Biblia haisomwi kama kitabu cha hadithi. Ukisoma kama kitabu kama kitabu cha hadithi utaona kimejaa contradictions. Ufahamu kuwa karibia kila andiko lililopo katika biblia, lina mazingira yake, kufuatana na hali iliyokuwepo kwa nyakati hizo.
Ukisoma kama kitabu cha hadithi unaweza kuishia kwenye mambo ya ajabu yaliyo kinyume kabisa na ne o la Mungu:
Unaona andiko kama hili:
1 Kor 14:34
Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo.
Ukisoma biblia kama kitabu cha hadithi si utaishia kusema wanawake wamezuiwa kusema chochote ndani ya kanisa, yaani wasisali, wasiimbe, wasihubiri wala kutangaza?
Kuelewa hasa kilichokusudiwa katika andiko la Biblia kunahitajika sana kuelewa mazingira ya agizo, tafsiri kutoka andiko asilia, na maana ya kuabudu. Usipoyajua hayo utakurupuka na vitu vya ajabu. Ufahamu kuwa kuna Encyaclopedis kwaajili ya ufafanuzi wa kila mstari wa biblia.
Unachotamiwa kufahamu ni kuwa imekatazwa kuitengeneza sanamu na kuifanya Mungu wako,ukaiabudu. Wote wanaoitwa wakristo, hakuna walio na sanamu miungu.