@x-paster
anyway partly yes partly no
we mwanamme ubaki home unafanya nini wakati mkeo kaenda kazini?
Kwa nini usiwe wewe umeenda kazini mkeo abaki anapika?
Familia ni taasisi na baba ni ceo
sasa ceo gani anamwachia kaimu majukumu muhimu
angalia Tz, entinty ya juu kabisa kukosa kuwa na msimamo nchi ka inayumba vile hata kama wa chini yake wana msimamo vipi
eti baba yuko jikoni anapika bintizake na mkewe wanatizama TV, duh hizo ni egoli tupu, kwa wanaoishi nje labda mazingira yamewalazimisha kuwa hivo
Mkuu, samahani kidogo maybe niliharakisha kujibu bandiko lako lililopita hapo juu... Dah! Sijui nianze vipi anyway...
Maisha ndugu yana mambo mengi sana, hivi nikuulize mkuu wangu, wewe na wife nyote ni wafanyakazi, kwa bahati ghafi mwanaume umepata ile kitu inaitwa lidandasi, umeondoshwa kazini, kwa ufupi huna kazi ya kuajiriwa, ndio tuseme na wife wako utamwambia awache kazi eti kwa kuwa tu wewe utabakia nyumbani na watoto!?
Wakati mwingine sisi wanaume tunaamua kuishi na fikra za kizimwi, yaani unaishi kwa kujitisha kuwa wewe ndiye wewe, mimi nakubaliana na wewe kuwa mwanaume ndio kichwa cha nyumba na haswa yanapokuja maamuzi mazito ya kifamilia, lakini si vibaya kuishirikisha familia yako kwa hikma na busara pale inapobidi... Mimi nawajuwa baadhi ya watu ambao wanachukuwa mawazo wya wake zao na wakija uku nje mbele ya wanaume wenzao wanasema kuwa lile wazo ni lake yeye baba mwenye nyumba, mimi sioni tatizo kwa ilo... Ndio maana nikasema kuwa haya maisha ya kwenye familia zetu ni nyinyi wenyewe jinsi mtakavyo amua kuyaendesha, mimi sioni kama ni haki kwa watu wanaoishi nje ya familia yako kuingilia vile mlivyojiamulia as long as hayo mambo hayaendi kinyume na haki za msingi za kibinadamu, mimi sioni tatizo...!
Mkiamua kufuata mila na desturi za makabila yenu, yote kheri mkuu, lakini ugomvi ni pale marafiki, ndugu na majirani wanapoanza kutaka kuwapangia jinsi ya kuishi wewe na familia yako, hiyo si sawa, ila kama unataka kuwapendezesha wao, basi si tatizo, kinachotakiwa ni upendo na amani ndani ya nyumba, basi ilo ndio la msingi.