Mrejesho wa kutafuta mwenza HIV+mwaka 2022

Mrejesho wa kutafuta mwenza HIV+mwaka 2022

Zagiara

Member
Joined
Sep 14, 2022
Posts
24
Reaction score
186
Habari ya siku ya leo wana Jamvi natumai wote ni wazima wa afya..kwa upande wangu sipo vizuri sanaa nipo kitandani siku ya 3 sasa afya kidgo changamoto,katika haya maisha ukiwa na afya njema basi wewe ni Tajiri sana hivyo tujifunze kushukuru,basi twende moja kwa moja kwenye lengo..mwaka 2021 na 2022 mm nilikuja kwenu nikiwa kama binti ambaye nilikuwa naitaji mwenza anaendana na afya yangu ili tulisukume gurudumu la maisha haya yenye mtihani mkubwa pamoja kwani kijana wenu tayari ni HIV+,basi bwana nikaleta ombi langu na bila hiyana wana jamvi mkaitika,nashukuru nikapata pm za kutosha kila mmja kwa upande wake,kwa walio chat tulichat,kwa walionana tulionana,kwa walio nitusi na kunivunja moyo hawakukosekana basi irimradi lengo litimie....mnamo tar 18 ya mwaka 2022 Mungu ni mkubwa nikakutana na kijana ambaye naweza kusema alikamata attention yangu kwa kiasi kikubwa kwa sababu kidg alionekana alikuwa seriously na hili swala sana..Tumuite Mr G,basi bwana tukaanza kuchat kwa muda kidg kabla ya kuonana coz alikuwa mkoani,kama miezi 6 ivi akafanikiwa kuja dar tukaendelea kuchat,tukaja tukapotezana Kisha tukatafutana tena coz kijana huyu kidg alikuwa na changamoto ya ajira,Mungu mkubwa akapata ajira akaja rasmi dar es salaam basi tukaamua kuonana baada ya kuwa tunawasiliana kwa muda wa mwaka.Yaani cku namuona uwezi amini nilizama mzima mzima palepale na mpaka leo ile siku naiona kama miujiza,na nikaapa kwa mungu wangu nitatoa shukran kwa zawadi aliyonipa,basi siku ile ilikuwa fupi sana maana nilikuwa natamani masaa yasimame,tuliongea tukafamiana vizuri,tulielezana yaliyotusibu,tulipeana pole,tulipongezana na tulishukuru kwa kila kitu na mipango tukaipanga na ilikuwa ni tar 1 ya mwezi wa sita...Inaendelea.... Nimerejea nilienda kupata sindano yangu ya 3 na kidogo naona nuru inarudi machoni na nguvu mwilini,unajua hakuna kipindi ambacho mtu anatamani asiwe mwenyewe kama kipindi cha maradhi hichi ni kipindi kigumu sana especially kwa sisi ambao familia zipo mikoani..basi bwana MrG kwa kipindi tunakutana alikuwa anahisi kama vile amechelewa katika maisha coz alikuta mm Nina kazi tayari Nina sehemu yangu naishi na yeye ni mwanaume ana aliosoma nao ambao walikuwa tayar wamemwacha nyuma so kidogo alikuwa kama ana pressure ya maisha,angalau apate cha kurudishia wazazi nyumban,so mimi nilimwambia tu avumilie kwani katika haya maisha kutangulia si kufika muda wake utafika tu, na uwezi kuamini nilikuwa naona kabisa atafika sehemu ambayo hatoamini kama atafika..Alikuwa ni mkaka flani ivi ata ukikaa nae unajiona mjinga..yuko very focused anajua nn anafanya,afanye vipi na kwa muda gani ili apate nini,I was so luck to have him by my side [nimeona niingize kudhungu ili mnipate zaidi]basi penzi likaanzia pale,tukapendana,tukashauriana,tukaliwazana dah unajua sio kwamba mwanamke awezi kuwa mwenyewe na maisha yakaenda hapana mahusiano yanakupa confidence Flani hivi unahisi kwamba ni sawa nikiwa Sina watu mia upande wangu lakini Nina mmja wa maana anatosha,na katika swala la sex watu wengi najua mtakuwa mnajiuliza ilikuwaje kwanza tulihakikisha tunafuatilia dawa vizuri na tunajali afya zetu zaidi na kwa upande wangu nilifurahi maana kitambo kupata chakula cha kimwili ambacho kiliukosha moyo wangu na kutibu vidonda vyangu vya mahusiano yaliyoniumiza sana nyuma na katika akili yangu nikaanza kuifikiria ndoa..kila sekunde katika haya mahusiano yakikuwa na maana kubwa sana kwangu,sikutaka hata kupoteza muda kwa kuwaza kuwa napaswa nisifurahie mahusiano yangu.Baada ya muda na mimi nikaweka wazi kwa ndugu,jamaa na marafiki na walinipongeza,nikaanza kuchangia mada za mahusiano ambazo nilikuwa nakaa kimya mwanzo nisijue cha kusema,nikajiamini mara mbili,nikanawiri na kupendeza kila mtu alinishangaa,Nikamshukuru mungu na kujitahidi kutoa Sadaka angalau nionyeshe ni jinsi gani nilishukuru na pia nikaweka Malengo yangu nifanye kazi kwa bidii ni save kwa ajili ya future yetu .Basi bwana mwenzangu akaanza kazi yake ,akaanza kusave visenti aweze kujitegemea maana alikuwa amefikia kwa kaka yake so alikuwa anahitaji kujipanga aweze kujitegemea,Mambo yalikuwa vizuri kwa kweli..mara paaah mwaka ukakata,tukasherekea sikukuu pamoja yaani ni neema tu...mara gafla akapata uhamisho ofisi kwao wa kwenda kituo kingine cha kazi mkoa mwingine kdg sio mbali sana hapa dar na hapo sasa ndio mapicha yalipoanzia.....naomba nipate japo supu jamani .....Itandelea...Basi mwaka huo anahama na mimi nikapata mtihani wa kuondokewa na baba yangu mzazi kilikuwa ni kipindi kigumu sana kwangu,nikatamani japo ningemuona tu angalau nipate faraja nilikuwa Nina ruhusa kazini hivyo kabla ya kusafiri kwenda kuzika nikaamua nimpitie maana ni njia moja,uwezi kuamini hakutokea ikabidi nilale lodge mwenyewe na vilio kama vyote..kulipokucha nikaenda kuzika,lakini kuanzia pale nikaona vi red flag watoto wa mjini wanaviita ila nikapuuzia nikaona labda ni ubize wa kazi maana kazi yake ngumu kidg.Msiba ukaisha ikabidi nirudi dar na majukumu yaendelee,mawasiliano yakaendelea mm na yy akanipa pole na blah blah nyingine maisha yakasonga,mara gafla nikawa simpti kwenye cm,kama mwezi mmja hivi nakumbuka alipotea gafla kwenye cm nilikuwa Nina wasiwasi kwelikweli, na ,sikujua nn kimemkuta nika akikaa sawa atanitafuta,kweli baada ya mwezi kuisha akanitafuta akasema sorry kazini tulisimamishwa na akaamua aende kwanza kwao akapumzike,mimi tena sikua na hiyana nikampokea nikamuuliza mpango wako nn akasema kuna kazi nyingine nasikilizia basi kweli miezi 2 hivi akapata kazi nyingine tena kampuni kubwa tu kuliko ile ya kwanza,tukashukuru mungu kwa ajili yake na maisha yakaendelea,Akafanya kazi kwa bidii akaanza kununua vitu vya ndani taratibu mwisho akafanikiwa kuanza maisha yake rasmi.Akapata nyumba nzuri maisha yakaanzia hapo,tukawa tunatembeleana hivyo mambo ya mahusiano tena...Mwaka ukapita tena,mara gafla mawasiliano yakapungua,simpati tena kwenye simu kwa muda mwingi,mara yuko busy kuniona,akablock no zangu zote na social media,nilikuwa na nguo zangu kwake nikifanikiwa kwenda nakuta kazitupa basi tafrani,kuna cku nakumbuka nimeenda kwake ucku nimetoka kazn nimekaa getini zaidi ya masaa mawili bila kifunguliwa,na asubuh kukikucha ananitimua kama mbwa anataka afunge mlango wake hata kama Sina shift asubuh inabidi nitoke tu na hapo akija kwangu namwachia funguo atoke muda atakao,mambo yakawa mengiii mara akasahau tar zangu zote muhimu ambazo mwanzo alikuwa nazo makini mf siku yangu ya kuzaliwa,valentine,vifo vya wazazi wangu nk...akaanza ahadi za uongo,anaweza kukwambia tunaenda kwenye harusi ya mfanyakazi mwenzangu wiki hii,nikaanza kutafuta gauni na kila kitu alafu ikifika hiyo cku kimya,izo diner dates za hewa sasa nahisi zinafika milioni...yaani kiufupi nikachoka nikaona kabisa hapa Sina changu tena masiki mm nishakutana tena na zimwi mla nyama...basi D day ikafika siku nimeamka najisikia kizunguzungu nikaenda hosp wakasema presha yangu iko juu nikapewa dawa na nikaambia niwe na mtu ambaye atanisaidia vitu vidg nikae nipumzike,basi nikawasiliana nae akanambia siko hiyo atakuwa nyumbn hatotoka nikaona niende ila sikumwambia km naenda..ile nafika mlangoni kwake kabadilika ananiambia kwanini hujasema kama unakuja nikapotezea nikaingia,nikamwambia vipi kwani una mtu unamwogopa akasema ndio,hapo nikaganda kwanza nikawa naprocess mara simu ikaaingia nikamsika anaongea vizuri kwa mahaba kuliko hata anavyoongea na mm tena na kuomba misamaha mingiii nikamuuliza mbona siwezi kukupigia kabisa nikajua simu yako inashida kumbe upo hewani akajibu kwasababu nimekublock..nikashtuka kwanza nikamuuliza kwann?hajajibu[kuna siku nilizidiwa nikadondoka kazini sasa akawa anapigiwa ili aje anichukue,sijawah kupata aibu katika maisha yangu km cku ile no zangu zote haziiti,hadi cm ya ofisi ambayo uwa natumiaga kumpigia mara moja moja nayo haiiti,Haiti, mfanyakazi mwenzangu kampigia kwa no yake...kumbe nikajua cku ile niliblokiwa...siku ile alivyokuja kunichua kanifukisha nyumban kwangu kanibwaga kaondoka bila hata kuaga..niko hoi hata kijiko cwez kushika] nikasema hapa nimekwishaa,alivyomaliza nikasogea kusoma caller juu ya kioo imeseviwa wife nikamuuliza ww ni mume wa mtu akanambia ndio,nikamwambia tangu lini?kabla au baada?akasema sio kazi yako kujua...nikamwambia kwann hujanambia akasema ningekwambia usingeelewa..nikamuuliza alikuwa wapi kipindi kile hata nauli ya kazn huna.mm nakopa kazini ili ww upate nauli?akanyamaza..nikaingia bafuni nikakuta mswaki wangu umebadilishwa nikaingia Kabatini nguo zangu hamna...nikamuuliza imekuwaje akasema nguo nimeziweka kwenye taka,kwann,sitaki mke wangu azione,ni mkavu hapepesi macho..Nikasema inetokea tena Sina jinsi I have to let go,,basi nikachukua pochi yangu na kizunguzungu changu nikaondoka ndani ya ile nyumba.....imenichuka muda kupona tena,nikapata mpka sonona,nikaona maisha hayana maana,nikaona Dunia ya mapenzi haipo na mm, nikaona Sina bahati,sasa nimepona baada ya miezi 3 nimekuja hapa nilipompata nimekuja kumwambia Mr G nilikupenda sana mpka nilianza kuplan future na ww,ckutaka vitu vikubwa kutoka kwako zaidi ya upendi kama ni pesa tungetafuta pamoja nilichotaka ni kampani yako katika maisha yangu...siwezi kusema nimefanya makosa kukutana na ww hapana ila najilaumu kwa kuendea kupalilia penzi ambalo lilishakufa...nimeacha uende,na usifanye ichi kitu kwa mwanamke mwingine...sio kizuri ...kuwa na hofu na mungu na uache kuumiza waliomia tayari na kuwasababishia vidonda visivyo pona,,nimekubali haukuwa riziki yangu ,lakn katika miaka 3 tuliyokuwa pamoja nimejifunza kitu kujipenda mimi kwanza,nijiweke mm badala ya kila kitu,na ni sawa kwa mwanamke kuwa bila mahusiano mpaka muda sahihi,na pia tuache vidonda vipone...na mwisho tuwe na Shukurani.....kwa wadada wenye hali kama yangu msikate tamaa kuna walio na stori nzuri zaidi ya yakw angu,mwenza anapatikana popote kikubwa ni kuamini pia kuna kitu nimejifunza sio kwasababu wewe + upate + mwenzio ndio atakupenda hapana...upendo unaanza kwanza Kisha afya inakuja baadae...hata -anaweza kuwa na wewe kubwa na kuamini na kuwa muwazi ili mjue jinsi gani mtaishi na kuendelea kujipenda wewe zaidi... sasa na mimi nasikiliza nyimbo za mapenzi bila kulia my favorite kwa sasa ni [die with a smile] natumai ipo siku nitaleta stori nzuri ....Asanteni sana na muwe na siku njema....mm Sina mahusiano tena na kwa muda huu sidhani kama nayahitaji. Nahitaji kujipa nafasi mm kwanza. Na kusubiri muujiza wa mungu....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom