Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,861
Ukifika pale Italia, kuna sehemu ndogo ya nchi, inaitwa Vatican. Hapo ndipo yalipo makao makuu ya Kanisa la Roman Catholic ambapo mkuu wa kanisani hilo ni Papa.

Pale Italia wana pesa yao, ila haitumiki ukiingia Vatican. Kule Vatican wana pesa yao na unaweza kuitumia hata Italia.

Rais wa Italia, Bwana Sergio Mattarella hana mamlaka katika serikali ya Vatican, ila Papa ana mamlaka makubwa katika serikali ya Italia.

Mtu wa Vatican anahesabika ni Muitaliamo pia, ila Muitaliano huhesabiki kama Mvatican.

Polisi wa Italia wakienda Vatican, kuna sehemu hawatakiwi kukanyaga kabisa, yaani wamewekewa mipaka ya kuvuka nchini humo.

Vatican ina raia 800 tu ila ndiyo wanaisshikilia dunia yenye binadamu zaidi ya bilioni 7.

Vatican hakuna hospitali, so hakuna suala la kusema umepata uraia kwa kuzaliwa. Wao washajiwekea ni watu 800 tu. Akifa mmoja, analetwa mwingine.

Hapo Vatican kuna museum 70,000 ambapo utaangalia historia za sehemu mbalimbali. Wana vitabu vya historia ya kila taifa duniani. So wanazijua nchi zote mpaka serikali zake. Na kwa siku hupokea watalii 25,000.

Vatican ina miaka 95 tu tangu alianzishwe.

Ndani ya Vatican, kuna maeneo mtu mwenye tattoo haruhusiwi kuingia.

Papa halipwi ila Vatican huingiza mapato ya dola milioni 300 kwa mwaka ambazo hutumika kwa ajili ya chakula, pesa kidogo kwa papa na kugharamia safari zake.

Wanajeshi kutoka nchini Uswisi ndio wanaoilinda Vatican.

Vatican haizitambui nchi mbili tu duniani, China na Korea Kaskazini.

Benki ya Vatican inamiliki assets ya dola bilioni 64.

Vatican inatumia benki ya Istituto per le Opere di Religione kuhifadhi pesa zao. Kuna kipindi wezi waliiba humo, walikufa vifo vya kutatanisha.

Unapoingia Vatican, unaruhusiwa kubeba kamera yako popote pale isipokuwa katika kanisa la Sistine.

Unapoingia kwenye museum yoyote pale Vatican, unaruhusiwa kupiga picha ila kamera isiwe na flash.

June 22 mwaka 1983 mwanamke aitwaye Emmanuela alipotea katika mazingira ya kutatanisha huko Vatican alipokuwa akisomea shule ya muziki.

Vatican inamiliki telescope kubwa huko Arizona ya kufanyia tafiti zao mbalimbali.

Huwa nawaambieni, mkisikia Papa, jua umemsikia mtu mkubwa sana, yaani mkubwa kuliko unavyofikiria. Na ukisikia Roman Catholic, jua umesikia kanisa kubwa mno kuliko unavyofikiria.

Kuna maamuzi huwezi kuyafanya pasipo ruhusa kufika Vatican.

Dunia ipo kiganjani mwao.
 
Sema wanashikilia ulimwengu wa wamagharibi sio dunia nzima
 
China imeshaingia kwenye mfumo, makanisa ya Catholi pamoja na makardinal wa kichina sasa wapo chini ya Vatican tofauti na mwanzoni ambapo China iliomba serikali iwasimamie yaani mamlaka yao isitoke Vatican.North Korea napo taratibu ukatoliki umeshaingia kuna makanisa na kardinal huko.
 
Na wameruhusu baada ya kuona nguvu yake imeshapungua na wanajua namna ya kuwa control pia, maana nao wanaweka humohumo mapandikizi ya watu wao kupata taarifa za upande wa pili
 
Sawa ila sidhani kama ni sahihi kusema dunia ipo kiganjani mwao. Ila naona ni sahihi kusema wana ushawishi sehemu kubwa duniani, sehemu ambazo zina wafuasi wengi wa kikatoliki.

Ila sehemu zingine kama China, Korea, Japan, India, Uarabuni na sehemu zingine zinazotukuza tamaduni zao, Vatican hawawezi fanya chochote.
 
Back
Top Bottom