Nafikiria kuhama Catholic

Nafikiria kuhama Catholic

Pole sana. Mimi mwenyewe nna changamoto na Kanisa katoliki ambayo ni Asili ya wazazi wangu ila sio kwa sadaka. Mimi Yale masanamu na mapicha ya Yesu na Maria huwa yananikwaza sana.
Kwa ushauri wangu Bora ubaki katoliki ila uwe na itikadi zako za kutokufuata baadhi ya mambo yao. Maana hakuna dhehebu hata moja la kikristo lililokamilika 100%. Nimebahatika kusali madhehebu yote ya kikristo na nkakuta Yana mapungufu mengi sana.
Uislam upo smart sema niliona haunifai kutokana na sera zao na mafundisho waliopewa na mtume wao hasa kuchukia wasio waislam,kuuwa wasio waislam and some other complications.
Mimi binafsi nimeamua nibaki katoliki ila kuna mambo sitoyafuata mpaka naingia kaburini ambapo mojawapo ni kuamini au kuheshimu sanamu yeyote ile.

Mungu yupo kila mahali. Usinikwoti, sawa mpinga Kristo?
Munguhayupo kila mahali?
Mungu yupo kwenye neno lake na ahadi zake.

Huwezi kumpeleka mungu kwenye uchafu. Ukasema yupo kila mahali.
Kamwe hayupo katoliki, na hajawahi.
Na si katoliki tuu.
Sehem yoyote ambayo watu wamejiwekea taratibu za ibada nje ya neno la mungu. Nje ya utaratibh Mungu alioweka kuabudiwa.
 
Mungu alichagua mahali pakuabudiwa na namna yakuabudiwa.
Nje ya apo woote wafanyao wanajifurahisha kwenge ushetani.
 
Hakuna kanisa ambalo halina michango.
Pia, sadaka unamtolea Mungu,hautoi kwa Mtu..zikienda kutumika vibaya ni juu yao na Mungu uliyempa hizo sadaka.

Thamani yako anaijua Yesu na MUNGU aonaye sirini atakupa thawabu
Usipende sana kuwa acknowledged na watu..Mungu mwenyewe akishaipokea sadaka yako inatosha.

Hakuna kanisa ambalo viongozi wake wote wamenyooka 100%
Kwahiyo hata ukienda kwingine, bado utapata tu disappointment..kusubiri kuthaminiwa na watu kwa sababu umejitoa,,utachelewa.
Nakazia hapa
Kote ni hivihivi me ata simshauri kuhama abaki tu na dhehebu lake
 
Umri wako ni muhimu kwa kupewa ushauri.
Maana hapo ndipo mzizi wa tatizo.
Tatizo halipo nje. Lipo kwako
 
Hi,
Happy New Year.

Binafsi nimekua mzito kushiriki ibada ya jumuiya, Misa za kanisani au mambo yoyote yahusuyo kanisa katoliki. Sijawahi kuwaza hivi toka nikiwa najielewa but now things are dreadful to me, nilikua naioenda sana hii imani and proud ila kwa sasa naona napoteza muda wangu.

Mkesha xmass nilienda kanisani ila ikabidi nikae nje tu mpaka ibada ilipoisha...never happened before. But niliona naenda poteza muda tu.

Why???
👉 Katoliki halimthamini mtu mwenye roho wa Mungu na mwenye Upako ndani yake, Ila yule anayetoa michango

👉Halithamini sadaka zako unazoto kwa yatima,wagonjwa,wazee, na wenye njaa..ila tu ILE MICHANGO UNAYOCHANGIA KANISANI
👉 Halithamini kujitoa kwako juu ya kanisa ila tu kwa PESA UNAZOTOA KANISANI.

👉Pesa tunazochanga zinaenda kuhusumia wanawake zao na watoto wao waliowapata nje ya utaratibu wao.

HIVYO.....
Yule anayetoa pesa kanisani na kua na ukaribu na viongoz wa kanisa, Mapadri nk ndio mwenye thamani zaidi.

Naomba mnipe mawazo chanya niweze kurudi relini aisee.... Mawazo ya kuhama yamenijaa ila sijui niende wapi ambapo THEY DON'T CARE ABOUT MATERIAL BUT SPIRITUAL AWAKENING

NB. Catholic sio mbaya ila wanao liongoza ndio shida.

Kweli there's a price to pay when you know a lot of things you weren't supposed to know
✖️
Jana nilikuona na wale wenzako wavaa madela pale ubalozi wa vatican...vipi ushahama ama badobado
 
Nilidhani unahama kwa mkanganyiko wa imani kumbe ni matoleo.

Mkuu sababu unataka ukiona wagonjwa na kusaidia yatima kanisa likutambue kwa namna gani yani??
Sio kwamba unafanya hayo kwa ajili ya nafsi yako??

Mimi nikienda kanisana michango ambayo siielewi huwa sitoi nakaa zangu tu, hujalazimishwa kufanya hayo.

Huko kwenye jumuia ndogondogo ndo wana michango balaa na mi huko wala sipo kabisa.

Ila kwa ninachoona unachokikimbia RC huko uendako utakutana nacho tena na tena.
Tena huko ndiko balaa kabisa kuna sadaka za kujimaliza! Mara sadaka inayouma kama zuzu vile!
 
Umri wako ni muhimu kwa kupewa ushauri.
Maana hapo ndipo mzizi wa tatizo.
Tatizo halipo nje. Lipo kwako
Kwanini umri wake ni muhimu kupewa ushauri??

Nje ya mada, Mtibeli mbona nyumba yako ipo juu juu sana, huko ulipojenga kunajaa maji au ni ghorofa?? Ina malumalu kila pahala, kwanini??
 
Nilidhani ungemshauri amuelekee kristo.
Enyi wa romani.
Ni lini mtapata akili.
Shida yake haipo huko unakoielekeza, hana tatizo la kiimani bali michango..

Umemfahamu mleta uzi leo?? Sina shaka na kummjua kwake Kristo.

Ewe usie mromani punguza ujuaji.
 
Muda wa magugu kujitenga na ngano umefika
 
Hi,
Happy New Year.

Binafsi nimekua mzito kushiriki ibada ya jumuiya, Misa za kanisani au mambo yoyote yahusuyo kanisa katoliki. Sijawahi kuwaza hivi toka nikiwa najielewa but now things are dreadful to me, nilikua naioenda sana hii imani and proud ila kwa sasa naona napoteza muda wangu.

Mkesha xmass nilienda kanisani ila ikabidi nikae nje tu mpaka ibada ilipoisha...never happened before. But niliona naenda poteza muda tu.

Why???
👉 Katoliki halimthamini mtu mwenye roho wa Mungu na mwenye Upako ndani yake, Ila yule anayetoa michango

👉Halithamini sadaka zako unazoto kwa yatima,wagonjwa,wazee, na wenye njaa..ila tu ILE MICHANGO UNAYOCHANGIA KANISANI
👉 Halithamini kujitoa kwako juu ya kanisa ila tu kwa PESA UNAZOTOA KANISANI.

👉Pesa tunazochanga zinaenda kuhusumia wanawake zao na watoto wao waliowapata nje ya utaratibu wao.

HIVYO.....
Yule anayetoa pesa kanisani na kua na ukaribu na viongoz wa kanisa, Mapadri nk ndio mwenye thamani zaidi.

Naomba mnipe mawazo chanya niweze kurudi relini aisee.... Mawazo ya kuhama yamenijaa ila sijui niende wapi ambapo THEY DON'T CARE ABOUT MATERIAL BUT SPIRITUAL AWAKENING

NB. Catholic sio mbaya ila wanao liongoza ndio shida.

Kweli there's a price to pay when you know a lot of things you weren't supposed to know
✖️
Tena hamia burundi itapendeza.
 
Shida yake haipo huko unakoielekeza, hana tatizo la kiimani bali michango..

Umemfahamu mleta uzi leo?? Sina shaka na kummjua kwake Kristo.

Ewe usie mromani punguza ujuaji.
Ni heri uwe mkristo.
Japo mmechagua kuwa madhehebu

Tatizo halijaanza kwenye michango. Michango ni matokeo ya mfumo uliooza
 
Basi ww ni mwabudu sanamu.

Ezekieli 33:8-9
[8]Nimwambiapo mtu mbaya, Ewe mtu mbaya, hakika utakufa, nawe husemi neno la kumwonya mtu huyo, aiache njia yake, mtu mbaya huyo atakufa katika uovu wake, lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako.

[9]Walakini ukimwonya mtu mbaya kwa sababu ya njia yake, kusudi aiache; wala yeye asiiache; atakufa huyo katika uovu wake, lakini wewe umejiokoa roho yako .
 
Hujui maana ya kuabudu sanamu
 
Back
Top Bottom