Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ashauri watoto na wazee kufuatilia shughuli za kumuaga Hayati Dkt. Magufuli kupitia runinga

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,875
Mkuu wa mkoa wa Mwanza mh Mongekla amewaasa wakazi wa Mwanza kutokuja na watoto siku ya kumuaga hayati Magufuli katika uwanja wa CCM kirumba.

Marufuku hii inatokana na uwepo wa watu wengi kutoka mikoa mbalimbali waliokuja kumuaga hayati Magufuli.

Source ITV habari!

------------

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amesema watoto wenye umri chini ya miaka 10 hawataruhusiwa kuhudhuria shughuli ya kutoa heshima za mwisho kwa Hayati John Magufuli kuepuka madhara yanayoweza kutokea kutokana na msongamano wa watu.

Akizungumzia na waandishi wa habari jijini Mwanza jana Mongella alitaja kundi jingine linaloshauriwa kufuatilia shughuli hiyo kupitia luninga badala ya kwenda uwanjani kuwa ni wenye maradhi mbalimbali pamoja na wazee.

“Maandalizi yote kwa ajili ya heshima za mwisho kwa Hayati John Magufuli katika viwanja vya CCM Kirumba yamekamilika. Hata hivyo, tunawasihi wazazi na walezi kuzuia watoto wadogo kuhudhuria shughuli hiyo kuepuka madhara ya msongamano. Wazee na wenye maradhi mbalimbali pia tunawashauri kufuatilia tukio hilo kupitia luninga,” amesema Mongella

Mkuu huyo wa mkoa amesema milango yote ya uwanja wa CCM Kirumba itakuwa wazi kuanzia saa 12 asubuhi kwa ajili ya waombolezaji kuingia kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho.

Kesho Jumatano Machi 24, 2021 wakazi wa Mwanza nao watapata fursa ya kumuaga kiongozi huyo atakayezikwa wilayani Chato Mkoa wa Geita Ijumaa Machi 26, 2021.

Chanzo: Mwananchi
 
Usalama kwanza wa walio hai, yupo sawa, utatatibu wa Dodoma leo ni sawia, mbali ya uwanjani apitiswe mitaa mbalix2 ni muafaka.
 
Kwani watoto si waombolezaji? Hao si ndo alikuwa anawakatisha masomo kipindi cha kampeni za kupora uchaguzi??
 
Mkuu wa mkoa wa Mwanza mh Mongekla amewaasa wakazi wa Mwanza kutokuja na watoto siku ya kumuaga hayati Magufuli katika uwanja wa CCM kirumba.

Marufuku hii inatokana na uwepo wa watu wengi kutoka mikoa mbalimbali waliokuja kumuaga hayati Magufuli.

Source ITV habari!
Umasikini ni umauti!!
 
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amesema watoto wenye umri chini ya miaka 10 hawataruhusiwa kuhudhuria shughuli ya kutoa heshima za mwisho kwa Hayati John Magufuli kuepuka madhara yanayoweza kutokea kutokana na msongamano wa watu.

Akizungumzia na waandishi wa habari jijini Mwanza jana Mongella alitaja kundi jingine linaloshauriwa kufuatilia shughuli hiyo kupitia luninga badala ya kwenda uwanjani kuwa ni wenye maradhi mbalimbali pamoja na wazee.

“Maandalizi yote kwa ajili ya heshima za mwisho kwa Hayati John Magufuli katika viwanja vya CCM Kirumba yamekamilika. Hata hivyo, tunawasihi wazazi na walezi kuzuia watoto wadogo kuhudhuria shughuli hiyo kuepuka madhara ya msongamano. Wazee na wenye maradhi mbalimbali pia tunawashauri kufuatilia tukio hilo kupitia luninga,” amesema Mongella

Mkuu huyo wa mkoa amesema milango yote ya uwanja wa CCM Kirumba itakuwa wazi kuanzia saa 12 asubuhi kwa ajili ya waombolezaji kuingia kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho.

Kesho Jumatano Machi 24, 2021 wakazi wa Mwanza nao watapata fursa ya kumuaga kiongozi huyo atakayezikwa wilayani Chato Mkoa wa Geita Ijumaa Machi 26, 2021.

Chanzo: Mwananchi
 
Wazo zuri lakini angeenda mbali kidogo kuwe na social distance maana corona bado ipo na inaua.
Kimsingi alipozungumzia wazee na wenye maradhi, ni kama alikuwa anatahadharisha corona, ila bado uoga wa kuitamka upo upo, anamsikilizia Samia
 
Tunatishana Sana
Wengine Siyo Waandishi Wa Habari Utawasikia Vigogo Wafa
By JPM
😎😎🙄😶😏
 
Back
Top Bottom