika umri wa kuoa/kuolewa bado anaishi nyumbani ila sasa mtoto akifika umri fulani anaanza kucheza na shule na/au utafutaji mpaka umri wa kuoa au kuolewa, hivyo jamii yake inakua haimjui kama anavyojifahamu yeye.

Kuna uzi wako pia ukitafuta mwanaume humu na sio kwa ndgu zako, bila shaka unafahamu kua kila mmoja ana sababu zake za kufanya hivyo kama ulivyokua nazo.
 
Nilitafuta sperm donar sio mwanaume wa kunioa ningetaka mwanaume wa kunioa ningewashirikisha wazee wangu, nisingekuja mtandaoni lakini hayo yalikua maoni yangu unaweza kuendelea kuchakura chakura huenda ukajipatia fupa lako ukawa unaliramba ramba, lol✌️
 
Halafu ukimpata huyo mwenza wako asiye na mtoto, na bahati mbaya mmoja wenu kati yako au yeye akawa ni tasa! Utakuja kutupatia mrejesho?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…