Wakatoliki wapo matatizoni

Jackwillpower

JF-Expert Member
Oct 4, 2017
2,301
3,414
Wakatoliki, kwa sakata hili, je! mtaendelea kutoa uaminifu (royalty) wenu kwa Papa [papacy] au kwa Maandiko Matakatifu?

Kupitia kauli za papa Francis juu ya kuwabariki wapenzi wa jinsia moja kumezua utata kwa viongozi wa kanisa na waumini na dunia kwa ujumla. Maana Papa ni mtu mkubwa sana duniani, hivyo kauli yake inapokelewa kwa uzito mkubwa sana.

Kwa kweli kauli yake imeleta mgawanyiko (schism) katika Kanisa Katoliki na kuupa ulimwengu wa dini mshangao.

Lakini mashoga naam wadau wa LGBTQ wao wamefurahishwa sana na tamko la papa, na kumwagia sifa za kutosha.

Lakini baadhi ya viongozi wa kanisa la RC wamejaribu hasa Afrika kuwa kinyume na kauli hiyo ya mkubwa wao. Ingawa wanatumia maneno ya kujificha ili wasioneshe kama wanampinga moja kwa moja boss wao. Lakini walisomea Cuba wameshaelewa kuwa kauli za papa hazijawafurahisha wadau.

Yule askofu wa Marekani ndiye pekee aliyethubutu kumpinga waziwazi kabisa mkubwa wake, akafutwa uongozi na kufukuzwa kanisani. Maana ameenda kinyume na kiapo chake.

Ingawa wapo viongozi wengine wanamuunga mkono na kuitetea kauli hiyo tata ila wanapata wakati mgumu kunyosha maelezo. Waumini wengi wanatatizika na kukosa amani mbele ya ulimwengu, wakijiuliza maswali yasiyo na majibu.

Msimamo wa Biblia

Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, bali myakemee; Efe‬ ‭5:11‬ ‭SUV‬‬

Matendo ya giza hayana baraka bali kukemewa. Kuhusu baraka na laana, Biblia inasema:

"baraka ni hapo mtakapoyasikiza maagizo ya BWANA, Mungu wenu, niwaagizayo leo; na laana ni hapo msiposikiza maagizo ya BWANA, Mungu wenu, Kum‬ ‭11:27‭-‬28‬ ‭SUV‬‬

Na moja ya agizo ni;

‭‭Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo. Law‬ ‭18:22‬ ‭SUV‬‬

Sasa utabarikiji kitu alichokilaani Mungu? Maana inajulikana wazi huwezi laani alichobariki Mungu hali kadhalika huwezi bariki kilicholaaniwa na Mungu.

Au una hekima kuliko Mungu aliyetenga giza na nuru? Kwake LGBTQ ni giza/ chukizo, wewe unatoa baraka, au ndiko kunena kinyume chake aliye juu? Dan 7:25

Turejee katika schism

Mnamo 1050 kauli za papa ziliibua mgawanyiko (Schism) na kutokeza mpasuko mkubwa uliozalisha makanisa mawili ya kikatoliki (Roman Catholic na Orthodox). Papa alimtaka patriaki mkuu wa Kostantinopo ajisalimishe chini yake yaani katika kiti cha Petro. Akakataa na wakaishia kutoleana maneno magumu ambayo yalipelekea vita baadae mnamo 1204, Kostantinopo ikavamiwa na Kanisa la Papa na kuharibiwa. Hii kauli ya sasa ya papa Francis nayo wachambuzi wengine wanaonelea kwamba inaweza kutokeza schism nyingine ya nyakati hizi.Tusubiri.

Schism (Mgawanyiko) unatokana na nini?

Ni "kukataa kujisalimisha kwa Askofu wa Roma (Roman Pontif) au umoja na washiriki wa Kanisa walio chini yake," kama inavyofafanuliwa katika kanuni ya 751 ya kodi ya Sheria ya Kanuni (code of canon law) aya ya 2089 ya Katekisimu ya Kanisa Katoliki.

kukataa kujisalimisha si tendo rahisi la kutotii, bali ni kukana mamlaka ya papa ya kuamuru aliyopewa na Mungu. Kukataa komunyo kunamaanisha kukataa kwa makusudi kushiriki katika maisha na ibada ya Kikatoliki. Katika Canon 1364 inasema kwamba mpingaji sharti kutengwa moja kwa moja. Na ndio maana askofu yule kule Marekani alitengwa haraka iwezekanavyo. Na Canon law ina maelezo mengine haya:

"Kristo si tu kawapa Mtakatifu Petro na waandamizi wake neema ya karismatiki ya kutokosea kufundisha bali pia aliweka ukuu wao wa upapa ili kutawala kimamlaka kama Kristo. Mathayo 16:19 inasema, "Nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni."

Hivyo Papa ni asiyekosea (infallible), na kauli yake haipaswi kupingwa na waliochini yake. Maana sauti yake si ya kibinadamu bali ya Mungu.

Watawala wa Ulaya katika zama za kati waliingia katika mtafaruku na papa sababu ya fundisho hilo. Maana kanuni hiyo iliwaweka chini ya askofu wa Roma, na wengi waliondolewa ushirika kwa kukataa matamko ya papa.

katika mwaka wa 1302 Papa Boniface VIII alirejelea kifungu hicho cha kanuni alipozungumza juu ya umuhimu mkubwa wa Wakatoliki kujisalimisha kwa mamlaka ya upapa. Katika tamko lake la kipapa (pope bull) lililoitwa Unam Sanctam, Boniface VIII alisema,

“This authority ... is not human but rather divine, granted to Peter by a divine word and reaffirmed to him (Peter) and his successors. ... Therefore whoever resists this power thus ordained by God, resists the ordinance of God [Rom 13:2]. ... Furthermore, we declare, we proclaim, we define that it is absolutely necessary for salvation that every human creature be subject to the Roman Pontiff.”

Kwamba, “Mamlaka haya [ya papa] ... si ya kibinadamu bali ya kimungu, yaliyotolewa kwa Petro kwa neno la kimungu na kuthibitishwa tena kwake (Petro) na waandamizi wake. ... Basi kila apingaye uwezo huu uliowekwa na Mungu hivyo hushindana na agizo la Mungu [Rum 13:2]. ...zaidi ya hayo, tunatamka, tunatangaza, tunafafanua kwamba ni muhimu kabisa kwa ajili ya wokovu kwamba kila kiumbe cha kibinadamu kiwe chini ya askofu wa Kirumi.”

Soma zaidi hapa: Church Authority and Schism

Hivyo mkatoliki yoyote au kiongozi moja wapo wa kanisa la Rumi, akipishana na tamko la Papa ni "MUASI" na anapaswa kutengwa mara moja. Zamani unauawa. Maana unapokuwa kiongozi moja wapo katika kanisa hili must ukubali na kuapa kutii kiti cha Petro (upapa) ambacho ni mwakilishi wa Kristo (vicar of Christ) duniani. Hivyo kumpinga Papa ni kumpinga Kristo. Na ndio maana nimeuliza swali?

Wakatoliki, kwa sakata hili, je! mtaendelea kutoa uaminifu (royalty) wenu kwa Papa [papacy] au kwa Maandiko Matakatifu?
 
Ukatoliki dini ya mchongo lakini ni kama wa katoliki wengi bado wamelala vipi mtu mwenye akili zake timamu utaenda kuungama mbele ya kiumbe kama were je yeye Hana makosa wala hakosei

Sababu kuu nikupenda kuskia kila wanachoambiwa na kuaminishwa

Ni kama akili IME stop ha ifunction
 
Ukatoliki dini ya mchongo lakini ni kama wa katoliki wengi bado wamelala vipi mtu mwenye akili zake timamu utaenda kuungama mbele ya kiumbe kama were je yeye Hana makosa wala hakosei

Sababu kuu nikupenda kuskia kila wanachoambiwa na kuaminishwa

Ni kama akili IME stop ha ifunction

Hakuna aliyesalama hata uliko nawe unaonekana boya tu,dini ni utumwa wa kifikra na imani ni shambulio la akili.
 
Ukatoriki mnausema, usabato mnautoa kwenye ukristo, ulokole ndio kabisa sasa ni thehebu lipi LA kikristo sahihi.?
 
Mimi nimeamua kuachana na mambo ya dini baada ya tamko kutolewa,saivi nasaka pesa tu kama una mchongo tustuane
 
Screenshot_20240101-143801.jpg
 
Back
Top Bottom