Dodoma: Mkuu wa Shule na Msaidizi wake waondolewa kazini kwa kuwachomesha Mkaa na kuwalimisha mashamba Wanafunzi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
1698033860320.jpeg

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Zaina Mlawa amewang’oa walimu wawili wa Shule ya Msingi Mayamaya chanzo kikiwa ni utumikishaji wanafunzi kwenye kuchoma mkaa, ajali ya moto iliyomuunguza mwanafunzi.

Waliotajwa kuondolewa ni Mwalimu Mkuu Mallika Billa Semghodo na msaidizi wake Mohamed Mochiwa ambao wamesomewa tuhuma nne na kuzikiri mbele ya wazazi na viongozi.

Tuhuma zilizosomwa mbele mkutano huo ni wanafunzi kuchoma mkaa huku wakibeba magogo makubwa,kulima mashamba ya walimu kama vibarua bila ujira, adhabu zilizopitiliza kwa wasiopeleka magogo ya mkaa na kutowapa taarifa ya mapato ya mazao wanafunzi ikiwemo ya miradi ya asali na nyuki.

Mlawa amekwenda kijiji hapo kufuatia vurugu zilizoibuka juzi Oktoba 20, 2023 baada ya mwanafunzi wa darasa la sita, Andrew Jacobo Nghalanzi (13) kuungua moto wakati yeye na wenzake walipokuwa wakiuzima kwenye eneo la shule.

Kwenye tukio hilo lililotokea Jumatano Oktoba 19,2023 saa 11 jioni inatajwa kuwa Mwalimu Mkuu aliwatuma wanafunzi wakazime bila ya kuwa na msimamizi lakini wakati huo haukuwa muda wa masomo kwani ilishakuwa jioni.

Mkurugenzi wa wilaya hiyo amelazimika kuwaomba radhi wazazi kwa mambo yanayotokea akisema hakuwa na taarifa kabla lakini ukweli umewekwa hadharani kwamba kuna uzembe mkubwa shuleni hapo.

“Naomba radhi kwa niaba yangu na watumishi wenzangu, haya mambo hayavumiliki hata kidogo na yamewekwa wazi hapa kila mmoja anasikia hivyo hakuna aliyeonewa, hawa walimu nitaondoka nao,”amesema Mlawa na kushangiliwa na umati wa watu.

Hata hivyo, ameomba wananchi wamvumilie siku nne ili Mkuu wa shule asimamie mitihani ya darasa la nne ambayo itafanyika keshokutwa na baada ya hapo walimu hao atajua pa kuwapeleka.

Mwalimu Billa aliomba wazazi na uongozi wa serikali kumsamehe akiahidi kutorudia makosa wala kuwafanya wanafunzi manamba wa kuchoma mkaa ingawa wazazi walipasa sauti wakimuomba Mkurugenzi kuondoka na walimu wake.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mayamaya, Jonathan Chibalangu amesema kilio cha wananchi kimekuwa cha muda mrefu na mara kadhaa wamekaa vikao vya kuwaonya walimu lakini hakuna mabadiliko.

Chibalangu amesema mambo mengi shuleni hapo yanafanywa kinyume na taaluma za watumishi kwenye shule hiyo huku akianika namna ambavyo taarifa za mapato na matumizi kwa serikali na kamati ya shule hiyo ambayo ina miradi mingi ikiwemo kilimo na ufugaji nyuki havisomwi.

Mwenyekiti amemwomba Mkurugenzi asiwaache walimu hao kwani ilivyo hawatakuwa na uhuru hata wa utendaji kazi huku wananchi nao wakijenga chuki na walimu.

Akichangia kwenye mkutano huo, Anna Mlulu amemwomba Mkurugenzi kuondoka na walimu hao kwa madai hawana imani nao na kama angewaacha wazazi hawatawapeleka watoto wao shule hiyo.

Anna amesema siyo mara moja au mbili wamekuwa wakifikisha kilio chao kwa viongozi kuhusu walimu wa shule ya msingi Mayamaya waliogeuza wanafunzi wao wakata miti na kuchoma mkaa lakini hawaoni hatua zichukuliwe.

“Tukuombe mkurugenzi uondoke na walimu wako, sisi tumewachoka,usipowatoa sisi tunawatoa watoto wetu na kuwapeleka shule nyingine lakini siyo hapa,” amesema Anna.

Wakati huo Mkurugenzi wa Halmashauri amewajulisha wazazi kuhusu hali ya mtoto Andrew kuwa inaendelea vizuri na kwamba viongozi wengi ngazi ya wilaya wanapeana zamu kwenda kumuona na kutoa maelekezo kuhusu matibabu yake ingawa alikiri baadhi ya majeraha yatamfanya achukue muda kwenye matibabu.

MWANANCHI
 
Lisinge tokea tukio lamtoto kuungua maana ake wala asingejua mtu yoyote na mazingira kaa haya vijiji vingi bado wanawaogopa walimu namgambo + mwenyekiti
 
View attachment 2789874

Chonde chonde Mkurugenzi!! Hao walimu unaowachukua wape kazi za ofisini, na sio kuwahamishia shule nyingine hawafai kukabidhiwa watoto!!
 
Back
Top Bottom