sioni tatizo mwanaume kuoika, awe bachela au ameoa. Kwanza bachela unatumia hala nyingi kula magengeni kuliko ukipika mwenyewe.
Hata aliyeoa ukipika au ukishirikiana na mkeo kupika huongeza mahaba sana...... Huzidisha ukaribu wenu.. Hivi ushajiuliza mkeo akiumwa ghafla? Nani atapika? Imagine hapo hana dada wa kazi?
Ila kutopika kwa wanaume wengi hutokana na baadhi ya watu kuwaona 'siyo' ingawa watu hao usshangae kukuta wanapika wakiwa na wake zao.
Ingawa makuzi yanachangia, nikupe mfano wangu, mimi baba yangu ni mfanyabiashara, mama mfanyakazi, kipindi tupo wadogo kuna wakayi hztukuwa na dada wa kazi, mama aliomba ruhusa wakamruhusu kutoka saa sita, (kipindi hicho mdogo wetu wa mwisho alikuwa na miezi kama kumi hivi), sasa mama akienda kazini asubuhi anaakikisha kila kitu kipo sawa, tunakunywz chai mimi na kaka zangu twaenda shule, tunamuacha baba na mtoto, tukirudi tunakuta babs keshatupikia, mtoto kala, maama akirudi baba ndo anaingia mihangaikoni, hii ilichukua takriban siku kadhaa(sikumbuki ngapi)
sasa imagine baba hawezi/hataki kupika kutokana na jamii inavyotazama swala hilo si tungekula ma.vi magengeni? What about kichanga? Nani angekiangalia? Au ingemlazimu mama kuacha kazi?
Wanaume pikeni halafu nyie ndo wapishi wazuri, chakula apikacho mwanaume kizuri sana. Who cares watu watachukuliaje?aaaaarrrrgh