Mwenye taarifa hii tafadhali atuwekee humu.: jeshi la polisi lakamata madereva 150 wa mabasi ya mikoani.

HOPEfull

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
1,726
2,082
Habari wanajamvi.
WIKI HII inayoishia leo 21 May 2022 Nilikuwa nimekaa mahali usiku nikasikia kwenye radio kwa mbali ilikuwa ni taaarifa ya habari nikawa interested kuisikia lakini bahati mbaya ikawa imepita.
Nimejaribu kuitafuta kwa bidii kwenye mtandao nimeikosa.Inaelekea haina intrest sana kwa waandishi wa habari lkn ni habari muhimu.Mara nyingi tunakimbilia kuripoti habari za ajali inapotokea na sio habari za kinga za ajali au jeshi linapofanya juhudi za kuzuia ajali.Ingekuwa ni habari ya ajali ningeipata dakika au sekunde tu.
Habari muhimu kama hii ilitakiwa kila mahali iwe imerushwa kila mahali kujua hawa madereva wahuni wanaotupotezea ndugu zetu.
Kwa mbali nilisikia madereva wa mabasi waliokamatwa ni wanaofanya safari za dar irnga mbeya na tunduma ambao wanaendesha mabasi kwa kasi na kwa fujo.Kama hii habari ni kweli basi nalipongeza jeshi pa polisi kwa kazi nzuri na huu utaratibu uendelee mikoa yote ikiwezekana kuchuja kabisa madereva wote waliovamia hii fani na kuwatoa kabisa kazi ziko nyingi za kufanya kama unapenda kuendesha gari basi fuata sheria.
Mod kama hii habari haipo basi futa uzi huu.
 
Mambo Ya Barabarani Hayo Yaani Kawaida
Geshi Linafanya Kazi Yake, Drivers Nao Hivyo Hivyo
 
Madereva 150 kila Mmoja akitoa Rushwa ya Laki tatu tayari kuna 45Mil, haina makato wala longolongo..

Hapo ukute wapo wakuu watatu walioshikilia Kesi, na wakiigawa gawa kwa "Vijana"; Take home haipungui 10m hapo kwa kila Mkuu.
Wana~Brush Viatu Tu Yule Baba Jamani
 
Kuendesha bus nyie rahaa! Hasa upate yenye engine ya SCANIA ya gia kumi. Ile imetengenezwa kwa ajili ya mizigo afu wewe ubebee binadam. Unakua kama umepakia 'unyoya' tu!
Kitonga unapanda na gia namba 6 😀😀😀 kushuka unashuka na namba kumi 🤗🤗🤗. Gari likiisha upepo 'unaliegesha' kwenye mlima traffic watakuja kulitoa.
 
Niko na madereza 130 wengne wametoka kwa dhaman.
Walobaki kesho nawapeleka mahakamani wakakutane na hakimu Juma
 
Kuendesha bus nyie rahaa! Hasa upate yenye engine ya SCANIA ya gia kumi. Ile imetengenezwa kwa ajili ya mizigo afu wewe ubebee binadam. Unakua kama umepakia 'unyoya' tu!
Kitonga unapanda na gia namba 6 😀😀😀 kushuka unashuka na namba kumi 🤗🤗🤗. Gari likiisha upepo 'unaliegesha' kwenye mlima traffic watakuja kulitoa.
Mkuu, tosha sasa rudi nyumbani kesho siku ya kazi.
 
Madereva hawa hawa ambao wapo siku zote barabarani ndio wamesimamishwa kweli?
 
Back
Top Bottom