Mwanaume asiye na gari mi hata simkubalii!

Mwanaume asiye na gari mi hata simkubalii!

ndyoko

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
4,971
Reaction score
1,655
Nikiwa nimekaa siti ya nyuma ambapo siti ya mbele walikaa mabinti wawili-nikiri kuwa walikuwa warembo-nikawasikia wakiongea mambo yako ya kike kike. Pengine kwa kunogewa na maongezi ya mapenzi-inaonekana muda mfupi kabla ya kupanda gari walitongozwa na wanaume-mmoja akaropoka 'kwanza wanaume wenyewe gari hawana, shida gani watu baada ya kutoka kupeana raha tuanze karaa ya kugombania daladala'? Mwingine akadakia, kweli shosti mtu umejichokea kwa dozi zake halafu anazidi kukukaraisha kukupandisha midaladala'.

Mmoja kageuka nyuma kuniangalia, akakumbana na bonge la tabasamu langu. Nikawaambia ujumbe umefika......wakacheeeeeeeeka! Nikaamua kuunga stori na kuwambia........'Jamani hata sie wapanda daladala tunahitaji raha ya mapenzi', yule muongeaji sana akanijibu eti labda hadi mwanaume awe amemuingia haswa moyoni mwake, vinginevyo kama ni issue ya kupeana raha tu, hapotezi muda kwa wanaume wachovu wa kupandishana daladala.

Nikabaki hoi mie, looooh! Nikaunga na ile 'issue' yangu ya ' Hivi jirani kwa nini hununui gari', nikajisemea moyoni heri nimeshaoa, maana kama ningekuwa bado walahi mwaka huu ningechanganyikiwa!
 
hahahha mkuu inabidi ununue tu gari maana unaonekana huna jinsi......

kweli aisee unaweza ukaishia kuwaza kuwa unasemwa wewe kumbe watu wako kwenye stori zao, hawakujui, huwajui, hamjuani!
 
wanasema ukweli bwana hao its wat tgwy want in apartner so kama huna u dnt make the cut....tumubali tuu mapwnzi siki hizi biasharaa
 
wanasema ukweli bwana hao its wat tgwy want in apartner so kama huna u dnt make the cut....tumubali tuu mapwnzi siki hizi biasharaa

duuuuuuuuu! nimeshindwa kujua umeandika kitu gani mkuu, yaani sijui we ni mtu wa sayari gani na umesoma wapi. au inawezekana UFOs nao wanatumia jf nini? Mediocre at its best level! Rudi facebook ndugu, khaaaaa!
 
kwa hiyo ni kusema wanaume wenye magari,wanapendewa magari yao

ukiwa huna kaazi kwelikweli,ukiwa nacho shughuli pia
 
duuuuuuuuu! nimeshindwa kujua umeandika kitu gani mkuu, yaani sijui we ni mtu wa sayari gani na umesoma wapi. au inawezekana UFOs nao wanatumia jf nini? Mediocre at its best level! Rudi facebook ndugu, khaaaaa!

arudi shule upya na si fb!!ataenda kuandika hizo lugha zake mpya bure
 
Ndyoko mkuu hii wiki naona imekuishia ukiwa umewaza sana neno 'GARI' kutokana na hizo scenario mbili..

Kuhusu hao wadada nadhani wako kibiashara zaidi siyo upendo..iweje mtu usihangaike na maisha yako usubiri kutongozwa na mtu mwenye gari na kuwadharau wasio na magari??! Halafu unaweza kukutana na watu wengine kwenye madaladala siyo kwamba hawana magari.
 
We acha tu madam!
 
duuuuuuuuu! nimeshindwa kujua umeandika kitu gani mkuu, yaani sijui we ni mtu wa sayari gani na umesoma wapi. au inawezekana UFOs nao wanatumia jf nini? Mediocre at its best level! Rudi facebook ndugu, khaaaaa!

Heeeheee nimesoma maandiko yake kwakweli nimejisikia aibu sana, kama huwezi kuandika kwa kiswahili basi andika kwa hiyo lugha ya kitumwa tu, sio kuharibu lugha yetu adhimu ya kikswahili!
 
Hata Ambulance ilimradi awe na uhakika wa kupanda gari unayo iendesha wewe...
 
Heeeheee nimesoma maandiko yake kwakweli nimejisikia aibu sana, kama huwezi kuandika kwa kiswahili basi andika kwa hiyo lugha ya kitumwa tu, sio kuharibu lugha yetu adhimu ya kikswahili!
hahaha jf bana full ng'aeng'ae,
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom