Mwanaume mtaalamu jikoni

Mwanaume mtaalamu jikoni

Hivi kuoa na kuolewa ni LAZIMA eeeeh?
Ni lazima ndiyo! Yaani kuuliza swali hili ni kama kuuliza " Vumbi stoo ! " hivi unafahamu biologically binadamu awe wa kike ambae yuko below 50 aged na still yet hv menstruation circle (yale mambo ya NASA) Na Mwanaume below 80 wakikaa 56 days w/out ejaculation wanapata side effects ? That effects e.g Kuchekacheka hovyo bila sababu maalumu imchekeshayo! Au kununa bila sababu. e.c.t
 
hobby za kike ni za kike tu
iwe kusuka, kuvaa hereni,

kike ni kike na kiume ni kiume tu

....usibadilishe somo haina maana mtu kama haoni tatizo la Mwanaume kuingia jikoni basi pia hataona tatizo la Ushoga. Hayo ni mambo ambayo hayana uhusiano wowote na wala hayawezi kuwa na uhusiano hata siku moja.
 
hobby za kike ni za kike tu
iwe kusuka, kuvaa hereni,

kike ni kike na kiume ni kiume tu


hahahahahah lol! na kula nayo ni hobby ya Wanaume au Wanawake!? Dah! achana na mawazo yaliyopitwa na wakati!!!! Eti njemba iogope kuingia jikoni kwa sababu ni hobby ya Wanawake!!!! lol!...
 
kuna swali nimekuuliza hujanijibu
aliyekuambia wewe unavaa suruali ni nani?

Tunakula wote anapika mwanamke
tunakuwa wazazi wote anazaa mwanamke
tunaishi wote anayejenga nyumba mwanamme

kama kuna misfit ndipo gender nyingine inachukua jukumu la mwenzie


hahahahahah lol! na kula nayo ni hobby ya Wanaume au Wanawake!? Dah! achana na mawazo yaliyopitwa na wakati!!!! Eti njemba iogope kuingia jikoni kmwa sababu ni hobby ya Wanawake!!!! lol!...
 
Unajua mstaafu, mimi katika huu mjadala nadhani pande zote mbili wako right as far as tradition na mazingira is concerned plus mtu binafsi mwenyewe anavyolichukulia hili suala. Tukubali au tukatae jamii inayotuzunguka ina athari kubwa katika lifestyle yetu ingawa this doesn't mean kwamba msimamo wa jamii uko right (hapa ndipo inapoingia mantiki yangu ya clash of civilisation)

Maisha ya nyumbani Afrika: Ni kweli ni ngumu kuingia jikoni kwa mwanamme kwa maisha ya nyumbani yalivyo hii ni kutokana na high social interaction iliopo afrika tafauti na kwa wenzetu, Mara nyingi kiafrika haichukuliwi kwamba jiko ni sehemu ya kupikia tu lakini pia mara nyingi inachukuliwa ni sehemu ya kijiwe cha kupigia soga kwa kinamama. Majirani wa kike, ndugu wa kike n.k wote wakifika nyumbani wanaweka kambi jikoni. Mazingira haya yanaweka ugumu kwa mwanaume kukaa jikoni na pia yanampatia picha mbaya kwa wageni wa kike ambao wanalichukulia eneo hilo ni kama eneo la kupeana michapo ya kimbea ya mitaani.

Maisha ya kwa wakoloni wetu: Hawa jamaa life system yao ni very poor kwenye social interaction, kuonana yao labda pub weekend na kwenye special ocassion kama krismass e.t.c. Sasa unakuta they are free to govern their house the way they want it na hakuna interference na watu wa nje, plus ni njia moja kwao kuonesha how much they care kwa wenza wao not to forget hawa jamaa wako serious kwenye uwajibikaji wa kusimamia maisha yao ya kila siku sasa unakuta mama na baba wote wanapindwa vibaya tena pengine swing shift, sasa hapo mstaafu ukisema usubiri jamaa arudi kipindo ndio upikiwe hehehe labda usubirie katiba mpya.

Sasa hapa mimi naendelea kusema tena tu mtabishana mpaka alfajiri lakini madamu ni swala la imani na utamaduni basi nakuhakikishieni hamtofikia muafaka
Mkuu, kijuujuu ninakubaliana na mawazo yako kwani huu ndio ukweli.
Cha ajabu, tuangalie kwenye malezi ya Kiafrika na ya "Wakoloni wetu".
Afrika: Watoto mara nyingi huwa wanashiriki kikamilifu katika mgawano wa kazi na inapobidi hata mvulana anaingia jikoni kuwapikia wadogo zake ikiwa wazazi wamedharurika. Lakini kijana huyu huyu, akiwa mjane kujipikia mwenyewe ni "uhitaji". Siku akioa tu akiingia jikoni atasemwa majina yote yliyokwisha tajwa.

Kwa wakoloni wetu: Mtoto ana haki, na haki zake ni pamoja na kutowahesshimu wazazi, seuze kufanyakazi za nyumba. Kuna baadhi ya wazazi (mama zao) wanalipalilia hili. Niliwahi kumsikia mama akisema "mwanawe mwanamume hatandiki hata kitanda kwani yeye si cameroun". Lakini mvulana huyu huyu akishakuoa anasaidia kikamilifu katika kazi za nyumba wala haitwi jina lolote.

Mema tuyafate mabaya tuyawache: Hapo nyekundu, hivi kuna ubaya wowote ikiwa hao akina mama waliokuja kupiga umbea (ikiwa unaliruhusu hilo nyumbani mwako) kwa nini wasiende sebuleni wakuwachie jikoni upike? Au umbea haunogi hadi iwe jikoni?
Kwa nini kazi nyengine kama vile kuvalisha nepi, kuwakogesha watoto, kuwabeba wanapolia mume anaruhusiwa? Jikoni kuna nini?
 
kuna swali nimekuuliza hujanijibu
aliyekuambia wewe unavaa suruali ni nani?

Tunakula wote anapika mwanamke
tunakuwa wazazi wote anazaa mwanamke
tunaishi wote anayejenga nyumba mwanamme

kama kuna misfit ndipo gender nyingine inachukua jukumu la mwenzie


....Kwani weye huvai suruali? naona unajaribu kutoka nje ya mada. Mjadala huu hauhusu kuvaa suruali au kutovaa suruali. Wanawake na Wanaume wote wanavaa Suruali. Dunia ya leo hakuna kazi ambayo ni ya Mwanamke tu au Mwanaume tu. Tumeona na kusikia Wanawake ambao ni maengineers, doctors, pilots etc. Hivyo ndani ya mahusiano pia kama wahusika hawaoni tatizo Mwanaume ndani ya nyumba kuingia jikoni basi society ambayo bado iko nyuma sana kwenda na wakati haina haki yoyote ya kushangaashangaa. Hakuna kitabu chochote kile hapa duniani hata vile vitabu vitakatifu vilivyosema kwamba kuingia jikoni au kubadilisha diaper mtoto, kumsafisha na kumlisha ni kazi ambayo Mwanaume hastahili kabisa kuifanya. Fungua macho ujue kwamba tuko 2011 na siyo 1947 huo mgawanyo wa kazi unaotaka kuusema hauko kabisa.

SAYONARA

 
....usibadilishe somo haina maana mtu kama haoni tatizo la Mwanaume kuingia jikoni basi pia hataona tatizo la Ushoga. Hayo ni mambo ambayo hayana uhusiano wowote na wala hayawezi kuwa na uhusiano hata siku moja.

Binafsi nimeshangaa sana hayo mawili kuwekwa pamoja.Sioni wala sitarajii kuona uhusiano kati ya hayo mambo kwakweli.
 
I got a question for you guys,

Katika mazingira yetu ya kibongo bongo bado hakikubaliki sana kwa mwanaume kuingia jikoni na kupika, haswa na wanaume wengine. Akifanya hivyo basi ataitwa majina kibao na yatasemwa mengi juu yake mf.mume bwége,kakaliwa, kalishwa limbwata, sio mwanaume kamili n.k.
Sasa swali langu ni kama hayo hapo juu yanamhusu mwanaume ambae anaishi na mwanamke , vipi yule asieishi na mwanamke(mpenzi/mke)?Pengine anaweza akawa anaishi na ndugu, dada wa kazi au hata mwenyewe.Huyu tumwite nani? Maana kama kukaliwa kakaliwa na nani?Limbwata kapewa na nani?Ubwége kavishwa na nani?Uanaume kavuliwa na nani?

Nadhani ni muda sasa tuanze kukubali wanayofanya wengine na kuwaacha wajihukumu wenyewe.Kama wewe hutaki/huwezi hamna haja ya kumwita anaefanya majina ya ajabu.Baki tu ukishangaa!!

Wee binti, naona unakokwenda sio kwenyewe KIAFRIKA!
 
@bak
mbona wewe huvai gauni?
Nani kakuambia usiave gauni?

Naona imekuwa ngumu sana kuukumbatia mbuyu kwenye hiko swali

Hata mwanamke kuvaa suruali ni umagharibi tu, naye kakumbwa kama walivyokumbwa wanamme na upishi

imeandikwa ' amelaaniwa mwanamke avaaye mavazi ya kiume...'
 
@xpaster
on every rule/principle kuna exceptions
sometimes we call them limitations

mwanamme kupewa lidandansi na kubaki home ni sawa
na hutokea
lakini ndani ya time t
anatakiwa awe amepata suluhisho
apate kitu kingine cha kufanya

hivi ukiwa ceo, na kampuni ikakumbwa misukosuko utaiacha ife eti sababu yalitokea matatizo?
Ni wajibu wako kuiokoa na kuhakikisha inasavaivu
same aplies kwa baba wa familia
lazima awe kichwa cha familia
hasa kwenye kuresolve matatizo
kwani ukipika mwanaume akipika ndio hawi tena kichwa cha familia?
 
ambaye anaingia jikoni akiwa hajaoa huitwa h.a.n.i.t.h.i, kwa nini haoi

hakuna exkuzi ya mwanamme kuingia jikoni

Maana ya hanith.i ni mtu ambaye hapigi Machine (Machine yake kwishney),sasa inamaana watu wote ambao hawajaoa hawapigi machine!!!!!Mbona we Dada unatoka nje ya Uzi sasa
 
kwani ukipika mwanaume akipika ndio hawi tena kichwa cha familia?

Kichwa cha familia atapikaje bana,ni sawa na rais wa nchi afanye kazi ya sekretari wake!
 
Sasa chakusikitisha hapo ni kipi?
No wonder hata watoto hawajui ukaribu wa baba zao kisa majirani watasema.

mi
mi naona ni ushamba na hao wanaopika hotelini na wanafamilia zao kwahiyo hotel imewalisha limbwata? wacheni mifumo dume akiugua mkeo huwezi kupika sio? ata chai utamuomba jirani akupikie kisa usiitwe -----? NI USHAMBA TUU
 
hobby za kike ni za kike tu
iwe kusuka, kuvaa hereni,

kike ni kike na kiume ni kiume tu
Hahahahahaha Kongosho bana..nimekumiss Konnie, heri ya mwaka mpya.
Judgement ushaoa wewe?! Maana ulisema kuoa/kuolewa ni LAZIMA.
BAK. kongosho siku hizi kabadili mtizamo bana. Alisumbua sana kwenye hii mada.

Heri ya mwaka mpya JFers.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom