Mambo ya kuyaepuka sana wakati wa maombezi kwenye makongamano na semina

Nov 16, 2023
14
22
🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥
===================================================================================
Ujumbe Maalumu Kwa Mitume, Manabii, Wachungaji, Maaskofu, na Waumini Vituo Vya Maombi na Maombezi Duniani;
_______________________________________________________________________________

Ipo Tofauti Kati Habari Njema, Siri za Ufalme wa Mbinguni na Hekima Ya Mungu...

Hekima Ya Mungu Aliye Hai, imebeba ; SIRI NGUMU SANA, ZA KUTISHA, ZA PEKEE, MAALUMU NA ZA AJABU , Kutoka Ofisi Ya Mungu Baba kwa ajili Ya Ulinzi na Usalama wa Kanisa la Yesu Kristo Hapa Duniani....... Lengo Langu mimi; mzee Jordan Twarindwa... Ni kukupa Maarifa na Fahamu, Hasa Waumini, Watumishi Wote Wa Madhabahuni, na Maalumu sana kwa Hawa niliyowataja kule Juu Kabisa...... Yeremia 3:15..... NAAGIZA MZINGATIE SANA KWA FAIDA YENU NA USALAMA WA KAZI YA MUNGU , Hasa Waumini wenu........

°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°
Ezekieli 28:2-3
[2]Mwanadamu, mwambie mkuu wa Tiro, Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa moyo wako umeinuka, nawe umesema, Mimi ni Mungu, nami nimeketi katika kiti cha Mungu, kati ya bahari; lakini u mwanadamu wala si Mungu, ujapokuwa umeweka moyo wako kama moyo wa Mungu.

[3]Tazama, una hekima kuliko Danieli; hapana neno la siri watu wawezalo kukuficha;

°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°
[12]Mwanadamu, umfanyie maombolezo mfalme wa Tiro, umwambie, Bwana MUNGU asema hivi; Wewe wakitia muhuri kipimo, umejaa hekima, na ukamilifu wa uzuri.

[14]Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto.

°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°

MAMBO YA KUYAEPUKA SANA WAKATI WA MAOMBEZI;--

1. Epuka kuwaambia Waumini wenu HAPO Kanisani au katika makongamano WASHIKANE MIKONO WAWILI WAWILI NA KUOMBEANA.... kama haujaagizwa na Roho Mtakatifu ufanye hivyo maana; ni Hatari Sana....
Watumishi WENGI wafanyao mchezo Huu au tukio Hili Wameiga Watumishi wenzao, hawajatumwa na Mungu Aliye Hai wafanye hivyo.....

Kwa wewe Muumini , Nakushauri ; USIKUBALI, NA USITHUBUTU TENA KUSHIRIKI MTINDO HUU WA MAOMBI, AU MAOMBEZI YA KUSHIKANA MIKONO WAWILI WAWILI NA KUOMBEANA........ ACHA..!, maana Ni Hatari Sana kiroho, kihuduma, katika wakovu na kiutumishi.....
Kama Siku Hiyo kuna wachawi, wamejipenyeza kwa hila....... Ayubu 2:1-5, au wenye mapepo kutoka ngazi ya falme, mamlaka na wakuu wa giza,.... Mjue wote mlioshikana Hasa Ambao ni wachanga katika wokovu na kiroho, fahamuni kuwa; imekula kwenu..!

2. Miongoni mwa madhara yatakayojitokeza wakati huouo au baadaye, ni Kupukutika kiroho, kupoteza kiu ya ibada, kupoteza kiu ya NENO LA MUNGU ALIYE HAI, AU MAFUNDISHO..., Pia waweza kuingiziwa mapepo kwa MTINDO HUU WA MAOMBI YA KUOMBEANA WAWILI WAWILI KATIKA, SEMINA, MAOMBEZI, MAKONGAMANO NA KUSANYIKO..... Baadhi ya Waumini wachache wenye Ufahamu niliyoongea nao wamenieleza kuwa; wameanza kuyakwepa Maombezi ya aina Hii ya KUOMBEANA WAWILI WAWILI..

Wakati Mwingine ebu TAFAKARI KWA MSAADA WA ROHO MTAKATIFU... Mtu hakujui, na wewe haumjui vizuri kiroho, anawezaje kukuombea???..... Kama ni mganga mchawi amekuja ibadani Siku Hiyo kuokoka, mtu wa Hivi anakuombeaje??... Ukishikana naye mikono na kuomba WAWILI WAWILI, akaweka mkono wake katika utosi wako, kifuani mwako, Tumboni, au kiunoni.... utasalimika WEWE ??.......... TAFAKARI.... Chukuwa Hatua..!

3. Epuka kuwaambia Waumini wako Wakumbatiane na kuombeana WAWILI WAWILI... Hii ni Hatari nyingine KUBWA SANA na balaa... Kukumbatia ni Busu Takatifu, linaloweza kuhamishia NEEMA, upako, Moto wa Roho Mtakatifu, vipawa.... Au mapepo... Kabla ya KUFANYA Hivi, hakikisha ROHO MTAKATIFU Amekuagiza uwaambie Watu Hivi HAPO Kanisani au katika makongamano au Maombezi ya wagonjwa.......
Na unatakiwa uwe WEWE Mtumishi, unaye waagiza Watu vivyo, uwe na; UPAKO WA KUTOSHA..... FORCE, ….MOTO WA KUTOSHA,.... 🔥...fire NA UNAOWEZA KUUTUPA, AU KUURUSHA ILI UWAFIKIE WATU WOTE KATIKA IBADA, MAKONGAMANO, SEMINA ZA MAOMBEZI.....
PIA unatakiwa uwe na nguvu za MUNGU ALIYE HAI za KUTOSHA, ..... Power of Almighty God...... ...ndipo uwaambie Watu Hivi.... Vinginevyo Kama umeiga Watumishi wengine uliowaona YouTube, au katika makongamano uliyohudhuria NAKUSHAURI ACHA..!

4. Maombi ya Aina Hii yanapukutisha Sana kanisa, na kuleta madhara makubwa kwa Kiwango cha kutisha, maana; shetani hutumia njia Hii kwa sura ya hekima yake ili kuangusha Kazi ya Mungu Aliye Hai... Daniel 28:3
_______________________________________________
Chunguza Sana Yale unayowaagiza Watu wayafanye au kuyasema wakati wa IBADA ukiwa unahubiri...... ili ujue kuwa; JE YANATOKANA NA UFUNUO WA ROHO MTAKATIFU, UNABII AU , umeongozwa na Hekima Ya shetani ???..... Daniel 28:3
________________________________________________
Kama hauna Ufunuo , acha manjonjo, au vituko unapokuwa Madhabahuni.. fundisha, hubiri, ukimaliza, nenda kakae..... WEWE !!....
________________________________________________

5. Epuka maombi au Maombezi ya kushikana MABEGANI NA KUOMBEANA WAWILI WAWILI... maana Kama MTU mwaribifu, amejipenyeza kwa siri ili kuja kushambulia kanisa au Waumini, halafu akakuwekea mkono utosini, mabegani, kiunoni NI HATARI SANA.... NAKUSHAURI ; Usishiriki maombi au Maombezi ya Aina Hii popote pale hata Kama Ni Kanisani kwenu ...USISHIRIKI..!!

KWANINI USISHIRIKI??? ..... Fahamu kuwa; utosini, mabegani, kiunoni, kifuani, ni MALANGO....GATES... Zab 24:7... Ni maeneo yanayoweza KUPITISHA, chochote kutoka Ulimwengu wa Roho wa NURU, au Ulimwengu wa roho wa giza na kuingia ndani yako, na KUFANYA Mabadiliko mazuri au mabaya....
utamlilia nani yakikukuta??.........
________________________________________________
Fahamu siri Hii NGUMU SANA,.. kuwa; baadhi Ya madhila na mapepo yanayokutesa hivi sasa umeyaokota Kanisani bila kujua kwa kushiriki maombi ya kushikana MABEGANI, mikono na kuombeana WAWILI WAWILI
🔥 🔥 🔥🔥🔥🔥🔥🔥 🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥
________________________________________________
Utafiti wa miaka 38, na kwa MSAADA WA ROHO MTAKATIFU, umefunua Siri Hii NGUMU SANA iliyofichika........ 1Kor 2:10-15

°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°°
Zaburi 24:7
[7]Inueni vichwa vyenu, enyi malango,
Inukeni, enyi malango ya milele,
Mfalme wa utukufu apate kuingia.
________________________________________________
Lift up your heads, O ye gates; and be ye lift up, ye everlasting doors; and the King of glory shall come in.
________________________________________________

1 Wakorintho 2:6-7,9-10,13
[6]Walakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilika;
--------------------------------------------------------------------------
Howbeit we speak wisdom among them that are perfect: yet not the wisdom of this world, nor of the princes of this world, that come to nought:
--------------------------------------------------------------------------
[7]bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu;
--------------------------------------------------------------------------
But we speak the wisdom of God in a mystery, even the hidden wisdom, which God ordained before the world unto our glory:
--------------------------------------------------------------------------
[9]lakini, kama ilivyoandikwa,
Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia,
(Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,)
Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.
--------------------------------------------------------------------------
But as it is written, Eye hath not seen, nor ear heard, neither have entered into the heart of man, the things which God hath prepared for them that love him.
--------------------------------------------------------------------------
[10]Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.
--------------------------------------------------------------------------
But God hath revealed them unto us by his Spirit: for the Spirit searcheth all things, yea, the deep things of God.
--------------------------------------------------------------------------
[13]Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni.
--------------------------------------------------------------------------
Which things also we speak, not in the words which man's wisdom teacheth, but which the Holy Ghost teacheth; comparing spiritual things with spiritual.
________________________________________________
Mwalimu; JORDAN GADI TWARINDWA..
 
Back
Top Bottom