Mwanaume asiye na gari mi hata simkubalii!

Sasa huyo mnajimu hawezi kukushushia kitu cha landrover hivi badala ya busha? Angalia kama anaweza kukushushia kanyumba upanga pia, itakusaidia. Huyo mama usimchunge bana, acha apewe lifti na jirani, kuku wako manati ya nini?
Nna mtaalamu mmoja ni koboko kwa kushusha mishipa wezi wa wake za watu! Ajaribu aone, ikishindikana hiyo anapata zile 'siku' sawia na mkewe, acha kabisa aisee, anga hizi wezi huwa hawakatizi, lol!
 
We nishakujua unataka gari ila huna hela ya kununulia maana stori zako daily ni hizihizi
 
Kwahiyo we unapenda wenye magari tu!inaonyesha dhahiri huna mapenzi ya kweli na huyo ulienae akae chonjo akifulia tu amekwisha!nb ngoma sio mafua!
 
Mie nikishikwa na kawivu kiduchu tu ama kununa anajipiga ban. PAW anajua kupenda acha tu! Na ana helicopter, kwa hiyo sina wasiwasi na vidada vya jf,lol
Unamuongelea PAW huyu moderator wa jukwaa la jokes? si fundi baskeli uyu? acha kumpaisha bana
 
Ulishawahi kusutwa na mdundiko wa kwa mtogole? Wakikuvalisha vikoi naviomba afu kama una gari ntakuwa bibi yako valentine ijayo
Huna lolote king'a... Watu ngoja wamuibukie huyo kizuka wabebe mzigo we na shem wako nito mna huu.....!

Anamaliza nekst wik, halaf habari za jikoni zinasema nitonye kakamatwa boda la guinea bissau anavusha biblia na misahafu kimagendo. Sweetlady aspoangalia anaweza akawa kizuka soon
Mkuu hawa kina king'a wamemzuga mtoto wa watu ona sasa kaingia heda bila kutarajia,
 
Kweli hiyo mademu wa siku sijui ni ufala au ulimbukeni maana hata mimi leo kuna demu nimemwomba kuonana nae akaniuliza ja una usafiri binafsi? nikamjaribu kumdanganya kua sina ila nakuja kwa daladala,baada ya kusikia daladala akaamua kuniblock kwenye facebook na kunitukana kinoma, wakati mi nilikua namjaribu tu gari nilikua nayo ila nilitaka kujua imani yake
 
Bahti mbaya zaidi kuna sheria ya maisha isemayo kila kizuri kina gharama..........waache wawapnde wenye magari!
 
Nitonye anahonga wewe acha tu! Mie nna kipara wigi la nini?
Yaani wamemtaftia mtu ndo kwanza ana undergo evolution? uskute king'asti kumtetea kote pengine kahongwa hela ya wigi la nywele tu. Sweetlady wenyewe analala kwa jirani hela ya kodi imeisha na mzembe nitonye ndo kadakwa boda.
 
Endelea kusema hivyo hivyo ili wanaochat na waume za watu wakae mbali na PAW wangu! Kwanza hana hela wala nini, ila mapenzi motomoto baba! Anajali na kujaliwa! Mtajibeba!
Unamuongelea PAW huyu moderator wa jukwaa la jokes? si fundi baskeli uyu? acha kumpaisha bana
 
Wasitutishe bana , kwanza siku hizi kuna Bajaji, Mnamalizana gesti kisha unachukua bajaji unamrudisha kwao, kama ishu ni kupanda daladala...........................
 
Wenzako hata kama ni tetracycline ya police ukipiga honi utasikia Hiii!!!!! mwanamke gari bwana. Itauma zaidi utakapokuwa na mpenzi wako halafu ikapita gari, ukimchungulia unaona kaweweseka moyoooni! kinadada mtatufanya tufungwe kisa gari.
 
Ndyko naona kutokuwa na gari kunakutesa sana.......umeachana ha yule jirani mnyanyasaji wa lifti?

wala hainisumbui sema watu hawaelewi, mie naelezea mkasa tu mkuu. Iweje uweze kuwa na mahala pa kulala ushindwe kununua gari mkuu. Nnacho amini ni kwamba kuna wengine wamejifunza kwa mikasa yote miwili. Labda uniambie vituko tunavyokutana navyo maishani tusivielezee humu
 
Makahaba wana tabia mbaya sana!! Kama una nia ya kuolewa haijalishi kijana anamiliki kitu gani, zaidi utu ndo unaotakiwa na pawepo na amani katika familia. Hilo gari ndo liteleta amani? Bora ungeniambia awe na gari inayoleta kipato(asset), hii ingeleta maana kidogo kuliko kumtaka mawanaume atakae kubeba kutoka kwenye starehe zako! Ndo maana umaskini wa fikra umetamalaki kwenye vichwa vya mabinti wengi! Mwanamke anaedumu kwenye ndoa ni yule anaechuma kwa pamoja na mume wake. Huyu anaetaka mwanaume mwenye gari ataishia kutumiwa na kutemwa kama big G.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom