Uchaguzi 2020 Mwanza: Shule zasitisha masomo, Wanafunzi waambiwa wakampokee na kumsikiliza Mgombea wa CCM Dkt. Magufuli Uwanja wa CCM Kirumba

Mwalimu ambae hato hudhuria atahesabika kama mtoro na atakatwa mshahara. Pia mwanafunzi ambae hato hudhuria atahesabika kama mtoro na kesho atapewa adhabu ya viboko.
Nimejikuta nawaza tu hivyo...
Hawa jamaa hawaachagi ushetani.... Wanaweza kufanya hivo
 
Yes ndio maana wanawaacha wanafunzi kuhudhuria kampeni badala ya kwenda shule ili kujaza uwanja. Tena wafanyakazi waeambiwa kufika bila kukosa.
Kweli kabisa.... Hii ilikua Magu jana👇👇
 

Attachments

  • 2509840_Screenshot_20200906-142422 (1).png
    2509840_Screenshot_20200906-142422 (1).png
    237.1 KB · Views: 1
Thibitisha, mm ni MWALIMU hapa Mbugani S/msingi madarasa yanaendelea.Lakini hazuiliwi MTU kwnd kumsikiliza mkuu wa nchi mahali aliko Karibu.
OVER..
Hakuna darasa lolote linaendelea leo mkuu....
 
Wakuu nilisikia jana lkn sikuamini mpaka asubuhi hii nilipoamua kupiga simu kwenye shule mbili za binafsi ambako watoto wangu wanasoma.
Wameagiza hakuna shule leo na watoto waruhusiwe kwenda kwenye mkutano bila uniform.

Wakuu hii maana yake nini?
Kwa nini kulazimisha kwa kiasi hiki?
Ni kweli mikutano ya magufuli ni Muhimu kuliko elimu ya watoto wetu?

Nimesikitika sn kuhusu amri hii haramu.
Kwa mfano hao wa kwako wamelazimishwaje wakati wako nyumbani hawajaenda shule?
 
Wasanii hawatoshi kuvutia watu mpaka walazimishe watumishi na wanafunzi ili kujaza uwanja!

Halafu utasikia,"asanteni sana kwa kujitokeza kwa wingi,sikutegemea mngejitokeza kwa wingi hivi!Nina deni kubwa kwenu"!
Pumbav,unajitekenya na kucheka mwenyewe!
 
Kwani na hao watoto wa shule ya msingi na hata baadhi ya wale wa sekondari(ambao hawajafikia umri wa kupiga kura), wataenda kupiga kura?


Au ndiyo matatizo ya akili ndogo kuongoza?
 
Wasanii hawatoshi kuvutia watu mpaka walazimishe watumishi na wanafunzi ili kujaza uwanja!

Halafu utasikia,"asanteni sana kwa kujitokeza kwa wingi,sikutegemea mngejitokeza kwa wingi hivi!Nina deni kubwa kwenu"!
Pumbav,unajitekenya na kucheka mwenyewe!
Jamaa wanalazimisha kukubalika
 
Huko ndiko kufilisika kimvuto mpaka inafikia kuanza kuwakusanya watu kinguvu. Wana hali mbaya.Japokuwa hayo yanafanywa na viongozi wa chini ili kumfurahishwa bwana yule kuwa wamefanya maandalizi mazuri.
 
Sio niulize Mwanza, mi naishi hapa hapa Mwanza......ukiangalia hili nyomi la leo kwenye mapokezi ni zaidi ya mara 3 ya ule upumbafu mliokuwa nao hapa juzi kati viwanja vya furahisha
ENDELEA KUCHEZA VIDUKU, HIZI HOJA NZITO TUACHIE
 
Katika hali isiyo ya kawaida Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela amesitisha kufunguliwa kwa shule zote hapo kesho ili waalimu na wanafunzi washiriki kampeni za chama Cha CCM.

Hali hiyo imesababishwa na chama hicho kukosa ushawishi wa watu kuhudhuria mikutano yake bila kulazimishwa na hali imejionyesha pamoja na kutumia wasanii haijasaidia kitu.

Mgombea wa Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu aliingia Mwanza kwa kishindo kikubwa wiki iliyopita na kuvuta umati wa watu ambao wachunguzi wa mambo wanasema huenda ukawa umati mkubwa zaidi kutokea jijini Mwanza.

Wazazi kadhaa wamelaani hatua ya kutumiwa ujumbe mfupi na wakuu wa shule kadhaa wa maandishi unaowataka wasipeleke watoto shule kesho.

Wazazi hao wamesema hiyo ni kinyume na kanuni za Tume ya Uchaguzi na inaonekana waziwazi CCM imeamua kukanyaga sheria hizo.
Sasa hivi sheria hamuna kuna shelia baba kayaii
 
Yaani huu upuuzi sijui utaisha lini. Nimeshangaa asubuhi hii, watoto wakiwa wanarudishwa majumbani.

Hata taarifa ya kuahirisha masomo imetolewa asubuhi ya leo.

Sababu kubwa ni kuwa walimu wote wamelazimishwa kuhudhuria mkutano wa kampeni!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom