Ndani ya uanaume: Mambo 3 yanayoiongoza akili ya mwanaume

sonofdory

Member
Jul 4, 2016
78
38
Ukimuuliza mwanamke yeyote ni aina gani ya mwanaume anayemhitaji, unaweza kukutana na majibu kama vile, mpole, mcheshi, mwenye uwezo wa kunihudumia na anayenipenda kama ninavyompenda mimi. Wakati haya yote yanaweza kuwa sahihi isipokuwa kigezo cha mwisho hapo juu, namna ambavyo wanaume wanawasilisha upendo kwa wenzi wao ni tofauti na namna ambavyo wanawake wengi hutarajia.

Utofauti huu unaletwa na mambo makuu matatu ambayo kwa kweli yamesimikwa ndani ya vinasaba vya wanaume wote duniani. Kuanzia Ruvuma mpaka Mwanza, Afrika ya Kusini mpaka Tunisia, China mpaka Marekani hata Brazil na Urusi. Kabla mwanaume hajawaza na kutilia maanani mambo yote haya matatu, upendo wake kwa mwenzi wake haujadhihirika kwa asilimia za kuridhisha. Nia ya kutamani kuwa katika mahusiano haiwezi kuwa thabiti, zaidi sana atakuwemo tu kwa sababu anatakiwa kuwemo.

Kama wewe unayesoma hapa ni mwanamke, huu ndio ukweli; mwanaume wako hataweza kukubali kwa moyo mmoja kukuoa, hataweza kukubali kwa moyo mmoja kuwa baba wa watoto wako, hataweza kukubali kwa moyo mmoja kujitambulisha kwa wazazi wako kabla hajawa na uhakika wa mambo haya matatu. Hata kama akionesha upendo wa dhati sana kwako, akili yake hukosa amani kama mambo haya matatu yasipokuwa bayana kwake.

Nisikuchoshe, hebu sasa tuyaangalie mambo yenyewe.

Katika kitabu chake cha "Act Like a Lady, Think Like a Man.", Steve Harvey anayaelezea mambo haya katika mfumo wa maswali. Mwanaume anaishi maisha yake yote akitafuta majibu ya maswali matatu tu; "Yeye ni nani", "anafanya nini" na "Anapata nini kutokana na anachokifanya". Kama majibu ya haya maswali matatu hayajawa bayana akilini mwake, itamchukua muda sana kuishi kwa amani katika uhusiano na mwenzi wake pengine na jamii inayomzunguka. Kibaya zaidi, wapo wanaume ambao wanaamua kabisa wasiingie katika mahusiano bila kupata majibu ya haya maswali matatu.

JAMBO LA KWANZA: YEYE NI NANI?

Nilipokuwa mdogo baba yangu alikuwa na kawaida ya kuniuliza, "Lucky ukiwa mkubwa unataka kuwa nan!?". Majibu niliyoyatoa nadhani unaweza kuyakisia na ukawa sahihi. Watoto wengi wanaokutana na swali kama hili huwa na majibu kama vile rubani, daktari, mwalimu na mengine yanayoeleza namna wanavyotamani kutambuliwa pindi watakapokuwa watu wazima.

Kadiri mtoto anavyozidi kukua ndivyo uzito wa swali hili unavyozidi kuwa kipengele muhimu katika akili ya aliye wa kiume kuliko ilivyo kwa aliye wa kike. Mwanaume hujali zaidi namna atakavyotambulika katika jamii yake. Hujali zaidi namna ambayo mwenzi wake, familia iliyomlea na jamii wanamtambua na kiasi ambacho anajitofautisha na wanaume wengine wa rika lake.

Kama mwanaume hajatengeneza utambulisho anaoutaka yeye, ambao mara nyingi huelekea zaidi kumtambulisha yeye kama kiongozi, hawezi kuwa katika nafasi ya kufurahia malavidavi. Katika kupata ukamilifu wa jibu la swali hili, swali la pili huja juu yake; anafanya nini?

JAMBO LA PILI: ANAFANYA NINI?

Kuanzia asubuhi mpaka jioni, pengine usiku, mwanaume huwa kazini. (Natambua uwepo wa wanawake wanaoshinda kazini pia) Unadhani ni hamasa gani inayomfanya asitamani hata siku moja hata kuchelewa kazini? Yeye huamka asubuhi na mapema na wakati mwingine husahau hata kumuaga mke wake ili tu aweze kuwahi kazini.

Ninachozungumza hapa ni kwamba wanaume wanapenda kutambulika kwa vitu wanavyovifanya. Kama mwanamke wake asipolitambua hili na akashidwa kumpa mwanaume huyu hamasa na msaada katika kutekeleza majukumu yake, kamwe mwanamke huyu hatapata nafasi ya kumwona mwanaume wake akiwa na muda wa kuwahi kurudi nyumbani mapema. Ukweli ni kwamba, ukimpa changamoto ya kuchagua kati ya kazi na mapenzi, mwanaume atachagua kazi. Kwa sababu wanaume wanapenda kutambulika kwa vitu wanavyovifanya.

Katika jamii zetu tumekuwa na aina za kazi au fani ambazo zinaonekana kuheshimika zaidi kuliko nyingine. Udaktari kwa mfano. Mwanaume yu radhi kuachana na kila kitu na kuwekeza muda wake ili kujibu swali hili la pili. Simaanishi kuwa mbele ya kazi, mwanamke hana nafasi tena kwa mwanaume. La hasha! Nafasi ya mwanamke ipo na itaendelea kuwepo. Lakini kuna uwezekano mkubwa sana mwanamke huyu akawa na mwili wa mwanaume wake zaidi kuliko akili! Kwa kweli hili sio jambo zuri. Inaleta furaha zaidi pale mwili na akili vyote vinapobwagwa penzini kwa pamoja. Au sio?

Ninaamini unayo mifano mingi sana ya nyakati ambazo wanaume wamekuwa wakidanganya kuhusu kazi zao ili tu kutengeneza mvuto na utambulisho fulani kwa watu anaowalenga. Haya yote yamejengewa kwenye msingi wa kujibu swali la yeye ni nani? Kama mwanamke aliye katika mahusiano na mwanaume asipolitambua hili, atakuwa mwenye kulalamika mara zote kwamba mwanaume wake hana muda na yeye.

JAMBO LA TATU: ANAPATA NINI KUTOKANA NA ANACHOKIFANYA?

Umewahi kusikia vijana wakijiita majina ya matajiri wakubwa duniani? Bila shaka jibu ni ndiyo. Hulka ya kutamani kutambulika kwa kitu anachokipata au kukitengeneza ni ya asili kwa kila mwanadamu lakini ninakwambia leo, kama mwanaume hajajua ni mshahara kiasi gani ataupata katika kazi fulani, hawezi kubali kuanza hiyo kazi.

Kuona familia inapata mahitaji yote muhimu; inaishi katika nyumba nzuri, watoto wanapata mahitaji yao, wanakwenda shule, wazazi wanapata msaada wanapohitaji na bado ziada inasalia ni hitaji la kila mwanaume. Kama kila mwanamke akilitambua hili, wanaume hawa watapata wasaa mzuri wa kufurahia mahusiano na ndoa zao.

Nazungumza na wanawake sasa. Mama, tambua tu kuanzia sasa kuwa kama mwanaume wako hajawa na majibu yanayomridhisha juu ya maswali haya matatu, ni vigumu akawa na muda wa kutosha kwako. Hata kama hivi sasa hana kazi yenye hadhi au pesa nyingi, lakini kama yuko kwenye nafasi ya kuwa na matumaini ya kujua yeye ni nani au atakuwa nani, anafanya nini au atafanya nini na anatarajia kuvuna nini kutokana na anachokifanya basi anaweza kuwa na amani na utulivu kiasi.

Kadiri uwezavyo, tafuta namna ya kumsaidia mwanaume wako kujiona kuwa yeye ndiye kiongozi wako (Yeye ni nani). Mtambue kwa heshima kwa kazi anayoifanya (Anafanya nini). Ridhika na kile anachokupa au anachokileta nyumbani (Anapata nini) na ikiwezekana, kuwa sehemu ya mchakato wa yeye kuongeza zaidi kile anachokipata kwa sababu matokeo yakiwa mazuri, hamasa huzidi pia.

Jambo la muhimu zaidi kufahamu ni kwamba, ukamilifu wa pamoja katika mambo haya matatu ndio unaomfanya mwanaume ajione kuwa yeye ni mwanaume. Kama hajakuoa, ukiwa sehemu ya kumsaidia kupata majibu anayoyatafuta, basi utakuwa umeshajinyakulia pointi tatu za muhimu sana.
 
Kwa maisha haya yaliyojaa stress ni ngumu maranyingi watu kutulia na kutafakari haya.. Na sometimes hao wasaidizi wanajiwa na moyo wa kusaidia kabisa lakini kuna vikwazo na changamoto za
Muda
Uwezo
Kipato
Na by the way baadhi hujiuliza NITASAIDIA WANGAPI?
 
Hapa Bwashee umemaanisha nini? Wazazi, ndugu, jamaa pamoja na MWANAUME! Au Umemaanisha hao viumbe baadhi hujiuliza NITASAIDIA WANAUME WANGAPI? 😳

Binafsi nimekubaliana na hoja ya Mtoa mada. Napenda kuwa na mwanamke ambaye ana kitu kichwani mwake! Na siyo yule anayewaza tu kula vizuri, kuvaa vizuri na kujipamba muda wote.
 
Hapa Bwashee umemaanisha nini? Wazazi, ndugu, jamaa pamoja na MWANAUME! Au Umemaanisha hao viumbe baadhi hujiuliza NITASAIDIA WANAUME WANGAPI?

Nisahii baba mkuu hakuna apendae watu wa bata
 
Hapa Bwashee umemaanisha nini? Wazazi, ndugu, jamaa pamoja na MWANAUME! Au Umemaanisha hao viumbe baadhi hujiuliza NITASAIDIA WANAUME WANGAPI?

Binafsi nimekubaliana na hoja ya Mtoa mada. Napenda kuwa na mwanamke ambaye ana kitu kichwani mwake! Na siyo yule anayewaza tu kula vizuri, kuvaa vizuri na kujipamba muda wote.
Wahitaji ni wengi kuliko uwezo.. Ndugu na wasio ndugu.. Marafiki na wasio marafiki...
 
Ukimuuliza mwanamke yeyote ni aina gani ya mwanaume anayemhitaji, unaweza kukutana na majibu kama vile, mpole, mcheshi, mwenye uwezo wa kunihudumia na anayenipenda kama ninavyompenda mimi. Wakati haya yote yanaweza kuwa sahihi isipokuwa kigezo cha mwisho hapo juu, namna ambavyo wanaume wanawasilisha upendo kwa wenzi wao ni tofauti na namna ambavyo wanawake wengi hutarajia.

Utofauti huu unaletwa na mambo makuu matatu ambayo kwa kweli yamesimikwa ndani ya vinasaba vya wanaume wote duniani. Kuanzia Ruvuma mpaka Mwanza, Afrika ya Kusini mpaka Tunisia, China mpaka Marekani hata Brazil na Urusi. Kabla mwanaume hajawaza na kutilia maanani mambo yote haya matatu, upendo wake kwa mwenzi wake haujadhihirika kwa asilimia za kuridhisha. Nia ya kutamani kuwa katika mahusiano haiwezi kuwa thabiti, zaidi sana atakuwemo tu kwa sababu anatakiwa kuwemo.

Kama wewe unayesoma hapa ni mwanamke, huu ndio ukweli; mwanaume wako hataweza kukubali kwa moyo mmoja kukuoa, hataweza kukubali kwa moyo mmoja kuwa baba wa watoto wako, hataweza kukubali kwa moyo mmoja kujitambulisha kwa wazazi wako kabla hajawa na uhakika wa mambo haya matatu. Hata kama akionesha upendo wa dhati sana kwako, akili yake hukosa amani kama mambo haya matatu yasipokuwa bayana kwake.

Nisikuchoshe, hebu sasa tuyaangalie mambo yenyewe.

Katika kitabu chake cha "Act Like a Lady, Think Like a Man.", Steve Harvey anayaelezea mambo haya katika mfumo wa maswali. Mwanaume anaishi maisha yake yote akitafuta majibu ya maswali matatu tu; "Yeye ni nani", "anafanya nini" na "Anapata nini kutokana na anachokifanya". Kama majibu ya haya maswali matatu hayajawa bayana akilini mwake, itamchukua muda sana kuishi kwa amani katika uhusiano na mwenzi wake pengine na jamii inayomzunguka. Kibaya zaidi, wapo wanaume ambao wanaamua kabisa wasiingie katika mahusiano bila kupata majibu ya haya maswali matatu.

JAMBO LA KWANZA: YEYE NI NANI?

Nilipokuwa mdogo baba yangu alikuwa na kawaida ya kuniuliza, "Lucky ukiwa mkubwa unataka kuwa nan!?". Majibu niliyoyatoa nadhani unaweza kuyakisia na ukawa sahihi. Watoto wengi wanaokutana na swali kama hili huwa na majibu kama vile rubani, daktari, mwalimu na mengine yanayoeleza namna wanavyotamani kutambuliwa pindi watakapokuwa watu wazima.

Kadiri mtoto anavyozidi kukua ndivyo uzito wa swali hili unavyozidi kuwa kipengele muhimu katika akili ya aliye wa kiume kuliko ilivyo kwa aliye wa kike. Mwanaume hujali zaidi namna atakavyotambulika katika jamii yake. Hujali zaidi namna ambayo mwenzi wake, familia iliyomlea na jamii wanamtambua na kiasi ambacho anajitofautisha na wanaume wengine wa rika lake.

Kama mwanaume hajatengeneza utambulisho anaoutaka yeye, ambao mara nyingi huelekea zaidi kumtambulisha yeye kama kiongozi, hawezi kuwa katika nafasi ya kufurahia malavidavi. Katika kupata ukamilifu wa jibu la swali hili, swali la pili huja juu yake; anafanya nini?

JAMBO LA PILI: ANAFANYA NINI?

Kuanzia asubuhi mpaka jioni, pengine usiku, mwanaume huwa kazini. (Natambua uwepo wa wanawake wanaoshinda kazini pia) Unadhani ni hamasa gani inayomfanya asitamani hata siku moja hata kuchelewa kazini? Yeye huamka asubuhi na mapema na wakati mwingine husahau hata kumuaga mke wake ili tu aweze kuwahi kazini.

Ninachozungumza hapa ni kwamba wanaume wanapenda kutambulika kwa vitu wanavyovifanya. Kama mwanamke wake asipolitambua hili na akashidwa kumpa mwanaume huyu hamasa na msaada katika kutekeleza majukumu yake, kamwe mwanamke huyu hatapata nafasi ya kumwona mwanaume wake akiwa na muda wa kuwahi kurudi nyumbani mapema. Ukweli ni kwamba, ukimpa changamoto ya kuchagua kati ya kazi na mapenzi, mwanaume atachagua kazi. Kwa sababu wanaume wanapenda kutambulika kwa vitu wanavyovifanya.

Katika jamii zetu tumekuwa na aina za kazi au fani ambazo zinaonekana kuheshimika zaidi kuliko nyingine. Udaktari kwa mfano. Mwanaume yu radhi kuachana na kila kitu na kuwekeza muda wake ili kujibu swali hili la pili. Simaanishi kuwa mbele ya kazi, mwanamke hana nafasi tena kwa mwanaume. La hasha! Nafasi ya mwanamke ipo na itaendelea kuwepo. Lakini kuna uwezekano mkubwa sana mwanamke huyu akawa na mwili wa mwanaume wake zaidi kuliko akili! Kwa kweli hili sio jambo zuri. Inaleta furaha zaidi pale mwili na akili vyote vinapobwagwa penzini kwa pamoja. Au sio?

Ninaamini unayo mifano mingi sana ya nyakati ambazo wanaume wamekuwa wakidanganya kuhusu kazi zao ili tu kutengeneza mvuto na utambulisho fulani kwa watu anaowalenga. Haya yote yamejengewa kwenye msingi wa kujibu swali la yeye ni nani? Kama mwanamke aliye katika mahusiano na mwanaume asipolitambua hili, atakuwa mwenye kulalamika mara zote kwamba mwanaume wake hana muda na yeye.

JAMBO LA TATU: ANAPATA NINI KUTOKANA NA ANACHOKIFANYA?

Umewahi kusikia vijana wakijiita majina ya matajiri wakubwa duniani? Bila shaka jibu ni ndiyo. Hulka ya kutamani kutambulika kwa kitu anachokipata au kukitengeneza ni ya asili kwa kila mwanadamu lakini ninakwambia leo, kama mwanaume hajajua ni mshahara kiasi gani ataupata katika kazi fulani, hawezi kubali kuanza hiyo kazi.

Kuona familia inapata mahitaji yote muhimu; inaishi katika nyumba nzuri, watoto wanapata mahitaji yao, wanakwenda shule, wazazi wanapata msaada wanapohitaji na bado ziada inasalia ni hitaji la kila mwanaume. Kama kila mwanamke akilitambua hili, wanaume hawa watapata wasaa mzuri wa kufurahia mahusiano na ndoa zao.

Nazungumza na wanawake sasa. Mama, tambua tu kuanzia sasa kuwa kama mwanaume wako hajawa na majibu yanayomridhisha juu ya maswali haya matatu, ni vigumu akawa na muda wa kutosha kwako. Hata kama hivi sasa hana kazi yenye hadhi au pesa nyingi, lakini kama yuko kwenye nafasi ya kuwa na matumaini ya kujua yeye ni nani au atakuwa nani, anafanya nini au atafanya nini na anatarajia kuvuna nini kutokana na anachokifanya basi anaweza kuwa na amani na utulivu kiasi.

Kadiri uwezavyo, tafuta namna ya kumsaidia mwanaume wako kujiona kuwa yeye ndiye kiongozi wako (Yeye ni nani). Mtambue kwa heshima kwa kazi anayoifanya (Anafanya nini). Ridhika na kile anachokupa au anachokileta nyumbani (Anapata nini) na ikiwezekana, kuwa sehemu ya mchakato wa yeye kuongeza zaidi kile anachokipata kwa sababu matokeo yakiwa mazuri, hamasa huzidi pia.

Jambo la muhimu zaidi kufahamu ni kwamba, ukamilifu wa pamoja katika mambo haya matatu ndio unaomfanya mwanaume ajione kuwa yeye ni mwanaume. Kama hajakuoa, ukiwa sehemu ya kumsaidia kupata majibu anayoyatafuta, basi utakuwa umeshajinyakulia pointi tatu za muhimu sana.

Hoja ya mzingi lakini wanawake wa sasa wachache sana wanaweza kumsaidia mwanaume
 
Haya ni maswali ya msingi kwa Mwanaume anayejitambua. Na wanaume halisi wanazidi kupungua dunia. Sasa hivi kuna wanaume wenye akili kama za wanawake. Hawafikiri wala kuona mbali. Hawa ni kama wale ambao wako tayari kuishi na kulelewa na wanawake.

Hutafuta njia za mkato kupata hela na kuisha kupata matatizo.

Uwepo wa single mothers wengi na watoto wa mitaani ni ishara tosha kuwa wanaume wa ukweli hawapo.

Pengine ni wakati sahihi sasa kwa wataalamu kurudi maabara na kutengeneza chanjo ya kurudisha au kuongeza nguvu ya vinasaba vya kiume ili kuwafanya wanaume wafikirie kama wanaume. Kama hili halitafanyika dunia itazidi kuwa mahali pabaya pa kuishi.
 
Pale mwanaume unapokazana kuwa mwanaume (akili, mwili na malengo) ili mwanamke akutuze, halafu unaemhangaikia anachungulia walleti ina shilingi ngapi...
 
Back
Top Bottom