Mwanza: Rais Samia aongea na Vijana wa Tanzania katika Uwanja wa Michezo wa Nyamagana

Nasema ivii Mimi Goguryeo nisipopata hii, basi kuna mkono wa mtu hii nchi..
 
Mmmh!

wakishamaliza Bank kwa misingi ya jinsia wataanza bank ya makundi mbalimbali sasa, mfano, Bank ya Boda boda, bank ya wachomeleaji, bank ya wafanyakazi migodini, bank ya wanafunzi wa vyuo vikuu, bank ya wastaafu nk. mwisho tutajikuta mtu mmoja kakopa mabank zaidi ya 5
 
Hii imekaa sawa ila shida sio bank shida ni masharti ya vijana kukopa
Yaani wanasiasa wanacheza sana na akili zetu. Katika financial institutions hakuna kitu benki ya fulani! Benki inatakiwa ifanye kazi kifuata banking principles and rules. Benki ya wanawake iko wapi?

Nyerere alianzisha benki ya ushirika iko wapi? Ilikuwa Tanzania Rural Development Bank baadaye Cooperative and Rural Development Bank na mwishowe ikabinafsishwa tu ndiyo hiyo CRDB.

Hawajifunzi tu. Juzi kati tu hiyo ya wanawake imefeli ndiyo ya vijana itafaulu? Yaani wanacheza na akili zetu sana hawa!!!!
 
..WHY?

..tutaanzisha benki kwa ajili ya kila kundi ktk jamii?

..kwanini tusitatue changamoto zinazopelekea vijana kukosa mikopo toka ktk mabenki yaliyoko sasa hivi?

It really does not make sense. Hatujajifunza tuu kutoka kwa benki yetu ya wakulima? Benki kama hizi haziwezi kufanikiwa hata siku moja. Benki ya Ushirika imefaikiwa tu baada ya kuingiza private sector.

Mimi sidhani ni lazima awe na majibu pale pale kwa changamoto zote. Angetoa tu ahadi ya kuangalia kwa undani hizo changamoto na kutafuta njia ya kuyatatua kwa kushirikiana na wataalam.

Haya majibu mepesi kwa maswali magumu ndio yaliyo tufikisha hapa. hatuna watalii kwa hiyo tutanunua ndege ziende kuwabeba waje! Hatujaridhika na bei ya korosho basi tutaagwana wenyewe tuzile. Tuna upungufu wa nishati, tutajenga bwawa letu bila hata kufanya EIA.


Amandla...
 
vijana wa CCM sasa hivi ni vikumbo vitupu!!
Naangalia kwa mbali naona upepo ukiwaendea vizuri sana waganga wa jadi, wasafisha nyota, Waombezi kwenye makanisa, Manabii na wahubiri, watabiri na wanajimu. Hakika vikumbo vitakuwa vingi sana. Stay tuned!
 
Daaah!!!!! Yaani Imebaki Kuteuliwa tuuuu...Professional zenu mlizosomea mmeamua kuziacha zipotee
 
Tanzania hatuna bank ya wanawake kwa sasa.

Ila sawa tu hata CRDB ilianzishwa kuhudumia vijijini lakini IPO mijini tu. Acha atengeneze ajira na ulaji kwa watu
 
Mama ana Maono ya mbali kuliko yule Ibilisi
Acha ujinga wewe. Huwezi kuongea bila kukashifu marehemu? wewe umeona kawaza mbali sana hujui kuwa zinaweza zikawa ngonjera? Taifa la watu mazo....bi mnapenda kusikia maneno ya kuwafurahisha hamtaki ukweli.
 
Back
Top Bottom