Uchaguzi 2020 Mwigulu Nchemba: Rais wetu ni Magufuli, waambieni waliowatuma enyi wenye tamaa ya Madaraka

Umeongea kila kitu haswaaa.kwa kifupi wapo watu wachache huenda matamanio yao ni kuona vurugu nchini mwetu, la msingi wafahamishwe kuwa Watanzania hatuongozwi na maneno ya kuunga unga tuna Kiongozi imara na shupa yupo makini kutuvusha.
 
nimeielewasa sana hyo point ya 4, mimi siipendi ccm, unafiki unasumbua sana watu, wanaoikimbia ccm wanapaswa kuogopwa kuliko ccm yenyewe
 
Mwaka 2015, wewe na wenzio mlitaka JK apewe kipindi cha 3! JK mwenyewe akakataa. Leo mnataka kutoa ukomo wa Urais kwa Magufuli. Hivi hamuwezi kuishi bila kujikomba? Mbona watu wengi tu tunaishi bila kujulikana ama kujikomba?
.
Huwa inashanga sana.Wakati mwingine inakuwa vigumu kuamini kuwa hawa watu ni wasomi.
 
Yaani ni majanga mkuu,watu wanasoma lakini hawaelimiki kabisa
 
Ila wewe kaka noma kwa "propaganda" tu hujambo. Ni bahati mbaya wanaofahamu haya maigizo yako ya kila siku ni wachache saana bahati mbaya hata jiwe hajakustukia na juzi juzi kaingia mkenge kwa ulaghai wa kauli zako na kukurudisha katika ufalme wake...Unachokiongea ni tofauti na unachowaza rohoni mwako.....vice versa...is true
 
Nimemshangaa sana tena sana Msomi mwenye Phd na Waziri kusema kuwa Bungeni kuna Wabunge wa Upinzani eti ni kipimo cha kuwa Tanzania ina Tume Huru ya Uchaguzi. Napenda nimuulize waziri wetu hivi wanaposema Tume Huru anaelewa maana yake?

Inawezekana hajui ,Tume iliyopo iliyoundwa wa wanachama wa chama kimoja na ambao wanateuliwa na mwanachama wao na bado huyo anayewateua ni mgombea wa chama hicho hicho utaiitaje hiyo Tume ni Huru?

Ni suala la kutumia akili ndogo tu kujua Tanzania haina Tume Huru ya Uchaguzi.
 
Mwigulu ni chagua la watu amezaliwa kuwatumikia watanzania

Mungu ambariki
 
Povu la Nini mtu katoa yake ya moyoni na kwa kweli kwa wale tuna nchi moja tu iitwayo Tanzania, yupo sahihi! Membe na kundi lake ni wahuni tu!
 
Mungu ni mwema sana, naamin kwa watanzania walio wengi hawawez kumbeza rais wetu kamwe. Amepitia changamoto za kutosha, but he is still firm katika uongozi wake. MUNGU ambariki sana walau nasi tuwe na mengi ya kuwa proud of as a nation!

Sent from my SM-N910U using JamiiForums mobile app
 
"Afrika ukishindwa unakuwa umeibiwa kura ukishinda unakuwa unahujaibiwa kura ,ukishinda kunakuwa hakuna tume huru ya uchaguzi ukishinda kuna kuwa na tume huru ya uchaguzi " rais kikwete
 
Hyu siku alipotemwa aliacha Yale maskafu aliporudi tu...akayavaa...
 
Hata Rais mstaafu, Mh. Mkapa, katika kitabu chake, aliongekea umuhimu wa kuundwa Tume huru ya uchaguzi. Hii ni ishara kuwa hii "taasisi" haiko huru!


Naye huyo alikuwa mnafiki, mbona alipokuwa madarakani alishindwa kuunda hiyo tume huru, kutoka tu madarakani anajifanya mwema sana kuandika habari hiyo ili ajaze kurasa za kitabu chake kufanya kiwe kikubwa ili kipande thamani, mjanja kweli huyo jamaa.
 
Hyu siku alipotemwa aliacha Yale maskafu aliporudi tu...akayavaa...
Madelu ni kibaka mmoja fulani aliyesogezwa karibu na Ikulu n' nothing else!!
Watz rejeeni yale mauaji ya Olasiti pale Arusha ndiyo mtajua hili Jinyiramba ni jitu la aina gani.....Over n' out!
 
Mwigulu Nchemba tokea uwe supastar (waziri wa fedha) huonekani humu. What's reason, au uko bize na kuhesabu pesa.
Afu mfanye kurekebisha hizi tozo za miamala sio poa. Yule mbunge zungu aliwaingiza cha kike.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…