Nikiwa nimekaa siti ya nyuma ambapo siti ya mbele walikaa mabinti wawili-nikiri kuwa walikuwa warembo-nikawasikia wakiongea mambo yako ya kike kike. Pengine kwa kunogewa na maongezi ya mapenzi-inaonekana muda mfupi kabla ya kupanda gari walitongozwa na wanaume-mmoja akaropoka 'kwanza wanaume wenyewe gari hawana, shida gani watu baada ya kutoka kupeana raha tuanze karaa ya kugombania daladala'? Mwingine akadakia, kweli shosti mtu umejichokea kwa dozi zake halafu anazidi kukukaraisha kukupandisha midaladala'.
Mmoja kageuka nyuma kuniangalia, akakumbana na bonge la tabasamu langu. Nikawaambia ujumbe umefika......wakacheeeeeeeeka! Nikaamua kuunga stori na kuwambia........'Jamani hata sie wapanda daladala tunahitaji raha ya mapenzi', yule muongeaji sana akanijibu eti labda hadi mwanaume awe amemuingia haswa moyoni mwake, vinginevyo kama ni issue ya kupeana raha tu, hapotezi muda kwa wanaume wachovu wa kupandishana daladala.
Nikabaki hoi mie, looooh! Nikaunga na ile 'issue' yangu ya ' Hivi jirani kwa nini hununui gari', nikajisemea moyoni heri nimeshaoa, maana kama ningekuwa bado walahi mwaka huu ningechanganyikiwa!