Mwanza: Rais Samia aongea na Vijana wa Tanzania katika Uwanja wa Michezo wa Nyamagana

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
1,683
9,611
Katika muendelezo wa Rais Samia kukutana na kuongea na Makundi mbalimbali nchini, leo ataongea na Vijana wa Tanzania kupitia vijana wa mkoa wa Mwanza katika Uwanja wa Michezo wa Nyamagana.

Taarifa zaidi zinafuata:
Mkuu wa mkoa wa Mwanza ameanza kwa kuwatambulisha watu mbalimbali kwa makundi yao mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan. Uwanja wa Nyamagana ukiwa umefurika vijana wengi sana kutoka sehemu Mbalimali Jijini Mwanza na mikoa ya Jirani. Salamu kutoka kwa wakuu wa mikoa mbalimbali zinaendelea.

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani akabidhiwa zawadi ya Ng'ombe dume na jike. Zawadi hiyo imetolewa na vijana wa mkoa wa Mwanza ikiwa ni shukrani kwake kwa kuendelea kusikiliza mahitaji ya vijana na kuyafanyia kazi.

Hasrat Hanje apendekeza Rais aanzishe baraza la vijana ambalo litakalounganisha vijana wote ili kuwasememea vijana changamoto zao, vijana hao ni kama mama lishe, bodaboda, watu wa migodi, wanafunzi nk.

Hotuba ya Rais Samia Suluhu Hassan, akizungumza na vijana Mwanza

Kusema kweli sikutaraji Umma mkubwa kiasi hiki kusema kweli hii inaonyesha mnajali serikali yenu, kwakweli mmetia fora vijana.

Vijana na watanzania mnaonisikiliza Vijana ni ni kundi muhimu katika Taifa lolote hiyo inatokana na takwimu kuwa vijana ni kundi kubwa kitakwimu, angalau katika nchi zetu za kiafrika ila kwa wale waliozuiliwa kupata watoto wao wana tatizo la vijana ila kwetu vijana ni kundi kubwa.

Na kwa hapa Kwetu Tanzania kwa mujibu wa sensa ya ya watu na makazi 2012 kila kundi la watu 10 basi 4 vijana ni watu wenye umri miaka 15 hadi 35 lakini hii ni tafsiri ya kisera na sheria ya vijana lakini tukihesabiana vijana hapa wanakwend ampaka miaka 40, 50 bado ni vijana, hivyo hii inafanya vijana wawe kundi kubwa.

Lakini kwa tawimu za sasa nchi yetu inakadiriwa kuwana vijana milioni 20 na laki saba, karibu milioni 21. Ukiachilia mbali na takwimu hizo vijana ndio wenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi na ndio maana wanaitwa nguvu kazi ya Taifa.

Ni walinzi wa Taifa ni watu wenye ubunifu watu wenye uthubutu ni wajasiri na ndio waliobeba maono na na matarajio ya Taifa kwa sasa na siku zijazo. Kwa maneno mengine uhai, maendeleo na ustawi wa taifa unategemea vijana hakuna taifa lisilotegemea uwepo wa vijana katika ukuaji wake.

Lakini kundi hili linakabiliwa na changamoto nyingi kama mlivyozisikia hapa nami nazitaja na hatua tulizochukua ,
  • Tatizo la Ajira
Nchi hii kama ilivyo kwa nchi zote duniani inakabiliwa na tatizo kubwa ajira, ambapo kwa wastani asilimi 11.4 ya vijana wenye uwezo wa kufanya kazi hawana ajira, kama mnavyofahamu serikali ndio mwajiri mkuu hata Tanzania na tumekuwa tukitoa nafasi za ajira na matangazo mbalimbali ya ajira na vijana wamekuwa wakiomba lakini wengi wao wakiondoka bila kupata nafasi hizo.

Mfano, Hivi karibuni tumetoa ajira za walimu nafasi elfu sita mia sita na sitini naaa..lakini maombi ni zaidi ya vijana elfu ishirini wameomba nafasi hizo vilevile tumetangaza ajira kutoka kada ya afya vijana wengi sana wamejitokeza kuomba ajira hizo watachukuliwa lakini ni uhakika wengine watabaki na ajira katika sekta za umma huendana na ukuaji wa kiuchumi ili kuwa uwezo wa kulipa mishahara.

Lakini kwa upande mwingine serikali hutekeleza miradi mikubwa ya kitaifa ili iweze kutoa ajira za moja kwa moja na isiyo ya moja kwa moja miongoni mwa miradi mikubwa ya kimkakati inayotoa ajira ni kama hiyo ya ujenzi wa reli bwawa la kufua umeme, barabara miradi ya madaraja ambayo iko nchi nzima yanapishana tu kwa ukubwa lakini yote hiyo hutoa ajira na hii ni baadhi tu ya miradi ambayo serikali inafanya.

Hivi karibuni tutaanza kutekeleza bomba la mafuta kutoka Hoima Uganda kuja Tanga na mradi huu kwa sehemu kubwa upo ndani ya Tanzania na hapo vijana wengi watapata ajira, Tanzania yote ina fursa za ajira kupitia miradi ya aina hii.

Pia Tanzania kuna fursa ya ajira kupitia sekta binafsi hapa serikali hujenga mazingira ili wenye mitaji waweze kuwekeza katika viwanda na kufungua biashara mbalimbali ili waweze kuwekeza na kutoa ajira kwa vijana.

Pia tutofautisha kati ya ajira na kazi, hapa ni pale kijana hajaajiriwa ila kuna sehemu anafanya shughuli zake ili kuweza kujipatia kipato chake hili ni eneo ambalo serikali hujenga mazingira kwa vijana kujiajiri wenyewe mmoja mmoja au katika makundi yao.

Serikali katika kutengeneza mazingira ya kukuza ajira katika sekta binafsi na kuwezesh awananchi kujiajiri imefanya mambo kadhaa ikiwemo kufuta tozo kwenye kilimo, mifugo na uvuvi. Pia imerahisisha upatikani wa leseni ili vijana waombe leseni za biashara kupitia mitandao pia tumefuta tozo au kodi kero za osha, zimamoto na na kodi za aina hiyo ili kuwapa vijana fursa za kuweza kujiajiri

Kwenye madini tumefuta tozo na kodi mbalimbali na kutenga maoneo mbalimbali ya wachimbaji wadogo yenye ukubwa wa hekta Thelathini na nane elfu mia tano na sitini na saba. Maeneo mengine ambayo tumeboresha mazingira ili kuweka mazingira ya vijana kujiajiri ni katika sekta ya utalii ambapo tumeongeza mbuga tano mpya za kitaifa na kununua ndge 11 na kupunguza ada ya leseni ya kusafirisha watalii kwa wakala mwenye magari chini ya manne kutoka dola za kimarekani 2000 hadi dola 500.

Kwenye tehama serikali imejenga data center yaani kituo cha taarifa Dar ili kuwekeza kwenye mambo ya kidijitali, hii ni fursa kwa watanzania kuwekeza kwenye mambo ya mtandao. Pia serikali imewekeza kwenye kuzalisha umeme na watu watumie umeme kwenye kukuza uchumi.

Sanaa na Utamaduni ni eneo lingine la Ajira, kama mnavyofahamu hivi karibuni sanaa imekuwa ikitoa ajira kwa vijana katina muziki, filamu na michezo na wasanii wataanza kulipwa miongoni mwa hatua tulizochukua ili sekta hii iendelee kukuza ajira ni kusimamia haki miliki ya wasanii. Na napenda kuwaarifu wasanii kuwa kuwa mwaka huu Desemba 2021 wasanii wataanza kulipwa mirahaba ya kazi zao zinapotumiwa na redio, televisheni na mitandao.

Na katika Michezo tumeanzisha mfuko wa maendeleo ya michezo ili kuvisaidia au kuziandaa timu zetu za taifa na pia kama mlivyosikia kwenye bajeti ijayo tumefuta kodi ya nyasi bandia ili viwanja viweze kuwekwa nyasi bandia. Na pia niseme na chama changu cha mapinduzi viwanja vingi vinamilikiwa na chama cha mapinduzi ila hali yake hairidhishi, tafute program ya kuviboresha viwanja hivyo na kama hamna uwezo tafuteni namna na pia kila anaye tumia viwanja hivyo alaipe pesa inayostahili.

  • Elimu na ukosefu wa ujuzi
Serikalai imechukua hatua mbali mbali, tumehakikisha kila mtoto anaezaliwa Tanzania apate elimu hadi kidato cha nne na hiyo ndio tunaita elimu ya lazima, tumejiongeza kwa kuongeza sekondari na ili kijana anaetoka sekondari aweze kuingia kwenye sekondari za juu na wakitoka hapo tumetunisha mfuko wa mikopo mwaka hadi mwaka ili vijana waweze kuingia vyuo vikuu.

Kuhusu ujuzi tumeanzisha vyuo mbalimbali vyaufundi na umahiri ili vijana waweze kupata ujuzi. Kuanzishwa kwa vyuo vya umahiri ikiwemo na chuo cha teknolojia Dar, chuo cha umahiri Mwanza kitabobea kwenye ngozi na chuo Cha Arusha kitaboboa kwenye mambo ya anga. Pia kwenye mabo ya sanaa na michezo chuo cha Bagamoyo kitapewa hadhi stahiki. Pia waziri wa michezo waanze kufikiria kujenga academy za michezo mikoni.

  • Ukosefu wa mitaji
Kukosa vigezo za kuweza kupata mikopo kwenye taasisi za fedha, kukosa taarifa ya wapi wanaweza kupata mikopo na vijana wenyewe kushindwa kutumia fursa zilizopo. Serikali imeanzisha mfuko wa maendelea ya vijana, mikopo kwa vijana kupitia serikali kuu ni moja ya hatua zilizochukuliwa. Tutaanzisha bank ya wajasiriamali na vyuo vya veta.

Kutenga maeneo ya kuweka wajasiriamali wadogowadogo ili wajasiriamali waende wakafanye biashara zao kule bila kubughudhiwa.

Niliona Morogoro watu wametengewa maeneo mbali wakafanyie biashara zao na kwa sababu hawauzi wakarudi maeneo ya awali na baada ya hapo miga,mbo wakawapiga kuwafukuza na kuharibu bidhaa zao. Niseme tu kuwa tukio lile lilinisikitisha na kuniudhi sana na niseme tu kuwa mkurugrnzi na mkuu wa wilaya ya eneo lile hawana kazi kwakuwa kulikuwa na njia nyingine ya kufanya na sio vile.

Vitambulisho vya ujasiliamali vinatakiwa kufanyiwa marekebosho, ili viwe na taarifa ya mjasiriamali na aweze kufanya kazi zake bila bughudha. Pia mnatumika vibaya na wenye maduka kwa kupewa bidhaa na wenye maduka ili muwauzie na wao kukwepa kodi hivyo mnaturudisha nyumba kwenye kufanya maendeleo, sitarajii tena mtumike vibaya. Lakini hatutarajii muendelee kuwa wajasiriamali wadogo tunataka kuweka mpango wa kuwatambua na mkue kutoa wadogo wa kati na wakubwa.

Vijana tunaomba mjitambue kuwa nyiyi vijana ndio wenye maoni ya taifa hili kwa sasa na vijana na karibu wateuliwa wote ni vijana na kuna mkeka wa maDC utakaotoka hivi karibuni nataka kuwaambia kuwa wote ni vijana lakini vijana baadhi mnapopata fursa hizi mnatuangusha napenda kuwaambia kuwa mkipata fursa hizi mkafanye kama ilivyotarajiwa.

Vijana waliopata nafasi wajiulize je wana ufanisi wa kutosha, wana uzalendo wa kutosha na mambo kama hayo nakumbuka hayati Magufuli alisema kuwa hawa vijana wa 80 wananiendesha sana na zile tumbua tumbua zote ni vijana wa 80 ila bado kuna vijana wa 80 wanafanya vizuri. Nakumbushwa kuwa kunamkeka wa wakurugenzi bado haujatoka.

Kama vijana mnakutana wapi kuweka ajenda za taifa bila kujali itikadi ? Muweze kuongea bila itikadi zenu na hii inanikumbusha jambo alilosema bintiyangu juu ya jukwaa la vijana. Na hii tutakwenda kuwaandalia jukwaa la vijana tutajadili kwa nini halikuanzishwa shida nini na nk likianzishwa muweke ajenda za kitaifa.

Rais Samia Suluhu Hassan amesema "Vijana mnatumia Mitandao vibaya, kama una mawazo toa mapendekezo sio kulaumu, kushutumu haina faida. Tumieni Mitandao vizuri”

Ameongeza "Kama una jambo la kulaumu, laumu na toa ushauri, kama unakosoa kosoa na toa mapendekezo nini kifanyike. Amewataka Vijana kushirikiana, akisema wakati mwingine malengo hayafikiwi kwasababu kila mmoja kazi anafanya peke yake.

Asema ushirikiano ukiwepo itakuwa rahisi hata kwa Serikali kuwasaidia na kuwawezesha
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewataka Vijana kushirikiana, akisema wakati mwingine malengo hayafikiwi kwasababu kila mmoja kazi anafanya peke yake.

Asema ushirikiano ukiwepo itakuwa rahisi hata kwa Serikali kuwasaidia na kuwawezesha, amewataka Vijana kushirikiana, akisema wakati mwingine malengo hayafikiwi kwasababu kila mmoja kazi anafanya peke yake. Asema ushirikiano ukiwepo itakuwa rahisi hata kwa Serikali kuwasaidia na kuwawezesha.

======

Uzinduzi wa Chelezo( meli mbili zilizokarabatiwa) na uwekaji saini wa mikataba mitano ya ujenzi meli

Lakini nduguzangu leo tena tumeshuhudia uwekaji wa kuweka saini mikata ya kujenga meli tano na moja itakwenda kufanya kazi bahari ya hindi na hii ni kuendelea kuenzi kazi za Hayati Magufuli na dhamira yeti ni kuendelea kuifanya Mwanza kuwa kituo kikubwa cha biashara kati ya nchi za maziwa makuu.

Na ndio maana tunajitahidi kujenga bandari , meli, reli, barabara na pia kujenga kiwanja kikubwa cha ndege, Mwazna Mungu ameiweka sehemu nzuri na inazalisha mazao ya kibiashara kama pamba pia chakula mazao ya ziwani hivyo ndio maana serikali ina dhamira na Mwanza.

Serikali kuiwezesha Mwanza kimtandao ili biashara ziweze kufanyanyika kimtandao na wataokaokuja kukaa Mwanza waweze kuja kufanya biashara kimtandao.

Nishukuru sana wafanyakazi wa bandari na wafanyakazi wa meli na makontrakta na wale wote tuliowekekeana sahihi nasi kama serikali tutaisimamia vyema miradi. Na pia meli hizi zitunzwe na wote wanaohusika ili ziweze kukuza uchumi wetu.
 

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
4,904
5,532
Kinachonisikitisha Kwenye Ziara za Mh SSH Vyomho vya Habari vimemsusaa Sana, Kupata Taarifa na Kuona Live Inakuaa ni Ngumu Sana.
 

mikedean

JF-Expert Member
Mar 15, 2018
3,194
4,478
Sio kwamba vimemsusa bali havilazimishwi kama zamani...

Nasubiria siku mama atakapoamua kuongea na wanaume wa Tanzania, nami nijivinjari kiwanjani nikademke na mama....
Shikamoo mzee, mi nilijua wewe ni kijana mwenzetu(wa kiume). Kumbe ni mzee
 

kipara kipya

JF-Expert Member
May 2, 2016
10,609
10,855
Safi ni vyema kuwatia matumaini vijana kuwajengea uwezo wa kujiajiri kuliko kutumika kama mtaji wa wanasiasa wahuni!
 

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
19,618
33,772
Hatimaye show imejeuka ya Wasafi tuna safari ndefu
Baada ya hapo utaambiwa, tumeteua vijana kwenye vyombo vya maamuzi na tutaendelea kuwateua ili kuhakikisha tunakuwa na serikali shirikishi.

Mkitoka hapo mnapiga miayo ya njaa jua kalii, mnapitia Kandoro ya 100 kupoza koo huku mkielekea nyumbani🤣
 

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,921
3,220
Baadhi ya Sera/Sheria mbovu za nchi ni kuwanyang’anya vijana uwezo.

Hapa naongelea vijana kuminywa kwa kuporwa haki zao, kunyimwa haki na kupuuzwa (hawasikilizwi). Naanza kwa Kuongezeka kwa Deni la Taifa na Propaganda mfu za Serikali, zenye lengo la kuhadaa umma ili kubaki madarakani tu. Serikali ya AWAMU YA 5 ilitamka kuwa inajenga miradi mikubwa kwa FEDHA za ndani. Asilimia kubwa ya Watanzania waliamini na kushangilia, na wale wachache wenye uelewa hawakupewa nafasi ya kuhoji. Imekuja kujulikana kuwa, FEDHA za Mifuko ya Jamii zilichukuliwa na Wafanyakazi wakaporwa haki zao za kulipwa FAO LA KUJITOA na kuchelewesha malipo ya Wastaafu.

Vijana wasomi, waliosoma sayansi na wenye ujuzi wameajiriwa kwenye Makampuni, Mashirika na Viwanda. Hizi ni talent, na hazina za wasomi kwa nchi, na walivyoajiriwa kwenye haya Makampuni na Viwanda, wamepata fursa ya kuongeza utaalamu na uzoefu. Hii ndio Econonomic interelligency ambayo Serikali ilipaswa kutumia ili kunyanyua uchumi wa nnchi through Innovation.

Ajira na mikataba za hawa vijana (wenye utaalamu na uzoefu-Innovation) zilivyokoma, Serikali iliwanyima Akiba zao (PESA za NSSF). Kumbuka Serikali ilifuta fao la kujitoa mwaka 2018 na kuweka Fao la kukosa ajira. Watu wote skilled labour (wataalamu hawa), hawapewi akiba yao, Haki imepotea. Hawa watu wangelipwa fedha zao, wangeweza kujiajiri kwa kufungua makampuni, kujenga viwanda vidogo. Badala yake hawa skilled labour wanaambiwa wasubiri miezi 18 na kama hawataajiriwa, wakae hadi 55 years wastaafu.

Serikali ilitumia pesa za mifuko ya jamii (Kukopa au kupora kienyeji) ili kujenga miradi. Hapo awali serikali imesema inajenga miradi kwa pesa za ndani (propaganda)..Lakini ukweli wenyewe ni kupora haki za wafanyakazi vijana na mafao wastaafu. Pia Serikali ilikopa sana Nje na kwenye mabenki, ndio maana deni la taifa limepaa sana.

Serikali inapaswa kuwapa wafanyakazi akiba zao ili waweze kutumia skill zao na uzoefu waliopata katika makampuni/viwanda ili kufungua biashara mpya. Hii ndio namna ya kutanua wigo wa Kodi (MWugulu NCHEMBA TRA). Mitaji itatoka wapi ya biashara mpya kwa wazawa kama mikopo benki sio rafiki? Suluhisho ni Serikali kurejesha FAO LA KUJITOA NSSF na kulipa wafayakazi akiba zao kwa Haki.

Serikali inatakiwa kuwezesha vijana, kutoa International passport kwa graduate wote, ili wapambane fursa za ajira kokote duniani. Baadae watakuwa diapora kubwa inayotuma pesa Tanzania, kama ilivyo Zimbabwe, Kenya na India walivyoenda wengi Canada na UK. Serikali kurejesha Fao la Kujitoa, Hasa kwa Sekta binafsi, kwa kuzingatia kuwa Sekta binafsi Security ya ajira ni delicate sana.
 

Shehullohi

JF-Expert Member
Jul 21, 2020
3,467
3,172
Ndio wamejazana hapo na barakoa zai ila no social distancing. Barakoa bila ya social distancing wakati zote ninmbinu zinazotegemea. Acha Mungu wa Mbinguni aendelea kuwapiga upofu na kuwanyanganya kibali chake tuone huyo Mzungu wanayecmfurahisha na kumtegemea kama atachukua nafasi ya Mungu.
 

Bejamini Netanyahu

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
65,783
70,101
Baadhi ya Sera/Sheria mbovu za nchi ni kuwanyang’anya vijana uwezo.

Hapa naongelea vijana kuminywa kwa kuporwa haki zao, kunyimwa haki na kupuuzwa (hawasikilizwi). Naanza kwa Kuongezeka kwa Deni la Taifa na Propaganda mfu za Serikali, zenye lengo la kuhadaa umma ili kubaki madarakani tu...
CCM haitaki mtu ambaye ana akili timamu anaweza kuwaza kama wewe hivi, inataka maboya ya kupiga makofi.
 

kidereko

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
884
1,244
Ndio wamejazana hapo na barakoa zai ila no social distancing. Barakoa bila ya social distancing wakati zote ninmbinu zinazotegemea. Acha Mungu wa Mbinguni aendelea kuwapiga upofu na kuwanyanganya kibali chake tuone huyo Mzungu wanayecmfurahisha na kumtegemea kama atachukua nafasi ya Mungu.
Dikteta alijifanya kuipuuza Covid19, alijua anawakomoa mabeberu, kumbe anachezea uhai wake,

Kilichompata kila mtu ashajifunza,ukitaka kujua dikteta nini kimemuua, jibu ni ilo namna wenzie walivyo makini kuchukua tahadhali ya Covid19
 

Bejamini Netanyahu

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
65,783
70,101
Baada ya hapo utaambiwa, tumeteua vijana kwenye vyombo vya maamuzi na tutaendelea kuwateua ili kuhakikisha tunakuwa na serikali shirikishi.

Mkitoka hapo mnapiga miayo ya njaa jua kalii, mnapitia Kandoro ya 100 kupoza koo huku mkielekea nyumbani🤣
Hatari sn
 

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
49,999
36,333
Sio kwamba vimemsusa bali havilazimishwi kama zamani...

Nasubiria siku mama atakapoamua kuongea na wanaume wa Tanzania, nami nijivinjari kiwanjani nikademke na mama....
uko bandarini mlikuwa mnalzimishwa nini kipindi cha mwendazake?
 
4 Reactions
Reply
Top Bottom