Mzee Butiku anasema kwa namna kelele zilivyo nyingi kuhusu suala la bandari serikali Ina namna mbili tu..
1. Kiheshimu hofu na maoni ya wananchi kwamba hawajaridhika na suala hili, au
2. Kuwapuuza wananchi na kuendeleza na suala hili.
Lakini wapime madhara ya kila uamuzi watakaoifanya.
Alipoulizwa kuhusu ushirikishwaji wa wananchi kama haukuwa wa kutosha. Mzee Butiku amesema hadhani kama ushirikishwaji ulikuwepo, na kama uliikuwepo basi ulifanywa ktk namna ambayo haikuwa bora, kwani hata yye ni mwananchi lkn hajauona huo ushirikishwaji.
Ameulizwa endapo hoja za serikali kutetea suala la DP je, zinajibu hoja za wananchi? Mzee Butiku amejibu kuwa hazijubu ndiyo maana mjadala haukomi.
Ameonya wale wanaowatisha wanaotoa maoni kinzani na kusema tabia hii inajenga hofu na kujenga taifa la woga.
Anaongeza kwa kusema kuendelea na suala hili ni kuhatarisha umoja na muungano wetu.
---
"Nianze kwa kutoa shukrani kumshukuru na kumpongeza Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa mabo mawili kwanza kuruhusu Watanzania kuzungumza...tulikuwa na woga...lakini tangua Rais aingie ametuambia tuzungumze, waziwazi...ukweli
"Kwa maoni yangu Watanzania bado wanao uwoga...wana wasiwasi...hawana hakika kama maamuzi haya yaliyofanywa na serikali ni kwa faida ya nchi yao, hiyo sauti unaisikia wakati wote kwa ngazi zote"
Source: ITV Kipindi cha dk 45.