Mwanza: Rais Samia aongea na Vijana wa Tanzania katika Uwanja wa Michezo wa Nyamagana

Yaani wanasiasa wanacheza sana na akili zetu. Katika financial institutions hakuna kitu benki ya fulani! Benki inatakiwa ifanye kazi kifuata banking principles and rules. Benki ya wanawake iko wapi?

Nyerere alianzisha benki ya ushirika iko wapi? Ilikuwa Tanzania Rural Development Bank baadaye Cooperative and Rural Development Bank na mwishowe ikabinafsishwa tu ndiyo hiyo CRDB.

Hawajifunzi tu. Juzi kati tu hiyo ya wanawake imefeli ndiyo ya vijana itafaulu? Yaani wanacheza na akili zetu sana hawa!!!!
Mkuu hawa vijana wanajifariji tu hata ikianzishwa watakopeshwa watoto wa kibosire wewe kapuku utausukia tu mkopo. Nimeshasema hamtaki ukweli mnapenda maneno matamu subirini matokeo. Kila kundi la watu mnataka lianzishiwe bank? kweli ? Serkali inatakiwa ifanye reforrms kwenye taasisi za kibanki mtu aweze hata kutumia cheti chake cha chuo kama dhamana kwa mikopo midogomidogo ili kubusti wijana wengi kuwekeza katika maeneo mbali mbali kama kilimo na nk.
 
Hapo kwenye kuanzisha bank ya wajasriamali ni propaganda na kupiga mark time tu! Hakuna tija yoyote.
Ni vyema kuanzisha idara ndogo kwenye bank za kibiashara zilizoenea nchi nzima ili kuwasaidia na kusimamia miradi ya vijana.
Tujiulize, je banki ya kilimo, wanawake, walimu n.k zimetoa mchango gani kulinganisha na gharama za uendeshaji?
 
Jamani wadau napendekeza huu mkeka ambao utakuwa na vijana tu awemo Bi Fatma Karume na Maria sarungi ama mnazemaje wadau ,mashangaz hawa huenda wakatutoa kimasonaso ,
 
Chalamila anatamani angekuwepo hapo
Kwa ujumla Chalamila majira yake yalikuwa yalishakwisha maana tayari falsafa ya Chalamila haikuendana na mama hata kidogo. Na kwangu mimi naona kabisa Chalamila hakuongea kwa bahati mbaya yale maneno alijua kabisa hana nafasi kwa mama akaamua kujitoa mapema maana hata mama ukisikia kauli yake kipindi anawaapisha RCs na wateuliwa wengine alitoa kauli tata amabayo pasina shaka Chalamila hakuipenda.
 
Vijana wanasubiri ajira 40,000 ulizoahidi sio hizo 150 za wakuu wa wilaya. Mama be serious huku mtaani hali ni mbaya. Wewe ndio mwokozi utakayeokoa hiki kizazi
 
Jamani wadau napendekeza huu mkeka ambao utakuwa na vijana tu awemo Bi Fatma Karume na Maria sarungi ama mnazemaje wadau ,mashangaz hawa huenda wakatutoa kimasonaso ,
Hao ni vijana? 50s seasoned veterans wanakuwaje vijana?
 
Vijana wanasubiri ajira 40,000 ulizoahidi sio hizo 150 za wakuu wa wilaya. Mama be serious huku mtaani hali ni mbaya. Wewe ndio mwokozi utakayeokoa hiki kizazi

Tumpe muda ,Mwendazake aliharibu nchi sana mkuu.



NDANI YA SIKU 100, RAIS SAMIA AMEFANYA MAMBO MAKUBWA

Kama kuna jambo lolote linalonipa amani na Faraja kwenye nafsi yangu katika siku 100 zilizopita, basi ni kuona kuwa tuna rais wa aina ya Mama Samia Suluhu Hassan.

1. Ndani ya siku 100 tu za utawala wake, Keshaondoa zimwi la 6% retention fee kwenye mikopo ya elimu ya juu, Hii retention fee ilikuwa ni pasua kichwa sijawahi kuona, mtu ulikywa unalipa lakini deni haliishi, na kinshahara chako kinakwanguliwa tu month after month.

2.Wale standard 7 waliotimuliwa na Magufuli kipindi cha Uhakiki mama kasema walipwe stahiki zao, Hii ni faraja kubwa kwa ndugu zetu wa darasa la Saba ambao walivuja jasho kwa haki kabisa kwa ajili ya Taifa hili.

3. Serikali ya mama iko serious kwenye kupandisha madaraja ya watumishi wa serikali yaliyosimama kwa miaka 5 ya Magufuli.

4. Samia anarudisha uhuru wa habari kwa mfano online TVs sasa zimefunguliwa

5. Wafanyakazi wa serikali wamepunguziwa PAYE hadi 8%

7. Ameshatoa bilion 172 kwa ajili ya kuboresha barabara za vijijini angalau barabara hizo ziweze kupitika. Ifahamike kuna watu wanashindwa kuwahisha wajawazito hospitali kujifungua kwa sababu ya barabara mbovu, Hatua hii ya mama itasaidia sana.

8. Serikali yake imeweka utaratibu wa watoto wanaopata ujauzito waendelee na masomo, hili ni jambo zuri katika vita dhidi ya umasikini, ujinga na maradhi. Maana huwezi kumsaidia mtoto kwa kumfukuza shule maana ukifanya hivyo unamtia yeye na mwanae umasikini wa kutisha, na litakuja kuwa ni mzigo kwa Taifa mbeleni

9. Mama karudisha common sense kwenye suala la Korona, sasa hivi hatusemi tena "Changamoto ya kupumua", bali tunasema Korona—Huwezi kupambana na ugonjwa usiotaka kuuita hata jina lake ukaushinda, lakini sasa hivi tunapambana nao kitaalamu na siyo kienyeji

10. Rais Samia karudisha nidhamu ya wateule, wasijimwambafy na kuzichukulia poa mamlaka, Sasa hivi yule kijana jeuri ananyea ndoo

11. Rais Samia kakataa kupora pesa za watu ili eti kuongeza makusanyo, yeye anataka kodi za haki

12. Rais Samia keshafungulia account za watu zilizofungwa kimagumashi

13. Rais Samia anataka mabenki yatoe interests rate ndogo, anataka 10% ili wananchi waweze kuafford kukopa na kuendesha biashara zao, Riba ya mabenki enzi za nyuma ilikuwa pasua kichwa, ilikuwa inaenda hadi 25%

14. Rais Samia kaamua mradi wa Gesi Lindi uendelee, faida za mradi huu ni kubwa, tutapata gesi kwa ajili ya viwanda vyetu, tutauza nje, na tutazalisha umeme mwingi zaidi.

15. Kesi za Kubambikiza rais Samia kazifuta, watu 172 waliobambikiziwa kesi na TAKUKURU rais Samia keshazifuta, Huu ni utu na ubinadamu ulioje!

16. Mama kafuta adhabu ya kulipa 10% kwa wale wanaochelewa kuanza kulipa mkopo wao bodi ya mkopo

17. Mama Samia keshashusha bei za bando ambazo utawala uliopita uliacha umepandisha na kupelekea kuleta taharuki kubwa nchini, Imagine eti ulikuwa ukiweka sh 2000 hupati GB hata moja, lakini sasa hivi angalau kwa sh 2000 unapata GB 1 na kuendelea

18. Rais Samia keshafanikisha uuzwaji wa mahindi yetu Kenya Wakulima sasa hivi mioyo yao kwatu, imetukia tuli.

19. Rais Samia keshafanikisha utiwaji saini dili la kuiuzia Kenya gesi, hili ni dili safi safi sana, tuna gesi nyingi tu, tukitumia wenyewe na ziada tukiuza na kupata mpunga mrefu itasaidia kwenye uchumi wetu

20. Rais Samia ameendeleza miradi ya kimkakati ya mtangulizi wake, amepeleka hela kwenye miradi yote ya maana ya mtangulizi wake.

21. Ndani ya siku zake 100, Rais Samia ameshatangaza ajira zaidi ya 9000 za walimu na wahudumu wa Afya na vijana wetu maelfu kwa maelfu wameomba. Hili ni jambo zuri sana, na huu ni mwanzo tu Mama anaendelea kumwaga ajira kwa vijana wetu.

Kwa hiyo by all Standards, Rais Samia ameupiga mwingi sana ndani ya siku zake hizi 100 za utawala wake.
Na namtabiria makubwa kwa sababu ana Hekima, Utu, Subira, Yuko open minded, Ni mchapakazi sana, ana exposure, ana uzoefu mkubwa.

We are Lucky kuwa mama is our president.
 
Vijana mjiajili,serikali itaajili watu wangapi, nendeni pwani nunua samaki tembeza mtaani, au tafuta kijiwe weka meza uza pwezi na ngisi, Au tafuta eneo kanunue kokoto Lugoba uza kwa madebe zina faida sana, Kuna fursa nyingi sana za kujiajili mwenyewe kwa TZ,
 
Vijana mjiajili,serikali itaajili watu wangapi, nendeni pwani nunua samaki tembeza mtaani, au tafuta kijiwe weka meza uza pwezi na ngisi, Au tafuta eneo kanunue kokoto Lugoba uza kwa madebe zina faida sana, Kuna fursa nyingi sana za kujiajili mwenyewe kwa TZ,
Dah. Hapo ndio umetoa ushauri
 
Vijana mjiajili,serikali itaajili watu wangapi, nendeni pwani nunua samaki tembeza mtaani, au tafuta kijiwe weka meza uza pwezi na ngisi, Au tafuta eneo kanunue kokoto Lugoba uza kwa madebe zina faida sana, Kuna fursa nyingi sana za kujiajili mwenyewe kwa TZ,
Aliyekwambia its possible kila mtu kuingia mtaani ni nani? Yaani mtu awe producer, promoter na pale pale afanye marketing (hio ni asilimia ndogo sana katika jamii)

Ni wangapi walijaribu kulima mpunga mwaka jana bei hazikupanda..., au wale vijijini wanaolima mahindi hawapati soko la uhakika ?, Au turudi kwenye wakulima wa Korosho au pamba ambao bei kupanda na kushuka inafanya maisha yao yamekuwa kama kamari ?

Viongozi wasikimbie wajibu wao wa kutengeneza Policies nzuri ambazo zitawatoa watu katika hii "RAT RACE" Hususan kwa nchi tajiri kama hii ni Aibu kwa taifa lake wananchi kuwa wabahatishaji...., Siongelei watu wawe matajri..., Hapana ninachokisema tuongeze watu wa middle income na kuondoa masikini (so called wanyonge) Na hawa kuendelea kwao kuishi from hand to mouth ni Threat kwa National Security...
 
Back
Top Bottom