Mwanaume mtaalamu jikoni

ha ha ha
i know
maana nimemuimagine dc kabeba viboko kwenye pikipiki yake kama mzigo wa kuni
akija kukuchapa
ikabidi nikutetee
Thanks, the message was directed to Dc as he promised kwamba wanaume wanaopika wanatakiwa watandikwe bakora
 
hehehe Kongosho siongelei kuishi ulaya au nje ya Tanzania, naongelea mazingira. Kuna sehem unakuwa hauna mjomba wala shangazi na hakuna mama ntilie ya kuponea kwa bei za kizembe plus majukumu kibao sasa mida imefika wewe utasubiri waifu arejee akupikie? Hao wazungu wengi wao wamesukumwa na mazingira kama sisi tulivyosukumwa na mazingira.
pal, its a clash of civilization/culture or even understanding and beliefs... iit is also becoming a "clash in terms of uelewa na misimamo", kupika ni kitu ingine, ni art ya pekee
 
pal, its a clash of civilization/culture or even understanding and beliefs... iit is also becoming a "clash in terms of uelewa na misimamo", kupika ni kitu ingine, ni art ya pekee
Not to forget ni ajira pia, Si unampata Jamie Oliver (dume flani) "The naked chef" mzembe anakusanya hela mbaya sana samtaim anapata mwaliko wa kumpikia mpaka queen.
 
@xpaster
on every rule/principle kuna exceptions
sometimes we call them limitations

mwanamme kupewa lidandansi na kubaki home ni sawa
na hutokea
lakini ndani ya time t
anatakiwa awe amepata suluhisho
apate kitu kingine cha kufanya

hivi ukiwa ceo, na kampuni ikakumbwa misukosuko utaiacha ife eti sababu yalitokea matatizo?
Ni wajibu wako kuiokoa na kuhakikisha inasavaivu
same aplies kwa baba wa familia
lazima awe kichwa cha familia
hasa kwenye kuresolve matatizo

Mkuu Kongosho, hapa kuna mambo matatu, aidha sikuelewi, au mimi unielewi au namba tatu hatuelewani kiswahili.

Hivi ni watu wangapi leo hii wamepata kuachishwa kazi na hawana jinsi ya kuajiriwa au kujiajiri, mkuu ni muhimu sana kuishi kulingana na mazingira yako na vile wewe unaona kuwa ndio sahihi bila ya kumkwaza mwenza wako... Siwezi kushangaa kumkuta mwanamume ambaye hana kazi, akimsubiri mke wake arudi kazini aje apike ili wale yeye na watoto, hayo ni maamuzi yao.

Ndio maana kama umenisoma hapo juu, nilipoanza kuchangia nilisema si mbaya kama mtaamua kuishi kwa kufuata mila na desturi za kikabila, kwa sababu ndizo desturi zilizo athiri tabia na mienendo yetu, na nikasisitiza kuwa haya mambo ya kifamilia ni vile wewe na mke wako mtakavyo amua kuyaendesha maisha yenu, hakuna wa kuwacheka au kuwaona mnaishi maisha ya kijima eti tu umemwachsha mkeo kazi ili alee watoto nyumbani, hayo ni maamuzi yenu kwa kuona ni vyema watoto wakakuwa kwa malezi ya mama akiwa nyumbani badala ya kumtumia mfanyakazi wa ndani, tena ambaye hujui malezi yake uko atokako.

Na ikitokea kuwa huna kazi na huna jinsi, si vibaya kusaidia kazi za nyumbani zikiwemo zamu za kufagia uwani, bafuni na chooni kwa wale wanao ishi nyumba za kupanga... (Usitowe macho... ah ah ah ah).

Kwa ufupi taratibu za kimaisha, ni jinsi wewe na mwenzako mtakavyo ona inafaa jinsi ya kuyaendesha...!
 
sioni tatizo mwanaume kuoika, awe bachela au ameoa. Kwanza bachela unatumia hala nyingi kula magengeni kuliko ukipika mwenyewe.

Hata aliyeoa ukipika au ukishirikiana na mkeo kupika huongeza mahaba sana...... Huzidisha ukaribu wenu.. Hivi ushajiuliza mkeo akiumwa ghafla? Nani atapika? Imagine hapo hana dada wa kazi?

Ila kutopika kwa wanaume wengi hutokana na baadhi ya watu kuwaona 'siyo' ingawa watu hao usshangae kukuta wanapika wakiwa na wake zao.

Ingawa makuzi yanachangia, nikupe mfano wangu, mimi baba yangu ni mfanyabiashara, mama mfanyakazi, kipindi tupo wadogo kuna wakayi hztukuwa na dada wa kazi, mama aliomba ruhusa wakamruhusu kutoka saa sita, (kipindi hicho mdogo wetu wa mwisho alikuwa na miezi kama kumi hivi), sasa mama akienda kazini asubuhi anaakikisha kila kitu kipo sawa, tunakunywz chai mimi na kaka zangu twaenda shule, tunamuacha baba na mtoto, tukirudi tunakuta babs keshatupikia, mtoto kala, maama akirudi baba ndo anaingia mihangaikoni, hii ilichukua takriban siku kadhaa(sikumbuki ngapi)
sasa imagine baba hawezi/hataki kupika kutokana na jamii inavyotazama swala hilo si tungekula ma.vi magengeni? What about kichanga? Nani angekiangalia? Au ingemlazimu mama kuacha kazi?

Wanaume pikeni halafu nyie ndo wapishi wazuri, chakula apikacho mwanaume kizuri sana. Who cares watu watachukuliaje?aaaaarrrrgh
 
Nimetoka kukorofisha kiti moto na sasa hivi najichana hapa na lemonade yangu bariiiidi iko pembeni.

Binafsi sina tatizo kabisa na kupika na uanaume wangu hauwi defined na kupika au kufanya kazi zingine za ndani ya nyumba, iwe nina mke au la!
 
Not to forget ni ajira pia, Si unampata Jamie Oliver (dume flani) "The naked chef" mzembe anakusanya hela mbaya sana samtaim anapata mwaliko wa kumpikia mpaka queen.

Kuna huyu Wolfgang Puck

Wolfgang Johannes Puck (born Wolfgang Johannes Topfschnig; July 8, 1949) is an Austrian-American celebrity chef, restaurateur, businessman and occasional actor. Wolfgang Puck restaurants, catering services, cookbooks and licensed products are run by Wolfgang Puck Companies, with three divisions. He has been titled as "The Greatest Chef In The World"

Source:Wolfgang Puck - Wikipedia, the free encyclopedia

Na hii hapa ndo tovuti yake Official site of Wolfgang Puck with news, recipes, catering details, products information, and fine dining reservations
 
...aisee wewe ropoka tu bana, usijali kuitwa majina...halafu hii tabia ya kujitegemea kila kitu ndiyo inayoinizidisha na kiburi cha kutotafuta msaidizi wa maisha....
labda siku nikitamani chapati, kidogoo nalegeza kamba ya nani atanifaa...Oopss

MTM fagilia sana hizo service apartments kamanda, hats off bro...tangu nigundue raha zake
sifagilii tena mambo ya vyumba.


....Wakuu Mbu, MTM Kloroquin hongereni sana kwa kujua kukaangiza ndani ya jiko. Haya mawazo ya kwamba mume/mwanaume akiingia jikoni basi kuna walakini, ni maneno yaliyopitwa na wakati, we kama unajua kukorofisha msosi basi wala usione aibu kufanya hivyo eti kwa kuogopa kwamba dada, kaka, wakwe, majirani, marafiki, wajomba, mashangazi, wazazi n.k. wataanza kuulizana huyu ni aje? Mbona anaingia jikoni? kishalishwa vya kulishwa? Tena wakati mwingine unaweza kukuta msosi wako ni mtamu mno kuliko ule unaopikwa na mwenzio na hata yeye anajua hivyo.

Inasikitisha sana kuona tuko 2011 bado kuna watu wana mawazo ya mwaka 47 kwamba mwanaume hastahili kabisa kuingia jikoni!!!! Akifanya hivyo basi kuna hitilafu tena kubwa sana ya aina moja au nyingine!!! :shock:....Lizzy ahsante sana kwa huu uzi.

 
Tunajadili suala jepesi mno kimtazamo lakini linauzito mkubwa kiutamaduni.

Kuingia jikoni kupika kwa mwanaume kimtazamo ni rahisi tu na haimletei tabu kwa wale ambao ni waelewa(wanaosimamia nyajibu zao), Katika upande mwingine ni mtihani mkubwa sana kwa mwanaume kuingia jikon tunapoangalia tamaduni zetu.Kwa asili ya utamaduni wetu unamubagua mwanaume kushiriki kazi za jikon moja kwa moja hali hii inaletwa na mgawanyo wa kazi katika jamii(division of labour and specialization). Katika hali hiyo mwanaume atafanya kazzi za jikoni anapokuwa hajaoa akishao atasita kuwajibika kwa sababu atakuwa na wa kuzifanya shughuli husika. Kwa kifupi hapa ni kufahamu nn asili ya jambo hili.
 
Kuhusu jina gani litumike kuwaita wanaoingia jikoni inategemea lkn majina kwa kawaida huwa hayana maana mfano, zoba ,***** n.k. Hii ni lebeling tu ambayo haina uhusiano wa moja kwa moja na kitajwa japo katika mazingira fulani fulani yana reflection. Mimi sipendekezi jinz lolote la kuwaita.
 
Binafsi nipo too selective linapokuja suala la chakula na ndio maana nikapenda kupika....sioni kama ni jambo la ajabu kwa mwanaume kupika....
Na kumpika is a such a romantic idea....
I cook n i cook a lot...
 
Bora hata ambaye hajaona anaweza kusema anasevi kost kupika yeye mwenye japo na yeye si aoe sasa anasubiri nini kuoa

ila manamme aliyeoa kupika duh????
Basi tusimshangae Vasco dagama wetu kutembea dunia nzima wakati anaweza hata kutuma katibu tarafa kuwakilisha na yeye kubaki home akifanya mambo ya msingi kwa taifa.
Anaweza kuwa kusafiri ni hobby regardless anapoteza muda kiasi gani wa kufanya mambo mengine ya msingi

mgawanyo wa majukumu upo tu
 
Bora hata ambaye hajaona anaweza kusema anasevi kost kupika yeye mwenye japo na yeye si aoe sasa anasubiri nini kuoa

ila manamme aliyeoa kupika duh????
Basi tusimshangae Vasco dagama wetu kutembea dunia nzima wakati anaweza hata kutuma katibu tarafa kuwakilisha na yeye kubaki home akifanya mambo ya msingi kwa taifa.
Anaweza kuwa kusafiri ni hobby regardless anapoteza muda kiasi gani wa kufanya mambo mengine ya msingi

mgawanyo wa majukumu upo tu
 
Binafsi nipo too selective linapokuja suala la chakula na ndio maana nikapenda kupika....sioni kama ni jambo la ajabu kwa mwanaume kupika....
Na kumpika is a such a romantic idea....
I cook n i cook a lot...


"...Nakuona umechoka sana leo, basi kaoge tu upumzike wakati nakorofisha msosi huku jikoni, nikimaliza nami nitaenda kuoga halafu tuje tujichane." Kwa wengine hili si jambo la ajabu kabisa.
 
Lizzy,

Believe it or not hakuna mwanaume *****. Ni watu wanajidanganya tu. Bottom line, huyo mwanaume anayeonekana ***** ana mambo ya ajabu ambayo mkewe akisikia anaweza kufa na pressure. Mbele ya mkewe anakuwa *****. Ndio maana hawa wanaume wanapofariki, kunakwua na mambo ya ajabu sana. mwanume aliyekuwa anaonekana ***** na mwanamke kujisifia amemtawala, ustangaa siku ya msiba wake watoto wa mitaani wanavyoletwa, na ukiangalia ni photocpy...

Hakuna mwanaume ***** hata mmoja.....
 
Mimi huwa napika,nna nnainjoy kumpikia mupenzi wangu.Mwanamke sio mashine ya kufanya kazi tu.Mtunze akutunze ,tuachane na mfumo dume wajameni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom