Kitanzi cha mwisho

kapingili

Senior Member
Jul 4, 2012
155
192
IMEANDIKWA NA : RICHARD MWAMBE

*********************************************************************************

Simulizi : Kitanzi Cha Mwisho

Sehemu Ya Kwanza (1)

Maisha yanayotuzunguka yana mambo mengi sana, chuki, wivu, furaha, inda na mengi yanayofanana na hayo. wakati wewe unafanya kilicho halali wenzako wanafanya kilicho haramu, wewe ukinunua wenzako wanaiba ilimradi tu dunia ni kama tambala bovu.
wapo wasiopenda uishi kwa raha na wapo wanaokuombea maisha mema.
Binadamu tuna mambo mengi... kutana na msichana Yaumi uone shida alizopata kutokana na furaha ya watu wengine, Yaumi anaingia kwenye mzozo na watu asiowajua wala kujua... anataka kulipa kisasi kwa nini? twende pamoja....

TRAILER...

KELELE za watu waliokuwa wakikimbizana wakipanda ngazi za jengo moja zilisikika. Alikuwa ni mwanamke mmoja aliyevalia gauni tepe, refu lakini alilishika kwa mikono yake na kuifanya miguu yake kuwa huru, alionekana ni mwanadada aliyepitia kama si JKT basi MGAMBo maana alipanda ngazi kwa kukimbia huku nyuna yake akifuatiwa na kijana akiyeevalia suti nadhifu ya kijivu akiwa na bastola mkononi. Mbio zile ziliendendelea huku yule mwanaume akisikika akisema
"Simama, au la nakulipua,"
lakini yule mwanamke hakusimama aliendelea kupanda ngazi kwa kasi ileile, lakini mbio za sakafuni huishia ukingoni. Ilikuwa ni juu kabisa ya ghorofa ambako mwanamke yule alisimama akijiandaa kujirusha chini.
"Tulia hivyohivyo!" yule kijana alimnyooshea bastola yule mwanamke, akiwa anahema kama mbwa, yule mwanamke aligeuka upande ule wa yule kijana.
"Nimechoka, nimechoka kuandamwa nanyi kila wakati, sioni haja ya kuishi, nimehukumiwa kifo lakini mnanitesa tu, bora nijiue mwenyewe" alifoka yule mwanamke.
Akiwa bado kamnyooshea bastola yule mwanamke, Kamanda Amata alishusha pumzi na kutulia,
"Sikia mrembo, hapa upo kwenye mikono salama, sitaki kukudhuru, na kitendo cha kile kitanzi kukatika ni mimi niliyefanya hivyo, nakuhitaji wewe kwa shughuli za kiusalama, hakuna atakayekugusa, naitwa Kamanda Amata kutoka idara ya usalama wa Taifa kitengo kisicho na mipaka"
Yule mwanamke akashusha punzi na kuliachia lile gauni lake limfunike sehemu kubwa ya chini iliyokuwa wazi. Kamanda Amata alirekebisha tai yake na kuirudisha bastola yake katika kikoba maalum ndani ya koti lake. Akamsogelea yule mwanamke
"Unaitwa nani?" alimwuliza
"Yaumi" yule mwanamke alijibu kwa utulivu sana, hamu yake ya kujiua ilipotea ghafla na hamu ya kutimiza azma yake ilipata matumaini, kamanda Amata alimshika mkono na kuteremka nae ngazi za upande wa nje kwa maana alisikia kuna watu walipandisha juu kwa mgazi za ndani wakibishana kuwa mwanamke huyo yupo huku juu, polisi.
Waliteremka mpaka chini, Land Cruiser V8 yenye vyoo vyeusi ilisimama mbele yao, kamanda Amata almsukumia ndani Yaumi na yeye kufuatia, kisha ile gari ikaondoka kwa kasi.
****
YAUMI aliketi katika kiti cha mbao mikono yake miwili akiishikamanisha na kuiweka juu ya meza mbele yake na kuinamisha uso wake juu yake, nywele zake ndefu ziliuficha uso wake. Mawazo yalimtawala, hasira ilimshika, kisasi kikiujaza moyo wake, kwa nini Yaumi?

MAHAKAMA KUU

JAJI Ramson alitulia tuli juu ya kiti chake maalum, pembeni yake mezani kukiwa na kijinyundo kidogo, alitulia akisikiliza hati ya mashitaka iliyokuwa ikisomwa na mwendesha mashitaka wa serikali, mwanzo mpaka mwisho, ushahidi uliwasilishwa na Yaumi alkutikana na hatia ya mauaji dhidi ya mumewe bwana Kajiba A. Kajiba,
baada ya kuahirishwa mara nyingi kwa kesi hiyo hatimaye siku ya hukumu ilifika na jaji Ramson akasoma hukumu kwa lisasa limoja nanusu, Yaumi alihukumiwa kunyongwa hadi kufa, kwa kosa la kumuua mumewe na watu wengine watatu zaidi.
Jaji Ramson alimtazama Yaumi kwa huruma lakini sheria ilishachukua mkondo wake.
Askari polisi wa kike alimuongoza Yaumi kwenye landrova ya magereza na kuchukuliwa mpaka gereza la Segerea akisubiri kunyongwa kwake. Yaumi aliketi sakafuni kwenye chumba kidogo sana, pembeni yake kukiwa na kijindoo kwa ajili ya haja zake. Moyo wake uliuma sana, hasira ilimshika kwa nguvu, 'wangeniacha nimalizie kazi yangu, kwani alibaki mmoja tu' alijiwazia.
* * *
YAUMI, alikuwa akiishi na mumewe huko Tabata Kimanga, ndani ya nyumba yao walibaki wawili tu kwani watoto wao wawili wote walikuwa masomoni nje ya nchi. Yaumi na mumewe Kajiba walipndana sana daima walipenda kutoka wote kwenda outing, mara baharini au kwenye hoteli kubwakubwa, maisha ya upendo kati yao yalikuwa ndiyo nguzo imara.
"Mke wangu Yaumi, tumeishi kwa muda mrefu sasa maisha matamu ya ndoa, lakini kuna kitu sikuwahi kukushirikisha" Kajiba aliongea taratibu huku akinywa juice yake taratibu, akaendelea, "Sasa hv mimi mumeo naishi na roho mkononi, kuna watu wanataka kuitoa roho yangu, watu wangu wa karibu tu," Kajiba akashusha pumzi na alionekana wazi kutetemeka tangu moyoni.
"Oh mume wangu, mbona wanitisha honey?" Yaumi aliuliza kwa hofu yenye mashaka
"Siku zote, unayekula nae na kunywa nae hutokea kuwa adui mkubwa na mbaya sana" Kajiba alisema.
"Ah! Sitakubaliana na hilo, kuna nini sweetie?" Yaumi alizidi kuhoji.
"Nitakwambia kila kitu, lakini kabla ya yote, nataka nikwambie kitu kingine cha msingi," walitazamana kwa majonzi, Kajiba akainuka kitini na kumsshika mkono mkewe, wakatoka katika eneo lile na kutembea taratibu huku wakiwa wameshikana mikono,
"Nitakapokufa, utunze watoto wetu vizuri kabisa, hakikisha wanasoma mpaka mwisho, unajua tuna pesa nyingi sana kwenye benki za nje, hilo la kwanza, la pili nitakupa funguo, ya posta endapo nitakufa uende ukachukue kilichopo kwenye box hilo ujumbe wote utaupata humo," wakiwa waktika ma zungumzo, mara ghafla
Toyota Prado nyeusi ilisimama jirani kabisa ya miguu yao, Kajiba akamvuta mkewe ypande wapili na kuwa nya wote waanguke chini kutokana na ule msukumo.
Kioo cha upande wa dereva kiliteremka taratibu wakati gari ile ilikuwa imesimama huku ikiunguruma, mtu mmoja aliyevaa miwani myeusi aligeuka kulia na kuwatazana Kajiba na Yaumi waliokuwa pale chini, hakuongea kitu ila alisonya na kupandisha kioo juu kabla ya kutimua mbiyo na gari hiyo. Kajiba na mkewe waliinuka kutoka vumbini na kujikung'uta vumbi.
"Nani yule?" Yaumi aliuliza.
"Ah! Wadau mke wangu" alijibu Kajiba.
"Lakini mume wangu, mi nahisi kuna kitu katikati yake huniambii" Yaumi alilalama.
"Wanaitafuta Roho yangu" Kajiba alijibu kifupi kama kawaida yake. Alisimama kidogo na kushusha pumzi huku mikono akiwa kaiweka kiunoni, akatikisa kichwa kisha akamshika mkono mkewe na kuendelea kutembea.
Walipofika mbele ya geti la nyumba yao Kajiba alisimama akamgeukia mkewe,
"Mke wangu, nenda dukani ukanunue ile wine unayoipenda, wakati tunakunywa nukueleze mambo yote," alitoa wallet yake na kuchomoa noti kadhaa nyekundu kisha yeye akaingia ndani kumsubiri Mkewe ambaye alikuwa amekwenda dukani.
* * *
SARGEANT Magreth alibaki katega masikio akiwa amezungukwa na polisi wenzake pale kituo cha Tabata Jalil, mbele yao kulikuwa na simu ya kizamani kidogo iliyochakaa hapa na pale ilitoa sauti ya mtu anayelia na kutaabika.
"Mke wangu, mke wangu tafadhali, w....ananiua,"
mara ukasikika mlio wa risasi na kufuatiwa na kilio chenye maumivu, simu ile ikakatwa, ukimya ukatawala.
Land cruiser ya polisi ilifunga breki mbele ya nyumba ya mzee Kajiba na polisi wanne wakiwa na sargeant Magreth walikimbia na kuingia getini.
"Msishike geti!" Magreth aliwatahadharisha, wakaingia ndani na kukuta na mlango wazi, moja kwa moja macho yao yalitua kwa Yaumi ailiyekuwa ameshika kisu mkono mmoja na mwingine bastola akilia kwa kutetemeka huku mwili wa mume wake ukiwa umelala chini katika dimbwi kubwa la damu, jeraha la kisu kifuani mwake na tundu la risasi kichwani katika paji la uso.
Sargeant Magreth alimtazama Yaumi aliyekaa karibu na mwili wa mumewe akilia kwa kwikwi, Magreth alimuamuru askari mwingine kuchukua kile kisu na ile bastola kwa ajili ya uchunguzi. Baada ya itifaki za kiusalama kumalizika mwili wa marehemu ulichukuliwa.
" jamani mume wangu mimi wamemuua!" alili Yaumi huku akivalishwa pingu na Magreth,
"Nimekosa nn mimi?" aliendelea kulia Yaumi huku akipakiwa garini, watu mtaa mzima walisimama kwa huzuni wakiangali mwili wa Kajiba ukitolewa hali umefunikwa kwa shuka jeupe.
* * *
"Haya sasa! Hii ndiyo nyumba yako mpaka ukipata amri nyingine" ilikuwa ni sauti ya sargeant Magreth ikimuamuru Yaumi huku akimsukumia ndani ya chumba hicho na kumfungia kwa kufuli nyuma yake.
Yaumi aliendelea kulia na kumuomboleza mumewe, kilichomuuma zaidi ni ile hali ya kusubiri kuambiwa siri ile na mumewe, lakini likatokea la kutokea. Yaumi alijitazama jinsi alivyolowa damu katika dela lake alilovaa, aliuona mwisho wake, Yaumi akasimama akauegemea ukuta na taratibu akausotea kukaa chini.
'Lazima nilipe kisasi, haiwezekani kama kufungwa ntafungwa tu lakini lazima nimsake muuaji' mawazo hayo yalipita moyoni mwa Yaumi kwa kasi ya ajabu.
* * *

SIKU YA KESI

"YAUMI Masharubu, umri miaka 36, kabila Mzaramo. Mnamo tarehe 26 mwezi wa 8 mwaka 1996 siku ya alhamis, saa moja na dakika 25 jioni katika nyumba yenu ya Tabata Kimanga, ulifanya mauaji na kumuua mumeo bwana Kajiba kwa kutumia kisu na bastola aina ya Magnum, ulikutwa ukiwa umeshikilia vitu hivyo huku mwili wako ukiwa umetapakaa damu za marehemu" ilikuwa ni sauti ya muendesha mashitaka PP Kibona.
Yaumi hakutakiwa kujibu kesi hiyo kwani mwenye haki ya kuifanyia maamuzi ni jaji pekee. Yaumi alipakiwa garini tayari kurudishwa Segerea kusubiri siku ya kesi itakapotajwa mara ya pili. Yaumi alitulia kwenye karandinga akiwa na mawazo tele, akipanga na kupangua juu ya hatima yake.
Yaumi alirudishwa lumande kusubiri siku nyingine ambapo kesi ile itasomwa tena. Usiku wa mng'amung'amu ulimpa tabu sana, ndoto za jinamizi na makorokoro mengine viliujaza usiku huo.
****
KICHWA cha Yaumi kilikuwa na mengi ya kuwaza na kuwazua, kupanga na kupangua, jinsi gani ya kumpata muuaji na kwa nini alimuua mumewe, ijapokuwa kwake alijua wazi kuwa kesi hiyo hana budi kuhukumiwa kifo, lakini asingependa kufa bila kuhakikisha kuwa kisasi dhidi ya muuaji wa mume wake kumalizika.
Akiwa ameketi katia kijitanda chake, Yaumi alikuwa akifikiri jinsi ya kuupata uhuru wake ili azma yake itimizwe. Alipojiridhisha na mipango yote kichwani alitulia na kupata usigiizi.
Asubuhi ya siku ilofuata ilimkuta Yaumi akiwa kakaa na kauegemea ukuta huku kichwa xhake kikiwa kimeegemea magoti yake.
"we!" sauti ya kiume ilisikika na kumgutusha, alimtazama kijana huyo polisi aliyesimama mbele ya mlango huo wa chuma.
"We ndio Yaumi?" aliuliza
"Ndiyo"
"Ok," akaingiza mkono mfukoni na kutoa funguo kisha akafungua lile geti na kumpa ishara ya kumfuata naye akafanya hivyo. Hatua chache ziliwafikisha katika chumba fulani kikubwa tu chenye vitu vichache, meza moja na viti kadhaa, kila kiti alionekana kuketi mtu mmoja isipokuwa kimoja tu, Yaumi alijua kuwa kiti hicho bila shaka ni chake, alikiendea akaketi juu yake, mbele yake kulikuwa na kijana mmoja polisi aliyevaa kiraia ila muonekano wake wa nwele ulimtambulisha kuwa huyo ni polisi, walitazamana kidogo na Yaumi, kisha yule polisi akajikooza.
"Sasa Yaumi, nipo hapa kwa kazi moja tu, tunapenda utueleze ukweli kabisa juu ya mauaji ya mumeo ili tuone jinsi ya kuiweka kesi hii na we urudi uraiani, haya nambie kwa nini ulimuua mumeo bwana Kajiba?"
Yaumi alitumbua macho kwa swali hilo,
"Nani amekwambia kuwa mimi nimemuua mume wangu?"
"Faili lako linaonesha hivo, na umekutwa ukiwa umeshika kisu na bastola, bila shaka kwa macho ya kibinaadamu hapo wewe utatuhumiwa kuwa muuaji"
"Ni kweli afande lakini mimi si muuaji, na wala sijamuua mume wangu, na nina hamu ya kumjua aliyefanya hivi"
"Yaumi usituzungushe sana, tuambie umeua au la?"
"La" Yaumi alijibu huku machozi yakimtoka na mwili kuanza kutetemeka.
"Utanyongwa Yaumi kama hutosema ukweli" yule polisi aliendelea kumchokonoa.
"Acha tu waninyonge, kwanza sioni faida ya kuishi bila mume wangu" akajibu.
Kila alichoeleza Yaumi kilikuwa ni ngumu kukubalika na watu hawa.
Baada ya hapo Yaumi akarudishwa lumande na kuwaacha wale jamaa pale.
"Anaonekana hajui kitu" aliongea mtu mmoja mwenye ndevu nyingi.
"Umeona ee! Basi hili limekwisha, tuangalia mengine" akasema yule polisi. Ilionekana wazi kuna kama mchezo unaochezwa lakini kwa nini? Hakuna ajuae.
* * *
Nyumba ya Kajiba ilikuwa imefungwa, hakuna mtu aliyeishi kila kitu kiliachwa kama kilivyo, mchana huo mtu mmoja alikuwa ndani ya nyumba hiyo ambayo ilikuwa chini ya uchunguzi wa polisi kwa kufungwa utepe maalum wa njano, lakini huyu ni nani hata aingie ndani humo na asionekane na watu. Alizunguka chumba hiki na kile akafungua hapa na pale, ilionekana akitafuta kitu fulani ambacho hajui wapi kimewekwa, aliendelea bila mafanikio, meisho akaamua kurejea alikotoka bila kupata tafutishi yake.
Uchunguzi uliendelea lakini katika kila walilolifanya bado ilikuwa ngumu kujua chanzo cha mauaji hayo.
"Nyie mnasumbuka bure, hata ile simu aliyopita marehemu, kama mnakumbuka alikuwa akimtaja mke wake kuwa anamuua, sasa nyie hapo mnafanyaje? Huyu ndiye muuaji"
wote walitazamana na kuonekana kuafiki.
Yaumi alikuwa kasimama katika mlango wa selo mara tu yule askari alivoondoka, akagundua kitu kuwa lile kufuri halikubanwa sawasawa, akalishika na kulitikisa, he! Kumbe halikufungwa sawasawa, aalilizungusha taratibu na kulitoa pale kwenye komeo kisha akafungua mlango mdogo na kuikanyaga sakafu ya coridor ndefu inayoelekea huku na kule, akatazama kushoto kisha kulia na kutoka kwa minyato kuelekea kushoto, mwisho wa ridor ile kulikuwa na kijimlango kidogo ambacho alikitumia kutoka nje na kuukabili uwanja uliokuwa hapo, lakini mataa makali yalikuwa yakimulika eneo hilo, akafikiri mara mbilimbili atapita vipi, hakupata jibu. Kutoka pale alipo akambaaambaa na ule ukuta mpaka katika ukingo wa jengo hilo kisha akakatulia kuongalia kama kuna anyekuja upande huo, mara kivuli kikubwa kikawa eneo hilo, kumbe ile taa iliyo katika kibanda cha mlinzi huwa inageuka huku na kule, Yaumi aliona hiyo ni bahati ya mtende, alikimbia kwa hatu ndogondogo na kukatisha kale kauwanja mpaka chini ya banda mlinzi na kujificha chini yake akitazama huo ukuta mrefu ulimuwekea pingamizi, machozi yalimtoka hakujua afanye nini kutimiza lengo lake, hakukata tanaa, kwa njia ya kificho aliendelea kutembea huku akiiangalia ile taa kama inamgeuki ili ajifiche, akiwa katikati ya ule ukuta, Yaumi alihisi ile taa inammulika na tayari wakati huo alibakisha kipande kidgo afike upande wa nyuma wa gereza hilo....
YAUMI alijificha karibu na nguzo iliyoushika ukuta ule wakati ile taa kubwa ilipokuwa inamulika upande huo, mwanga mkali ulimulika pale alipo kwa sekunde kadhaa, Yaumi alishikwa na woga mkuu akajua kuwa sasa atakamatika, mara ule mwanga ukageukia upande mwingine.
TARATIBU aliambaa na ukuta ule, Mungu si Athumani mbele yake alikuta matofali yaliyopangwa tayari kwa ujenzi, kwa hadhari kubwa akakwea yale matofali na na muda kidogo akajikuta juu ya ukuta ule na upande wa pili kulikuwa mti wa muarobaini, 'Aliyepanda mti huu, abarikiwe na Bwana' alijiwazia wakati akishika moja ya tawi la mti huo na kuteremkia kwa nje.
* * *Ulikuwa ni usiku wa mbala mwezi pevu, Yaumi aliiona nyumba yake kwa mbali akiwa katika tax.
"Simama hapa dukani," alimuamuru dereva, "Nakuja sasa hv usiondoke" aliongeza, kisha akavuta hatua na kupita kati ya kichochoro kimoja kilichotenganisha nyumba mbili, upande wa pili alitoke nyuma ya nyumba yake aliyokuwa akiishi na marehemu mumewe, hakukuwa na dalili ya watu eneo hilo kwani msiba ulihamishiwa kwa dada wa marehemu. Moja kwa moja alikwenda katika sehemu yao ya siri na alipohakikisha usalama alichimba kishimo pembezoni mwa ukuta na kuchomoa kijaruba cha ngozi kisha akafuata ule ukuta na kufikia mlango mdogo uliopo pembeni mwa ukuta huo, Yaumi aliutomasa kwa moja ya zile funguo nao ukafunguka, akaingia ndani ya ua mkubwa sana, pale alikuta gari zake tatu zikiwa salama kabisa, akausogelea mlango wa kuingilia ndani na kutulia kidogo, alipohakikisha ukimya akaufungua mlango huo na kuingia ndani kisha akavuta hatua fupifupi na kupanda ngazi kuelekea chumbani kwake na kuingia, moja kwa moja aliliendea kabati na kwa kutumia kitambaa maalumu alichojifunga kiganjani aliivuta droo ya kabati hilo,
'Ewaaaaa' alijitamkia moyoni alipohakikisha kile anachokitaka kipo, akatoa basola moja na risasi kumi na nne kwenye kikasha chake, kisha akachukua kisu na documents fulanifulani, droo ya pembeni alitoa kijibriefcase kidogo na kuvitia vitu hivyo, aliendea droo ya kitanda na kutoa kadi za benki na burungutu la pesa lililowekwa hapo, Yaumi alitazama chumba chake vizuri, aligundua wazi kuwa kuna vitu havijakaa sawa, wasiwasi ulimjaa, akashuka ngazi mpaka sebuleni akiwa na peni na karatasi, mwendo wake uliishia kwenye dimbwi la damu ambayo sasa ilishaganda na kutoa harufu nzito, aliitazama ile damu ya mumewe na kupiga magoti kisha akaandika vitu fulani kwenye ile karatasi yake huku akitazama sehemu ile iliyo na damu.
+256-16841-5576 pos, Yale maandishi yaliyojalizwa kwa namba nyingi yaliishia hapo, Yaumi alifikiria sana juu ya namba zile hakujua maana yake nini na hakujua kwa nini mumewe aliandika namba hiyo kwa kutumia damu yake kabla ya kukata roho. Alikikunja kile kikaratasi na kukifutika katika nguo yake ya ndani. Alipokuwa katika harakati za kutoka alisikia mngurumo wa gari ikisimama huko nje na watu waliokuwa wakiongeaongea walisikika wakiuendea mlango mkubwa wa nyumba hiyo.
Yaumi, alijificha nyuma ya kabati la jikoni ambapo alihakikisha anaweza kuona watakapoingia, mara mlango ukafunguliwa watu wanne wakaingia ndani ya sebule hiyo, wakasimama katikati ya sebule kwa mshangao, wakikodolea macho pale palipokuwa na damu iloganda ambayo sasa haikuwepo kama mwanzo ilikuwa imesafishwa yote lakini iliachwa kwa maandishi 'REVANGE' kisha mbele yake kukiwa na risasi moja.
Kutoka pale alipojificha, Yaumi aliwaona wale jamaa jinsi walivyochanganyikiwa.
"Mh!" mmoja aliguna huku akiivua kofia yake aina ya pama.
"Ina maana kuna mtu aliingia humu ndani?" aliuliza mmoja wao
"Kitendawili hicho" mwingine alijibu.
"Naanza kuwa na wasiwasi, nani huyu? Vijana, tumsake tummalize atatuletea shida huyu kabla hatujaanza msako wetu. Ila hakikisheni leo lile faili tunalipata" kiongozi wao alieleza.
"Faili lipi boss?"
"Kuna faili tumehifadhi mambo yetu nyeti ambalo huyu Kajiba analo, kwa maana nina uhakika na hilo, kile kibegi kule nyumbani ni cha kwake, so ina maana yeye kachukua cha kwetu baada ya ile ajali pale Magomeni, hebu chunguzeni"
* * *
YAUMI alitetemeka pale alipo, sasa picha ilianza kumjia juu ya kifo cha mumewe, alikumbuka siku ambayo mumewe alirudi usiku sana akamwambia kuwa walipata ajali magomeni hivyo katika pilikapilika za huku na huko alichelewa kurudi nyumbani, alifika na kutupia mezani briefcase ndogo nyekundu na yeye kwenda kuoga huku akimuachia mkewe kazi ya kuweka sawa makabrasha yao ya biashara ambayo yapo ndani ya briefcase ile. Kilichotokea ni kuwa Yaumi alishindwa kuifungua kwa zile namba alizozizoea akampa taarifa mumewe naye alipojaribu alishindwa, akahisi kuchanganyikiwa, akamruhusu kuvunja ile briefcase, Yaumi akafanya hivyo, ile briefacase ikavunjika na macho ya Yaumi yalikutana na faili moja jekundu, alipigwa na butwaa akamtazama mumewe.
"Vipi mbona unashangaa?" Kajiba alimuuliza mkewe huku akiivuta ile briefcase upande wake.
"Hili faili humu ndani mbona siyo nililolizoea mpenzi?" Yaumi aliuliza.
Kajiba alilitazama lile faili akaliinua kutoka pale lilipokuwepo na kulifungua kuona vilivyomo.
Kajiba alibaki kaduwaa juu ya hilo faili, kurasa ya kwanza, ya pili na ya tatu zilimuwacha mdomo wazi. Hakujua nini kimetokea, alilichukua lile faili na kuliweka juu ya kitanda kisha akaenda zake kuoga akimwacha Yaumi akiwa pale chumbani.
Baada ya kuoga alirejea kitandani kuungana na mkewe lakini kabla alilipitia tena lile faili na kushtushwa na yaliyoandikwa, akalifunga na kulihifadhi vizuri kabatini kisha akajilaza lakini kichwani mwake kulikuwa na mawazo mengi sana.
* * * *
YAUMI aliendelea kuwaangalia na kuwasikiliza wale watu waliokuwa bado pale sebuleni.
"hebu kafanyeni upekuzi huku na huko tuondoke" huyu mmoja aliwaamuru wenzake, nao wakatii amri na kufanya upekuzi katika nyumba ile. Baada ya dakika kadhaa wote walirudi pale sebuleni,
"Hamna kitu boss!" mmoja alitoa taarifa.
"Dah! Huyu jamaa katuweza aisee, sasa hapa tudili na mkewe lazima anajua kitu" yule boss alisema
"Sasa mkewe yuko lumande tutampataje?" mwingine aliuliza
"Aaa hilo lisiwaumize kichwa, uko huko lumande ataeleza kila kitu. Boss anataka jibu haraka iwezekanavyo" aliongea huku kasimama na kuuelekea mlango wa kutokea nje akifuatiwa na wale wenzake kisha wakaufunga mlango.
Yaumi alisikia mngurumo wa gari alitamani hata japo ajue namba zake lakini haikuwa hivyo. Aliitazama ile briefcase yake pale chini na zana alizozichukua kule chumbani, akaiangalia saa ya ukutani, ilikuwa yapata saa saba za usiku.
'Yanipasa kurudi' alijisemea kisha taratibu akatokea mlango wa nyuma ule ule alioingili na kuficha funguo mahali pale pale. Akiwa ndani ya baibui hakuna aliyeweza kumtambua alipokuwa akipita mbele ya nyumba yake na kuiona ikiwa bado imefungwa ile mikanda ya plastiki 'police line'.
Akavuta hatua za haraka haraka na kusimama barabarani, kidogo tu ilipita tax akaisimamisha.
"Tabata tafadhali" alimwambia dreva tax. Haikuchukua muda aliwasili na kumlipa dreva tax kisha yeye kutokomea gizani.
Mwendo wake uliishia mbele ya nyumba ya wageni Bondeni Lodge akapanga chumba kimoja kidogo cha thamani ndogo. Akaweka kibegi chake cha nguo na ile briefcase akaificha juu ya dari ili wafagizi wakija wasiione, akafanikiwa.
Aliketi kitandani na kuichukua simu ya mumewe, marehemu Kajiba na kuiwasha kisha akatulia kusubiria kitakachotokea katika simu hiyo.
'Usipotupatia lazima tukupoteze'
Ilikuwa ni meseji iliyotumwa saa 24 kabla ya kifo cha mumewe, akapekua tena na tena.
'Endelea kujifanya jeuri, lakini utaiona faida yake'
Ilikuwa meseji nyingine.'Tunajua kuwa umechukua briefcase yetu kama sisi tulivyoichukua ya kwako, tuko tayari kukupa ya kwako, utupatie ya kwetu pia'
Ilikuwa meseji ya nyuma zaidi.
Yaumi aliishiwa nguvu, 'kwa nini siku zote hakuniambia' alijiuliza huku macho yake yakijawa na machozi.
Aliichukua ile simu na kujaribu kuangalia namba iliyotuma meseji zile; private namba, akaishiwa nguvu lakini alijipa moyo. 'Lazima nilipe kisasi kwa ajili ya mume wangu mpendwa', aliizima ile simu na kuipandisha darini kisha akatoka na kuufunga mlango.
"Dada natoka naenda kazini mara moja nitarudi kwa kuchelewa sana, usishangae kutokuniona si unajua kazi zetu za usiku sisi warembo" alisema huku akimkabidhi funguo na noti ya shilingi elfu kumi.
"Hii utakunywa japo soda" kisha akaondoka zake na kupotelea gizani.
Kwa mtindo uleule Yaumi aliuzunguka kwa tahadhari ukuta wa gereza la Segerea mpaka upande wa nyuma kulikokuwa na nyumba chakavu akavua lile baibui lake na kulisweka ramboni kisha kuuficha ule mfuko kwenye kijichaka na yeye kuufuata ule mti wa Muarobaini na kuukwea ili kuingia ndani, alipofika juu alitulia kuangalia usalama na alipoona pana ukimya akashukia ndani kupitia yale matofali, huku akiukwepa ule mwanga wa ile taa kubwa alifanikiwa kurudi mahali pake na kujifungia kwa ndani, mara alisikia nyayo za watu zikielekea upande ule
"Una uhakika lakini?" mmoja alimuuliza mwenzake
"Aaa sana nimekwenda mpaka pale hakuna dalili mi naona yale ni mashuka tu, katoroka huyu" mwingine alisema. Yaumi aligundua kuwa kuna uwezekano kuwa walikuja kumtazama na wakamkosa, alijifunika shuka lake la jela na kutulia kitandani, uzuri ni kwamba lumande ya wanawake huwa haijai kwa hiyo wanalala kwa raha tu.
"Itakuwa aibu sana kutorokwa na maabusu, sijui tutaeleza nn sisi?" sauti zile zililizidi kukaribi na mara wadada wawili wakatoke pale mlangoni na kutazama ndani ya chumba kile.
"Ha! Si yule pale au macho yangu?" alisema mmoja wao
"Mh, hii miujiza, mi nimefika mpaka pale hakukuwa na mtu" alisisitiza yule wa kwanza.
"Tutamhoji kesho vizuri muache alale"
* * * *
MAWAZO yalikijaza kichwa cha Yaumi, mambo mengi yalipita kama mkanda wa filamu, wakati yeye akiwa amejikalia juu ya kijitanda kidogo mwili wa mumewe ulikuwa bado mochwari ukigandishwa kwa barafu mapaka mamlaka husika itakapoamua uzikwe.
Kila mtu aliyemjua bwana Kajiba alisikitishwa na kifo hicho, japokuwa watu wengi walisikia kuwa Kajiba kauawa na mkewe, wengine wengi hawakuliamini hilo.
"Hata kama ni mahakamani nitamtetea" alisikika mzee mmoja wa kipemba akisema hayo.
+256 Iilikua ni namba inayokuja na kutoka kichwani mwa Yaumi, hakujua kuwa ile namba yote ni ya simu au ni ya kitu gani, kama ni ya simu simu hiyo ina maana gani, ulikuwa ni mtihani mgumu kwake.
'Leo nikifanikiwa kutoka nitapiga hii namba', lakini atamueleza nini mtu atakayepokea? lilikuwa ni swali lingine ambalo halikupata jibu. Alikirudisha kile kikaratasi kweny chupi yake tena baada ya kusikia kuwa kuna watu wanakuja upande ule.
Askari wawili wa kike walikuja na kusimama mlangoni, mmoja alikuwa na chupa ya chai na mkate,
"Chukua unywe! muuaji wewe" aliongea kwa ukali, maneno hayo yalimchoma sana moyoni Yaumi, alitamani amrukie amafanye lolote lakini haikuwezekana. Alisogea hadi mlangoni na kuchukua vile vitu.
"Kwanza jana usiku ulienda wapi?" yule askari alimuuza Yaumi.
"Nitaenda wapi wakati mi mmenifungia humu?"
"We mwanamke usijifanye mkorofi, jana usiku nimekuja hapa sijakukuta"
"Basi hujaja!"
Sonyo refu lilimtoka yule askari, kisha akampa ile chai na kuondoka zake. Yaumi alirudi na kuketi katika kile kitanda akinywa chai taratibu huku bado mawazo yakiwa mengi kichwani, hakuelewa kama alionekana wakati anatoroka au huyu askari kaamua tu kusema hivyo, hofu ilimuingia na akajihisi kutetemeka kwa woga.
Alimaliza kunywa ile chai na kusogeza vile vyombo jirani na mlango kisha akarudi na kuketi palepale na kuendelea na fikra zake, alijaribu kuvuta hisia kurudi nyuma kukumbuka matukio ya mumewe kabla ya mauaji yale labda angepata picha. Kama kuna kitu kilimjia kichwani ni zile meseji alizosoma kwenye simu ya mumewe usiku ule '...uliichukua katika ajali pale Magomeni...' hii ilimvuta zaidi, ajali ya Magomeni, akakumbuka siku ambayo mume wake alirudi na ile briefcase alimsimulia kwa kifupi tu kuwa kulitokea ajali, hakuwa na shaka kwa kuwa briefcase ile ilikuwa vilevile kama ya mumewe cha kushangaza tu iligoma kufunguka kwa namba zilizozoeleka.

TUKIO LA AJALI MAGOMENI...

ILIKUWA usiku wa saa mbili katika makutano ya barabara ya Morogoro na ile ya Kawawa, mvua ya rasharasha ilikuwa ikinyesha, Toyota Coaster moja iliyokuwa na abiria ilikuwa ikitokea Ubungo kwenda Kariakoo kwa kasi ya hatari, ilikuwa ikifanya ovateki za ghafla mpaka kila abiria alikuwa akilalamikia uaendeshaji huo.
"Utatuua bwana watu tuna familia nyumbani!" alisikika mama mmoja.Kiti cha tatu nyuma ya dereva alikuwa ameketi bwana Kajiba mikononi ameikumbatia briefcase yake yenye makabrasha yake ya biashara , vitabu viwili vya hawala za fedha na kitita cha milioni nne, alikuwa akirejea nyumbani kutoka katika makusanyo ya biashara zake. katika mtindo uohuo kiti cha nyuma kabisa kulikuwa na watu wawili walioketi hapa na hapa, mmoja wao alikuwa na briefcase ndogo inayoshahabiana kabisa na ile ya Kajiba kwa kila kitu.
Ile Coaster ilishafika katika taa za makutano ya barabara, haja ya dereva ilikuwa awahi kuvuka na taa zile za kijani lakini la, alipokaribia tu taa ya nyekundu ikawaka bila kutanguliwa na ile ya njano, kuangalia kushoto barabara inayotoka Kigogo tayari kuna semi Trailler ilikuwa imeshaingia kwani ni zamu yake kupita. Dereva akakanyaga breki kwa nguvu zake zote breki zikafeli na ile coaster ikaendelea kutiririka sasa kwa kasi zaidi na kuingia ubavuni mwa ile Trailer, lo! vilio vilisikika kila kona ile gari haikutamananika hata kidogo. Katika harakati za kutaka kujiokoa kila mtu alikuwa akifikiri njia yake, Kajiba alisimama kutoka katika kiti alichokaa baada ya kujitutumua kwa nguvu zote kwani alilaliwa na watu kutoka viti vya nyuma, alipofanikiwa aligundua kuwa ile briefcase yake haipo mkononi, akatazama huku na huko akaiona kwa mbali ikiwa kwenye sakafu ya gari hiyo, akaiwahi na kuicvhikua kisha akatoka nje ya gari na kuitazama ajali hiyo jinsi ilivyokuwa mbaya, alipogundua kuwa hajaumia popote aliamua kuondoka eneo hilo na kurudi nyumbani....
UBONGO wa Yaumi ulivuta kumbukumbu nyingi juu ya matukio ya nyuma. Alilisogelea geti lililokuwa limetenganisha yeye na wengine walio upande wa pili. Katika geti la mbele yake ambalo lilitazamana na lake na kutenganishwa na ujia wenye upana wa kupita suzuki kulikuwa na mwanamke mwingine aliyevaa juba lililomfunika mwili mzima.
Alizishika nondo za geti lile kwa mikono yote miwili na kichwa chake kukiegemeza kwenye nondo hizo kwa kugusisha paji la uso.
Mara akasikia mtu akipiga kofi moja hafifu, Yaumi aliinua uso wake na kutazama ilipotokea sauti ile. Macho ya wanawake hawa yaligongana, Yaumi alimtama mwanamke yule kwa tuo, zaidi ya macho yake aliyoweza kuyaona ni juba kubwa la kijani, zito, lililomfunika sawia. Mtazamano ulichukua sekunde kadhaa,
"Hey!" Yaumi aliita kwa sauti ya kunong'ona, lakini alishangaa yule mwanamke alikuwa akimtazama tu huku akigeuzageuza kichwa chake, Yaumi alimtazama akiwa amekunja uso, yule mwanamke akapiga tena kofi lamtindo uleule na kutoa ishara fulani kwa kutumia miko yake akimuonesha Yaumi kuwa yeye alikuwa hasikii, kiziwi.
Bahati iliyoje kwa Yaumi, kukutana na mtu wa mtindo huo. Yaumi alitikisa kichwa kuashiria ameshukuru kwa hilo, alimkumbuka baba yake mwalimu Juma Saanane aliyekuwa akifundisha shule maalum kwa watu hao, alikumbuka siku moja baba yake alimwambia,
"... Mwanangu Yaumi, jifunze lugha ya alama, siku moja utajikuta kwenye matatizo na wa kukupa msaada anajua lugha hiyo tu..."
Yaumi aliangusha machozi kumkumbuka marehemu baba yake, akamshukuru moyoni kwa unabii wake, alijifuta machozi na kuanza kuongea kwa ishara. Walipojikuta wanaelewana vizuri, urafiki mkubwa ukajengeka kati yao. Yaumi alijua kuwa yule dada ni Msomali aliyekamatwa kwa kuuza mirungi na bangi katika maeneo ya Buguruni, hayo yote alimueleza kwa lugha hiyo ya alama. Yaumi aliona kuwa ni jambo zuri kufahamiana hasa kwa lugha ambayo hakuna mwingine anaijua, kwa kutumia lugha hiyo, Yaumi alimueleza juu ya namba ile +256 na nini maana yake, bial kusita yule dada alimueleza juu ya maana ya namba hiyo kuwa ni international code ya Uganda, Yaumi alishtuka kidogo 'Uganda' akajiwazia. Baada ya kujua kuwa huyo dada Msomali anaishi Buguruni kwa Mwinyi Amani au kwa Mnyamani kama inavyotamkwa na namba ya nyumba, Yaumi alifurahi sana, aliona kuwa huyu anaweza kuwa msaada pekee kwake.
* * *
"Wewe jana usiku ulienda wapi?" sargeant Marina alimuuliza Yaumi huku wakiwa wanatzamana ndani na nje ya geti la chumba kile.
"Mi nilikuwapo, nililala uvunguni" Yaumi alijibu, jibu lilimkera sana yule askari magereza Sargeant Marina.
"Acha upumbavu we mwanamke,"
"Sio upumbavu, mi nitatokaje huku na kumefungwa, we askari mbona hutumii akili?!"
"Hivi wewe unajiamini nn? Kwa taarifa yako sasa, hukwepi kifo, jana ulitoroka na taarifa zako tunazo, usirudie tena, muuaji mkubwa wewe"
Kama kuna kitu kilikuwa kinamuudhi Yaumi ni kuitwa muuaji, alimtazama kwa jicho kali yule askari kisha akamsonya sonyo la haja lililomtia hasira yule askari.
"Kwa nini we mwanamke unanifuatafuata sana? Nimeshakumaki sura, ntadeal na wewe, najua kuwa unafahamu mengi juu ya ishu hii," Yaumi alizungumza hayo kisha akavigongesha vidole vyake, aliiona wazi hasira iliyomshika yule askari mwanzo mwisho. Sargeant Marina alimtazama kwa tuo Yaumi.
"Najua nitakachokifanya kwako subiri" Marina alimjibu kisha akaondoka zake eneo lile.
Yaumi alishusha pumzi ndefu na kujikaliza kitandani huku akipambana na mbu wa mchana, alimtazama yule swahiba wake upande wa pili hakumuona, muda ulikwenda masaa yakakatika hakumuona kurudi, hata wenzake waliporudi kutoka mahakamani yeye hakurudi, hii ilimtia hofu Yaumi, moyoni mwake alijiwekea tu kuwa swahiba wake ametoka kwa dhamana, kwa hiyo lazima amtafute labda atapata msaada kutoka kwake.
Yaumi aliendelea kutulia, alijua wazi kuwa baada ya siku tatu ni kesi yake itasomwa mara ya pili, alijuwa wazi kuwa mchezo mchafu unasukwa juu yake, bila kipingamizi alijua wazi kitanzi kilikuwa kinasukwa ili kummaliza,
'Kabla sijanyongwa, lazima nilipize kisasi kwa lifo cha mume wangu'
alijiwazia Yaumi huku akipigapiga ngumi kile kijitanda chake kisha akainamisha kichwa chake na kulia kwa kwikwi.
'Mume wangu, niongoze nijue siri ya kifo chako, nilipize kisasi kabla sijaja kuungana nawe huko kuzimu, wewe wajua kila kitu mimi sielewi chochote...'
Yaumi alifuta machozi, na kuketi kwenye kona moja ya kijichumba hicho akisukwasukwa na njaa kali maana mchana huo hakuwa nachochote cha kula, hata chai ya asubuhi hiyo hakujua ni nani aliileta. Alijaribu kufikiri kama ni busara kutoroka usiku huo ili kuweza kumuona yule Msomali japokuwa hakujua kuwa kafungwa au yuko nje kwa dhamana.
»»»
YAUMI alijilaza sakafuni njaa ilikuwa ikimnyanyasa kuliko unavyofikiria, akiwa bado katika hali ile mara alihisi muanguko wa kitu kando ya miguu yake, alipofumbua macho yake japokuwa kwa shida kidogo aliweza kuona mfuko wa plastic uliofungwa vizuri ndani yake kukiwa na mkate, pemeni yake kuna chupa ya maji aina ya Ndanda, aliviangali vitu vile lakini hakuona nani aliyevirusha humo ndani.
“Nyanyuka ule mrembo muuaji,” sauti ya sergeant Marina iliingia kwa mara nyingine masikioni mwa Yaumi, sauti asiyoipenda hata kidogo. Aliinua zaidi uso wake na kukutana na sergeant Marin aliyekuwa katika nguo zake za kazi, shati jeupe na sketi yake ya rangi ya ugolo.
YAUMI alivichukua vile vitu na kuvitazama kwa makini, kisha akamtazama tena Marina ambaye bado alikuwa amesimama palepale kwenye lile geti.
“Ulizoea kukaa kwenye meza kubwa ukila mapochopocho ya kila aina, sasa unalo hilo, kula mkate huo shushia na maji, maana usiku wa leo una wageni” Marina aliendelea na maneno yake ya unyanyasaji yaliyokuwa yakimtesa sawia Yaumi. Kma alitarajia kuwa Yaumi angekula ile mikate basi haikuwa hivyo, Yaumi alisonya na kuirushia uvungu wa kitanda, kisha akajilaza pale chini na kufunga hisia za masikio na macho yake. Sergeant Marina alikasirishwa kwa kitendo cha Yaumi, hakusema neno zaidi ya kumtazama kwa dharau na nyodo, ndipo akafuangua mdomo wake,
“Utakula tu, na njaa inavyonyanyasa, haya nitarudi baadae” akaondoka kutoka pale aliposimama. Yaumi akatazama na kumtomuona askari yule aliyekuwa mwiba mchungu kwa maneno yake.
‘Kwa nini ananifuatafuata hivi? Lazima kuna kitu’, Yaumi aliwaza akawazua; ‘Labda nisitoke humu ndani, nitakula nae sahani moja’ Yaumi alijiapia kwa hilo.
Baada ya kama masaa mawili jioni ilipoanza kuingia, Yaumi alisikia jina lake likitajwa na mmoja wa askari waliokuwa eneo hilo, mara yule askari msichana mdogo ambaye hata maziwa yake bado hayajaanguka alikuja na kumpatia chai pamoja sambusa nne, alivipokea, kutokana na njaa aliyokuwa nayo hakuuliza hata vimetokea wapi na vimeletwa na nani, alianza kuvishambulia kwa fujo, alipochukua sambusa ya pili aligundua kitu tofauti, kitu kama karatasi ndogo kilichoviringwa kwa ustadi katikati ya chembe za vitunguu ndani yake, Yaumi akakitazama kisha akakifungua na kukuta unga mweupe sana mithili ya vumbi kwa udogo wake, kwa kuwa hakujua ni nini alikikunja tena kwa mtindo uleule na kukirudisha ndani ya sambusa ile kisha akaiweka pembeni na kula ile ilobakia.
Giza lilianza kutawala nuru ya nje na mataa nayo yakaanza kuwaka kila kona, kelele za ndege katika mapori ya Segerea na Kinyerezi yalianza kupotea na ukimya kuchukua nafasi yake, ‘lazima nitoke, liwalo na liwe’ alijiwazia wakati mwili wake ukikusanya nguvu kutokana na chai ile aliyoipata jioni ile.
“Yaumi!” sauti iliita, alitazama na kumuona yule askari msichana akiwa amesimama pale katika mlango wa nondo uliokidhibiti kijichumba kile, akamuoneshea ishara ya kumuita kwa kidole kimoja, nae akaitii akaenda mpaka pale, watazamana kwa muda, yule askari akamuoneshea ishara ya kutaka kitu, Yaumi akachezesha akili yake kwa haraka, hakutambua mara moja askari yule alitaka nini.
“Unasemaje?” alimuuliza yule askari msichana
“Sambusa” alijibu. Yaumi mara moja akenda na kuitoa ile sambusa ambayo aliyokuwa ameimega kipande akamletea yule askari, akaipokea na kuchomoa kile kikaratasi kilichoviringwa na kuondoka nacho si kuelekea nje bali ndani zaidi ya lile gereza la mahabusu la Segerea. Yaumi hakuelewa kinachoendelea, alirudi na kuketi akisubiri muda wa tarumbeta ya kulala ufike ili afanye yake.
˜˜˜˜
“Sijawaelewa mnachokisema, ina maana kuna shetani lilikuja na kuingia ndani ya nyumba hiyo? Ilhali tumeifunga na ipo chini ya ulinzi kwa uchunguzi.” Sauti nzito ilisikika ikiwauliza swali hilo vijana watatu na kiongozi mwingine mmoja ambaye alionekana kuwa ndiye wa kujibu maswali hayo.
“Kwa kweli hatujaelewa katika hilo, ila hali halisi ndiyo hiyo tuliyokueleza boss” alijibu.
“REVENGE! Alitamka neno hilo kwa mara nyingine kwa utulivu wa hali ya juu, ok niachieni mimi nitajua nani na nini kimetokea, kaeni tayari kupata amri nyingine kutoka kwangu muda wowote” aliyeitwa Boss mwenye ile sauti nzito aliwaeleza kisha wote wakaondoka….
GABRIEL Matinya alivujwa na kijasho cha kwapa kwa habari aliyopewa na vijana wengi, alijaribu kuunga matukio hayakuungika, REVENGE, neno lililoandikwa kwa kutumia damu ya marehemu liliashiria hatari, lakini ni nani aliyeandika? Wakati gani? Anataka nini? Yalikuwa ni maswali machache kati ya mengi yanayotaka majibu, lakini la.
Kiti hakikutosha kutokana na hali hiyo, amani ilitoweka moyoni, afanye nini bwanyenye wa watu? Akainua mkono wa simu na kuzungusha namba fulani, kisha akasubiri sauti ya upande wa pili iitikie simu hiyo, ilipoitikia aliongea maneno machache na kutoa maagizo kadhaa ya kufanyiwa kazi..
“Hello!” sauti kakamavu ya kijana ilisikika.
“Hivi kwenye nyumba ya tukio mliweka ulinzi wa kutosha pale?” Kambale aliuliza.
“Ndiyo mkuu” akajibiwa
“Ok, naomba vijana watatu leo jioni twende pamoja nami tukahakikishe usalama”
“Sawa mkuu,” ile simu ikakatika. Baada ya dakika chache, jioni hiyo OCD Kambale alifika kituoni hapo na kukuta tayari vijana wamejiandaa, bila kuchelewa waliingia garini na kuelekea eneo la tukio.
“Sasa tukutane pale pale ili tuhakikishe tunalitia mkononi faili hilo au kujua chochote juu ya wapi lilipo” Kambale alitoa maagizo kupitia simu yake.
Haikuchukua muda kufika katika nyumba ya marehemu Kajiba, askari wawili walikuwa pale kuweka ulinzi na wale wengine nao walijiunga pamoja, OCD Kambale akifuatana na vijana watatu ambao walifika jana yake usiku na kukuta hali ya kutatanisha walizama ndani ya nyumba hiyo na kuanza kupitia kitu kimoja baada ya kingine wakipekua huku mikono yao ikiwa ndani ya gloves maalumu kuhakikisha hawaachi alama yoyote ya vidole vyao. Ijapokuwa upekuzi ulikuwa wa makini sana lakini hakuna walichokiambulia zaidi ya REVENGE iliyokuwa pale pale kwenye dimbwi la damu.
Baada ya kumaliza kazi yao wakaondoka na kurudi kituoni lakini OCD Kambale aliachana nao na kwenda kuonana na bwana G. Matinya.
Wakiwa katika sebula kubwa ya kifahari na vinywaji vikali vikiteketea katuika matumbo ya wawili hao mazungumzo yaliendelea.
“Kambale, nina hofu sana hii nyaraka ikaingia kwenye mikono isiyo salama halafu wote tukawa matatani,” Matinya alimueleza Kambale
“Yeah, ni kweli mzee, lakini nina wasiwasi mmoja, ile nyumba walikuwa wakiishi wawili tu, Kjiba na mkewe, sasa baada tu ya tukio mkewe tukamsweka rumande na nyumba tukaifunga, sasa nani anayeweza kuingia katika ndani na asionekane na askari wanaolinda! Labda shetani.” Kmabale alijibu hoja ya Matinya
“Kusema mkewe, hilo ondoa, haiwezekani, labda kama kuna mtu anayepata taarifa kutoka kwa mkewe” Matinya alieleza. Kambale alitulia akiwaza jambo, akainua bilauli yake iliyojaa pombe na kuigigida yote kinywani mwake kabla haijaenda kutulia tumboni na kuishusha mezani.
“Mzee, kuna mtu anazunguka katika hili,” Kambale aliongea kwa utulivu huku akigonga konzi kioo cha meza hiyo.
“Mmh! Unasemaje kijana?” Matinya alishtuka kidogo kama aliyekurupuliwa kutoka usingizini.
“Nasema, kuna mtu hapa anazunguka, na asipojulikana ataharibu kila kitu” kambale aliongea kwa msisitizo.
“Kambale, fanya unachoweza, mtie mkononi anayejihusisha, lakini kitu kikubwa kuliko vyote inabidi tumpate yule mwanamke ikiwezekana na tumbane atueleze juu ya hiyo nyaraka.” Matinya alikandamizia.
“Aaa mzee, yule mwanamke atafia kitanzini usiwe na shaka, sanasana hapa ni kuona tunafanyaje kumbana bila kumteka au kumtorosha pale lumande” Kambale aliongea.
“Kambale fanya hivyo nakuaminia, ile ni nyaraka nyeti sana ya serikali, jeshi litakupa zawadi kijana”.
Baada ya mazungumzo hayo waliagana na kila mtu kuendelea na hamsini zake. Matinya alinyanyuka kitini na kuuelekea mlango wa chumbani kwake kisha akaingia zake chumbani na kufunga mlango nyuma yake.
“Mh beibi kwa maongezi, hayaishi, mi mwenzio nasubiri mpaka mwili unapoa jamani, njoo unishikeshike beibi” sauti ya kike ilitokea pale kitandani ambapo Matinya alijitupa juu yake na kutokana na ukubwa wa mwili wa mzee huyo kitanda kililalamika, alipotulia alijiinamia na kuonekana mwenye mawazo sana.
“Marina!” aliita
“Be!” Marina aliitika
“Kazi niliyokupa mpenzi uliifanya?”
“Niliifanya beibi, vipi kwani?”
“Habari ninazozipata zinanipa shida moyoni, kama yule Malaya itashindikana kufa kwa kitanzi basi kitanzi cha mwisho kitanimaliza mimi” akashusha pumzi ndefu, na kuendelea, “Sikia, wewe ni sergeant wa jeshi la Magereza umejifunza medani za uchunguzi, unalionaje hili swala, nani anaweza kuingia kwenye ile nyumba ilhali imefungwa ba iko chini ya ulinzi?” Marina aliinuka na kuketi kitandani,
“Beibi, yule mwanamke ni Ninja, mi nina uhakika ni yeye aliyafanya hayo yote, lakini bado kuna utata, atatokaje katoka ulinzi madhubuti wa Magereza, labda kama ni njama za mtu mwingine nitakubali. Sasa kwa upande wa Magereza kule niachie mimi, usiku huu nitapita kuona kama yupo au hayupo, kisha utakuwa ndiyo mwisho wake, si unajua kesi yake inasomwa kesho kutwa kwa mara ya pili na ushahidi wote utakuwepo, hivyo yuko mbioni kufungwa au kunyongwa, tukichelewa tumekwisha,”
SARGEANT Marina alijitupa kitandani na bwana Matinya, mapenzi motomoto yakachukua nfasi kati ya wawili hawa, yaliyowafanya kusahau hata kama duniani kuna kufa, utundu na ufundi wote wa kuweza kumtuliza mume wa mtu yalifanyika. Baada ya zoezi zito kausingizi ka rasharasha kaliwapitia wote wawili, kengele ya saa ndiyo ilimgutusha Marina, muda wa kwenda kazini ulifika. Alikurupuka na kukimbilia maliwato kujiswafi kisha akaagana na buzi lake na kujiandaa kutoka kuliacha jumba hilo kubwa alilojengewa na bwana Gabriel Matinya, mume wa mtu aliyesahau familia na kujiweka katika hekalu hili pamoja na kimada, askari wa jeshi la magereza, sergeant Marina, mh! Duniani kuna mambo, ukishangaa ya Musa utayaona ya Firauni.
Askari wa zamu waliingia na kubadilishana na wale waliokuwapo tangu saa nne asubuhi, makabidhiano ya lindo lao yalikuwa salama kabisa, askari wanaume walikabidhiana upande wa wanaume na wale wa kike nao walikabidhiana upande wa kike. Marina aliwasili mbele ya gereza hilo na kuegesha gari lake aina ya Suzuki Swift aliyohongwa na bwana Matinya, alishuka akiwa kakunja sura kanakwamba kagombana na mtu lakini sivyo.
“Mh keshafika huyo ‘mama gereza’,” mmoja wa askari aliwaambia wenzake huku akitoka eneo lile.
“Enhe, vipi hapa kila kitu shwari?” Marina aliuliza na akajibiwa, “Shwari afande” huku wakiwa wamebana mikono yao vizuri na kwa ukakamavu mkubwa kuonesha nidhamu ya kijeshi.
Marina alipitiliza moja kwa moja na kuingia ndani kwenye ‘cell’ selo walizohifadhiwa mahabusu wale wa kike, huku akipitisha fimbo yake katika nondo za ile milango na kusababisha kelele zisizo na mpango. Alipofika kwa Yaumi akasimama na kumtazama, Yaumi alikuwa amejilaza kwa kujikunyata kwenye kona ya chumba hicho, Marina alimtazama na kuita, lakini Yaumi hakuitika, akaita mara ya pili lakini hali ikawa ileile, Marina akatulia kidogo na kuuliza mlango wa pili yake, akaambiwa tangu mchana alikuwa katika hali hiyohiyo, Marina alipatwa na hofu akawaita askari wenzake wakafungua mlango na kuingia ndani walipomtazama, walikuta amejitapikia sana, wakawafungulia mahabusu wawili wamsaidie mwenzao kasha wakamkimbiza zahanati ya magereza apo hapo katika kambi ya Segerea na kulazwa.
“Shoga vipi?” dokta Omongwe alimjulia hali Yaumi pale kitandani.
“Nataka kutimiza azma yangu,” yaumi alijibu
“Azma? Azma ya nini?” dokta alisaili kwa tuo
“Azma ya kuwasaka waliomuua mume wangu, kulipiza kisasi” Yaumi aliongea.
“Mbona wewe ndiye uliyeua shoga?” dokta Omongwe aliuliza
“Shoga, mbivu na mbichi utazijua, fsnys tulivyoongea”
“haina shida shoga, wewe nakuaminia hata tulivyokuwa jeshini mambo yako niliyajua, ulivyokuwa ukimtoroka afande Yombayomba, ila shoga tafadhali usichelewe maana utaniharibia hapa, namba yangu unayo, haya mzigo wako huu hapa”. Omongwe alimkabidhi Yaumi mfuko wa Rambo na kuuficha chini ya godoro na kujilaza kimya.
Usiku wa saa sita, dokta Omongwe almuamsha Yaumi. Yaumi alielekea chooni na kuvalia baibui lake kisha tax ilikuja mpaka pale, tax iliyozoelewa kumchukua Omongwe mara kwa mara na kumpakia Yaumi kisha kuondoka nae, walitoka pale gerezani mpaka stendi ya daladala ya segerea.
“Niache hapa kaka,” alimwambia dereva
“Sista kasema nikuache home” dreva alileta ubishi kidogo
“Mi mwanamke bwana nina mambo yangu bwana, niache hapa ntakucheki baadae”
Yaumi akashuka na kusubiri yule dereva aondoke eneo lile, alipohakikisha kila kitu kipo sawa alichukua bodaboda. “Kaniache Tabata Liwiti” alimwambia jamaa wa bodaboda na safari ikaanza mpaka Kimanga, pale alitembea kwa mguu na kukatiza vichochoro viwili na kufika Bondeni Lodge, akingia mapokezi na kuomba funguo ya chumba chake akapewa na kuingia, jambo la kwanza ni kuangalia ile mali yake aliyoificha juu ya dari akaikuta kama ilivyo, jambo la pili akavalia jeans yake iliyomkaa vizuri kabisa na kuibana ile bastola iliyoshibishwa risasi nane na za akiba katika mfuko wa suruali, pesa kidogo mfukoni, tshirt nyeusi na kakoti ka ngozi juu, kofia ya cape ilimfunika sawia kichwa chake, kiatu cha raba ‘saucony’ kikauhifadhi mguu wake, Yaumi alikuwa tayari, akatoka na kuaga pale mapokezi.
“Dada hupumziki? Kufika na kuondoka na jana hivyohivyo” alihoji muhudumu wa mapokezi.
“Kazi mdogo wangu lazima niwe hivyo” alimjibu huku moyoni akimwambia ‘acha umbea mtoto wa kike’, yaumi akaingia mtaani, safari ya kwanza ikiwa nyumbani kwake Kimanga kuona kama mtego wake umenasa lolote, hicho tu.
Alifika na kupita mbele ya nyumba ile, alishangaa kuona ule utepe wa polisi haupo tena na hakuna ulinzi wowote, alizunguka nyuma na alipohakikisha hakuna anayemuona aliuchukua ufunguo pale anapouweka na kufungua mlango wa uani kisha wandani, na kwa tahadhari kubwa alitembea kwenye kikorido kwa nuru hafifu inayoto nyumba jirani na kuingia kupitia dirisha kubwa la mbele, moja kwa moja alifika kwenye pazia la kutengenisha sebule na korido akatulia na kusikiliza kama kuna lolote, kimya, akaingia sebuleni huku bastola yake ikiwa mkononi maana alihisi nywele kumsisimka, kisha akaliendea kabati kubwa na kusukuma kioo na kuchukua kitu Fulani alichokihifadhi hapo, alipokuwa anageuka kutoka eneo lile, alisikia stuli ikisogezwa,
“Tulia apo hapo, nilikuwa nakusubiri wewe mwana haramu unayeharibu mipango ya watu, kumbe mwanamke!” aliyasema hayo kijana mmoja mkakamavu aliyekuwa amekaa katika stuli iliyokuwa kwenye kona moja ya nyumba, Yaumi alijua hapa habari imekwisha, kama umeme aligeuka akiwa tayari bastola yake imeshaondolewa usalama, kidole kwenye trigger, bila kuangalia sawasawa aliona tu kivuli cha mtu, moja kwa moja akalenga alipoona yeye ni sahihi na kufyatua, Colt 45 ikafunguka na kupiga pigo moja la karibu, risasi iliyotua sawia katikati ya uso wa mlengwa, na kupaishwa kabla ya kujibamiza ukutani na kuanguka kama mzigo juu ya meza ndogo iliyopambwa kwa ua la kichina, bila kutoa sauti, roho ikaacha mwili. Yaumi akasonya na kuirudisha bastola yake vizuri kasha kitendo cha haraka, akausogelea ule mwili na kuingiza mikono mfukoni akatoa kila kilichopo, hakujali damu inayomwagika kwenye kichwa kilichofumuliwa vibaya cha mtu huyo ambaye hata sura yake hakuitambua kama ni mjomba wake au la, alipohakikisha kila kitu anacho akatoka pale sebuleni haraka haraka, akasimama, akakumbuka kitu, akarudi na kuwasha kitochi chake akatazama huku na huku apale chini na kuokota ganda la ile risasi na kulitia mfukoni kisha akatokea mlango alioingilia, safari hii hata funguo hakuona haja kuiacha, akatokomea zake mpaka barabarani, akachukua bodaboda mpaka Tabata Liwiti kasha Bondeni Lodge.
“Dada, mi sikai tena nimepata safari ya dharula” akalipia chumba na kuchukua vitu vyake na kutokomea kusikojulikana.
˜˜˜˜
GABRIEL Matinya alikuwa amejilaza kitandani usiku huo akisubiri habari yoyote imfikie lakini kimya kilitawala hadi saa tisa usiku, mawazo yalimchukua akili yake, akaivuta simu yake na kutazama, hakuna ujumbe wala nini, akabofya namba ya mmoja wa vijana wake, Scogon, lakini namba iliita na haikupokelewa, ‘Hawa jamaa vipi, mbona siwaelewielewi’, Matinya alionekana kuchanganyikiwa, alinyanyuka pale kitandani na kuliendea kabati la nguo aliposimama mbele yake akajicheka maana hakujua hata anaenda kufanya nini au kuchuku nini, akarudi kitandani na kuchukua tena simu yake kwa mara nyingine, sasa lipokuwa anabonyeza tu na simu nyingine ikaingia kwa fujo, alipotazama kioo ‘Opereshen 01’, Matinya akatabasamu na kuipokea kwa madaha,
“Nipe habari haraka”, ukimya ukatawala, kilichosikika ni mihemo ya mtu kama anakimbizwa, “We nini, sema basi mbona unanihemea tu kama unavyomuhemea mwanamke wako kitandani,” aliwaka Matinya.
“Kiongozi,” akatulia kidogo, “Sema,” Matinya akaamuru, “Man down,” akajibu na kutulia, “What, very good vijana, mmemmaliza ee? Nakuja sasa hivi” aliingea kwa shangwe Matinya
“No, no, Kiongozi,” yule mtu aliikatisha furaha ya Matinya, “Sasa nini?” aliliza kwa mshangao wa taharuki,
“Tumepambana na adui, Mdumi ameuawa na adui katoroka” Scogon alitoa taarifa ya uongo ili tu isionekane kama yeye na mwenzake walitoka na shughuli zao zingine. Matinya alijikuta akikaa chini na kushusha pumzi ndefu, akabaki machokodo…
“Adui umemuonaje? Mwanamke au mwanaume?” Matinya aliuliza. Scogon aliona swali hilo kuwa ni la mtego, alitulia kidogo kisha akafungua kinywa chake, “ Aaa, alikuwa amevaa suruali na tshirt na pia eneo la mapambano lilikuwa na giza, hivyo sikung’amua kama ni mwanamke au mwanaume”
“Ok, rudini na muuache huo mwili huko nitaongea na mhusika aushughulikie” Matinya alimueleza Scogon kisha amri ikatekelezwa.
Scogon, na Simbila walionoka eneo lile na kurudi maskani.
Wakijipanga njiani ni lipi la kusema pindi wakikutana na boss Matinya.
*****
YAUMI alichukua boda boda na kuomba apelekwe moja kwa moja eneo la Ukonga njia panda Segerea, alishuka na kumlipa mtu wa bodaboda kisha alipohakikisha ametoweka eneo lile akatafuta mahali pa kujihifadhi. Mshangano Guest House, Majumba sita, ilikuwa ni gesti sahihi kwake aliijongelea na kuuliza kama vyumba vipom jibu halikuwa lingine zaidi ya vipo.
Akiwa ndani ya chumba alijitupa kitandani na kujilaza, mara usingizi ukataka kumchukua akaamka ghafla na kutizama saa yake ilikuwa saa tisa kasoro, akaifikiria nafsi yake akajiuliza maswali mengi, hakujua nini cha kufanya, ameua, jambo ambalo hakuweza kuliamini moyoni mwake. Aliichukua simu ya mumewe na kuiwasha kisha akaiweka mezani kwa dakika kadhaa ili aweze kupata ujumbe wowotw kama utaingia, lakini haikuwa hivo. Yaumi alirudia kusoma zile meseji za vitisho alizotumiwa mumewe na kulaumu kwa nini mtumaji aliificha namba yake, kwa maana kama asingeificha basi ingekuwa kazi ndogo kumpata, lakini kwa kuificha namba ile kazi kwa Yaumi ilikuwa ni ngumu lakini alijiapia kuwa lazima ampate, kwa udi na uvumba. Simu ya Yaumi iliita alipotazama kioo alikuwa ni dokta Omongwe.
“Oya muda, fanya fasta wanoko washaanza pitapita” Omongwe alimaliza na kukata simu. Yaumi alifunga vizuri vitu vyake na kama kawaida alivipandisha darini, alikuwa na bahati kila chumba anachopanga ndicho chenye tundu la kuingilia juu a dari. Alitoka mpaka mapokezi na kumwambia yule mhudumu kuwa anatoka anaingia kazini atarudi jioni inyofuata. Kisha kama kawaida akachukua bodaboda mpaka Segerea na kuikuta tax ikimsubiri, ileile aliyokuja nayo.
“Ah, mi nilifikiri ndiyo umeondoka vile!” aliuliza dereva tax
“Aaaa, hapana mi nilienda kwa shemeji yako tu sasa narudi kwa sista ili alfajiri tuondoke wote.
Ile tax ilisimama mbele ya zahanati ile na dokta Omongwe akaja na kutazama uku na huku alipoona hakuna shida yoyote alimshusha Yaumi na kumwambia aende chooni moja kwa moja.
˜˜˜˜
Sergeant Marina, alikuwa ameketi katika kitanda cha Yaumi pale zahanati, aliingia pale muda mfupi tu kabla ya Yaumi kurudi. Mara Yaumi aliletwa chumbani na dokta Omongwe akisaidiwa na nesi mmoja, yaumi alikuwa na drip iliyochomwa mkononi mwake, huku yule nesi akiwa ameishikilia kwenye kile kining’inizio chake, Yaumi alikuwa akitembea taratibu kwa maumivu makali mpaka kitandani, Marina alimpisha na kusaidia kumlaza kitandani.
“Jikaze mwanamke, hujui kesho unasimama kizimbani?” Marina alianza maneno yake ya uchokozi. Yaumi alimtazama na moyoni alipata uchungu sana, ‘Ipo siku yako’ alijisemea moyoni mwake na kujilaza kitandani. Marina alinyanyuka na kumuaga dokta Omongwe kisha akarudi gerezani kuendelea na kazi zingine. Omongwe alimwangalia mpaka anapoishia akatikisa kichwa na kuendelea kujipumzisha pale alipoketi. Yaumi alitoa lile shuka usoni na kutulia akiwa mwenye mawazo mengi, Omongwe alikuja kumtazma,
“Vipi maendeleo yako?” alimuuliza
“Naendelea vyema,” Yaumi alijibu “Umeanza kupata nafuu dhidi ya ugonjwa uliokuleta huku?” Omongwe alihoji,
“Ndiyo, kidogo afadhali naanza kuona mwanga wa matumaini, mwanga ambao bado una giza jembamba” Yaumi alimjibu Omongwe huku akimkabidhi kitu mkononi mwake, Omongwe alikipokea bila kujua ni kitu gain kisha akakitazama, ganda la risasi colt 45 lilikuwa mkononi mwake, “Vipi tayari?” alihoji.
“Ndiyo, one down! Kasikilize redio na TV utasikia”alipomaliza kusema hayo akajilaza tena na kujifunika kisha akaanza kulia kumuomboleza mumewe, mr Kajiba.
˜˜˜˜
HARD ROCK CAFÉ – Dar es salaam
“Sasa, mheshimiwa ni nimekuita hapa kwa swala dogo sana, wewe unanijua mimi ni nani na mimi nakujua wewe ni nani, kama sijakosea wewe ndiyo umeshika ile kesi ya mauzji ya yule dada Yaumi, sivyo?” aliuliza bwana Gabrieli Matinya huku akimtupia macho makali aliyekuwa mbele yake, jaji Ramson Semindu.
“Aaa, yeah, ni mimi nimepewa ile kesi, na kesho itasomwa tena pale mahakama kuu ya Kisutu” alijibu Ramson.
“Oooh! Good, nafikiri ushahidi wote wa kesi ile umekamilika bila shaka” Matinya aliongea kwa sauti ya upole.
“Aaa mzee, sasa tusiendeshe mahakama hapa, sio mahali pake, tusubiri kesho tuone ushahidi umekamilika kiasi gani.
Gabriel Matinya alimtazama jaji huyu kijana aliyeonekana mkakamavu wa mawazo na maamuzi, Ramson alipatwa na maswali, kwanza kwa nini huyu mernyrji wake anakuwa na maswali ya mtindo huo. Akiwa katika kutafafakari, alishtushwa na kishindo juu ya meza, alipogeuka alikutana na kitita cha pesa kilichotulia juu ya meza hiyo iliyopambwa kwa glass mbili za juisi. Jaji Ramson alitahamaki, alizitazama zile pesa na kisha kumtazama yule bwana mkubwa,
“Unataka kunipa rushwa?” Ramson aliuliza kwa mshangao
“Hapana hii si rushwa hii ni hongera kwa kazi unayotakiwa kuifanya, kijana usiwe mjinga watu tupo kazini pokea kisha usikilize maagizo nitakayokupa” Matinya alizungumza kwa sauti kavu.
“We nambie tu unachotaka nifanye lakini si kwa kunipa rushwa, tena mtu mkubwa kama wewe, hapana, sema unachotaka nami nitakusikiliza na kukusaidia,” Jaji Ramson alisema..
“Ok, ipo hivi, yule mtuhumiwa ni binamu yangu, najua sheria lazima ichukue mkondo wake kadiri ya kesi itakavyokwenda, ninachotaka mimi yule mtuhumiwa umpe dhamana kesho ili arudi uraiani kwani kukaa kule anateseka ukizingatia watoto wake karibu wanakuja likizo,” Matinya alimueleza Jaji Ramson.
“Hilo lisikupe homa mkuu, haina haja ya kupoteza pesa zote hizo wakati dhamana ni haki ya mtuhumiwa.”
Siku ilofuata… Mahakamani Kisutu
Watu walijaa mahakamani siku hiyo tangu saa 2 za asubuhi, waandishi waliokuja kujua nini kitajiri juu ya kesi ya Yaumi walijana wenye canera za mnato na mjongeo wote walikuwa hapo, achana na wale wanaoitwa waandishi wa kujitegemea nao walikuwepo kujua kitachojiri. Polisi walikuwa na kazi ngumu ya kutawanya watu na kuwapanga vizuri. Ndugu wa Yaumi walifika nao kusikiliza shauri la ndugu yao, lakini hakuna hata ndugu mmoja wa bwana Kajiba aliyefika kwani wote walimtuhumu Yaumi kumuua ndugu yao, hivyo walijenga chuki juu yake.
Mara king’ora cha land cruiser ya magereza kilisikika kikitokea barabara ya Bibi Titi kueleka hapo Kisutu, ikiwa imewasha taa zake gari ile ikunja kona kushoto na kuingia katika lango kuu la mahakama hiyo kwa mbwembwe huku askari sita walikokuwa na silaha walikuwa wakiweka ulinzi wa kina katika gari hilo.
Sekunde chche baadae, Toyota vitz nyeusi iliingia taratibu na kusimama katika maegesho ya mahakama hiyo. Hakuna aliyeshuka na wala hakuna aliyekuwa na muda wa kuliangalia gari hilo. Kutoka kwenye ile gari ya Magereza watuhumiwa kama watano hivi walishuka wakiwa na pingu mikononi mwao, Yaumi alikuwa na pingu mikononi na minyororo iliyofunga miguu yake, alisindikizwa na askari Magereza wa kike mpaka kwenye benchi maalumu ndani ya mahakama hiyo na kuketishwa.
Haikupita muda, mahakama ilianza, Jaji Ramson aliketi katika kiti chake huku upande wa chini kukiwa na muendesha mashitaka, karani wa mahakama pamoja na wakili wa serikali, wote wakiwa tayari kuendesaha kesi hiyo iliyovuta wengi. Kama ilivyo ada, muendesha mashitaka alisoma hati ya mashitaka kwa mtuhumiwa kama alivyofanya siku ya kwanza, baada ya kumaliza alimuachia jaji shauri hilo, naye jaji alimuuliza swali moja tu mtuhumiwa kama ni kweli au si kweli yale aliyosomewa, Yaumi alikana mashitaka na kwa kuwa upelelezi ulikamilika kadiri ya upande wa serikali, ushahidi uliletwa na kutolewa maelezo.
Kutoka katika kitengo maalum cha polisi cha utambuzi wa alama za vidole au nyinginezo kilichojulikana kama identification beureau ambacho kwa sasa kinajulikana kama foresinc beureau walisema kuwa alama za vidole zilizopatikana katika, mpini wa kisu na bastola ambazo alikutwa nazo Yaumi pembeni ya mwili wa marehemu zilikuwa ni zake bila kificho, alama za mtu wa mwisho kumshika marehemu zilikuwa pia ni za Yaumi, ushahidi wa WP Magreth ulithibitisha kuwa simu iliyopigwa marehemu alilalamika kuwa ‘Mke wangu w…ananiua’, kwa ushahidi huo, Yauimi alijikuta akitetemeka mwili mzima, lakini bado alishika msimamo wake kuwa yeye hajaua. Baada ya mambo ya ushaidi kukamilika, jaji Ramson alitoa nafasi ya dhaman kwa mtuhumiwa, ndipo alipojitokeza kijana mmoja mtanashati na kumuwekea dhamana ya shilingi za kitanzania milioni thelathini, na Yaumi akaachiwa huru kwa dhamana, kesi ikaaihirishwa mpaka baada ya mwezi mmoja uchunguzi bado ukiendelea.
Baada ya yule kijana kukamilisha mambo yote ya dhamana, Yaumi alifunguliwa pingu na ule mnyororo akaachiwa huru akitakiwa kufika tena siku ya kesi, yule kijana alimchukua Yaumi na kuingia nae katika ile Toyota Vitz.
Ile gari ilitoka maegeshoni taratibu na kuuacha uwanja wa mahakama hiyo huku ikisindikizwa na picha za waandishi wa habari.
Ndani ya Gari hiyo kulikuwa na watu wawili tu, yule kijana na dereva tu, walichukua barabara ya Bibi Titi mpaka makutano ya Ohio, na Ally Hassan Mwinyi kisha wakachukua uelekeo wa kwenda Morocco.
“Mwanamke!” yule mdhamini wake aligeuka nyuma na kuitoa miwani aliyoivaa na kumtazama Yaumi, “Uko sahihi kukana mashitaka, kwani wewe hujaua, ila kabla ya hukumu yako kuna kazi unatakiwa utukamilishie ndiyo mahakama iendelee na utaratibu wake,” maneno hayo Yaumi aliyaelewa sawia bila hata msaada wa mfasiri, aligundua kuwa ametekwa!
“Inabidi ufike kwa boss, ukatoe ushirikiano wa kutosha, tuipate briefcase yetu kisha utaachiwa huru ili usubiri hukumu yako” yule kijana alimueleza Yaumi huku aakimtumbulia macho. Yaumi akiwa kiti cha nyuma alimtemea mate yule kijana, kabla hajajiweka sawa akiwa anajifuta yale mate usoni alstukia kofi moja kali la macho, dereva aliposikia hayo ikabidi atoe gari pembeni kwa usalama. Mdumi akiwa katika kupambana na Yaumi, yule dereva alikuja kuingilia na kumshika Yaumi kwa nyuma, Mdumi kwa hasira alimpiga ngumi nzito tumboni mpaka Yaumi akajitoa yoe la uchungu.
MDUMI alimtazama Yaumi aliyekuwa kajikunja kuinamia tumbo alipoachiwa na yule dereva, akasonya na kujiweka vyema kitini huku yule dereva akijiweka tena vizuri nyuma ya usukani, Yaumi aliiona bastola iliyopachikwa vyema katika mkanda wa suruali ya Mdumi, hakufanya ajizi, kwa wepesi wa ajabu alimrukia Mdumi na kuichomoa ile bastola kisha kuimiliki mikononi mwake, kama Mdumi alifikiri mwanamke huyo hajui kutumia chombo hicho alikosea sana kwani alishuhudia ikiondolewa usalama kwa ustadi wa hali ya juu, kabla hajafanya lolote, Mdumi alifungua mlango na kutoka nje akiwa haamini kinachoendelea, mlango ukiwa umebaki wazi, Yaumi akimshuhudia mwanaume huyo akiduwaa bila kujua la kufanya, akIsogea karibu na mlango na kuufunga kisha akamuamuru dereva kuliondoa lile gari haraka,
“Tunaelekea wapi?” aliuliza yule dereva“Nyoosha tu mpaka nikikuamuru vingine” Yaumi alimjibu.
Ile Vitz ilirudi barabarani na kuvuka mataa ya Morocco ikaelekea Mwenge, hakuna aliyeongea ndani ya gari ile, dereva hakutaka hata kutikisika zaidi ya kuloa jasho ambalo halikuwapo kabla. Baada ya mwendo mrefu sana walipita Lugalo barracks na kufika maeneo ya njia panda ya Kunduchi, yaumia akamuamuru dereva kukunja kushoto na kuelekea Salasala mpaka eneo moja linaloitwa machimbo.
“Simama hapa!” Yaumi aliamuru, yule dereva akaweka gari pembeni, eneo lote lilikuwa ni mikorosho na miembe tu, hakukuwa na nyumba za watu maana zote waliziacha nyuma.
“Nataka unieleze kwa tuo, kila nitakalokuuliza, ukileta ujeuri sintosita kukufumua kichwa chako,” akameza mate na kugusisha domo la ile bastola kwenye kisogo cha yule dereva,
“Dada samahani hiyo kitu haina masikhara hata kidogo, itoe tafadhali” yule dereva alioangea kwa woga akitetemeka.
“Hilo mi silijui, haya nieleze ni nyie mliomuua mume wangu mpendwa sivyo?” alianza kwa swali la mwisho badala ya la kwanza.
“Aaah, mi sijui kwa kweli, mi naagizwa kuendesha gari tu” alijibu. Yaumi hakuisjiwa na maswali, akaendelea, “Ok, na gari lako huwa unaendesha kuanzia wapi, nataka nijue”
“Inategemeana dada angu” akakatishwa na sauti ya hasira ya Yaumi, “We bwege mi sio dada yako, na wala usinipotezee muda, sema haraka kabla sijakumaliza kama yule hayawani mwenzenu aliyevamia nyumba yangu usiku wa majuzi,” kwa maneno yale yule dereva alishtuka na kugeuka nyuma akiwa kakunja ndita usoni mwake, na kuuliza,
“Kwa hiyo we ndiyo ulimuua Jamal?”
Hapo yaumi akagundua kuwa yule maraehemu alikuwa anaitwa Jamal, akaendelea kumtazama yule dereva ambaye sasa hakuonesha uwoga tena wa ile bastola, wakati Yaumi akishangaa alistukia mkono wake ukipigwa kwa nguvu na ile bastola kumtoka mkononi, kabla hajakaa sawa ngumi nzito ilitua usawa wa shavu lake na kumfanya kudondokea upande wa pili huku kisogo chake kikijipiga kwenye kioo cha dirisha, mguno hafifu ulisikika huku akiona kama taji la nyota likizunguka mbela yake, yule dereva akajitahidi kupita kati ya zile siti mbili za mbele ili kuja upande wa nyuma, akiwa katika kupenya ili amshambulie vema Yaumi alijikuta akicharazwa kofi moja kali lililochana shavu lake na damu zikaanza kutiririka, pete ya uchumba ya Yaumi aliyovalishwa na bwana Kajiba ilikuwa imejizungusha upande wa pili wa kidole chake cha shahada ikikingwa na ile ya ndoa ili isitoke, sehemu ya lile jiwe la yaspi lilimchana vibaya yule dereva, Yaumi hakulitegemea hilo aliitazama ile pete na kuibusu, yule dereva akajishika shavuni na kukutana na damu nyingi, mara kila mmoja akakumbuka bastola na wote kwa pamoja mikono yao ikakutana kwenye sakafu ya gari hiyo wakigombea bastola, kikiri kakala, huku na kule, mikono yote iliishika bastola amabayo tayari ilikuwa imeondolewa usalama, hamad! Kidole kimoja kikafyatua trigger na risasi moja ikafyatuka na kuchimba kwenye ile sakaru ya gari, bila kipingamizi ilipenya na kulifikia tank la mafuta, petrol, bila mzaa yale mafuta yakakutana na risasi ya moto.
Lipppppp!!! Mlipuko wa ghafla ulitokea ile Toyota Vitz ilinyanyuliwa na kurushwa upande wa pili kutokana na ile nguvu ya mlipuko. Ndani ya gari hiyo kulikuwa mshikemshike, sasa sio ule wa kugombania bastola bali ule wa kutafuta pa kutokea, Yaumi alifanikiwa kutoka katika kioo cha nyuma ambaco kilikuwa kimesambaratika huku akimuacha yule dereva ambaye kwanza alitafuta jinsi ya kujinasua kati ya vile viti viwili ndipo apate nafasi ya kutoka lakini haikuwa hivyo, moto ulizidi na moshi mzito kumfanya akose nguvu na kuishia humo.
˜˜˜˜
Tumbo kubwa la bwana Gabriel Matinya lilikuwa likikisaidia kifua kupanda na kushuka kwa hasira huku macho na masikio yake yakiwa bado yameelekeza nguvu zote kwa Mdumi aliyeketi mbele yake na chupa kubwa ya maji akikata kiu.
“Unajua mi haingii akilini kabisa kama huyu mwanamke anaweza kufanya yote haya,” aliongea kwa hofu na kushusha pumzi, kisha akaendelea, “Na bila shaka yeye ndiye aliyetekeleza mauji ya Jamal,” ijapokuwa alisema hayo, Matinya bado alikuwa na utata ndani ya kichwa chake, ‘Itawezekanaje kutoka chini ya ulinzi wa askari makini wa magereza?’ jibu lilikuwa gumu.
Mara mlango ulisukumwa na wanaume wawili wakaingia, Scogon na Simbila walikuwa pale wakimtazama Mdumi aliyekuwa ameketi akiwa hana swaga. Kisha wote wakachukua nafasi zao na kuketi.
“Najua tulipanga tukutane sasa ili tumshughulikie yule mwanamke, lakini mpango wetu hauko vile” Matinya alizungumza huku akijifuta jasho kwa kitambaa chake, yule mwanamke katoroka na Sergie na hatujui huko waliko nini kinaendelea, simu ya Sergie haipatikani, ilikuwaje muulizeni Mdumi” Matinya alimaliza na kujiegemeza katika kochi lile kubwia. Mdumi alichukua nafasi hiyo kuwasimulia kilichojiri na kila mtu alishangaa.
Scogon alimuangalia Mdumi na kujiweka vizuri kitini, akasema, “Mzee, nafikiri hapa tunapambana na mtu makini, na mwenye roho mbaya ya revenge,”
“Ni kweli, sasa sikiliza Scogon, panga kikosi chako kamili ingia kazini, nataka mniletee yule mwanamke akiwa hai kwa gharama yoyote ile na pia mjue hatima ya Sergie, kwa shida yoyote nipigieni,” Matinya alitoa amri na vijana wakaingia kazini.

˜˜˜˜
ITAENDELEA


Smart911
mahondaw
tembobreki
Malimi Jr
Six Man
Laki Si Pesa
ludist
MALOLO
CaptainRobinMorgan
@Ntalukwisa
mnadhimu mkuu wa jf
mtzmweusi
Tonyblair
big jambo
seeker of knowledge
Lee van
Kibo Jr
kagulilo1
Songa Heri
Jackal
kizaytor
Dam55
Washawasha
william
Jackal
dan oseko
kizaytor
ADK
Iron 2012
kuku mweusi
Daudi1
popie
tonier
Mtepetallah
Kanungila Karim


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simulizi : Kitanzi Cha Mwisho

Sehemu Ya Pili (2)

BUGURUNI kwa Mwinyi Amani, au kwa mnyamani kama walivyozoea kupaita wakaazi wengi wa Dar es salaam, barabara zake zilijaa tope hasa ile ya kutokea Kiembe Mbuzi, watu walikuwa wakijaribu kuruka matope hapa na pale huku wenye magari nao wakipita kwa fujo na kusababisha adha kubwa kwa watembea kwa miguu, wengine wakiwatukana kwa kukosa ustaarabu na wengine wakiishia kukasirika tu. Jioni hiyo tayari na wauza samaki walikuwa wamekwishaanza kazi yao, mioto ya vibatari iliangaza hapa na pale kiasi kwamba usipokuwa makini kwenye dimbwi la maji utakanyaga sponge ukijua tofali kumbe watoto wa mtaani wamekutegeshea ili ukitumbukia majini kwao burudani.
Miongoni mwa wote hao, mwanadada mmoja mwenye mwili wenye nyama kidogo alikuwa akitembea kwa kuchechemea akijitahidi kuvuka yale maji na matope huku macho yake yakiangaza angaza huku na kule kuangali kinachoendelea, hakuna mtu aliyemtzama mwanamke huyo kwa maana jiji hilo kubwa kila mtu kivyake. Kwa hatua zilezile za kuchechemea alivuka reli na mbele kidogo akasimama, alipoona watu hawamwangalii aliingiza mkono ndani ya nguo yake kwenye maeneo nyeti na kutoa kijikaratasi kidogo na kukisoma, sekunde kadhaa alimaliza zoezi hilo dogo na kuendelea na safari yake.
Yaumi alisimama mbele ya nyumba moja iliyoonekana kuukuu na kupanda ngazi zake taratibu hadi mbele ya mlango uliyomkaribisha kwa maandishi BGN/MNI 612 B zikiashiria namba ya nyumba na kiwanja, kabla hajafanya lolote akatokea motto mdogo wa kiume mkononi akiwa na andazi, akamwamkia Yaumi na Yaumi hakuona haja ya kumuacha bila kumuuliza, “Ujambo motto mzuri? Eti unamjua mama Naksadi?” yule mtoto badalaya kujibu alikimbilia ndani na punde tu alitoka mwanamke mrefu aliyevalia baibui kuanzia usoni mpaka miguuni, Yaumi alimtazama yule mwanamke na kumtambua mara moja akatumia lugha ya alama kuongea nae naye badala ya kujibu alishuka ngazi mbili na kumshika mkono Yaumi kisha kuingia nae ndani, moja kwa moja mpaka chumba cha wageni na kumketisha humo, kisha akatoa lile baibui lake na kubaki na jeans na tshrt nyekundu maridadi mwilini mwake, kifua chake kilichobeba matiti madogo kilimfanya aonekane mwanamke mrembo wa kuweza hata kugombea umiss, wote walibaki wakitazamana.
*****
KIKAO cha maafande wachache kilichukua nafasi katika kituo kidogo cha polisi Tabata Kimanga, taarifa za uchunguzi wa awali juu ya mauaji ya mtu mwingine katika nyumba ya marehemu Kajiba zilikuwa zikiwasilishwa. Utata uligubika juu ya kifo hicho lakini swali lilibaki kuwa je mtu huyo alifuata nini katika nyumba ya marehemu, nyumba ambayo kwa wakati huo haikuwa imekaliwa na mtu baada ya mke wa marehemu, Yaumi, kuwekwa rumande.
“Hivi tukiliongea hili jambo kitaalamu, inaingia akilini kweli mtu asiye na uhusiano wowote na nyumba hiyo aingie na kujificha ndani? Anatafuta nini? Anamngoja nani? Wakati mwenye nyumba amekufa na mkewe yuko rumande” ilikuwa ni sauti ya ACP Chonde, aliyeonekana mara kwa mara akitikisa kichwa kana kwamba kuna mdudu ndani ya ubongo wake. Akawatazama wale vijana aliowapa kazi ile na kuwauliza, “Ok, sasa ninyi mnamhofia Yaumi ndiye muuaji?”
“Ndio afande,” mmoja lijibu
“Nipe uthibitisho wako kama askari,” ACP Chonde alisema huku akijiweka sawa kitini.
“Afande, ulipotutuma kufanya uchunguzi wa ule mwili wa marehemu, pia tulijaribu kuona jeraha lake litakuwa limesababishwa na risasi aina gani, japo ilikuwa ni vigumu kwetu kutambua lakini mtaalamu kutoka makao makuu alihisi kuwa marehemu ameuawa kwa risasi ya Colt 45, na katika kumbukumbu za usalama, marehemu Kajiba alikuwa anamiliki silaha ya aina hiyo ambayo mpaka sasa haijawasilishwa kwetu, ni hayo tu afande,” alijibu yule askari.
ACP Chonde alishusha pumzi na kuizungushazungusha kalamu yake mkononi kisha akavuta kijidaftari kidogo na kuandikaandika vitu Fulani. Bado swala moja lilikuwa gumu kichwani mwa ACP Chonde, kama ni kweli aliyeua ni Yaumi, je aliwezaje kutoka rumande na kutekeleza uhalifu huo, nani alimruhusu kufanya hivyo, akili ya ACP Chonde ilivurugika na moja kwa moja akaona wazi kuwa hapo kuna jambo kama si mambo, alitaka kuwapa kazi hiyo wale vijana kukamilisha uchunguzi kule magereza lakini akaona si vyema ni bora swala hilo akalifanya mwenyewe. Aliwashukuru wale vijana na kuwaruhusu kwenda zao. Ofisini alibaki peke yake, alijaribu kupitia lile jalada upya na kuandika maswali Fulani juu ya kila kurasa aliyoona ina shida ya kueleweka na mwisho akaandika mambo ya msingi ya kufanya ili kupata utatuzi wa hilo.
˜˜˜ Kijua kikali kililitawala anga la Dar es salaam, ACP Chonde aliketi katika moja ya viti vilivyopo katika bar maarufu iitwayo Mangumi katika eneo la Segerea akijipatia kinywaji baridi kupoza kiu iliyobana koo lake kwa fujo huku akiangalia wahudumu warembo waliovalia sare maridadi wakitoa huduma safi katika bar hiyo. Akiwa mkononi na gazeti fulani alilolinunua hapo muda si mrefu aliendelea kunywa taratibu bia yake ya safari lager ladha kamili inayoridhisha zaidi, alilifungua gazeti hilo na kusoma habari mojawapo iliyopamba gazeti hilo, ‘Mauaji ndani ya nyumba ya marehemu yaitatanisha polisi,’ aliisoma habari ile kwa kina na kutikisa kichwa kuonesha kuwa umbea wa wanahabari tayari ulichukua nafasi wakati hata polisi wenyewe hajaliweka wazi jambo hili.
Aliporidhika na kinywaji hiko alinyanyuka na kulipia kinywaji chake, “Karibu tena kaka,” mhudumu mmoja alimkaribisha huku akiipokea noti ile ya elfu tano, “Keep change,” Chonde alitoa ofa hiyo bila kujitegemea, kwa kudanganywa tu na macho ya mwanadada huyo wa Kimburu.
Geti la gereza la Segerea lilikuwa limefungwa kama kawaida ya magereza yote, ACP Chonde alisukuma kijibati kidogo kilichopo kwa ndani ya lango kuu na mara mlango ukafunguliwa, akajitambulisha na kuonesha kitambulisho chake, alipoeleza shida yake moja kwa moja akapelekwa katika ofisi maalum ya ‘admission’.
Mbele yake aliketi askari mmoja mkakamavu aliyeonekana kuwa na macho mekundu kama anavuta bangi lakini ndivyo alivyozaliwa. ACP Chonde akaeleza shida yake na askari yule aliielewa vyema.
“Sasa hilo swala afande, nikupeleke kule upande wa wanawake ili wakusaidie, ila kwa uzoefu wangu sijasikia tukio kama hilo kwani hapa pana ulinzi mkali kama unavyojua magereza,” yule askari alimjibu na kisha kunyanyuka kumpeleka upande wa wafungwa wanawake, pale akakutana na staff sajini mmoja ambaye alimsikiliza lakini nay eye alionekana kupigwa na butwaa.
“Unasema ameua? Atauaje na wakati yeye tulikuwa nae hapa siku hiyo?” akamtupia swali ACP Chonde.
“Si kwamba ameua ila tunataka kujua wakati wa tukio hilo kule nyumbani kuna mahusiano yoyote? Inawezekana labda alitoroka je; yote yanawezekana afande,” Chonde alimueleza yule mwanamama sajini.
“Siwezi kukupinga, na wala tusiandikie mate,” yule mwanamama akavuta likitabu likubwa na kulipekuapekua vyema kisha akatulia kwenye kurasa fula akitembeza kidole chake kutoka juu kwenda chini, kisha akavuta simu ya mezani na kubofya namba Fulani na kumngoja mtu wa upande wa pili. Alipomaliza kuongea na simu hiyo haikupita muda mrefu akaja afande mwingine wa kike, mwembaba, mrefu na kujibu maswali kadhaa aliyoulizwa na ACP Chonde.
“Usiku wa siku hiyo zamu nilikuwa mimi, sauda na afande Marina, na nakumbuka siku hiyo Yaumi alikuwa anaumwa na alilazwa hapo katika hospitali yetu, na nilifunga mimi pingu pale kitandani,” alijibu yule dada. Kichwa cha ACP Chonde kilionekana kupata shida kidogo katika hili, akioanisha taarifa za askari wake, zinaleta ukweli kidogo na hizi huku zinamaliza kabisa, kipi ni kipi, jibu halikupatikana, akashusha pumzi nzito na kutoa kitambaa chake kujifuta jasho, akaandika vitu Fulani katika kijitabu chake, akaaga na kuondoka zake akiwa nusu kachanganyikiwa nusu mzima.
Baada ya lisaa limoja alikuwa ofisini kwa mkuu wa upelelezi wilaya ya Kinondoni akitaka kuoanisha matukio kadhaa anayohusishwa Yaumi.
“Yeah tumefanya uchunguzi wa kina sana, inasemekana kwenye ile gari kulikuwa na mwanamke pia, ila sasa hajulikani alipo, ila bado tunamsaka kwa udi na uvumba, afande unafikiri matukio haya mawili yana uhusiano?” aliuliza yule mkuu wa upelelezi.
“Aaa hatuwezi kusema yana uhusiano au hayana, lakini kitu kimoja, yule dada alipewa dhamana, na akachukulia kwenye gari aina ya vitz iliyokuwa na watu wengine wawili ndani, na hiyo iliyoungua umesema ni vitz huoni kuna uhusiano hapo?” Chonde aliuliza. Yule afisa upelelezi akatikisa kivhwa juu chini kuashiria kuwa hapo kuna kitu anaking’amua kwa wakati huo.
“Sasa na mtu wa tatu yuko wapi?” lilikuwa swali lililowatoka wote kwa pamoja kisha wakacheka na kugonganisha viganja vya mikono yao mikakamavu. Baada ya mazungumzo mawili matatu walinyanyuka na kutoka pamoja nje ya kitu hicho.
˜˜˜
Meseji moja kwenye simu ya marehemu jambazi ilifurahisha sana Yaumi alipokuwa akizisoma meseji zile, ilikuwa ni ya mapenzi, yaumi aliiangalia sana ile meseji na kubaini yule msichana ni wapi anapatikana baada ya kufuatilia mtiririko wa mazungumzo hayo, hiyo kwake ilikuwa ni jambo zuri kwani alijua akimtia dada huyo jambajamba lazima atasema tu kazi nay ale yote aliyokuwa akijishighulisha nayo huyo bwana wake. Hakuona haja ya kupoteza muda, aliitazama saa yake na kugundua tayari ilikuwa saa mbili usiku ikienda saa tatu, alijiweka tayari na kuipachika bastola yake kiunoni, tshirt ndefu iliyofuniko makalio vizuri ilimsitiri kwa hilo, akajitazama kiooni akaona yuko poa, akatumbukiza vikorokoro vyake vyote mkobani, aliamua kuhama gesti hiyo ili sasa akajipange kwa shoga yake Fasendy na siku inayofuata arudi kwenye nyumba yake aliyojenga na mumewe. Alijiweka begi lake mgongoni na kutoka ndani ya chumba chake, wakati akifunga mlango wake aligeuka upande wa pili akasimama kama aliyepigwa na shoti ya umeme na kukodoa macaho yake kuelekea upande ule.
MACHO ya afande Marina yalikutana na yale ya Yaumi, hakuna aliyeingea na mwenzake, Yaumi alianza kutweta akimwangalia Marina, mara akatoka jamaa aliyekuna Marina nakuuzungusha mkono wake kiunoni mwa Marina kisha wakatoka kuelekea nje Yule bwana akiwa hajui kilichotokea. Yaumi alikuja nyuma yake taratibu mpaka nje, akawatazama mpaka walipoingia kwenye gari moja na kuondoka. Sonyo refu likamtoka Yaumi, akaita bodaboda na kuondoka zake.
Yaumi alitembea polepole kuuelekea mlango wa nyumba hiyo iliyoonekana kuchokachoka sana kwa kuwa na umri mrefu. Aligonga mlango, binti mmoja akaja kuufungua, yaumi akaulizi kama Yule dada anayemhitaji yupo ndani, akajibiwa kuwa hayupo kaenda msibani Kimara. Akajua mara moja kuwa utakuwa ule msiba wa Yule jambazi. Akaiacha nyuma hiyo na kukodi tax kuelekea kwa Buguruni kwa Mnyamani moja kwa moja kwa Fasendy, akaingia ndani ya chumba kilekile.
“Niambie shoga,” alianza Fasendy
“Ah majanga, kule gesti nimekutana na Marina Yule askari magereza,”
“Hajakuletea noma? Simpendi mwanamke Yule!” Fasendy alilalama
“Ipo siku yake, nitamtia mkononi,” yaumi alijibu na kusonya.
“Ok, sasa ile kazi yako nimeifanya sawasawa,” Fasendy akaanza kutoa mrejesho, “Ile namba ulonipa ni namba za posta huko Kampala, Uganda.”
Yaumi alisikiliza kwa makini sana habari yote aliyokuwa akiambiwa na Fasendy, ‘Kampala’ alijiwazia, alikumbuka siku moja katika uhai wake akiwa na mumewe marehemu Kajiba waliwahi kutembelea jiji hilo, akakumbuka sehemu mbalimbali walizotembelea ikiwemo ofisi moja kubwa ya posta, akatikisa kichwa kuashiria kuwa ameelewa, ‘Kuna nini kampala?’ alijiuliza, ‘Niende?’ hakupata jibu la moja kwa moja, lakini pia hakumwambia Fasendy juu ya hilo, akalimezea moyoni na kujipanga kimawazo kwa safari hiyo.
˜˜˜
ACP Chonde aliingia ofisini kwake, moja kwa moja macho yake yakatua mezani na kukutana na bahasha ya kaki iliyofungwa vizuri, akainyanyua na kuitazama vizuri, ‘ACP Chonde’ iliandikwa kwa mashine juu yake, akaigeuza geuza na kuichana, ndani kulikuwa na karatasi dogo tu la ukubwa wa A5 limeandikwa maneno machache,
‘…najua ni jinsi gani unaipenda kazi yako na unaifanya kwa akili zako zote,lakini nakupa onyo acha kufatilia lolote linalomhusu Yaumi, ubishi wako utakuingiza matatizoni…’
ACP Chonde, akashusha pumzi ndefu na kuiweka barua ile mezani, haikua na jina la muandishi wala anwani ya ilikotoka. ACP Chonde alijikuta akitiririkwa na kijasho chembamba, na pumzi zikienda mbio kidogo kugombana kutoka katika matundu madogo ya pua za askari huyo, akaiweka bahasha ile mfukoni na ikuketi kwenye kiti chake cha chuma kilichowekwa nyuma ya meza chakavu iliyojaa majalada yaliyozagaa bila mpangilio.
Tafakari iliyoambatana na mawazo viliuteka moyo wa Chonde, alijaribu kufikiri barua hiyo ni wapi itakuwa imetoka, lakini hakupata jibu, labda angetazama muandiko ili ajue umefanana na nani lakini haiukuwezekana kwani barua hiyo iliandikwa kwa mashine, haikuwa na tarehe wala saini, ilikuwepokuwepo tu, alipouliza wenzake ni nani kaileta barua hiyo jibu alilopata ni kuwa imekutwa juu ya kaunta ya kituo, ilikuwa ni barua iliyoharibu siku ya Chonde, aliahidi moyoni mwake kuivalia njuga kesi hiyo na lolote liwalo liwe, alituliza mawazo kabla ya kuanza kufanya maamuzi juu ya hilo, ‘najua jinsi ya kumpata muandishi wa barua hii lazima niendeleepa na uchunguzi wa hii kesi,’ aliwaza peke yake huku akilivuta faili Fulani lililopo hapo juu ya meza na kuandika mambo kadhaa ambayo yeye aliona wazi kuwa yatamfaa katika kazi zake.
ACP Chonde, alikuwa askari mahili sana katika katika kazi yake, aliipenda na hata kuifanya kwa umakini wa hali ya juu, hakuogopa mtu wala kitu, daima alipenda kufanya kazi ambazo huatarisha maisha yake au hata kazi yake kama hii, alijikuta akiingia kwenye uchunguzi wa ksi hii kwa sababu tu ilikuwa katika eneo lake la kazi, Tabata Kimanga, kutokana na utata ulioigubika kesi hiyo ndipo alipoona umuhimu wa kujua zaidi nini kimejificha ndani yake.
Habari za uchunguzi huo zilimfikia bwana Matinya kupitia Marina, askari magereza wa kike, mwenye mahusiano ya kimapenzi naq bwana huyo, mtu mzito, alitwanga barua hiyo haraka na kuiingiza kituoni hapo pa si mtu kujua, na ikakutwa asubuhi ikiwa hapo, aliyeiokota ndiye aliyeiingiza ofisini kwa Chonde.
˜˜˜
YAUMI aliamua kupanga safari kwenda Kampala, Uganda. Alichokumbuka mara moja ni safari ya mwisho aliyoifanya na mumewe bwana Kajiba miaka mine iliyopita, zaidi ya hapo ni mwenyewe Kajiba tu alikuwa akienda kwa biashara zake. Yaumi hakujua jinsi ya kufika pale Kampala kwa maana ilikuwa ni mara moja na ya mwisho kwenda huko, kutokana na ujanja aliozaliwa nao aliamua kwenda kwa kupitia njia zilezile alizotumia na mumewe mwaka ule. Siku hiyo alijidamka mapema sana kama saa tisa hivi alfajiri, na breki ya kwanza ilikuwa ni CRDB tawi la Ubungo, akacheza na ATM na kutoa kitita kama cha shilingi laki mbili hivi, akihakikisha anapata nauli na hela ya matumizi njiani, alipekua kwenye kibegi chake chenye tafutishi zile alizochukua kwenye kabrasha za mumewe, akaikuta tiketi aliyosafiria miaka mingi nyuma, kama alijua kuwa itamsaidia alikuwa ameihifadhi vizuri sana. Akamba Bus Service, ilikuwa imeandikwa juu yake na jina lake lilikuwa pale chini likiwa limeandikwa kwa wino. Yaumi aliifananisha ile ya zamani na ile mpya aliyoikata alfajiri hiyo pale Ubungo zilitofautiana kidogo, hii ya sasa ilikuwa nzuri zaidi, ‘mambo hubadilika,’ alijiwazia. Saa kumi na mbili asubuhi, Yaumi alikuwa katika moja ya viti sitini vya basi hilo la Kenya, akiwa katika safari ya kuelekea Kampala Uganda, lakini kila alipojiwazia anaenda kufanya nini alikosa jibu, lakini alijipa moyo kuwa kitaeleweka uko huko akifika.
Yaumi hakupenda kumshirikisha mtu yeyote juu ya safari yake, alimuaga shoga yake Fasendy kuwa anakwenda kwao Monerumango kwa mapumziko mafupi na angerudi baada ya siku chache.
˜˜˜
Taarifa za safari ya yaumi zilimfikia Matinya, taarifa zilizotoka kwa wapelelezi wake waliokuwa wakifuatilia nyendo za Yaumi kila aendako tangu muda ule alipotoka pale nyumba ya wageni ya Mshangano, mara tua baada ya kukutana na Marina, bila kuchelewa Marina alimpa taarifa Matinya akijifanya alikuwa akimfuatilia kumbe alikuwa na mwanaume mwingine, amejikosha.
Yaumi akiwa hajui kama anafutailiwa na watu wa Matinya, aliendelea kufanya shughuli zake kama kawaida ikiwa ni pamoja na kwenda nyumbani kwake ambako sasa alikuwa haishi kwa kipindi hiki, alikuwa akitaka kuhakikisha kuwa anakamilisha kazi yake ili hata akihukumiwa kifo basi awe amejiridhisha katika hilo.
Vibaraka wa Matinya waliendelea kumfuatili na wakagundua mara moja kuwa alikuwa amehifadhiwa na shoga yake Fasendy, siku hiyo usiku huo walipopanga kumvamia Fasendy ili wampate Yaumi, lakini walikosea, walipofika kwa Fasendy hawakumkuta Yaumi tayari alikuwa amekwishaondoka kuelekea Ubungo, baada ya kumpa kibano cha maana Fasendy hakuna walichoambulia zaidi ya kuelekezwa Monerumango. Lakini kwa akili za ziada waligawana kazi, wengine Ubungo na wengine Buguruni kufuatilia gari za kwenda huko Kisarawe mpaka Monerumango. Bingo ilikuwa kwa wale wa Ubungo ndiyo waliomuona Yaumi akichukua usafiri huo wa Akamba bus, baada ya taarifa hiyo kumfikia Matinya akaona wazi kuwa lazima kuna jambo haraka kabisa akatuma watu wawili akiwemo Scogon kwa ndege ya KQ ili kufika Kampala kabla yake na kuendelea kumfuatilia ili kujua nini anakifuata huko…

KAMPALA
SAA 5:15 ASUBUHI

BASI la Akamba lililokuwa likifanya safari zake kutoka Dar es salaam mpaka Kampala kupitia Nairobi liliingia katika stendi kuu ya mabasi ya kampala, Yaumi akiwa ndani ya jeans nyeusi, fulana nyekundu iliyobeba maandishi ‘Mbongo Halisi’ alijivuta taratibu kuingia mjini, kutokana na jua kua kali, aliipachika miwani yake na kuvuka barabara mpaka upande wa pili, akaingia katika moja ya mgahawa uliopo hapo na kuketi, akaagiza kinywaji, juice ya maparachichi iliyochanganywa na maembe kwa mbali, akawa anakunywa taratibu. Alijaribu kuvuta kumbukumbu ya jiji hilo tangu alipofika miaka kadhaa nyuma, alikumbuka tu kuwa yeye na mumewe walifikia kwa rafiki yake lakini hakukumbuka mtaa gani wala uelekeo wake, baada ya kuumiza kichwa sana kwa hilo, hakuona sababu kwa kuwa alichokitaka yeye kilikuwa ni kufika ofisi za posta tu na si kingine, hakujua kuna nini hadi afike huko lakini alitaka kuhakikisha anafika siku hiyohiyo. Akanywa juice yake haraka haraka na kunyanyuka, akatoka nje na kutafuta usafiri wa kwenda huko posta, kwa kuwa alikuwa hapajui ilimbidi kuchukua tax ambayo ingemfikisha moja kwa moja mahali anapopataka.
Dakika kama kumi na tano hivi, ile tax iliegeshwa karibu na office ya posta pembezoni mwa barabara ya Kampala, Yaumi akashuka na kumlipa Yule dereva kasha akatembea taratibu kuelekea geti la kuingia katika ofisi hizo, kitu kikubwa kilichokuwa kikimpa tabu ni lugha, watu wa Uganda walikuwa wakizungumza Kiganda na kiingereza tu, alisukuma mlango na kuingia ndani, mbele yake kulikuwa na mwanadada mweusi aliyesuka nywele zake katika mtindo wa kuvutia, Yaumi aliketi kiti cha mbele yake na kumtazama dada huyu,
“Habari!” alimsalimu, Yule dada akabaki kumtazama Yaumi.
“Are you a Tanzanian?” (Wewe ni Mtanzania?) alimuuliza. Kwa kuwa Yaumi hakuelewa anachoambiwa, alifungua kibeki chake na kutoa kikaratasi kidogo akampatia Yule dada, Yule dada akakiangalia na kuingiza zile namba katika kompyuta yake, kasha akamtazama Yaumi. Yule mwanadada akamuoonesha Yaumi ishara ya ufunguo kama anao, Yaumi akatikisa kichwa kuwa anayo funguo. Wote wawili wakaongozana mpaka upande wa pili wa jengo hilo, walipofika, Yaumi aliona zile namba zikiwa zimeandikwa katika moja ya vijisanduku vidogo vidogo. Akaichukua ile funguo na kuitumbukiza katika tundu husika, ndipo alipogundua nkuwa hakuwa peke yake, mkono wenye nguvu ulimkamata kiganja chake na kuzungusha ufunguo katika kile kisanduku. Yaumi aligeuka nyuma na kukutana na mwanaume mrefu kidogo mwenye tambo la haja, kidevu chake kilichafuka kwa ndevu zilizokaa kitambo bila kunyolewa, lakini zilizokolea mafuta kwa jinsi zilivyong’aa.
“Mbio za Sakafuni, huishia ukingoni, leo huna ujanja fungua chukua kilichomo turudi Tanzania kwa ndege ya usiku wa leo,” Yule bwana akamwambia Yaumi ambaye alikosa ujanja katika hilo, akafungua kile kisanduku huku moyo wake ukienda mbio kwani hakujua ni nini atakachokikuta ndani yake, akaingiza mkono lakini hamna kitu isipokuwa kadi ndogo iliyolala ndani yake, kwa bahati mbaya alipokuwa anataka kukichukua alikisukumia ndani kikadondoka kwa ndani, akautoa mkono wake, na kumtazama Yule bwana.
“Hakuna kitu, “ alimwambia. Yule bwana akajisahau akamvuta nyuma na na kutazama ndani ya kile kijisanduku, hamna kitu! Alipogeuka nyuma kumtazama Yaumi, hamna mtu. Akasimama akaanza kuangaza huku na huku kumtafuta mwanamke huyo. Akatoka pale aliposimama na kuwaendea vijana waliokuwa wakipiga soga mitaa hiyo na kuwauliza, wakamuonesha upande ule alioelekea, Yule jamaa akavuka barabara na kujaribu kutazama, akmuona Yaumi akiishia ndani ya jengo Fulani, akamuendea mpaka katika lile jengo, hakumuona, akaingia ndani, ilikuwa ni supermarket kubwa sana, watu wengi walikuwa wakifanya manunuzi yao wakiwa hawana hili wala lile. Yaumi alikuwa bado akimtazama Yule mtu kila hatua aliyokuwa akipiga nay eye akijificha nyuma ya mashelf ya bidhaa. Yule jamaa bado alikuwa akimtafuta Yaumi kila kona hakumuona. Yaumi aliwaendea askari wanaolinda mlango katika jengo hilo, na kuwaambia kuwa kiuna jambazi linalomfuata humo ndani linataka kumuibia, wale askari wakawaita wenzao ambao walikuwa maha;lip engine kwa kutumia redio zao za upepo, wakafika na kuwapa taarifa hiyo, Yaumi akawaonesha wale askari waliokuwa na virungu mikononi mwao, wakaingia kumfuata Yule jamaa. Wakati yote hayo yakifanyika Yule jamaa alikuwa akiwaona wanavyoongea na Yaumi pale mlangoni, akaona sasa hapa mambo yataharibika, hakujali alienda palepale mlangoni na kukutana na wale askari ambao walimzuia wakitaka kumkamata, purukushani zikatokea pale mlangoni, Yule bwana aliwakamata wale askari kila mmoja kwa mkono wake na kuwagongesha vichwa kasha akapita katikati yao na kutoka nje akiangaza macho huku na huku, Yaumi hayupo.
¤¤¤¤¤ ACP Chonde alikuwa ameketi na afande Magreth, wakibadilishana mawazo juu ya kazi yao, ugumu na wepesi wake.Chonde alimshirikisha Magreth juu ya ile barua na mwenendo mzima wa kesi ile ya Yaumi jinsi inavyokanganya.
“Sasa Yaumi yupo nje kwa dhamana,nani alimuwekea hiyo dhamana?” Magreth aliuliza
“Unajua hapo ndipo penye utata, nimefanya upelelezi wangu nimegundua kuwa hii kesi ina utata ndiyo maana nimekuita uniambie siku ile ya kwanza mliyoenda na kumkamata Yaumi ni nini mlikigundua?” ACP Chonde alimuuliza Magreth. ASfande Magreth akatulia kimya kidogo na kukumbuka tukio la siku ile, simu iliyoita pale kituoni, ikisikika maneno machache “…mke wangu, mke wangu, ananiua…”, alikumbuka walipofika pale na kumkuta Yaumi akiwa ameshika kisu na bastola pembeni mwa mwili wa marehemu akiwa amechafuka kwa damu kutokana na majeraha ya marehemu. Alama za vidole zilizochukuliwa katika kitasa cha mlango na sehemu zilizotakikana zilikuwa za Yaumi. ACP Chonde akatikisa kichwa kwa taarifa hiyo, na ni kweli upelelezi uliokamilika ndiyo huo.
“Nimepata hii barua asubuhi ya jana,” Chonde akaitoa ile barua na kumpa Magreth, akaisoma, na kumrudishia.
“Kuna mkono wa mtu,” Magreth alisema, “Nasema hivyo kwa sababu hata m I nimeona vikwazo vingi sana katika upelelezi wetu, unajua ile gari iliyoungua kule Salasala na mtu mmoja kufa ni Yaumi aliyeua baada ya kuichunguza kwa kina ile gari iliypungua, ndiyo ileile iliyomchukua pale mahakamani, kifo cha Yule mtu mmoja pale nyumbani kwake ni yeye aliyeua kutokana na kwamba hakuna mtu anayejua wapi funguo ya pili ilipo au inapofichwa, hatukuaokota ganda la risasi lakini mtaalamu wa majeraha ya risasi amesema lile jeraha la marehemu ni Colt 45, na hiyo ndo silaha ambayo alikuwa anamiliki Marehemu kajiba, mpaka sasa haijapatikana na haijulikani ilipo,” Magreth aliongea kwa kirefu sana.
ACP Chonde alitikisa kichwa kukubaliana na hilo, sasa alikuwa amefunguka kimawazo katika tukio hilo, “Kwa kuwa hawataki niendelee kuchunguza, basi sasa nitachunguza nani yupo nyuma ya hili,” Chonde alimwambia Magreth.
“lakini angalia kama kuna wazee nyuma yake wasije kukukatiza maisha” Magreth alimuasa Chonde. “Ah potelea mbali tutaogopa mpaka lini?!” Chonde aling’aka.
“Kesi itasomwa tena siku mbili zijazo, unajua mtuhumiwa hayupo hapa,” Magreth alisema.
“Umejuaje?” Chonde akauliza.
“Tulikuwa tunafuatilia tujue kinachoendelea, hayupo kila kona,” magreth alijibu.
Magreth na Chonbde waliongea mengi sana siku hiyo mwisho wakaamua waunganishe nguvu kufuatilia sakata hilo iwe kwa shari au kwa heri.
¤¤¤¤¤
Ilikuwa ni katika kijia kimoja ambako Yaumi alikuwa katika harakati za kujiokoa jioni ya siku hiyo, mara ghafla mbele yake vijana watatu walisimama kumzuia njia alipotaka kugeuza arudi alikotoka Yule mtu anayemfuata naye alikuwa anakuja. Yaumi alisimama, mara wale vijana ambao mmoja wao anamfahamu fika walikuwa wakimjia pale alipo, Yaumi alichomoa bastola yake na bila kukosea maana al;ijua hapa ni ama zao ama zangu, risasi ya kwanza ilimpiga kijana mmoja kifuani ikamtupa huko, watu wakaanza kupiga makelele kuwa majambazi wamevamia eneo hilo, kizaazaa, wale waliobaki walijikuta wanashindwa kumdhibiti Yaumi, alipojaribu kufyatua risasi nyingine, lol, bastola imeishiwa, haina risasi, kumbe ilibaki moja tu na alisahau kujaza nyingine.
Kabla lolote halijafanyika, gari ya polisi ilifika eneo hilo wakashuka na kuanza kumkimbiza Yaumi ambaye alikuwa na bastola mkononi, kila walipompigia kelele asimame, yaumi hakutii, alikimbia na nyuma akifuatiwa na polisi, polisi walipoona hatii amri, mmoja wao akaamua kutumia risasi, akafyatua ya kwanza ikapiga kiatu na kumparaza kidogo wayo wa mguu wake, yaumi akaanguka chini, wakamfikia na kumtia pingu. Mtaa mzima uligubikwa na kelele za wapiti njia waliokuwa wakishuhudia tukio lile.
Polisi wa kampala walimchukua Yaumi na kumytia kwenye gari, pembeni alikuwa akiwaona wale watu waliokuwa wakimfukuza, aliwaangalia kwa jicho baya lililowaambia kuwa ‘dawa yenu ipo jikoni’.
Gari ya polisi iliondoka taratibu huku kelele za watu bado zikiwa zikipaa hewani. Yaumi alifikishwa katika kituo cha polisi kikuu pale Kampala na kutupwa ndani. Polisi waliomchukua Yule aliyepigwa risasi walitoa ripoti kuwa Yule bwana alifia palepale kwani risasi ile ilipita kwenye moyo. Mkuu wa kituo kikuu cha polisi alitulia kimya kwa muda, akaiangalia kile bastola aliyotumia Yaumi ambayo ilikuwa kwenye mfuko wa plastic, kasha akachukua hati za kusafiria za Yaumi ndipo alipogundua kuwa mwanamke huyo ni Mtanzania. “Tangu lini Watanzania wakawa na tab ia ya kuchezea silaha ovyo namna hii? Kwa jinsi walivyo waoga,” aling’aka Yule bwana mkuu wa kituo. “Nileteeni huyo mwanamke hapa,” aliamuru na Yaumi akaletwa mbele yake, wakatazamana. Yule mkuu wa kituo aliishuhudia sura ya kisasi ya Yaumi, iliyojaa hasira na uchungu, “Wewe ni nani?” akamuuliza.
“Yaumi, kutoka Tanzania,” Yaumi alijibu baada ya kuona mkuu huyo anajua Kiswahili japo cha kuombea maji.
“Kwa nini unafanya ,mauaji ya holela kwenye mitaa ya mjini wewe, wewe ni jambazi?” Yule mkuu alimuuliza Yaumi.
“Mimi sio jambazi, wala sipendi kutumia silaha, lakini nilikuwa najilinda dhidi ya watu waliokuwa wakinifuata kutokea stendi kuu ya mabasi,” akajibu.
“Ina m,aana wewe umefika leo hapa? Umefuata nini?” Yule mkuu aliuliza
Yaumi alitaka kujibu lakini akasita, akanyamaza kimya, akamtazama Yule mkuu wa kituo.
“Kwa kuwa umefanbya mauaji ndani ya nchi hii, sheria ya Uganda itakuhukumu na ikibidi utafungwa hapahapa” Yule mkuu alisema hayo na kunyanyuka akaamuru Yaumi arudishwe mahabusu….
YAUMI alirudishwa mahabusu, uso wake wote ulisawajika kwa matatizo yanayomkabili, ‘Heri ningekuwa Tanzania, ningepata wa kunisaidia, huku ananijua nani?’ alijiuliza na kuanza kulia kwa vikwifukwifu, kumbukumbu za mume wake zilirudi kichwani mwake upya kabisa akimkumbuka kwa mema yote aliyokuwa akimtendea kwa upendo mkuu. Alikumbuka alipokuja mara ya kwanza na mumewe Kajiba katika jiji hilo la Kampala, majengo marefu na mazuri yalimlaki kama mgeni mashuhuri, maisha ya raha katika mahoteli makubwa yalimfanya ajisikie peponi lakini leo hii ule ubaya wa mji huo uliojificha nyuma ya majengo yake mazuri ulimtokea waziwazi mbele yake, Yaumi alishindwa kuamini kile kinachotokea kwake kwa wakati huo, afanyeje? Hakuna la kufanya alijikunyata hapo alipo pamoja na wanawake kadhaa waliorundikwa katika chumba hicho cha mahabusu.
˜˜˜˜
TAARIFA za kukamatwa Yaumi zilifika siku ya pili katika makao makuu ya polisi Tanzania, mkuu wa kitengo maalumu cha kushughulika na Watanzania wanaokamatwa nje ya nchi kwa makosa mbalimbali aliipokea fax ya kukamatwa Yaumi baada ya kufanya mauaji hadharani katika nchi ya kigeni, kumiliki bastola ambayo hakuwa na vibali nayo kinyume cha sheria, taarifa ilisema kuwa mwanamke huyo atapandishwa kizimbani katika mahakama kuu ya Kampala kusomewa mashitaka yake baada ya masaa 24 kupita, zaidi ya hapo taarifa hiyo iliomba msaada wa polisi wa Tanzania kufikisha taarifa zozote kama mtu huyo ana makosa mengine au la.
‘Yaumi,’ Yule bwana alilifikiria hilo jina, akawasha kompyuta yake na kuingiza jina hilo kisha kuita kama kuna maelezo yoyote juu yake katika idara za usalama. Hakutegemea lolote lakini alishangazwa na faili lililofunguka mbele yake, lenye jina na picha ileile iuliyotumwa kutoka Kampala, hakuamini, aliitazama kwa makini, ‘Du, kumbe kuna wanawake Tanzania ni maninja!’ alijisemea peke yake ndani ya ofisi hiyo, akanyanyua simu yake na kuwasiliana na mwanasheria mkuu wa jeshi la polisi nchini na kumuomba kuonana nae, akakubaliwa. Yule bwana akakusanya ile fax na kuitia bahashani kisha akaelekea ofisi iliyopo kama mlango wan ne hivi kutoka yake katika jengo hilohilo la makao makuu ya polisi.
Meza moja ilikuwa katikati yao walipokuwa wakizungumzia swala hilo, “Huyu dada ana kesi pale mahakama kuu, na yupo nje kwa dhamana, hakutakiwa kutoka nje ya Dar es salaam,” alizungumza Yule mwanasheria mkuu wa jeshi la polisi, akajivuta kwa mbele kidogo na kumuinamia Yule bwana, “Hilo tayari ni kosa linguine, kesho anatakiwa asomewe shitaka lake tena pale Kisutu, wape hiyo taarifa halafu tutaona wanasemaje ili tuweke mambo sawa,” alimwambia, kisha wakaagana na kila mmoja kubaki na shughulio zake
Bwana Matinya aliketi ofisini mwake akiwa na mawazo mengi sana juu ya habari aliyoipokea, hakuamini alichoambiwa na Scogon kilichotokea huko Kampala, unyama alioufanya Yaumi, jambo lililomchanganya zaidi ni Yaumi kukamatwa, ‘Harakati zetu zitaishia wapi?’ alijiuliza huku akikunakuna tumbo lake kubwa na kubembeabembea kwenye kile kiti chake. Kwa ujumla hakuwa na raha siku hiyo, kila mlango ulipogongwa yeye moyo ulimwenda mbio, akiwaza labda watu wa usalama au sijui nani, kwa kuwa alijua dhambi inayomtafuna. Akanyanyua simu yake na kupiga namba Fulani, “Hey, Scogon, achana na huyo Malaya, panda ndege na mwenzio mrudi mara moja huku tupange plan B maana naona hiyo A imefeli, ila kitu kimoja kabla hujaondoka hakikisha unamulika ofisi ya posta ambayo huyo mwanamama alikwenda, fanya hima nasubiri habari,” kisha akaizima simu bila kusubiri jibu na kuitia mfukoni. Akanyanyuka kitini lakini kabla hajaondoka akakumbuka kitu, akaiwasha tena ile simu na kumpigia afande Marina na kumuomba wakutane chumba chao cha siri kwani alikuwa na mazungumzo ya falagha.
˜˜˜
Jioni ya siku hiyo ilimkuta ACP Chonde katika zahanati ndogo ya jeshi la Magereza pale Segerea, akitazamana uso kwa uso na Dr Omongwe, sura zilionesha wazi kama kuna kitu ambacho hakiendi sawa mahala hapo.
“Lakini wewe si nilishakupa jibu, unataka maelezo gani tena kutoka kwangu?” Omongwe alimwambia Chonde.
“Sikatai, lakini dada yangu nataka nikwambie kitu, kitu ambacho hakuna anayekijua ila mimi nakihisi nah ii itamsaidia Yule mwanamke mwenzako,” Chonde alimlainisha Omongwe kwa namna ya pekee.
“Kitu gani?” Omongwe aliuliza lakini kabla hajasema lolote, mara mlango ukafunguliwa afande Marina akaingia ndani ya ofisi ile bila hata kukaribishwa.
“Eh, jamani hugongi hodi!?” Dr Omongwe akauliza.
“Nigonge hodi hapa chumbani au chooni, nomba ule mzigo wangu maana naona huko na shem nisiwapotezee muda mie…” Marina alisema hayo huku macho yake yakitazamana na Chonde na kila mmoja kumsoma mwenzake kwa kina, alipopewa anachotaka akaondoka zake.
“Wambea wenyewe ndio hawa,” Dr Omongwe alimwambia Chonde. “Ok, unatoka kazini saa ngapi nataka tuonane mahali maana hapa hapana usalama kwa mazungumzo yetu,” Chonde alimwambia Omongwe. “Bado kama lisaa limoja hivi,” Omongwe akajibu. “Sawa, wapi tunaweza kuonana nikakusubiri?” Chonde akauliza. Dr Omongwe alishusha pumzi na kumtazama Chonde usoni, “Sikia, mi ni mke wa mtu, siwezi kukaa ovyo na mwanaume mahali popote pale zaidi ya nyumbani kwangu, kwa hiyo kwa hilo itakuwa ngumu kaka, we zungumza hapahapa” Omongwe alimwambia Chonde.
“Yaumi amekamatwa Kampala, anashikiliwa na polisi wa huko na kesho anapanda kizimbani kwa kosa la kuua,” Chonde alimwambia kwa sauti ya chini, Omongwe alishtuka na kujishika kifua kwa uchungu, “Masikini Yaumi,” alisikitika. “Yaumi una nasaba nae?” Chonde akamuuliza, badala ya kujibu Omongwe alianza kuangusha machozi, “Masikini Yaumi,” aliendelea kusikitika kwa hilo, “Ni rafiki yangu sana, nilikuwa naye jeshini JKT,” alimueleza Chonde. “Basi ndio hivyo, sasa unafikiri shoga yako utamsaidiaje kwa hilo?” akauliza tena Chonde. “Chonde, naomba nitafute kesho mchana tulizungumze hilo sasa hivi siwezi kufanya maamuzi,” alijibu Omongwe na kumuomba Chonde aondoke.
Akiwa katika pikipiki yake aina ya Kawasaki, Chonde alikuwa na maswali mengi yasiyo na majibu, alitafuta ukweli hasa wa kujua ni nini kinamfanya Yaumi kufanya mauaji hayo katika mtindo huo, ilikuwa haingii akilini. Akiwa bado na mawazo hayo, hakuangalia vizuri barabara ile ya Baracuda, gari moja aina ya Spacio ilifunga breki kali sana na kumfaya Chonde kuyumba vibaya na kuingia mtaroni, watu wakajaa eneo lile lakini kwa kuwa pikipiki ile ilikuwa na maandishi ‘POLISI’ wakamsaidia kumuinua na kumtoa eneo lile.
Daktari Omongwe alitoka kazini majira ya saa kumi na mbili za jioni na kumuachia mwenzake Kinyerezi, kichwa chake kilikuwa kikifanya kazi ya ziada, kwanza kwa nini Chonde arudi tena kumuuliza maswali yale au kutaka kujua nini zaidi kwake juu ya Yaumi, hakujielewa afanye nini, alijitupa kitandani na kupitiwa na kausingizi katamu.
˜˜˜ AFANDE Marina alifika maeneo ya Mbagala kuu mida kama ya saa mbili usiku hivi, akaegesha gari yake katika kituo kimoja cha mafuta katika eneo hilo kisha akavuka barabara na kusubiri kidogo, haikuchukua muda ilikuja gari ndogo nyeupe, hakuwa na haja ya kuuliza, alifungua mlango wa nyuma na kuingia, ile gari ikaondoka.
Baada ya kukatisha mitaa miwili mitatu, ile gari ikasimama mbele ya nyumba moja nzuri iliyojengwa kwa na kuwekwa naksi za kisasa, “Asante kijana,” Marina alishukuru na kushuka garini kisha akaingia katika nyumba hiyo, moja kwa moja katika mlango alioukusudia, akajifungia. Haukupita muda mlango mwingine ukafunguliwa nao ulikuwa ukiendea chumba hicho, bwana Matinya akajaa ndani akiwa hoi kwa uchovu, alivua mkanda wa suruali yake na kuutupia pembeni, viatu akabwaga huko, akafungua jokofu ndogo na kutoa pombe kali GIN akanywa karibu nusu chupa bila kuzimua, mambo yote hayo Marina alikuwa akimtazama tu, alijua wazi mzee huyo siku hiyo hakuwa sawa kama alivyomzoea, lakini alisubiri muda muafaka wa kumuuliza.
Alipomaliza kugida mchupa huo, akaukita chini kwenye meza, akamtazama Marina na kufungua kinywa chake, “Tukileta mchezo tumekwisha!” akamwambia. Marina akamtazama tena na kumtupia swali, “Kuna nini mpaka useme hivyo?”
“Yaumi, amekamatwa Kampala, ameua mmoja wa jamaa tuliemkodi kule ili amfuatilie, sasa endapo polisi wa kule wakisema walivalie njuga ili swala siri itafichuka,” Matinya alimjibu. “Mh, ina maana hizo Kabrasha ziko Kampala?” Marina akauliza. “Nafikiri, kwa nini Yaumi aende Kampala? Na moja kwa moja aende posta? Napata mashaka, kama zipo humo posta na akisema hilo wakazikuta, Marina, sijui tutajificha wapi” Matinya alionge kwa uchungu uliochanganyika na hasira, akanyanyua tena ile chupa yake na kujimiminia kinywaji kile kikali bila kuzimua, akaishusha kwa mtindo uleule.
“Sweetie, nina habari mpya hapa!” Marina alianza kuingiza umbea wake. Sentensi hiyo ilimgutusha matinya kutoka kwenye mawazo yake, “Unasemaje, habari gani hiyo?” akauliza. “ACP Chonde, alikuwa magereza leo akiongea sana na Dr Omongwe, nahisi kuna kitu,” Marina alizungumza. “Aaaa Chonde, ina maana ile barua hajaipata au ni mkaidi wa moyo? Namhitaji haraka sana niongee nae, hawezi kuingilia maswala nyeti kama haya wakati yeye ni kisisimizi kidogo tu,” akanyanyuka na kuchukua simu yake akapiga namba fulani kisha akaweka sikioni, “Chumba cha siri tafadhali,” akakata simu, kisha akajiegemeza katika sofa lile akipiga mluzi, akiwa katika hali hiyo, simu yake ilipata uhai, meseji ya maandishi ikaingia, akaichukua na kuisoma,
“… JNIA…” akasisoma kisha nay eye akajibu, “Chumbani haraka,” akaitupia pembeni ile simu. Marina alikuwa ametulia tuli akitazama kila kinachoendele, bado mpaka dakika hiyo Marina hakujua hasa ugomvi wa Yaumi na huyu hawara yake, Matinya, alikuwa akishobokea tu bila kujua lililopo. Siku hii akaamua kuyavulia maji mnguo akamuuliza Matinya, “Hivi bebi wangu, mi mpaka leo sijajua kwa nini mna bifu na Yaumi wakati Yule ni muuaji tu?”
Matinya alimwangalia kwa jicho kali sana Marina, akaigeuzageuza sura yake tayari pombe zilikuwa kichwani, “Wewe unachotakiwa ni kufuata ninalokwambia, kuniburudisha kitandani, na kufanya ninachotaka, swala la Yaumi na mimi liache, utalijua siku ya mwisho nitakapokununulia ghorofa na helikopta au utakapokuwa jela ukisubiri kitanzi cha mwisho,” akanyanyua tena lile chupa na kugida kwa mtindo ule ule, alipolitua tena mezani akamwuliza Marina, “Au una tatizo? Sema, kama kuna tatizo utapatiwa ufumbuzi haraka,” akabaki akimtazama. “Hapana mpenzi sina,” Marina akajibu. “Ok vizuri kama huna, hebu njoo hapa nilipokaa uichezeechezee na kuinyonyanyonya hii ndungula nahitaji burudani ya kusahau matatizo yangu, asubuhi inafika hiyo.” Marina akanyanyuka kwenye kochi lake na kuhamia kwa Matinya, taratibu akamfungua zipu ya suruali na kulichoropoa lile lililopo ndani. Mara simu ya Matinya ikaita…..
“Aaaaah, nani tena watu tupo kwenye starehe zetu,” Matinya alisema huku akiinua simu yake iliyokuwa mezani na kumsogeza pembeni Maria. “Yeah kijana (…) Ok umefika? Sawa nisubiri hapo dakika 2 tu,” Matinya akanyanyuka na kumuacha Marina pale kwenye kochi kisha yeye akapotelea kwenye mlango Fulani ambao kwa jinsi ulivyojengwa, hupita chini ka chini kama handaki na kutoke nyuma ya tatu mtaa wa nyuma, huko utokea mlango ambao waishio humo siku zote hujua ni chumba chake cha kulala, kwa kuwa hakuna hata mmoja ambaye aliwahi kuingia ndani humo zaidi ya mfanya usafi ambaye pia huingia kwa nadra sana. Akatoka nje na kuiendea gari moja ndogo iliyoegeswhwa karibu kabisa na duka kubwa la vinywaji, alipofika alifungua mlango wa gari hiyo na kujitoma ndani katika kiti cha mbele.
“Sikia kijana, kuna kazi ndogo sana ya kufanya, katika kituo cha polisi cha Tabata Kimanga kuna mtu anaitwa ACP Chonde, chukua vijana, peleleza anapopatikana, kisha…” akamuonesha ishara ya kukata kuua kwa kutumia kidole gumba chake cha mkono wa kulia kukikatisha shingoni mwake, “Pesa?” Yule kijana akauliza. “Kama hauna swali basi husingeuliza,”Matinya akamtupia bahasha moja ya khaki na yeye akaondoka zake.
Alipofika katika kile chumba chake alichomuacha Marina peke yake sasa alikuta na wengine wawili wanaume, Scogon na Simbila walikwishajumuika pamoja nao. “Marina tupishe kidogo,” Matinya alimuamuru Marina ambaye aliingia chumbani. “Nipeni habari,” Matinya aliendelea.
“Habari si nzuri kama tulivyokwambia, jamaa tuliekodi kwa pesa nyingi lakini amezidiwa na Yaumi, sasa hatuna kazi nae kwa kuwa Yaumi yuko mikononi mwa polisi,” Scogon aliongea.
“Na aliyeuawa ni nani?” matinya akauliza
“Aliyeuawa ni mtu mwingine katia wale tuliowapanga kufanikisha zoezi hilo,” Scogon akaeleza. “Ok, na ile kazi nyingine je mmetekeleza?” Matinya akaendelea kuuliza kwa shauku. “Bila shaka mzee tumeweka kitu cha masaa hivi nyuma yetu kitanuka tu, we kodoa jicho luningani,” Scogon aliendelea kutoa ripoti ya kazi, “Mmetumia njia gani ambayo mna uhakika haitaweza kugundulika Simbila?”
“Mzee, tumetumia mbinu nzuri tu, kwa Yule mwanamke aliiacha funguo katika sanduku lake la posta, kwetu ilikuwa ni nafasi nzuri sana, baada ya kuhakikishwa amewekwa nguvuni na kama ulivyotupa maagizo tulimuweka mtoto ndani ya sanduku lilelile tukamuacha humo tukiwa tumeshampa maelekezo ya muda gani wa kuamka,” Simbila alieleza hayo kwa Boss Matinya. “Sawa, sasa kuna mtu anaingia anga zetu anaitwa SCP Chonde,” wakati Matinya anasema hayo Scogon akamkatisha, “Chonde wa Kimanga?”, “Ndiyo, uyo huyo, nimemtuma kijana akammalize haraka iwezekanavyo, ninyi mnajua hii ishu ilivyo nyeti, sasa hapa kila anayeonekana kujua ni kumpoteza tu, sawa jamani? Mimi kesho nina kikao nyeti na wazee kisha nitawapa taarifa”
Baada ya kikao hicho kifupi, Scogon na Simbila waliondoka zao, Matinya alibaki juu ya kochi lile lenye raha zote za dunia, akafungua vishikizo vya shati lake na kuruhusu tumbo lake lote lionekane ukubwa wake, alihisi kama kijasho kikimtoka, mawazo yalikusanyika, akaona wazi kuwa sasa kama ni arobaini basi zinakaribia kutimia, wakati mwingine alijipa faraja lakini kila alipokumbuka kuwa ni vipi likibumbuluka alikosa raha na alihisi tumbo lake likisinyaa ghafla. Gabriel Matinya, kigogo wa idara nyeti ambayo hata ukiambiwa huwezi kuamini, aliigeuka kazi aliyokabidhiwa na mheshimiwa Rais na kufanya yale anayoyajua yeye akishirikiana na vigogo wengine wenye dhamana. Alijiinua pale kochini na kuingia mlango wa chumbani, huko alimkuta Marina keshapitiwa na usingizi muda mrefu, ‘Wanawake wengine bwana, wavivu, ona sasa keshalala,” alijisemea moyoni kisha akjitupa na yeye kitandani, ukizingatia tayari alikuwa na pombe za kutosha kichwani haikuwa kazi kuukusanya usingizi.

KITUO CHA POLISI KATI - KAMPALA

“Tuambie kulikuwa na nini katika sanduku lako la posta hapa Kampala?” askari mmoja aliuliza huku akizungukazunguka kiti ambacho Yaumi alikuwa ameketishwa, kiti cha chuma. Yaumi alikuwa amegeuzwa na kufungwa katika kiegemeo chake, fulana aliyovaa iliondolewa akabaki wazi sehemu yote ya juu. Askari Yule wa kike aliyevalia sare nadhifu ya kipolisi alikuwa akizunguka huku na huko wakati Yaumi akiwa hoi katika kile kiti, damu ambazo hazikujificha zilichirizika kutoka majeraha ya waya ule aliokuwa akiutumia Yule askari kumchapa ili aseme. “Sijui, Sijui, nilikuja kuona kuna nini lakini sikukuta kitu,” Yaumi aliongea kwa tabu sana, maana hata kichwa tu alishindwa kunyanyua, “Wewe ni Mtanzania gaidi siyo?” Yule askari akauliza tena na wakati huo waya ulitua mgongoni mwake, Yaumi alijikunja mgongo kwa maumivu lakini haikumsaidia kwani hakuweza kufikisha mkono wake mgongoni japo kuyafariji majeraha yake.
Pamoja na mateso yote aliyoyapata kwa masaa zaidi ya mawili katika chumba hicho, Yaumi hakuweza kusema lolote kwa kuwa kiukweli alikuwa hajui nini kilikuwa katika box la posta la mumewe. Yaumi alitolewa katika kile chumba akiwa hoi kwa kipigo, hakuweza kujimudu kutembea, wale askari wengine wa kike waliokuwa katika chumba kile walimfungua kitini na kumburuta mpaka katika selo ile aliyowekwa mwanzo wakamtupia huko na fulana yake wakamtupia pia, Yaumi alijilaza kama mfu.
Katika kituo hichohicho cha polisi kati jijini Kampala kulikuwa na kikao kikiendelea katika moja ya ofisi zilizopo ghorofa ya juu yake, wazee wawili na mwanamama mmoja alieonekana ndiyo mkubwa wao walikuwa na mazungumzo mazito. “Hivi mnavyoona huyu mwanamke anajua juu ya hili kweli?” Yule mama aliuliza, “Kwa kweli kwa mateso aliyoyapata hata angekuwa gaidi angesema, nahisi hana hatia, ila yamemkuta,” mzee mwingine alijibu, “Lakini hata hivyo haitaeleweka kwa kuwa lile bomu kadiri ya uchunguzi wa awali limelipukia katika box lake la posta, nani atakuelewa kuwa yeye ahusiki?” kweli ulikuwa mjadala mzito sana kati ya wazito hao, mjadala uliokuwa ukiendelea katika ofisi hiyo usiku wa manane. Mkutano huo na mateso makali ya Yaumi vilikuja baada ya mlipuko uliotokea katika ofisi hizo za posta katikati ya mji, hakuna kifo kilichopatikana kwa kuwa wafanyakazi wote hawakuwapo muda huo, lakini mali na nyaraka nyingi ziliungua na kuteketea kabisa. Ilikuwa ni hali ambayo kiukweli iliwachanganya viongozi wa usalama wa Uganda usiku huo, ilikuwa hakuna kulala. “Hujuma, hii ni hujuma,” Yule mwanamama alikuwa akiwaambia wenzake, “lakini hujuma itakujaje kufanywa na Mtanzania? Hapana huu ni ugaidi,” kila mmoja katika kikao hicho alikuwa akitoa maoni yake kadiri ya upeo wake wa kazi.
Kazi ya uokoaji na uzimaji wa moto ilikamilika alfajiri ya ya siku iliyofuatani baadhi tu ya vitu ambavyo viliokolewa, mara moja uchunguzi wa kina juu ya moto huo na wahusika wa tukio hilo vilichukua kasi.

KULIPOKUCHA – SAA 2:00 ASUBUHI

Jiji la Kampala lilikuwa katika pilikapilika zake kama kawaida, waliokuwa wakiwahi kwenda kazini walifanya hivyo na wale wa biashara nao walifungua maduka yao, kilichoshangaza siku hiyo ni zile sehemu za kuuzia magazeti, ama ukute hazina gazeti la habari na kubaki yale ya michezo au ukute kundi la watu wakiwa wanaongelea tukio la jana yake usiku, tukio la moto katika ofisi za posta.
Ilikuwa ni asubuhi hiyo ambapo bwana mmoja katika mitaa ya ya nje kidogo ya jiji la Kampala alipoamka kwa kuchelewa sana, akiwa bado hajatoka kitandani mkewe bi Eliza alikuja chumbani kwa kasi kidogo na kuingia bila hodi, “We nini?” Yule mwanaume aliuliza. “Yaliyojiri huko mjini mume wangu, mi naogopa,” aliongea Yule bi Eliza sasa akiwa kamrushia gazeti mumewe. Bwana Godfrey Kyomukama hakuamini kile anachokiona, picha ya juu katika gazeti ilikuwa ni yaule moto wa usiku wake wakati habari yenyewe ilibebwa hujuma. Alipofngua kurasa ya ndani ndipo akakutana na picha Yaumi, aliisoma habari ile kwa makini sana, akamkumbuka shemeji huyo na akayakumbuka maneno ya rafiki yake bwana Kajiba
“…hifadhi huo mzigo, mpaka nitakapouhitaji, laity mimi nikifa basi mke wangua anaweza kuuhitaji…”
Ulikuwa ni ujumbe ambao aliuambatanisha na briefcase hiyo ndogo. Iliyotumwa kwa njia ya posta kwa jina na anuani ya Godfrey Kyomukama, lakini hakuweza kuifungua briefcase kwani alikuwa hajui code namba zake, aliuchukua na kuuhifadhi vizuri sana katika chemba yake ya kuhifadhi vitu vya thamani. Alinyanyuka kitandani na kuvuta hatua mpaka kwenye picha kubwa sana iliyopambwa ukutani, akaisukuma kidogo na kubofya namba Fulani katika ukuta huo kijimlango cha chuma kikafyatuka, akaufungua vizuri na kutazama ndani, briefcase ndogo nyekundu ilikuwa ndani ya chemba hiyo juu yake ikizibeba noti nyingi za kizungu. ‘Wakati umefika!’ alijiwazia bwana Kyomukama na kurudi kitandani, sasa akawasha televisheni na kutazama kile kinachooneshwa asubuhi hiyo, alishindwa kuvumilia alioga haraka haraka na kumuaga mkewe hata hakujali kunywa chai, aliingia kwenye gari yake na kutokomea mjini. Breki ya gari ya bwana Kyomukama ilikanyagwa sawia katika maegesho ya jengo la mahakama ambako umati wa watu ulikuwa umekusanyika kushuhudia huyo gaidi wa kike kutoka Tanzania aliyesemakana kutega bomu katika ofisi za posta. Aliteremka na kujaribu kupenyapenya kati ya vijana wengi waliojazana mahali hapo. Hatimaye alifika mahali ambapo angeweza kumuaona kama si kumshuhudia shemeji yake, Yaumi, akiletwa hapo, haja kubwa ni kuhakikisha kama ni kweli ni yeye au la. Haikuchukua muda, king’ora cha gari ya polisi kilisikika na kupewa heshima zake kwa kupisha njia, ile gari aina ya Toyota Land Cruise ilisisimama karibu kabisa na mlango wa jengo hilo, vurugu kubwa ikiatokea watu wakitaka kushuhudia hilo.
Bwana Kyomukama alikuwa ni mtu tajiri sana katika Kampala, alikuwa akimiliki maduka makubwa ya nguo na spea katika miji mbalimbali ya Uganda, alifahamiana na bwana Kajiba miaka karibu kumi nyuma walipokutana katika mambo yao ya kibiashara huko Kisumu nchini Kenya, wakatokea kuelewana sana hata kuwa kama ndugu, familia hizi zilikwishakutembeleana japo mara moja, hata watoto wao walikuwa wakisoma shule moja huko USA.
Ilikuwa ni wakati wa maumivu sana ya moyo kwa Bwana Kyomukama alipomuona shemejiye akiteremshwa garini na polisi watatu wa kike, hali aliyokuwa nayo ndiyo ilikuwa ya kushangaza, hakuweza kutembea kwa nguvu zake, akajuaa lazima mateso makali yamempata kwa maana aliwajua fika polisi wa Uganda. Akatoka katika lile kundi la watu, waliomjua walimpa heshima yake na wasiomjua walimkatalia hata pa kupita. Sliingis kwenye gari yake na kuketi kimya huku kiyoyozi kikimpa faraja, alichukua simu yake na kupoga namba ya Kajiba, haikujibiwa, haikuwa mara ya kwanza, karibu wiki kadhaa sasa, lakini hakujua bwana Yule ni nini kimempata, akatulia akavuta subira…. KYOMUKAMA alifikiri kumtafuta mkuu wa jeshi la polisi pale Uganda ajaribu kuongea nae, lakini akili yake ilikataa kabisa kwa kuwa alijua kama atafanya hivyo basin a yeye ni rahisi kuingia katika wimbi hilo akaonekana ni moja kati washiriki. Ijapokuwa aliumia sana moyoni, alitamani kumsaidia shemejiye lakini alikuwa hana jinsi, hana la kufanya, machozi yalimlenga, akawasha gari na kuondoka kwa kasi kurudi nyumbani.
Alipofika alimkuta mkewe ameketi kwenye kochi akiangali matangazo ya luninga na habari iliyotawala ilikuwa ni ile ya mlipuko wa ofisi ya posta, “Karibu mume wangu,” alimkaribisha mumewe huku akimshika mkono na kumuongoza chumbani akamkumbati mara baada ya kuufunga mlango nyuma yake. “Niambie mume wangu, ni yeye?” akauliza mkewe.
“Ndiyo ni shemeji Yaumi, lakini nashindwa nimsaidieje?” Kyomukama akajibu.
“Kwa nini? Mbona mkuu wa polisi ni rafiki yako sana na pia Yule jaji, wale ukiongea nao nafikiri watamsaidia,” mke wa Kyomukama alishauri. “Mke wangu unayoyasema ni sahihi, lakini kumbuka kuwa kesi yenyewe imeshaitwa ya kigaidi sasa tukijiingiza na sisi tutawekwa chini ya uchunguzi halafu balaa linguine litazuka, hapa cha kufanya tusijihushe, ila tufanye maombi,” Kyomukama akashauri na punde si punde maombi yalianza kuifunikiza nyumba ya Kyomukama, kumuomba Mungua avunje minyororo ya shetani.
§§§§§
Kama kuna kesi iliyovuta maelfu ya watu ni siku hiyo katika jiji la Kampala ni hiyo ya Yaumi, kila mmoja alitaka kumuona huyo mwanamama anayesadikiwa kufanya uhalifu huo. Waandishi wa habari wa magazeti, redio na televisheni walikuwa pale, mashirika kwa mashirika, kila mmoja alitaka habari ambayo gazeti lake au kituo chake cha redio kingevuta macho ya wananchi. Kila kona Yaumi alijaa katika midomo ya watu.
Akasomewa mashitaka matatu, la kwanza ni kumiliki silaha kinyume cha sheria za Uganda, la pili kutekeleza mauaji kwa silaha hiyo na la tatu kutega bomu ndani ya ofisi ya posta. Yaumi hakuna alichoongea zaidi ya kulia muda wote akiwa hajiwezi kwa njaa na kiu. Baada ya kesi hiyo kughairishwa Yaumi alipelekwa katika gereza la Luzira kusubiri mwezi unaofuata ili asomewe tena kesi hiyo kwa mara ya pili. Yaumi alikuwa mpole kama kondoo anayepelekwa machinjioni, akaswekwa ndani ya moja ya selo za mahabusu katika gereza hilo, akiwa peke yake kwani alitenganishwa na wenzake kwa sababu maalumu.
Akiwa amejibanza katika kona moja ya kijichumba hicho, Yaumi alitulia tuli kama maji ya mtungini akitafakari hili na lile, akiwa katika tafakari, mbele yake aliiona taswira ya mumewe aliyekuwa akiongea nae, alimwambia maneno mengi sana ya faraja. Yaumi alibaki akilia nguo yake ilijazwa na machozi, alipoinua sura yake hakumuona tena Yule mtu isipokuwa kipepeo kidogo chenye rangi nyrusi na madoa ya njano kikirukaruka huku na huko, alikiangali kile kipepeo na kutabasamu, kile kipepeo kikaja na kutua katika mikono yake aliyoikutanisha mbele ya magoti, yaumi alikitazama kwa makini sana mpaka kilipoondoka na kutokomea nje ya vyuma vya milango hiyo. Yaumi alijikuta anabaki na tabasamu pana, sauti ikimwambia ndani yake ‘Kila kitu kitapita, usikate tamaa,’ akaendelea kubaki palepale alipo akimezwa na tafakari, mara ghafla moyo wake ulienda mbio, alipokuwa katika tafakari hiyo aliona neon REVENGE lililoandikwa kwa damu, ambalo ni yeye mwenyewe aliliandika, likampa mshtukop, akajishika kifuani, akitweta kama mbwa aliyekimbizwa huku akipigwa mawe.
§§§§§

DAR ES SALAAM- TANZANIA saa 4:30 asubuhi

‘MLIPUKO mkubwa waiteketeza ofisi ya posta Kampala, Gaidi wa kike kutoka Tanzania ahusishwa,’
Kilikuwa ni kichwa cha habari katika gazeti moja la kila siku linalotoka hapa nchini, kichwa hicho habari kilivutia macho ya walio wengi waliojazana katika mbao za wauza magazeti katika kona mbalimbali za jiji la Dar es salaam. Ndani ya ofisi moja binafsi katika jengo kubwa na zuri ambalo limepambawa kwa maandishi mazuri ya kumetameta yenye rangi nyekundu yanayosomeka JM MALL, kijana mmoja alitulia kwenye kiti chake cha kuzunguka akizunguka huku na huku akiisoma habari hiyo iliyoonesha wazi kuwa ilimvutia kwa kiwango kikubwa sana, hakutaka hata kusemeshwa na mtu alizama kabisa katika habari hiyo iliyounasa moyo wake, baada e alifunga gazeti hilo na kulitupia mezani, kisha akafungua kompyuta yake kubwa iliyokaa juu ya meza hiyo ya kisasa, akatulia kidogo kuisubiri iwe tayari kwa kazi. Mkono ukiwa katika upande wa kiti hicho ambao ulistarehe na kidole chake cha shahada kikilibonyeza shavu la kulia.
“Vipi? Tayari damu inachemka? Maana we nakujua vizuri kama ninavyokijua kidole change cha mguuni,” ilikuwa ni sauti tamu ya kike iliyomgutua kutoka katika lindi la mawazo, akamtazama mwanadada huyo aliyekuwa akisogea mezani kwake akiwa na chupa ya chai kwenye chano iliyoambatana navikombe viwili, akaitua mezani na kumtazama kijana huyo.
“Unanichokoza wewe!” Kamanda Amata alimwambia Gina kwa utani kama kawaida yao wawapo pamoja, “Tena wewe ndio ulitakiwa upate uchungu juu ya hili lakini aaaaa umetulia tu,” akaendelea kusema.
“Uchungu katika lipi?” Gina akauliza. “Mwanamke mwenzio huyu, Gaidi, amekamatwa huko Uganda, tena isitoshe Mtanzania,” Kamanada amata alimueleza Gina huku akipokea kikombe cha kahawa kutoka kwake. “Kama ye gaidi muache sheria imnyooshe,” Gina alijibu, huku akivuta kiti na kuketi sambamba na kumwangali Kamanda Amata aliyekuwa akiichezea kompyuta yake. “Aliyekupa hizo nyota za upolisi kakupendelea, maana inaonekana wajibu wako hauujui,” Amata alizidi kutania. “Hebu nambie kwanza juu ya hiyo habari maana wewe huchelewi kuharibu mipango ya watu,” Gina alimwambia Kamanda Amata. Aliweka kompyuta yake vizuri na kuanza kuchambua habari mbalimbali alizoziscan kutoka katika vipande vya magazeti tangu alipoanza kuifatilia kesi ya Yaumi, kilichomvutia zaidi ni pale aliposoma habari ya Yaumi kupewa dhamana na kisha kusadikiwa kumuuwa huyo mdhamini wake, habari hii ilimpa kiulizo Kamanda Amata, na mswali lukuki yakafuatana na hilo, ‘Kwa nini amuue mumewe? Kwa nini aue mdamini wake?” kamanda Amata alijiuliza maswali mengi ambayo hakika yalimuacha njia panda, sasa anakutana na habari ya mtu huyo akihusishwa na mlipuko wa Kampala, Kamanda Amata kutokana na uzoefu wa kazi za kiintelijensia aligundua kuwa hapo kuna ulakini, akaanza taratibu kuzifuatilia habari zote za mwanamke huyo kupitia magazeti, na vipande vyake alikuwa akiviscan na kuvihifadhi katika kompyuta yake wakati yale magazeti akiwapa wauza maandazi huko mitaani.
“Gina, huyu mwanamke kwa jinsi habari yake ilivyo, naanza kupata wasiwasi hapa kuna mchezo ama unachezwa nay eye mwenyewe kupoteza ushahidi wa kitu Fulani au anafanya hivyo kwa kujenga defence kati yake na watu Fulani, nini kinajificha, mi na wewe hatujui, sasa leo lazima niwe mgeni wake, hata kama hayupo nyumbani,” Kamanda Amata alimueleza Gina. Gina hakuwa na la kusema alibaki kimya akiisikiliza habari ile. “Kwa nini uende nyumbani kwake? Si ukaanzie kazi yako katika kituo cha polisi alichoshtakiwa, pale ungepata habari ya kwanza kabisa pindi tu alipokamatwa na nina uhakika hata aliyeshika kesi yake utampata kiurahisi,” Gina alitoa mawazo. “Yeah, sasa umeongea kama WP kabisa aliyepewa cheo chake kihalali, nitafanya hivyo mrembo wangu na nitakujulisha, mi nina uhakika kabisa hapa kuna kitu na ni lazima nikijue ni kitu gani kipo ama mbele au nyuma ya pazia hili,” akamtazama Gina, “Washa gari twende Tabata Kimanga tukaanze taratibu kujua kinachoendelea,” Gina na Amata walitoka ofisini na kuondoka kwa kutumia gari yao, wakiwa wawili tu mazungumzo yaliendelea, huku wakiendelea kukata mitaa kuelekea Tabata. Walifika katika kituo hicho majira ya saa sita mchana, walteremka garini na moja kwa moja waliiendea kaunta ya kituo hicho na kupokelewa na askari mmoja aliyekuwa katika kaunta hiyo, “Sijui niwasaidie nini wapendwa?” akawauliza. Kamanda Amata hakuwa na haja ya kuzunguka, “Mimi ni ACP Jafarry Macholo kutoka makao makuu ya polisi, niko hapa kikazi nimekuja kujua zaidi juu ya kesi ya Yaumi Mwangemi” Yule askari akakunja sura, “Ok, kwa kuwa umevaa kiraia ningependa kuona kitambulisho chako tafadhali,” Yule askari akaomba, Kamanda Amata akatoa kitambulisho na kumpatia, akakisoma na kumrudishia kisha akampa saluti yake ya ukakamavu, “Afande kesi ya Yaumi Mwangemi, ilishatoka hapa kituoni na kwa sasa ipo chini ya mahakama,” akajibu kwa nidamu ya hali ya juu. “Sawa najua, lakini shida yangu kutoka makao makuu ni kuonana na aliyeishika kesi hiyo hapa kituoni kuna mambo ya kuweka sawa ili Yule mtuhumiwa arudishwe nchini,” Yule askari akamsikiliza Kamanda kwa makini, na kwa kuwa alikwishasikia kuwa Yaumi yuko Uganda mikononi mwa polisi haikuwa shida yeye kujua kuwa hakika ACP Jafarry kaja kwa kazi hiyo. “Ok, sasa kesi hii ina watu wawili, mara ya kwanza kabisa ilishikwa na afande Margreth kwa kuwa siku ya tukio yeye ndiye alikuwa kituoni na alifanya upelelezi wa awali, baada ya kwenda mahakamani, kukatokea tukio linguine ka mauaji ndani ya nyumba yake hapo sasa uchunguzi ukashikwa na ACP Chonde mwenyewe ambaye ndiye anashika kituo hiki kwa sasa, lakini bahati mbaya hajafika mpaka sasa na si kawaida yake,” Yule askari aliendelea kuzungumza kwa utulivu. Kamanda Amata alishusha pumzi na kumwangalia Gina, “Na huyo afande Margreth yuko wapi?” Gina akauliza. “Amekwenda kufanya uchunguzi wa tukio Fulani la ubakaji huko Kisukulu,” Yule askari akajibu. Baada ya mazungumzo mawili matatu katia ya Gina na Kamanda Amata, wakarudi tena kwa Yule askari, “Ok, sasa kwa kuwa tuna shida ya haraka, tunaomba tuonane na afande Margreth, popote alipo mwambie aje mara moja,” Yule askari akanyanyua simu ya upepo na kumuamuru afande huyo arudi mara moja, bahati nzuri alikuwa tayari yuko njiani kurudi hivyo haikuchukua muda mrefu akawa tayari kituoni hapo. Yule askari wa kaunta akawatambulisha na Magreth akatoa heshima ya kijeshi kwa Kamanda Amata. Kisha wakaingia ndani ya chumba Fulani na kufanya mazungumzo yao huko.
“Kwa hiyo yaumi kamuua mumewe?” Amata aliuliza,
“Ndiyo, na uchunguzi wote unaonesha kuwa ndiye muuaji hamna la kupinga, lakini kwa kuwa mimi baada ya hapo sikuifuatilia hii kesi, ila ACP Chonde anajua mengine zaidi, kwa sababu nay eye juzi amepata barua ya kuachana na uchunguzi wa kesi hiyo na hakujua ni wapi imetoka,” habari hiyo ya barua ikamshtua Amata, kengele za hatari zikagonga kichwani mwake. Wakati Magreth anataka kuendelea na mazungumzo hayo Kamanda Amata akamkatisha kwa kumshika mkono wake pale mezani, “Chonde ana tabia ya kufika kazini saa ngapi?” Kamanda akauliza, “Huwa hana tabia ya kuchelewa, lakini leo mpaka sasa na hatuna taarifa yoyote,” Magreth akajibu, “hamuoni kama kuna hatari yoyote ambayo imemkuta labda ukizingatia na alipata barua ya vitisho,” Kamanda Amata akamfungua masikio Magreth, ukimya ukatawala. “twende nyumbani kwake kama unapajua labda anaumwa au ana shida nyingine, afande lazima ujue mkuu wako hali ya mkuu wako kila wakati,” kamanda Amata akasema hayo huku akinyanuka kitini na kufuatiwa na Gina, kisha Magreth akafuata, wakaaga kaunta kuwa wanakwenda kumuona Chonde nyumbani kwake.
Haikuwachukua muda kufika katika nyumba ya ACP Chonde pale Vingunguti Kiembe mbuzi, walimkuta kijana wa kiume walipomuuliza yuko wapi mke wa Chonde walijib iwa kuwa kaenda kazini kwa mumewe kuulizia juu ya mume wake kwani hajarudi tangu jana yake. Kamanda Amata akamgeukia Magreth, kisha akamtazama Gina, halafua akarudi kwa Yule kijana. “Jana aliondoka saa ngapi?” Magreth alimtupia swali Yule kijana, “Alitoka asubuhi kama kama kawaida akaja kazini baada ya hapo hatukumuona tena, mapaka sasa shemeji amekwenda Kimanaga kuulizia, kwa si kawaida yake,” Yule kijana akajibu. “Ok, asante sana, tutarudi baadae,” Kamanda Amata alikata mazungumzo kisha wakarudi ndani ya gari. Kamanda alimgeukia Magreth aliyekuwa ameketi kiti cha nyuma, “Afande, hapa kuna jambo na si dogo, mi nimeshapata wasiwasi, ok, kwa kuwa tulikuwa tunataka kujua juu ya kesi ya Yaumi ili kufanya mpango wa kurudishwa nchini, basi we fanya uchunguzi kisha taarifa yote umtumie huyu dada,” Kamanda Amata akamwambia Magreth kisha wakarudi hadi Kimanga wakiwa njiani, Magreth alionesha nyumba ya Yaumi kwa mbali kutoka barabarani, wakafika na kumuacha Magreth kisha wao wakaondoka zao.
“Gina, umeona hii habari inavyochanganya?” Kamanda akauliza. “Hapo nimejua kwa nini ulikuwa unaifuatilia kupitia magazeti, sasa utafanyaje, hata hivyo hili swala liko polisi na mahakamani,” Gina alijibu. “Ndiyo, ila lazima nijue kwa nini mambo yanajipanga hivi? Chonde atakuwa kapotea katika mazingira ya kutatanisha, haya je na hiyo barua aliipokea kutoka wapi na kwa nani?”
TAARIFA ya habari ya saa kumi jioni ilitangaza juu ya kuokotwa mwili wa mwanaume unaoonekana kuuawa na kutupwa kandokando ya bonde la mto Msimbazi maeneo ya Mongolandege. Kamanda Amata alikuwa akiisikiliza taarifa hiyo kwa makini sana akiwa katika gari yake akielekea nyumbani kwa mapumziko ya jioni, alivutiwa na habari hiyo kiasa kwamba aliitoa gari yake pembeni na kusimamisha kisha akaisikiliza vizuri taarifa ile iliyoishia kwa kusema kwamba mwili huo umeifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Amana. Akili ya Amata ilizunguka ikifikiri kama atakuwa ni Chonde au la. Kwa kuwa taarifa ile ilisema tu kuwa mtu huyo hakujulikana jina lake, ilikuwa ni utata juu ya utata. Kamanda Amata akasukuti kama dakika mbili hivi, kisha akainua simu yake na kubofya namba Fulani, “Hallo, unaongea na ACP Jaffary, Magreth kuna mwili wa marehemu umeokotwa kule Mongolandege, fanya hima tukutane Amana hospitali tuutambue kama ni wa Chonde au la,” Magreth akakubaliana na Amata, kisha baada ya hapo akawasiliana na Gina na kumpitia nyumbani kwake, wote wawili wakaelekea Amana.

HOSPITALI YA AMANA – saa 11:30 jioni

KAMANDA AMATA aliegesha gari panapohusika na kuteremka akifuatiwa na Gina, hatua za harakaharaka ziliwafikisha katika korido ndefu inayoelekea mapokezi. Magreth alikuwa amekwishafika hospitalini hapo, alipowaona akawaendea moja kwa moja na kuanza kufanya kazi iliyowapeleka. Kwanza walionana na daktari aliyekuwa zamu wakati huo na kumueleza shida yao, Yule daktari alikiri kupokea mwili huo lakini aliwaeleza kuwa bado haujafanyiwa uchunguzi hivyo hawezi kutoa majibu yoyote ya kifo hicho. Baada ya hapo wakiwa na mhudumu wa chumba hicho walienda pamoja kuutambua mwili huo.
Mwanaume wa haja, wliyekuwa na siha hasa ya kibabe na upiganaji, alikuwa amelazwa ndani ya mfuko wa plastiki katika kitanda cha chuma katika chumba hicho chenye hewa nzito na baridi inayoshidwa kupambana na hewa hiyo. Kamanda Amata alikisogelea kitanda hicho akiwa na Yule daktari, wakafungua ule mfuko kisha Amta akamwita Amgreth kuutambua mwili huo kwa kuwa yeye alimfahamu vizuri mkuu wake wa kazi. Afande Magreth alipoutazama mwili ule, alipatwa na mshtuko mkubwa na kukosa nguvu, kama asingekuwa Gina karibu basi yangekuwa mengine kwa jinsi ambavyo angeanguka vibaya.
“Dokta, asante, nafikiri jibu limepatikana, huyu dada hasingepoteza fahamu kama marehemu tunayemtafuta si huyu, lakini jambo moja huu mwili uhamishiwe Muhimbili ili daktari wetu kutoka wizara ya mambo ya ndani ili afanye uchunguzi wa kifo hiki,” Kamanda Amata alimweleza Yule daktari naye bila kipingamizi aliwasiliana na mkuu wake wa kazi kisha kibali kikatolewa. Jioni ile kwa kutumia gari ya wagonjwa ya hospitali ya Amana ule mwili ulihamishwa mpaka Muhimbili ambako Dr Jasmine aliupokea.
Taarifa za umauti wa ACP Chonde zikafika kila panapohusika na mwisho kabisa nyumbani kwake Vinguguti Kiembe Mbuzi.
§§§§§

HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

DR JASMINE, Kamanda Amata na Gina walikuwa katika chumba maalum cha kufanyia uchunguzi wa maiti, huku Dr Jasmine akiendelea na kazi yake hiyo Kamanda Amata alikuwa akifuatilia hatua moja baada ya nyingine katika zoezi hilo.
“Kamanda, watu waliofanya mauaji haya ni wataalamu wa kazi hii,” Dr Jasmine alisema.
“Kwa nini unasema hivyo?” Kamanda Amata akauliza. “Kwa sababu uchunguzi wa kwanza wa kawaida, huyu mtu inaoneshwa hakunyongwa, hakukabwa, hakupigwa kwa kitu chochote kile,” Dr Jasmine alijibu. Kamanda Amata akatikisa kichwa. “Ok, sasa inakuwaje hapo?”
“Naingia hatua ya pili, hii lazima itatupa jibu tu,” Dr Jasmine alitoa matumaini kwa Amata. Uchunguzi ukaendelea sasa, mwili ule ukapasuliwa na kutazamwa kwa ndani, “Kamanda njoo hapa kama una uvumilivu,” Dr Jasmine alimwita, Kamanda Amata akasogea karibu na ule mwili na kutupia jicho sehemu hiyo iliyofunuliwa, lo, ni damu iliyoganda kwenye maeneo mbalimbali ya ndani ya mwili ule. “Mh!” Kamanda akaguna, akatikisa kichwa, akarudi nyuma hatua kadhaa na kugeukia sinki la kunawia mikono lililokuwa hapo, akajitazama kwenye kioo, akatikisa kichwa. “Wamefanyaje?” akauliza kutokea kulekule alikosimama, “Wamemuua kwa kumtikisa, kwa hiyo baadhi ya viungo muimu kwa mtyikisiko ule vimenyofoka kutoka sehemu yake ndio maana damu nyingi imemwagika kwa ndani,” Dr Jasmin alimueleza Kamanda.
Kazi ilikamilika, Dr Jasmine na Kamanda Amata waliagana. “Vipi mpenzi?” Gina aliuliza wakati akiliacha geti la Muhimbili na kuchukua barabara ya Mindu. “Watu wabaya sana, wamemuua kwa njia mbaya sana. Lakini uovu haulipwi na mshahara wa dhambi mauti.

SIKU ILIYOFUATA ASUBUHI SAA 3:20

GABRIEL MATINYA alikuwa ofini kwake alipopata taarifa ya kifo cha ACP Chonde, alijifanya kusikitika ili aonekane hivyo na wasaidizi wake, lakini moyoni mwake alikuwa akifurahi kwa kuwa kikwazo kimoja amekiondoa duniani hivyo alijuwa kuwa mambo yake yataenda vizuri, alinyanyuka kitini na kuaga kuwa atarudi baada ya masaa matatu kwani ana mkutano muhimu sana. Alitoka ofini na gari ya ofisini kwa kutembea na kupita nyuma ya jengo hilo mpaka jengo linguine zuri sana lililokuwa hapo, akaingia na kukutana na Yule anayemhitaji.
“Karibu Matinya, bila shaka una habari nzuri,” mtu mkubwa alieketi kwenye kiti hicho ambacho kilionekana wazi kuonewa kwa uzito alimkaribisha Matinya kitini.
“Asante sana, bila kuchelewa, ile kazi tayari, Yule kijana ameshaondolewa kiufundi kabisa,” Matinya alifikisha ujumbe. “Ok, sasa, kama nilivyokwambia, leo tunakutana saa sita mchana kwa kikao na wale wadau, hivyo lazima uwepo tujue sasa tunalimaliza vipi hili swala kabla halijaingia katika mikono isiyostahili, itakuwa ni aibu Matinya, mtu kama mimi au wewe ambao tuna dhamana na taifa hili,” Yule bwana aliongea kwa sauti ya wastani ili katibu wake asisikie. Baada ya mazungumzo machache, walitoka ofisini pamoja na kuingia kwenye gari ya bwana huyo na safari yao ikaanza, moja kwa moja mpaka posta bandari ya Zanzibar, wakateremka ngazi na kuingia kwenye boti moja ya kifahari, ndani yake walikuta watu wengine wawili. Watu wale waliketi katika mtindo wa mduara, mmoja alikuwa ana asili ya kiarabu na hawa watatu ni weusi yaani wabantu. Ile boti iliondolewa eneo lile na lusogea katikati ya maji ili kuwapa nafasi watu hao kuzungumza yao.
“Nafikiri katika hilo, tufanye tuwezalo Yule mwanamke afe kabla hajaleta madhala makubwa,” Yule mwarabu alizungumza kuliambia lile jopo. “Hapana, tukimuua Yule, itakuwaje kwa zile kabrasha zetu? Maana mpaka sasa ni yeye anajua zilipo,” matinya alijibu.
“Hapo Matinya unaeleweka, lakini kumbuka kama ni zile kabrasha zilikuwa posat kampala zimeteketea kwa moto, hivyo tuna uwezo wa kutengeneza zingine,” Yule mwarabu alijibu, lakini mjumbe mwingine akadakia hapohapo, “Kutengeneza mpya sawa inawezekana lakini bwana Salim, tuna uhakika gani kama zile za mwanzo zimeungua?” aliuliza mjumbe Yule aliyekuja na Matinya. Hapo ukimya ukatawala, kila mmoja akiwaza lake. Kati yao mjumbe mmoja aliyeonekana kusinzia muda wote wa kikao hicho alikurupuka ghafla, “Kwa hiyo tunauza hatuuzi?” kila mtu aliduwaa, hakuelewa bwana huyo anaongelea kuuza nini, “ Mbona mnashangaa, si tumegiza mzigo nje, uje na ndio huu mnasema documents sijui zingali nini sijui, ndio nauliza tuitauuza hatuuzi?” kila mtu akaangua kicheko kati kikao hicho, hakuna aliyekuwa na jibu kwa hilo walibaki kutazamana. Yule mwarabu akaktisha ukimya huo na kuwarudisha tena katika mstari, “Sasa tufanye kinachoeleweka, kontena la ule mzigo lnafika keshokutwa hapa dare s salaam, na inabidi litolewe mara moja bila kuchelewa, sasa ninyi hapo ndio wadau, mi sina sauti,” bwana Salim alimaliza kuongea na ujirudisha katika kiti chake huku akikiruhusu kinesenese kumpoa raha. “Mheshimiwa, fanya unaloweza, Yule mwanamke arudi hapa nchini, na anaporudi atekwe kabla hajafika Mahabusu,” Yule bwana mkubwa akamwambia Matinya. “Sawa nitaandaa mazingira kwa jinsi ninavyoweza na Yule mtuhumkiwa atafika kabla ya kontena kufika,” Matinya akawapa uhakika wa hilo kisha wakavunja kikao, wakakubaliana kukutana siku inayofuata. Kila mtu alirudi kuendelea na majukumu katika ofisi yake, hilo linguine lilikuwa tu jukumu la ziada. Wajumbe waliokuwa kati kikao kile wote baada ya kupata taarifa ya kuuawa kwa Chonde iliyotolewa na bwana Matinya walionekana wazi kufurahishwa kwa hilo.
§§§§§
GABRIEL MATINYA alikuwa amekutana na vijana wake mchana wa siku hiyo, pombe zikiwa zimetawala vichwa vyao huku Afande Marina akiwa ndiyo mhudumu wa siku hiyo.
“Sasa vijana mmefanya kazi nzuri tangu tulipoanza, ijapokuwa bado Yule mwanamke anatusumbua lakini kikwazo kingine ni hiki mmekiondosha, safi sana. Sasa sikilizeni, mpango upo tayari, Yule mwanamke anarudi kesho chini ya ulinzi mkali, lakini lazima atekwe, na tukishamteka ni kesho hiyohiyo auawe mchezo uishe, tuanze plan B, tumeshachelewa sana mpaka hapa tulipo,” Matinya aliwaambia vijana wake huku sherehe isiyo rasmi ikiendelea, wakati mke wa Chonde, ndugu na watoto wakilia kwa uchungu, hawa wengine wakisherehekea kwa furaha zote, kweli dunia tambara bovu.
Marina alianza kuelewa kinachoendelea kwa mbali, alisikia mazungumzo ya watu hao na akaelewa wazi kuwa kuna mtu keshanyofolewa maisha, lakini afanye nini, hakuna jinsi, ilibidi tu aendelee kuwa mpole labda atajengewa ghorofa kama alivyoahidiwa na Matinya lakini vipi akikabiliwa na kitanzi? Kwa nini? Jambo hilo lilimpa wakati mgumu sana, alitamani kuachana na Matinya kimapenzi lakini kila alipokumbuka fadhila na utajiri alionao, wote ulitoka kwa mwanaume huyo mkubwa kiwadhifa serikalini, mwenye ofisi nyeti sana yenye dhamana kubwa na taifa hili. Marina alikuwa tayari kwa lolote hata alipoambiwa kunyonya dhakari, alifanya hivyo na vingine vyote alikuwa radhi kuvifanya ilimradi apate kitu kwa Matinya, mimba kadhaa alizitoa ili aendelee kuonekana bado kigoli mbele ya macho mawili ya bwanyenye huyo.
“Sasa boss, huyo mwanamke anakuja na usafiri gani?” Scogon aliuliza
“Anatua na na Rwandair, kesho saa sita kamili mchana, inabidi hujuma ifanyike, kama si kumteka basi auawe palepale.” Matinya alijibu.
“Na vipi ulinzi aliopewa? maana ameshapanda cheo amekuwa gaidi,” Scogon aliuliza tena kisha wote wakaangua kicheko. “Usiogope, askari wawili tu wa kike watakuja naye kutoka Uganda, ila hapa atapokelekwa kwenye gari maalumu ambalo hata ulipige risasi halidhuriki, tairi zake hazitumii upepo, haina dirisha nyuma isipokuwa kwa dereva na kuna tundu moja tu ambalo hutumika na mtu wa ndani kupenyeza mtutu wa bunduki kama inabidi kufanya hivyo,” Matinya alieleza. Scogon aliwatazama wenzi wake na kuwaona kila mmoja akiwa kimya akitafakari jambo, jambo ambalo hakulijua akilini mwake.
“Kwa hiyo mafunzo kule yanaanza rasmi lini? Maana mafunzo ya kawaida tayari vijana wamefuzu,”
“Kule, Kontena linaingia kesho jioni, hivyo siku tatu baadae mambo yatakuwa sawa,” Matinya aliwaeleza mkakati mzima ulivyo na kuwaahidi pesa nyingi kama watafanikiwa kuituliza hali hiyo iliyotawala harakati zao. Baada ya kumaliza mazungumzo yao wakatawanyika, kila mtu kuchukua njia yake wakiwa wamekubaliana siku inayofuata kuingia kazini, kazi ambayo ilihitaji taaluma ya hali ya juu kuifanikisha, Scogon hakuwa na hofu kupanga kikosi chake japokuwa alikuwa na pigo la kuondokewa na vijana wake mahiri.
§§§§
YAUMI akiwa na pingu mikononi na mnyororo miguuni aljivuta kwa hatua za polepole huku akiwa katikati ya askari polisi wawili kutoka Tanzania, waliokuwa wakimlinda kwa ukaribu mkubwa. Gari ya polisi iliyoandaliwa kumbeba mpaka uwanja wa ndege ilikuwa tayari ikimsubiri. Yaumi alionekana wazi akiwa amechoka kimwili na kiroho, hata uvutaji wa hatua zake zilikuwa za taratibu sana, macho yake yalijawa machozi yasiyokwisha, huku vimulimuli vya camera za waandishi wa habari vikiwa vinamsumbua macho asubuhi hiyo, alikuwa bado akitembea polepole kuielekea gari hiyo, akafika na kupakiwa garini kisha wale polisi wawili nao wakapanda mlango ukafungwa kwa nje na kwa ndani pia. Safari ya kuelekea uwanja wa ndege wa Kampala ikaanza. Gari ya Kyomukama ilikuwa kama ya nne hivi kutoka gari ile iliyombeba Yaumi, hakuweza kufanya lolote lakini alifurahi tu alipojuwa kuwa Yaumi anarudishwa nyumbani na mambo yote yatakuwa huko. Katika gari ya kyomukama aliyokuwa akiiendesah mkewe nay eye mwenyewe akiwa ameketi upande wa kushoto, hakuna aliyeongea na mwenzake, ilikuwa ni kama kumsindikiza tu Yaumi. Macho ya Kyomukama yalikuwa yakitoa machozi daima, alimhurumia shemeji yake huyo, lakini alijua wazi kwa nini yaumi alikuwa Kampala, ila kwa wakati huo hakuwa na lolote la kumsaidia.
Ule msafara uliiacha barabara kuu na kuingia katika uwanja wa ndege wa Kampala, uliojengwa katika maeneo ya vilima vya Kololo.
Yaumi alishushwa katika gari na kusindikizwa na polisi kadhaa wa Kampala, huku bado waandishi wa habari wakimwandama kwa picha. Aliingizwa ndani ya jengo na moja kwa moja alipelekwa chumba maalum kwa ukaguzi na kuruhusiwa kwa safari. Abiria wote walikuwa tayari wameketi ndegeni wakisubiri kuondoka, Yaumi alipakiwa na kuwekwa kiti cha nyuma kabisa katikati ya wale WP wawili waliovaa kiraia lakini walionekana kuimudu vema kazi yao. Majira ya saa nne asubuhi waliondoka kuelekea Dar es salaam, Yaumi alikua akilia muda wote, akijua kuwa sasa mwisho wake ulikuwa umefika bila kipingamizi, kitanzi kilikuwa kikimsubiri nyumbani Tanzania…

DAR ES SALAAM – 4:10 asubuhi

KIKOSI KAZI kilikuwa tayari kwa kile kinachowakabili siku hiyo mchana, Scogon alikuwa akipanga vijana wake tayari kwa kazi hiyo nzito na ngumu inayohitaji umakini wa hali ya juu.
“Eneo la tukio litakuwa Vingunguti mbele kidogo ya yadi ya Tata, kwa taarifa ambayo mzee ametupa gari itakayotumika, haipenyi risasi na wala tairi zake hazitumii upepo, kwa hiyo ile mbinu yetu ya kushambulia kwa risasi ili kumpata mateka wetu haiwezekani, inabidi tupange plan B,” Scogon aliwaeleza vijana wake. “Sasa ni mbinu gani tutatumia kukamilisha zoezi? Maana inabidi tulimalize ndani ya dakika tatu tu,” Mdumi aliuliza. “Usijali Mdumi, mpango upo hivi, sisi tutatega pale boza la maji, mmoja wetu atakuwa kama anatengeneza boza hilo, wao watakapofika pale itabidi kusababisha ajali amabyo itapelekea lile gari ama kuanguka au kupoteza uelekeo kisha tunafanya kazi yetu, gari yetu ya uokoaji itakuwa jirani.” Baada ya maelezo hayo Scogoni aliwapa mikono vijana wake na kuwatakia kazi njema kwani yeye alikuwa anahitaji kuonana na mzee kujua itakuwaje kwa mzigo unaoingia bandarini jioni hiyo.
“Ndiyo Scogon!” Gabriel Matinya alijiegemeza kwenye kiti chake na kutoa kauli hiyo tata ambayo msikilizaji hujui kama ni swali au hoja. Scogon alimwangali boss wake huyo aliyeonekana kukonda kwa siku chache tu. Akiwa amekalia kiti cha wageni alijiweka vizuri na kuegemeza mikono yake mezani, “Plan B tayari kiongozi,” akatamka Scogon. Matinya ambaye alionekana kuwa na mawazo sasa lionekana kidogo kupata uhai baada ya kusikia hilo. “Una uhakikia kilam kitu kitaenda sawa?” akauliza, “Ndiyo boss!” akajibu. “Ok maana kutakuwa na ulinzi mkali wa polisi, hivyo mjipange vyema na mfanye kazi yenu kiakili,” Matinya alitoa rai ya mwisho. Baada ya hayo machache Scogon na Matinya waliongea yao mengine juu ya kontena linaloingia jioni hiyo ambalo halitakiwi kulala zaidi ya siku moja bandarini, hivyo ilipangwa mwanamke huyo akipatikana tu lazima aeleze kila document ilipo ndani ya muda mchache na ili kumaliza mchezo akibisha basi auawe maana kumuacha nje kutasababisha hatari nyingine.
Matinya na Scogon walitoka na kuelekea ofisi nyingine lakini ndani ya jengo hilohilo, wakaenda kumuona mtu mwingine naye alikuwa ni mtu mwenye dhamana kubwa kwa wananchi, wakaingia bila ya hodi na kumkuta mtu huyo akiwa ametingwa na shughuli kadhaa mezani mwake, “Karibu mkuu,” alisimama na kumkaribisha huku akimpa salamu ya kijeshi iliyomstahili. Kiaha wote wakaketi na mazungumzo yakaanza, “Sasa ule mpango umekamilika,” Matinya alimwambia Yule bwana. “Sawa ulinzi uliopo sio mkali sana hivyo wajitahidi tu kufanya kazi kwa umakini, kama watashindwa kukata lile bati la ile gari basi nitawapa funguo za akiba za ule mlango,” Yule bwana alitoa maelekezo. “Hapana usitoe funguo ila tutatengeneza zingine ambazo watatumia, ili kama ikionekana hujuma basi funguo zikutwe ofisini” Matinya alieleza. Kisha Yule bwana akachukua zile funguo na kuzichora katika karatasi nyeupe kwa kuwa hakuwa na sabuni ya kuikandamizia, akampa Scogon ile karatasi na kuagana naye.
Scogon hakupata shida kwa hilo, moja kwa moja alifika Gerezani Kariakoo ambako kila kitu hupatikana na kila kitu hutengenezwa kasoro roho tu. Alifika katika kibanda kimojawapo ambacho kilikuwa na mtu anayefanya kazi hiyo.
“Kijana, una dakika ishirini na tano tu kuhakikisha funguo hii imepatikana, nakunywa bia pale ukimaliza uje nayo,” Scogon alimpa maelekezo Yule kijana. “Sasa kaka si unajua hii itakuwa ni express hivyo malipo yako juu,” Yule kijana lillalama, “Unapoteza muda tengeneza, pesa kitu gani,” Scogon alijibu.
Dakika zilezile alizopewa na Scogon ile funguo ilikuwa tayari imekamilika, Scogon aliitazama hakuamini, ilikuwa ni ileile kama aliyopewa kule ofisini akiwa na Matinya. Scogon alimpatia pesa yake ya ujira Yule kijana, hakuwa na muda wa kupoteza, aliondoka zake na kuelekea walipo vijana wake.
Kama walivyoagizwa, Mdumi na wenza walifika na gari bovu eneo la Vingunguti, kisha wakajifanya limeharibika na kuanza kulibomoa bomoa ilimradi lionekane kuwa liko matengenezoni, baada ya muda kidogo ilikuja gari ndogo aina ya McLaren GTI HP 450 ikaegeshwa kwa mbele kidogo na wakati huo huo landrovar moja mbovumbovu iliegeshwa katika moja ya vivuli vya miti iliyojirani hapo, ndani yake kukiwamo na mtu mmoja aliyeonekana kusinzia. Kikosi kilijipanga tayari kwa kazi, kilikuwa kikisubiri tu muda kufika.
§§§§§

MAKABURI YA SEGEREA

VILIO VYA WAOMBOLEZAJI vilikuwa vikisikika huku na kule, akina mama waliokuwa wakijitupa tupa kwa kilio kikali cha kumuomboleza ACP Chonde aliyekuwa akizikwa katika makaburi hayo.
Kamanda Amata akiwa amesimama kwa utulivu pembeni yake kukiwapo na Gina. Ibada ya mazishi iliendelea huku jua kali la mchana likiwaka, nyimbo za maombolezo zilizokuwa zikiwakumbusha waombolezaji kutenda mema duniani zilizikika.
Kutoka mbali Kamanda Amata alimuona afande Magreth akiongea na mtu mmoja ambaye sura yake haikuwa ngeni sana.
“Gina, Yule anayeongea na Magrteth ni nani?” kamanda akamuuliza Gina. Gina akatazama kwa wizi kisha akarudisha macho yake mbele na kumjibu Amata, “OCD Kambale, namfahamu sana Yule mzee,” kamanda Amata akatikisa kichwa kuwa ameelewa alichoambiwa na Gina.
Saa 6:45 mwili wa ACP Chonde ulikuwa ukishushwa kaburini, kila mtu alikuwa akifuatilia tukio hilo kwa huzuni kubwa sana, vijana walikuwa wakiongea yao katika vikundivikundi, Kamanda Amata alijichanganya na vijana wengine kuona labda atapata lolote katika hayo mazungumzo. Katika kundi moja alivutiwa sana na kile walichokuwa wakiongea kwani alisikia wakitaja jina moja na kulisifia sana kuwa ni mtu hatari na anyeogopwa, Kamanda ASmata alitaka kujua zaidi juu ya mtu huyo ‘Chilungu’, akamkariri Yule kijana aliyekuwa akizungumza na wenzake, ili asimpoteze kwenye macho yake kwani baada ya maziko alijua atakuwa na kazi naye.
Miongoni mwa waombolezaji waliokuwa hapo, dokta Omongwe alikuwa miongoni mwao, mara baada ya zoezi la kufukia lilipoanza, kutokana na vumbi lililokuwa linatimka, Omongwe alichomoka na kurudi kwa nyuma, katika harakati hizo akakutana Magreth, wawili hawa walikuwa wanafahamiana hasa kutokana na sakata la Yaumi ambalo liliwafanya wakutane si zaidi ya mara mbili kila mmoja akiwa katika majukumu yake. Walisabahiana na kisha wote wawili kusimama kando wakisubiri zoezi hilo liendelee.
“Hivi afande ile kesi ya Yaumi inaendeleaje?” Omongwe alimuuliza Magreth.
“Si unajua aliyoyafanya Uganda?” Magreth akmuuliaza na Omongwe akajibu kwa kutikisa kichwa.
“Kuna kazi kubwa maana ni visa juu ya visa, mchana huu anarudishwa nchini kuendelea na kesi yake, lakini sasa imeongezeka upana kutokana na yale ya Kampala, keshokutwa ndiyo kesi yake,” Magreth alijibu kimbea si unajua akinamama wakikutana tena.
Wakati wa kuweka mashada ya maua ulifika, ukiacha mke, ndugu wa karibu, pia OCD Kambale wa kituo cha Tabata alipewa nafasi hiyo kuwakilisha askari wa kanda hiyo, Magreth kama mfanyakazi mwenzake wa karibu nae alipata fursa hiyo ya kuweka shada la maua.
Mara baada ya shughuli nzima kumalizika, Kamanda Amata alikuwa jirani sana na kile kikundi cha wale vijana kilichoonekana kujua mengi, wakiwa katika kutoka makaburini pale alikuwa akiwatazama kama watapanda magari yaliyopo au wana ajenda nyingine. Kamanda Amata akasogea chini ya mkorosho huku mkono mmoja amemshika Gina. Pembeni kulikuwa na grosary ndogo yenye vinywaji, akaingia na kuketi karibu na mlango wa kuingilia wateja, mara aliona lile kundi la vijana kama watano hivi wakiendelea na stori, sasa zilikuwa za Simba na Yanga, walipokaribia pale akawashtua.
00 CHANZO : Deusdedit Mahunda
“Oya, karibuni tujumuike, maana tumeanzia mbali kwa nini tumalize tofauti?” akawauliza, wale vijana wakacaheka huku wakitazamana, “Aah Braza we endelea tu si tunaenda mbele hapo,” wakamjibu, lakini Kamanda alikuwa akiwabembeleza mpaka wakakubali, wakajumuika nae, vinywaji vikaanza kupopolewa kutoka kaunta, kwa mwenye grosari ilikuwa neema kubwa, ama kweli kufa kufaana.
Baada ya lisaa limoja walikuwa tayari wamechangamka na kila mmoja akiongea cha kwake, ndipo hapo Amata alipoanza utundu wake wa kukusanya habari, muda wote Gina alikuwa akiongea kwa chati tu lakini alishajua kile ambacho Kamanda alikuwa akikitafuta. Mazungumzo yao ya kilevi yakaenda mpaka kwenye tukio la kuuawa Chonde, vijana wale wakafunguka kwa kile wanachokijua, jina la Chilungu likarudi tena mezani, wakimsifi kuwa ni jamaa asiyefaa, wakihofu kwa vyovyote itakuwa ni kazi yake. Kamanda Amata akapeleleza maeneo anayoishi, akaambiwa kuwa huyo jamaa ni nyoka hana sehemu maalumu ya kuishi, lakini alitajiwa kuwa anapatikana sana maeneo Baracuda Bar kwani hapo ndipo kijiwe chake kilipo. Baada ya hayo, kamanda Amata aliagana na wale vijana akawaacha hela ya bia tano kila mmoja kisha ye na Gina wakapanda gari yao na kuelekea mjini, “Unajua Kamanda, tupite barabara ya Nyerere, hii ya Mandela kuja buguruni sasa hivi ipo tight sana” Gina alieleza. Kamanda akapinda kulia na kuchukua barabara ielekeayo Kinyerezi kisha akaiacha ile ya Mbezi na kukunja kushoto kuja Majumba sita. Dakika tano zilwafikisha njia panda Segerea ambako walipinda kushoto na kukamata barabara ya Nyerere kuelekea mjini.

ITAENDELEA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simulizi : Kitanzi Cha Mwisho

Sehemu Ya Tatu (3)

Ni pale walipofika eneo la Vingunguti na kukuta lundo la watu, magari yalikuwa foleni, kamanda Amata akashindwa kujua kunani eneo hilo, kati ya vijana waliokuwa wakipitapita mmoja aliitwa na Kamanda Amata akasogea dirishani, “Vipi dogo kuna nini hapo, ajali?” akamuuliza.
“Yaani braza hapo palikuwa na mtanange wa polisi na majambazi, wengine wanasema sijui majambazi walikuwa wanataka kuteka gari, wengine wanasema ile gari ilikuwa na hela sasa walishindwa kufungua mlango, ns polisi wakawa wamefika,” Yule kijana akawa anaeleza.
“Kwa hiyo wamefanikiwa au ?” Amata akauliza.\
“Hapana, wameshindwa, jamabazi mmoja ameuawa palepale, wengine wamekimbia, na ile gari iliyokuwa inawindwa imeondoka mudfa si mrefu,” Yule kijana akajibu huku akianza kuondoka. Kamanda Amata akashusha pumzi, “Lo, nchi imekuwa kama Somalia hii, watu hawaogopi Serikali,”….
Akatoa gari yake upande wa kushoto kama wanavyosema vijana akatanua na kupita ‘service road’ kuelekea Tazara, akiacha eneo hilo bado watu wamejezana wakishangaa kinachoendelea.
“Amata mpenzi, kwani wewe hii kesi ya huyu mwanadada unaichukuliaje?” Gina aliuliza.
“Gina, mara ya tano unauliza swali hilohilo na mara zote nimekujibu, we inaonekana hata huko chuoni maprofesa wanapata tabu kukufundisha sio?” kamanda Amata aliongea kwa hasira kidogo huku akibadilisha gia na kuiacha barabara ya Nyerere na kupinda kushoto kuelekea Magomeni kupitia barabara ya kuelekea huko. Kamanda Amata alimtazama Gina kisha akaangalia mbele wakati huo alikuwa akiyavuka mataa ya Ilala Boma kuelekea Kigogo, “Gina, hili sakata la huyu mwanamke lazima lina mambo mengi ndani yake, kesi kama kesi ya mauaji kwa nini iwe katika mtindo huu? Wangapi wameua na wakanyongwa au kufungwa maisha mambo yakaisha lakini huyu kaua, sawa, ila ukweli anaujua yeye na Mungu wake, mimi na wewe hatujui. Sasa kwa nini matukio mengi yenye mkanganyiko yatendelee kuiandama au kumuandama mwanamke huyu? Lazima twende nyuma ya mapazia tuone kilichojificha, siifurahii hali hii lazima nifuatilie, kama ACP Chonde ameuawa kwa sababu ya sakata hili basi afande Magreth yupo hatarini, kwa nini wamuue Chonde na wamtafute kwa nguvu Yaumi, kuna jambo na jambo lenyewe sio dogo, lakini ukweli utajulikana nitahakikisha Yaumi hafungwi maisha wala hanyongwi, mimi ndio Kamanda Amata TSA 1,” aliongea kwa majigambo, huku akitabasamu na kumtazama Gina. “Haya mama umefika nyumbani kwako, au unataka name nishuke?” Amata akamwambia Gina wakati akiegesha gari yake vizuri pale mbele ya nyumba aliyopanga Gina, alipotaka kushuka Amata akashika mkono wa Gina, “Sikiliza, ni hatari sana na ni salama sana kwa wewe kuishi nyumba ya Kupanga, tafuta nyumba kubwa mbili, kampuni itazinunua moja yako na moja yangu,” kamanda akamuachia mkono baada ya kumwambia maneno hayo, Gina akabaki kumtumbulia macho kijana huyo shababi ambaye ukimuona sura yake ya upole hutoweza kujua kama ana purukushani za ajabu akiwa katika mapambano, labda utamuogopa tu kwa jinsi mwili wake ulivyojengeka kimazoezi.
“Mi nilijua unasema nitafute nyumba moja tuishi wote kumbe unataka mbili? Basi nitaishi hapahapa,” Gina alijibu hoja hiyo huku akiondoka zake, kamanda Amata alimsindikiza kwa macho mwanadada huyu ambaye kila mtu alimpenda kwa ucheshi wake na maneno mengi aliyonayonayo, shepu yake iliyojiumba sawia iliwafanya wanaume wengi wenye pesa zao za ukware kumsololea lakini waliondoka patupu, kutokana na kukaa muda mrefu uraiani tangu alipohitimu masomo yake ya sheria katika chuo kikuu cha Dar es salaam, Gina binti Komba Zingazinga hakujulikana kama ni WP. Ukichanganya na tabia yake ya kujichanganya ndio kabisa. Ni yeye na Kamanda Amata walilificha hilo mioyoni mwao pamoja na viongozi wake katika jeshin la polisi. Mwamvuli wa kampuni bubu ya AGI Int’ ilimfungia ndani na kuonekana ni mfanyakazi wa kawaida tu, ni Madam S alieomba mwanadada huyu machachari abaki na Kamanda Amata ofisini huku wakimtazama kama naye anaweza kuingian katika idara nyeti ya usalama wa Taifa, hata yeye mwenyewe hakulijua hilo, ni nyakati Fulani Fulani alikuwa akishangaa anapopewa majukumu nje ya ofisi yake kuyafanya na amri ikitoka kwa madam S. Gina alimuogopa na kumheshimu sana Madam S au mkwe kama alivyokuwa akimwita wawapo katika kutaniana. Madam S alimuona Gina kama mwanae, alimpenda kwa jinsi alivyo na hasa alipokuwa akimsaidia Kamanda Amata katika shuruba mbalimbali, akionesha umakini na uhakika kwa analolifanya, akiwamudu wale wanaomletea kashkash za maisha yake na pia jinsi alivyo mkakamavu, hakuwa na linguine, alikubalika machoni na moyoni mwa Madam S.
§§§§§

GEREZA LA KEKO

YAUMI alifikishwa katika gereza la Keko majira ya saa tisa alasiri akiwa chini ya ulinzi mkali, alifunguliwa pinmgu na ule mnyororo kwenye miguu yake akaingizwa katika selo ya peke yake. Hakuna askari aliyemuongelesha, kila kitu kilienda kimya kimya tu utafikiri wamelazimishwa kufanya hilo wakati ni wajibu wao. Yaumi alikuwa amechoka sana bado mwili wake ukiwa na maumivu ya kipigo alichokuwa akikipata toka kwa polisi kule Kampala, kila aliyemtzama Yaumi alimuonea huruma sana, alitamani aiambie serikali ‘muachieni huru lakini haikuwa hivyo’ sheria ilikamata mkondo wake. Yaumi alikiendea kigodoro kilichokuwa kwenye moja ya kona ya chumba hicho kidogo, akajilaza huku amejikunyata kana kwamba kuna baridi au mtoto mkiwa. Mawazo mengi yalikuwa kichwani mwake, alijua nwazi kuwa sasa hawezi tena kutimiza azma yake, alikiona kitanzi kilicho mbele yake, akajua mwisho wake umefika, hakuna msaada tena labda ule utokao kwa Mungu tu ambao wakati mwingine hata kifo huwa ni msaada kutoka kwake japo tunakuwa na mdioyo migumu kuelewa hilo. Ulinzi mkali ulikuwa kwa Yaumi, nje kidogo ya mlango wa chuma wa kuingiulia katika selo yake kulikuwa na askari wawili wa kike waliotakiwa kulinda hapo bila kuchoka wala kutoka hasa walipoambiwa kuwa, mwanamke huyo ‘ninja’ alikuwa anatoroka ulinzi na ngome ya Segerea na kuingia mtaani kufanya aliyoyafanya. Waliaswa na kuaswa, kuanzia ndani ya gereza hilo mpaka nje kuimarisha ulinzi. Siku hiyo eneo Keko lilikuwa na hali mbaya, kila kona ni polisi na askari magereza wakitembea kuzungukazunguka kuona kama kuna lolote.
Yaumi alikuwa akiiwazia kesho yake ambayo ndio ilipangwa hukumu ya kesi yake, alijua kwa vyovyote hana pa kuponyoka.

“Usiogope mke wangu Malaika mlinzi yupo anakulinda na atakuwa pamoja nawe, azma yako itatimia lakini si kwa mkono wako bali macho yako yatashuhudia na moyo wako utaridhia hayo yote, ukweli utadhihirika na wote waliohusika sherian itachukua mkondo wake,”
Ilikuwa ni sauti ya Bwana Kajiba iliyomjia katika ndoto usiku huo. Yaumi alikurupuka kama mtu anayekimbizwa, alihema kupita kiasi mpaka walinzi wa mlangoni walishtuka kwa mhemo huo, wakafungua kadirisha kadogo kumtazama, Yaumi akajilaza tena.
§§§§§
MAJIRA ya saa tatu usiku yalimkuta Kamanda Amata maeneo ya Barakuda bar katika njia panda ya barabara ya kutoka Tabata Bima kwenda Segerea na ile itokayo Vingunguti kwenda Tabata Chang’ombe, alichagua meza moja iliyokuwa peke yake na kuketi katika moja ya kona iliyomruhusu kuona kila aingiae na atokae. Akiwa ankunywa bia yake aina ya Safari Lager kwa utulivu wa hali ya juu, hakika hakujua anayemsubiri ni nani na atafika wakati gani, aliendelea kung’aa macho tu, akifanya mchezo wa kupiga ngumi hizani.
“Kaka jamani humalizi tu?” Kamanda Amata alishtuliwa na sauti laini yha mwanadada mhudumu wa bar hiyo, alipokuwa kainua chupa na kuitikisa, akaituta bado sana.
“Unataka kunipa nyingine?” Kamanda akauliza.
“Ndiyo maana yake,” Yule dada akajibu.
“Sawa lete nyingine pamoja na yako kisha ukae hapa name au unasemaje?” Kamanda alilianzisha, Yule mhudumun hakuwa na la kujibu aliona kapata bahati ya mtende, ukizingatia siku hiyo bar haikuwa na watu wengi hivyo ‘keep change’ hazikuwapo. Dakika tano baadae Yule dada aliungana na Amata pale mezani wakigonga cheers na kuendelea kupata kinywaji.
“Naona leo mnakula shush tu maana sioni watu leo,” Kamanda alianzisha mazungumzo na dada huyo.
“Ah leo pamekuwa hamna watu kutokana na zoazoa ya jana na juzi,” Yule dada akajibu.
“Umesema zoazoa ya jana na juzi? Ukimaanisha nini?” Kamanda Amata tayari alinasa kitu kwenye jibu hili nae hakutaka kupoteza nafasi aliendelea kumchimba dada huyo. “Ee kaka yangu we acha tu, maana juzi na jana wamesomba vijana hapa na kupelekwa Tabata polisi, si kulikuwa na mauaji yametokea juzi ilee usiku sasa ikasemekana waliomuua wanapatikana sana mitaa hii,” Yule dada alizidi kueleza huku akiwa hajui ni nani anayeongea nae muda huo. “Mh, sijasikia hiyo, nani ameuawa?” Amata aluliza kwa kunong’ona. “Kuna afande mmoja alikuwa huko Kimanga anaishi huku juu Vingunguti, walimkamata na kumuua hapo bondeni kisha maiti wakaenda kuitupa Ukonga sijui mto Msimbazi,” wakati Yule dada akijibu swali hilo aliingia mteja mwingine ambapo ikabidi ainuke kwenda kumhudumia, “Narudi kaka usijisikie mpweke,” akaaga na kuondoka. Kamanda Amata akajua hapahapa lazima apate kile anachokitaka, akatulia kimya akisubiri kujua nini ni nini kutoka kwa Yule dada. Punde tu Yule dada akawa anarudi kutoka kaunta akipita kwenye kijia kinachokuja mlango mkubwa ili afike kwa Amata. Pikipiki moja aina ya Kawasaki ikaegeshwa hapo nje kelele zake kila mtu alikerwa lakini alishindwa kumwambia huyo mwenye pikipiki hilo kuwa anawapigia makelele. Akashuka bwana mmoja mfupi aliyeshupaa alikuwa amevaa jeans nyeusi na Fulani kaba shingo nyeusi ikifunikwa na jaketi la ngozi ya rangi hiyo hiyo, aliingia kibabe akisindikizwa na mwenzake walioshuka katika pikipiki moja, akakutana na Yule mhudumu pale kwenye kile kijia, Yule bwana akambana kidevu Yule mhudumu kwa kiganja chake cha mkono na kumwambia kitu Fulani kama mtu anayemuonya mwingine, akamuachia na yeye kuelekea upande mwingine kuketi. Ilionekana wazi Yule dada alikerwa na kitendo kile alichofanyiwa na huyo jamaa, akatoa sonyo refu na kuelekea alikoketi Kamanda. “Vipi, mbona jamaa anaonekana mkorofi sana?” Kamanda aliuliza wakati Yule mwanadada akiketi katika nafasi yake. “Achana nalo hilo, siku mbili halikuwepo hapa tulikaa kwa amani, leo limekuja tena,” akalalama.
“Ni nani?” kamanda akauliza. “Ha, we kaka, hulijui hilo, linaitwa Chilungu, watu wanasemaga ni lijambazi, na lingekuwepo juzi lingesombwa,” jibu hilo kutoka kwa Yule mhudumu, liliushtua moyo wa Kamanda Amata, akaona kumbe aliyekuwa akimtaka kaja. Akajiuliza mara kadhaa ataanzia wapi kumtia nguvuni, hakupenda aonekane kuwa yeye ni mmoja wa makachero, hii ingemletea sifa mbaya mbele ya wanaomfahamu. Akafikiri kidogo na kupata jibu la haraka, akainua simu yake na kuchambua majina, la kwanza, la pili na la tatu, akaendele na macho yake yatua kwenye jina WP Magreth, akaandika meseji ya kumuuliza yuko wapi mida hiyo, sekunde chache akajibiwa
“… nipo maeneo ya Kisukulu kuna jambo tunalifuatilia,…”
Kamanda Amata akamuandikia kumuuliza kama yuko peke yake au na wengine, akajibiwa kuwa
“…Nikon a kampani kama watano hivi, kikazi zaidi,”
Hapo Amata akaona kuwa mambo si mabaya kwa maana kama yuko kikazi na wengine basi ina maana yupo kamili akiwa na silaha pamoja na vifaa vingine. Akatabasamu kidogo, akaandika meseji nyingine ya kufunga kazi.
“…Nipo barracuda bar hapa njia panda ya Segerea na Tabata Chang’ombe, kuna ndege unawahusu, njoo na kamba ya kufungia mabawa pamoja na manati ya kulengea kama ataruka, ukifika maeneo haya kabla hujaingia nishtue nikupe maelekezo…”
Ilikuwa meseji ya Kamanda Amata kwa afande Mgreth. Kamanda Amata akatulia pale mezani huku akiendelea kunywa bia yake. Meseji nyingine ikaingia kwa Kamanda Amata,
“…umesomeka na kueleweka, tuko njiani,…”
Mazungumzo kati ya Amata na Yule dada yaliendelea pa sin a Yule dada kujua lolote linaloendelea mahala hapo.
Zikaagizwa bia nyingine, wawili hao wakaendelea kunywa, Kamanda Amata alikuwa akihakikisha hawapotezi watu hao aliotaka wakamatike usiku huo, “Samahani nakuja,” alimwambia Yule dada kisha akanyanyuka na kutoka nje, baada ya muda akarudi na kuketi palepale. Alijua kitkachotokea hapo muda si mrefu hivyo akamwambia Yule dada akamtafutie sigara, akamtajia sigara ambayo anajua kabisa kwamba kwa hapo haipatikani, Yule dada alipoaga kaunta akatoka nje kuelekea madukani.
§§§§§
MAGRETH aliingia kama mteja mwingine katika bar ile akitanguliwa na Jamaa ambaye alienda moja kwamoja kaunta, kwa jinsi tu alivyo Kamanda Amata alijua kuwa kazi itakuwepo mahala hapo. Nje kulizungukwa na askari polisi wane wenye silaha zilizoshiba vizuri. Wakiwa wanajua wazi kuwa mbaya wao yupo hapo hawakutaka kuchezea hata nukta moja.
Yule jamaa wa kaunta akaagiza juisi ndogo ya boksi, akainywa polepole huku akimtazama Magreth aliyekwenda kuanzisha uchokozi wa makusudi, Kamanda Amata aliwaambia wawakusanye wote wawili katika meza ile.
“Habari yenu wakaka,” Magreth alisalimia. Chilungu al;ipoinua uso kumtazama mwanamke huyo akabaki katoa macho pima, alimfahamu WP huyu vizuri sana naye tayari alikuwa kwenye orodha yake ya watu aliyopewa kuwaondoa kwa donge nono, Chilungu akanyanyuka na kumkazia macho afande Magreth. “We mwanamke unafuata nini hapa, usiniletee usiku!!” akiwa katika kusema hayo aliingiza mkono kiunoni mwake na kutoa bastola alipomuoneshea Magreth tayari alikuta Magreth nae bastola mkononi, wakabaki wakitazamana kila mmoja bastola kwa mwenzake….
Ilikuwa kama sinema Fulani inayorekodiwa huko Hollywood, Kamanda Amata alikuwa bado ametulia pale kitini akishusha bia yake taribu kinywani huku nakitazama mchezo huo utaishia wapi, tayari bastola yake ilikuwa imeshawekwa kikazi, haikuwa mbali bali tayari ilikuwa mkono wa kulia ikiwa imebanwa na kiganja imara, kiganja kisicho na masihara katika kazi, ikiwa imeshaondolewa usalama na risasi tayari imedumbukia chemba.
“Shusha bastola yako wewe, kabla sijaamu vinginevyo,” Sauti ya Magreth ambayo daima ilikuwa nyororo leo ilibadilika na kuwa kavu kabisa ikionesha kutokuwa na masihara.
“Sishushi, huwezi kuniamulia, mwanamke Malaya wewe,” Chilungu alijibu kauli ya Magreth. Kosa alilofanya Magreth ni kuwa bado bastola yake haikuwa kikazi, bado alikuwa hatua moja nyuma, kidole chake kilicheza pale katika lock ya usalama, ilikuwa ni nafasi ya Yule jamaa mwingine pale chini, alipourusha mguu wake kwa ustadi mkubwa na kuupiga mkono wa Magreth ambao uliondoka katika shabaha na kwenda pembeni, Chilungu alijirusha mzima mzima na kutua juu ya meza, Magreth alifyatua risasi iliyopita jirani kabisa na kanyagio la mguu wa Chilungu na kutoboa meza kabla ya kuchimba chini, shabaha hiyo ilimkosa Chilungu wakati alipokuwa hewani akipiga samasoti kali na kutoka nje ya wigo wa bar hiyo, lakini akiwa juu alipiga yowe la maumivu, risasi kutoka kwa jamaa aliyekaa pale kaunta ilitua sawia kwenye kiganja cha Chilungu, akaanguka chini na Yule mwenzake alipotoka eneo lile baada ya kufanya lile la kumkosesha shabaha Magreth, alitoka eneo lile kwa kasi kuelekea kule alikoegesha pikipiki yao, akafika na kujitupia juu yake, akapiga kick moja likawaka, alipotaka kuondoka kwa manjonjo ambapo nia yake ilkuwa ni kumuendea Chilungu kumbeba na kuondoka eneo lile alikuta injini ya pikipiki ikizunguka peke yake, alipocheki cini, mnyororo haupo, upo chini, umekatwa au umekatika, akawaka hasira na kujitoa kwenye ile pikipiki, akajaribu bahati yake kwa kukimbia, “Simama kwa usalama wako!” ilikuwa sauti ya polisi mmoja aliyekuwa nje ya bar hiyo kulinda usalama, Yule jamaa hakusimama alitaka kujiokoa lakini nalisahau kuwa anacheza na mtu mwenye silaha, risasi mbili zilizotoka kwenye Sub Machine Gun (SMG) zilimsukuma na kumuongea mwendo wakati zikipenya mgongoni na kutokea kifuani, akajibwaga juu ya lundo la mchanga na kugalagala akiipigania roho yake.
Chilungu kabla hajanyanyuka eneo lile, afande Magreth alikuwa amefika, akiwa anajaribu kunyanyuka, teke kali lilitua tumboni mwake na kumrudisha chini, hajakaa sawa buti aliyovaa Magreth aina ya caterpillar ilikanyaga shingoni mwa Chilungu na kumnyima pumzi, “Afande unaniua afande,” Chilungu aliongea kwa tabu, “Usijali, hata ukifa hauna thamani kwa jamii san asana unaongeza mawazo na mateso kwa mwanamke mwenzangu aliyekuzaa,” afande Magreth aliongea maneno hayo huku akiuma meno kwa hasira, bastola ikiwa mkononi ikikilenga kichwa cha Chilungu.
Ilikuwa ni kelele eneo lote hilo, wananchi wakipiga makelele “Majambazi, majambazi,” huku wakirundikana katika eneo hilo kama kawaida ya Watanzania, watu waliokuwa kwenye bar ile, pombe ziliwatoka, wengine wakiwa wejikojolea kwa milio ile ya risasi, ilimradi tu kila kitu kilivurugika kwa dakika chache. Ni mtu mmoja tu alikuwa bado ameketi akiedelea kupata kinywaji chake pale mezani, Kamanda Amata, ambaye daima kwake mambo hayo ni kawaida sana, tena makubwa kuliko hayo, alitabasamu alipojuwa kuwa mpango umekamilika, yeye ni kama katumia rimoti kukamilisha swala lile, hakupenda kujionesha waziwazi. Mpaka dakika hiyo hata Magreth hakujua Amata ameketi wapi.
Land Cruiser ya buluu yenye namba za usajili zinazotanguliwa na PT iliingia kwa mbwembwe eneo na kuegeshwa jirani kabisa na mlango nwa bar hiyo, Chilungu alikokotwa akiwa na pingu mkononi huku mkono wake ukiwa unavuja damu, alipofikishwa pale katika gari kwanza kabla ya kupakiwa ndani alipata kipigo kitakatifu kutoka kwa maafande waliobakia garini, “Unatufanya watu tusistarehe na wake zetu tukeshe kukutafuta wewe hanithi,” alisikika mmoja aliyekuwa akimpa kipigo kikali, Chilungu alikuwa hoi hajiwezi chini, akiwa amelala nusu mfu. “Afande Godi,” Magreth aliita, “Muache huyo anatakiwa akahojiwe,” aliongezea kusema alipomuona Godi kaacha kumpiga Chilungu, “Haina haja Magreth, huyu ndiye aliyeua huyu,” alijibu huku wakimbeba na kumtupia nyuma ya gari hiyo, wakachukua na mwili wa Yule mwingine naye akatupiwa humohumo. Kisha wale polisi wote wakadandia nyuma tayari kwa safari, Magreth ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa msafara, akachukua nafasi ya mbele na safari ikaanza kuelekea kituo cha Polisi cha Tabata. Walichukua barabara ya kuja bima kwa mwendo wa kasi, walipofika katika zahanati ya Tabata karibu na shule wakakunja kulia na kuingia moja kwa moja kituoni.

BUGURUNI KWA MNYAMANI

FASENDY akiwa anawahudumia wateja wake katika chumba maalum ndani ya nyumba yake hakuwa na wasiwasi wowote wa maisha. Akiwa anajua wazi kuwa shoga yake Yaumi hayupo lakini alikuwa na uhakika kuwa siku yoyote atarudi tu kwani yeye alipenda kumwita mwanamke huyo ‘Ninja’.
“Mama mama kuna mgeni,” ilikuwa ni sauti ya motto wake aliyempa taarifa hiyo. Fasendy akanyanyuka na kuelekea huko kwenye huo wito, alifika mlangoni na kukutana na mwanaume mmoja akiwa ameongozana na mwanamke. Fasendy aliitambua sura ya huyo mwanamke mara moja ila ya mwanaume hakuitambua.
“Karibuni ndani,” akawakaribisha kwa kutumia lugha ya ishara wakati yeye akitangulia. Katika mtaa wote huo Fasendy alikuwa akitumia lugha ya viziwi kuwasiliana na watu, hakuna aliyekuwa akijua kuwa Fasendy hakuwa kiziwi isipokuwa Yaumi peke yake, alipowakaribisha watu hao, wakatazamana kisha wakamfuata, walijua kuwa wanayemtaka ndiye. Walipofika katikati ya korido ndefu, ukimya mkubwa ulikuwa umetawala nyumba hiyo, akasimama akawageukia na kuwaonesha karatasi lililofanyiwa lamination safi. Yule mwanamke akalichukua na kulisoma, akabaki kapigwa na bumbuwazi. Liliwekwa aina ya huduma au bidhaa zilizopo au zinazopatikana humo ndani. Bangi, Cocaine/Heroin/Mandrax etc, Gongo, Ngono za jinsi moja/jinsia tofauti; pamoja na hayo palikuwa na bei na kila kitu kiliainishwa vyema. “Mh!” Yule mwanamke aliguna, kisha wakamwambia japo kwa tabu kidogo kuwa wanataka kuzunguma nay eye, akawakaribisha katika chumba kimoja kikubwa ambacho ndani yake kulikuwa na samani za kisasa na kila aina ya vitu vya bei mbaya, akawakaribisha kochi moja na yeye akaketi katika kiti kingine, “Bila shaka wewe ndiye Fasendy,” aliongea Yule mwanaume, akatoa picha mfukoni na kumpa, Fasendy akaingalia kisha akavuta droo ya kabati lililo jirani naye akaitumbukiza ile picha na kufunga ile droo. “Sijakwambia uitumbukize kwenye droo, nataka unambie unamfahamu huyo mwanamke?” Yule mwanaume alisema kwa hasira huku akinyanyuka kumueleka Fasendy, kabla hajafika alijikuta anatazamana na domo la bastola iliyofungwa kiwambo cha sauti, akapewa ishara ya kurudi kitini, akatii na kujitupa kwenye kochi huku kijacho kikimtoka. Fasendy akafyatua pini iliyobana hijab yake na kuacha kichwa wazi kabisa, “Sikilizeni nyie,” akawaambia wale wageni huku akiwa anaongea kwa lugha na sauti ya kawaida, “Msifikiri duniani hapa binadamu tunaishi kwa shida tunataka, ni hali ya maisha hii, Yaumi kawakosea nini ninyi, mmh? Kwa nini mnamfuatafuata sana mtoto wa watu, kuua mmeua ninyi halafu mnamsingizia yeye, wanaharamu wakubwa nyie, utafikiri ninyi mmezaliwa na miti,” Fasendy alilalama huku bastola ile akiwa ameiweka mezani bila woga.
“Fasendy, kwa nini unamiliki silaha kama hii nyumbani, wewe ni nani?” ilikuwa sauti ya mwanamke mara hii. “Nyama kuku wa kike wewe, unafikiri uliyotufanyia kule gerezani Segerea na hapa? Hii himaya yangu, kumiliki silaha nchi hii si tatizo, na kuipata kwangu haiana tabu, mi ni Msomali, Napata silaha muda wowote ninaotaka, unasikia afande Marina, ila unachomfanyia Yaumi mwanamke mwenzio sio kizuri, nendeni mkamwambie Matinya, mpeni na salamu zangu kwamba jeshi la mtu mmoja linakuja kumkomboa Yaumi, namtaona kazi.” Wakati anasema hayo Yule mwanaume akainyakuwa ile bastola na kuiandaa kumfyatua Fasendy, lo, kabla hatimiza azma yake, chuma cha baridi kilipenya begani mwa Yule mwanaume na kuparanganya mifupa ya bega hilo. Marina alibaki akitetemeka huku akishuhudia bunduki aina ya Short Gun ikiwa imetulia mikononi mwa mwanamke huyo, hakuona hata ni wakati gani Fasendy aliichukua bunduki hiyo. “siwaui, nendeni mkamwambie Matinya niliyowaeleza, na msirudi hapa tena, nina uwezo wa kwenda kumchukua Yaumi Keko muda wowote nikimua.” Aliongea kwa kujigamba huku akiwataka watu hao kuondoka.
§§§§§
Ulikuwa ni wakati mgumu sana kwa Matinya, uzee ulikuja kwa kasi ya ajabu siku hiyo, asubuhi yake alikuwa kijana mtanashati lakini wakati huu alikuwa mzee kwelikweli tena mwenye kuchanganyikiwa mara kwa mara. Aliona wazi bila kificho kuwa mwisho wa udhalimu umefika. Akiwa kamaliza kugida Konyagi kubwa sasa alikuwa na chupa ya GIN mkononi mwake, mara mlango ukafunguliwa na Marina akaingia na kumkuta Matinya katika hali hiyo, “Vipi mpenzi?” akamuuliza Matinya. “Chukua bastola uniue,” ndilo jibu fupi lililotoka kinywani mwa bwana huyo. “Lakini na wewe ujiue kwani utapata shida sana baada ya kitendo hicho,” akamalizia kauli yake.
Muda huohuo Scogon na Simbila nao waliingia mle ndani, wakaketi.
“Sina lingine la kusema, tunakoelekea ni kubaya sana sana sana, Chilungu amekamatwa na jamaa yake ameuawa leo huko Baracuda bar, akitamka siri tu tumekwisha, Yaumi anapandishwa kizimbani kesho kwa hukumu, haya na wewe Marina nilikutuma wapi na mwenzako yuko wapi?” Matinya aliuliza kwa sauti ya kilevi. “Mpenzi Yule mwanamke kasema usimfatefate, Yule mwanamke ni komandoo, anamiliki silaha mle ndani sijapata kuona, mwenzangu niliyekwenda naye kapigwa risasi ya began a nimemuacha kwa daktari wetu akimtibia,” Marina alieleza kwa uchungu. Matinya alibaki kimya akiwa hajui cha kufanya, aliona wazi jinsi wingu zito likiwa limetanda mbele yake.

SIKU ILIYOFUATA
MAHAKAMA KUU KISUTU

JAJI RAMSON SEMINDU alikuwa na wakati mgumu sana katika kesi hiyo, alikuwa amejiinamia katika meza yake kubwa iliyoa eneo la mbele la chumba hicho kikubwa cha mahakama hiyo, watu wakiwa wamejazana kila upande wakitega masikio kujua nini kitajiri katika hilo. Waandishi wa habari kama kawaida wakiwa wamepewa eneo lao maalumu katika kupata kila kinachoendelea katika mahakama hiyo.
Utulivu wa hali ya juu ulikuwapo kama unavyojua heshima ya mahakama, ilisikika sauti ya mwendesha mashitaka tu na baadae ilikifuatiwa na wakili wa serikali, kila kitu kilikuwa tayari, ushahidi ulikuwa wazi na Yaumi alikutwa na kesi zaidi ya kujibu ukiachana nay a kumuua mumewe, alipewa kesi ya kuuwa watu wengine wawili, uharibifu wa mali, na kutuhumiwa pia na lile kosa la kuua huko Kampala na uharibifu wa jengo la posta huko Kampala, tafutishi zote ziliwasilishwa kwa Jaji Ramson, siku moja kabla ili aweze kafanya yale aloiyotakiwa kufanya.
Katika waliokuwapo mahakamani hapo, Gina alikuwa miongoni mwa watu waliojazana mahakamani hapo, Dr Omongwe pia alikuwapo, afande Magreth alikuwapo pamoja na wengine wengi. Ulinzi mkali ndani na nje ulikuwa umeimarishwa na askari wa kikosi maalumu cha Magereza kutoka Ukonga KM.
Baada ya mawasilisho yote yaliyotolewa, ilikuwa ni zamu ya jaji kutoa hukumu dhidi ya mwanamke huyo, aliyeitwa ‘Hatari’
Hukumu ilisomwa kwa lisaa limoja na nusu, katika hukumu hiyo jaji Ramson Semindu alisema upande wa mashitaka ulioongozwa na wakili wa serikali umethibitisha mashtaka hayo pasipo na shaka yoyote, pia ushahidi wa watu wanne zaidi umethibitisha kuwa Yaumi alimuua mumewe na watu wengine watatu zaidi akiwemo Yule wa Kampala ambapo ushahidi wake uliwasilishwa mahakamani na polisi kutoka Kampala.
Yaumi akiwa kainamisha kichwa chake chini ndani ya kizimba kilichojengwa kwa mbao safi zinazong’aa, alikuwa akifuatilia neon moja moja la jaji huyo kijana. Jaji Ramson akiwa katika sauti iliyojaa uchungu ndipo alipomhukumu Yaumi kunyongwa hadi kufa. Hiyo ilikuwa ndiyo hatima ya binti huyo, Yaumi.
Baada ya hukumu hiyo mahakama ilikwisha, jaji Ramson aliinua kinyundo chake na kugonga kwenye kitako chake pale mezani, akafunga kabrasha lake na kutoka huku watu wote mahakamani wakiwa wamesimama kwa heshima, alifika mlangoni na kugeuka nyuma akamtazama Yaumi kwa huruma sana, kisha akaingia katika chumba kingine.
Askari Magereza wa kike alimchukua Yaumi, pingu mikononi na mnyororo mmoja miguuni mwake, akaondolewa na kupakiwa katika Defender ya magereza, safari hii hakupelekwa Keko, bali alifikishwa katika Gereza kuu la Ukonga kusubiri tekelezo la hukumu hiyo.
§§§§§
MADAM S alimtzama kijana wake, Kamanda Amata, aliyekuwa ameketi kitini kwa mtindo wa kutazamana, huku glass mbili za kinywaji zikiwa kati yao zikisubiria mashambulizi.
“Kamanda najua wewe huwa ni mtu wa kunusa, una pua zenye nguvu ya kudaka harufu kama mbwa wa polisi,” Madam S alimwambia Amata kwa kumtania.
“Ndiyo kazi yangu Madam, na ndiyo maana leo nipo hapa kwa swala hili,” kamanda aliongea kwa utulivu.
“Nimekuelewa, unahisi kuna jambo zito, sawa, inawezekana, lakini sasa mtu huyo ameshahukumiwa kunyongwa unafikiri tutampataje kwa ajili ya mahojiano na hana nafasi tena ya kukata rufaa, angekuwa amefungwa sawa, lakini ananyongwa,” Madam S alionekana kuumiza kichwa kwa hilo, maelezo kutoka kwa Kamanda Amata mpaka hapo yalikuwa yamemuingia vyema mwana mama huyu hakuwa na shaka hata kidogo kwa lile analoambiwa na kijana wake, alimuamini sana kuliko mtu mwingine yoyote katika kazi zao za kiusalama.
“Ok, nafikiri fanya unachojua na mi nitafuatilia nijue kama tayari hati ya kunyongwa imesainiwa au la, kama bado tunaweza kufanya kitu na kama tayari basi hatuna la kufanya.
“Ok, nafikiri fanya unachojua na mi nitafuatilia nijue kama tayari hati ya kunyongwa imesainiwa au la, kama bado tunaweza kufanya kitu na kama tayari basi hatuna la kufanya,” Madam S alimaliza kauli yake na kujiegemeza kitini.
“Sawa mheshimiwa, nimekuelewa,” kamanda Amata alijibu kiutani kama kawaida yake awapo na Madam S. akakiacha kiti chake na kutoka taratibu, “Kamanda!” Madam S akaita, Amata akageuka kuonesha kuwa ameitikia wito, “Uwe mwangalifu sana, kila unalolipata unipe taarifa ili nijue tunafanya nini, sawa, usifanye uamuazi wowote bila kunishirikisha ili tuamue pamoja, sasa fanya utafiti wako lakini subiri amri yangu” Madam S alimuasa Kamanda Amata.
Kamanda Amata alipotoka alinyanyua simu na kupiga namba ya Jaji Ramson ambayo alikuwa ameipata kutoka katika vyanzo vyake.
“Hallo! Yeah, naongea na nani?” Ilikuwa sauti tulivu ya Ramson.
“Upo ofisini? (…) naomba nisubiri hapohapo nakuja muda si mrefu,” Madam S alimwambia Jaji Ramson. Alipokata simu hiyo akatoka ofisini na kumuachia maagizo Fulani katibu wake kisha yeye akaondoka na gari yake ya kazini, pembeni akiwa na dereva wake ambaye naye ni mwanamke. Dakika kumi na moja tu tayari gari hiyo aina ya BMW yenye rangi nyeusi iliegeshwa katika maegesho ya Mahakama ya Kisutu, kila mtu aligeuka kulitazama gari hilo maana walilijua kuwa ni gari la watu wa usalama. Madam S alishuka na kuwaendea walinzi waliopo eneo hilo, muda huo hakukuwa na vurugu ya watu kwa sababu kesi zilikuwa zimekwisha hivyo ni shughuli za kawaida tu zilikuwa zikiendelea, akaongozwa hadi katika mlango ulioandikwa kwa maandishi ya kujinyonganyonga RAMSON SEMINDU, aligonga na kukaribishwa ndani.
Jaji Ramson alimkaribisha Madam S katika kiti cha wageni huku yeye mwenyewe akiwa juu ya kiti chake cha kunesanesa, usoni hakuonekana kuwa na furaha sana lakini alijionesha kuwa yupo kawaida. Madam S ambaye amepitia mafunzo maalum ya kumjua mtu yuko katika hali gani na wakati gani alilitambua hilo.
“Jaji Ramson, naitwa Madam S, kutoka idara ya usalama wa Taifa,” Madam S alijitambulisha huku akimpa mkono.
“Ndiyo madam, karibu sana, mimi ni Jaji Ramson,” naye akajitambulisha ijapokuwa Madam S alikuwa akimfahamu siku nyingi, kama ilivyo kazi yao kufahamu watu nyeti kama hawa na kuwatumia inapobidi.
“Nakusikiliza madam,” Ramson alianzisha mazungumzo huku akimtazama madam S aliyejaa kitini kakunja nne huku sura yake ikiwa tulivu lakini isiyo na tabasamu lolote.
“Nimekuja kwa mazungumzo mafupi mheshimiwa, unakumbuka kesi uliyoihukumu leo asubuhi?” Madam S alienda ,moja kwa moja kwenye kiini cha habari.
“Yeah, nakumbuka, maana nimehukumu kesi moja tu leo iliyomhusu Yaumi,” Ramson akajibu.
“Yaumi amefanya nini?” madam S aliuliza ili kujua wapi pa kuanzishia mazungumzo yake vizuri.
“Yaumi alishtakiwa kwa kumuu mumewe na zaidi ya hapo ameua watu watatu zaidi na kufanya tukio la kigaidi huko Kampala,” Ramson alieleza kwa lugha ya kawaida.
“Lakini mheshimiwa, hujawahi kujiuliza kwa nini kesi hii ya mauaji imekwenda haraka sana na mtu kuhukumiwa kuliko kesi nyingine za namna hii?” Madam S alimkazia macho Jaji Ramson.
“Ni kweli, lakini kuwahi au kuchelewa si tatizo, kinachotazamwa ni ushahidi umekamilika na anahukumiwa kwa mujibu wa sheria, kama ilivyokuwa kwa Yaumi, upande wa mshtakiwa hakukuwa na mtetezi, hivyo moja kwa moja kesi haiwezi kuchelewa,” Ramson akajibu kwa ufasaha na kumwacha Madam S akitafakari.
“Unalosema sawa, kwa kuwa wewe ni mwanasheria, lakini kuna kitu nataka kukijua, ila nimechelewa kutambua hilo, ila nina wasiwasi sana na uwendeshaji wa kesi hii…” Madam S akaktishwa na Ramson, “Kwa nini unasema hivyo?” akauliza Ramson, “Jiulize mheshimiwa, Yaumi kaua mumewe, Yaumi kaua watu wengine watatu, kwa nini yaumi afanye hivi? Ana ujasiri gani? Lazima kuna kitu, je tazama mazingira aliyoua halafu utanipa jibu,” Madam S alimuachia kazi jaji Ramson, “Ok, Madam, kwa hiyo ulikuwa unasemaje labda? Maana hukumu kama ile haiwezi kutenguka,” ramson alimwuliza Madam S.
“Ah, mi nilijua kuwa labda kuna shinikizo nyuma yake lililokufanya uiendeshe kwa haraka hivi au ushahidi utafutwe kwa haraka namna hii,” Madam S alimweleza jaji Ramson. Akiwa bado anamwangalia usoni jaji Ramson, madam S aliona jinsi alivyo na aligundua lazima kuna kitu nyuma yake, “Hamna kitu madam, wala hamna shinikizo mama yangu, ni mambo tu yamekwenda harakaharaka basi…” kabla Ramson ahajamaliza kusema mlango ulifunguliwa na mtu mmoja mwenye mwili mnene uliojaa mafuta, mtu mzima aliingia nkatika ofisi hiyo bila ya hodi, labda kwa sababi ya cheo chake au ubabe alonao, akagongana macho na Madam S, kila mmoja alimtambua mwenzake kwa kuwa mara nyingi hukutana katika vikao vyao vya kiusalama, wakapeana mikono na kusalimiana.
Gabriel Matinya, alimkazia macho Madam S kisha akamtazama jaji Ramson, “Sasa mheshimiwa, mi si mkaaji maana naona mna mazungumzo,” lakini akaktishwa na madam S, “Hapana kiongozi, mimi nimeshamaliza yangu na sasa naondoka, pata nafasi ya mazungumzo tu,” Madam S alisimama na kuaga akaondoka mahali pale, aliteremka ngazi na kuingia katika gari yake, akatulia. Sekunde tatu baadae akafungua kijidroo cha gari yake na kuvuta kwa nje kitu kama kijiredio chenye uwezo wa kunasa sauti, akachomoa na kidubwasha kingine akakitumbukiza sikioni mwake akabofya sehemu Fulani na kile kijiredio kikawa kinawaka na kuzima taa ya kijani, huku nje ya gari antenna ilikuwa ikichomoka taratibu. “Ondoa gari,” alimwamuru dereva wake, ile gari ikatoka pale na kufika nje ya geti, ikakunja kushoto kama inaelekea Nyumba ya sanaa, ilipofika jirani na ofisi za Unicef akamwambia aegeshe pembeni, Yule mwanadada dereva akafanya hivyo.
“Huyu bibi alifuata nini hapa?” ilikuwa sauti ya Matinya katika kile chombo sikioni mwa Madam S.
“Ah, alikuja alikuwa ana wasiwasi na hukumu ya Yaumi, lakini nimemwelewesha kuwa amehukumiwa kwa mujibu wa sheria,” Ramson alimjibu Matinya.
“Ok, sawa, maana hawa ndio wambea wenyewe hawa, wakishalishika jambo au kuhisi harufu Fulani ni wafuatiliaji wa kimyakimya, mwishowe unakuta tu mambo yameharib ika,” Matinya alieleza na Madam S alisikia kupitia kile chombo.
Madam S alipoingia ofisini kwa jaji Ramson alikuwa na kidubwasha hicho ambacho alikishika mkononi mwake, si rahisi kwa mtu wa kawaida kukigundua, kina uwezo wa kunasasauti na kurusha sauti hiyo katika mfumo wa kidigitali umbali wa mita mia tano za mraba, ni kidubwasha kidogo kama kifungo kinachotumiwa sana na watu kama hawa ili kupata mazungumzo wanayoyahisi yana jambo Fulani la siri. Mazungumzo yalipokuwa yakiendelea Madam S alibaini kuwa kuna jambo zito kati ya jaji Ramson na Mheshimiwa Matinya, kwani mazungumzo yao yalikuwa ni mazungumzo ya mwisho kwa muonekano wake. Aliposikia matinya anaaga na kuwa ameweka ahadi na jaji huyo kukutana katika mgahawa wa Steers, Madam S aliridhika kwa hilo na akaona lazima alifanyie kazi. “Ondoa gari, nirudishe ofisini,” alimwambia dereva wake huku akitoa kile kidubwasha masikioni mwake na kukirudisha sehemu yake, akajiegemeza vyema katika kiti cha mbele cha abiria wakati ile gari ikiwa inaumaliza mtaa wa Ohio kabla haijazungukia barabara ya garden.
Madam S aliingia ofisini mwake na kuketi katika kiti chake kirefu kama kawaida, akavuta kitabu chake cha kumbukumbu na kukiweka jirani, akafunguan kurasa yenye tarehe na mwezi huo, hakuandika kitu kingine zaidi ya majina matatu, Yaumi lilikuwa juu kisha akaweka kamstari kuelekea chini akaandika Jaji Ramson kisha kamsatari kengine kutoka kwenye jina la jaji Ramson kikaelekea kulia akaandika Matinya, akafunga kitabu chake na kukiweka pembeni kisha akavuta gazeti la siku hiyo na kuendelea kusoma akisubiri habari nyingine kutoka kwa Kamanda Amata.
§§§§§
Toyota Land Cruiser ilisogea taratibu ikitafuta maegesho katika maeneo ya karibu kabisa na mgahawa wa Steers, ndani yake alionekana mwanadada aliyekua amenyoa upara akiliendesha gari hilo, utamjua kuwa ni mwanamke kutokana na rangi nyekundu iliyokolea mdomoni, viajana wa maegesho walimuongoza hadi mahali alipoona panafaa akalipachika hapo, akafungua mlango na kukanyaga chini taratibu kwa madaha akaufunga mlango nyuma yake. Kila mtu alimshangaa mwanadada huyu aliyeonekana kutokujali lolote, alikuwa mrefu, mwili wa wastani, hakika angefaa kuwa miss, matiti madogo yalishikwa na kifua bapa kisicho na tumbo uzembe, kichwa chake kidogo kilipendezeshwa na upara wa haja, fulana nyekundu yenye maandishi ya kijapani ilimsitiri upande wa juu wakati chini alikuwa katika jeans nyeusi aina ya HOLIFIGER, raba kali za SAUCON ziliupendezesha na kuufanya mguu wake usikutane na mchanga wa Bongo. Aliingia katika mgahawa huo na kuelekea katika meza iliyokuwa katika kona kabisa ikiwa imekaliwa na mtu mmoja tu. Muda huohuo mtu mwingine aliongezeka, sasa wakawa watu watatu walioweza kutambulika bila hiana. Gabriel Matinya ambaye kwa hadhi yake hakuwa mtu wakuwepo eneo hilo, jioni hiyo alikuwako hapo, pembeni yake jaji Ramson aliketi kwa utulivu na Yule mwanamke ambaye kwa vyovyote unapenda kufahamu ni nani.
“Ramson amefanya kazi niliyokuwa naitaka, na sasa nimefurahi kidogo kwa kuwa kuna aina ya kero ambayo imepungua upande wangu, nilimhusisha Ramson kwa sababu alikuwa na rungu katika mhimili mmoja wa serikali, ameshamaliza kazi yake na hapa nilikwambia uje umpe haki yake ya mwisho ili sasa atoke kwenye hili swala tubaki wenyewe,” Matinya alimwambia Yule mwanamke, “Lakini hujanitambulisha kwa undani,” Yule mwanamke akamwambia Matinya. “Oh samahani, uzee sasa unakuja kwa kasi, huyu ni Ramson yeye ni jaji katika mahakama kuu ila kama unavyomuona ni kijana sana hivyo unaweza kumkirimia atakalo. Bwana Ramson huyu ni rafiki yangu wa kibiashara anitwa Fasendy yeye ni Msomali, lakini huwa anakuja na kuondoka nchini kutokana na biashara zake, anaishi Masaki kama unapenda kumtembelea,” baada ya utambulisho huo, Fasendy aliifungua pochi yake na kutoa kijitabu kirefu hivi, kitabu cha hundi, akamuandikia hundi ya pesa taslimu shilingi za Kitanzania milioni moja na kumpatia, kisha Ramsoni akaaga na kuondoka, akawaacha Matinya na Fasendy.
“Niambie sasa kazi tunaanza lini?” Fasendy akmuuliza Matinya. “Sasa tunataka kushughulikia kontena la vifaa limeshafika, likitoka tu wewe utaongozana nalo mpaka mahali salama ambapo utakagua vifaa vyote, kama viko sawa, tutafanya utaratibu utaingia navyo msituni, kule vijana wako tayari wanakusubiri wewe tu ukaanze kazi ya kuwapa mafunzo makali kwa muda wa miezi mitatu, na pesa yako utalipwa kwa awamu tatu, mwanzo, kati na mwishoni. Sasa nina ahuweni kidogo kwa kuwa mtu ambaye alikuwa ni kikwazo tayari amehukumiwa kunyongwa na nina uhakika kama si kesho basi keshokutwa atapata kitanzi kwani njia yote tumekwishaitengeneza,” Matinya alifunguka kueleza mpango ulivyo. Fasendy alimsikiliza mtu huyu kwa makini sana, aliposikia swala la hukumu ya mtu kunyongwa, akashtuka kidogo, lakini alijitahidi asioneshe hali hiyo, “Nani ananyongwa na kwa nini?” Fasendy aliuliza, Matinya akamuelezea hali yote ilivyo kisa cha Yaumi mpaka dakika hiyo, Fasendy akabaki kapigwa na mshangao, ndio kwanza alikuwa akijua kuwa sakata la Yaumi linahusiana na biashara Fulani ya watu hawa ambao wamemwita yeye kutoka Somalia kuja kuwasaidia upande Fulani wa mpango wao. Fasendy alibaki kimya akimtazama Matinya bila kummaliza, alimkumbuka Yaumi, shoga yake, akajiwazia moyoni na kupata maumivu yasiyo kipimo, Fasendy akaanza kulia.
“Mmenyonga Yaumi?” akauliza.
“Ndiyo, we yaumi unamfahamu?” Matinya akauliza. “Hapana simfahamu, ila nimesoma sana habari zake katika magazeti, kesi yake ilikuwa inanipa shida sana, nilikuwa namuonea huruma sana, lakini wanawake wengine wana roho mbaya kumuua mumewe!” Fasendy alimwambia Matinya akijifanya kuwa hayupo kabisa katika hilo. “Ndiyo hivyo, na sisi tukatumia mwanya huohuo kwa kuwa mumewe alikuwa mshirika wetu sasa aliamua kutusaliti, tukaona Yaumi atakuwa kikwazo,” Matinya alimalizia mazungumzo huku akinyanyuka na kufuatiwa na Fasendy, “Sasa twende kwa bwana mkubwa la hapa tumelimaliza,” akasema Matinya na wawili hao wakaondoka na kuingia kwenye Nissan Patrol yenye namba za serikali wakatokomea mitaani.
Madam S akatikisa kichwa kuonesha kuwa kuna kitu kingine ameking’amua, akavuta droo ya dashboard ya gari na kutoa kitabu chake kilekile cha kumbukumbu akaongeza jina chini ya lile la Matinya, akaandika ‘msichana mwenye upara’ kwa kuwa hakujua jina lake. Akawasha gari na kuifuatilia ile gari waliyopanda Matinya na Yule mwanamke ili ajue safari yao inaelekea wapI.

KITUO CHA POLISI – TABATA

KAMANDA Amata alifika kituo cha polisi Tabata mchana wa siku hiyo, nje alikutana na afande Magreth akiwa pale, wakasalimiana na kusogea pembeni.
“Nipe ripoti amesema nini baada ya kumbana,” Amata alimuuliza Magreth.
“Tumembana sana usiku kucha, amesema tu kuwa yeye alipewa kazi hii kwa malipo maalumu, lakini boss kabisa wa kazi hiyo hamjui, kwa kuwa aliikuta bahasha mezani ikiwa na pesa na ujumbe wenye kazi ya kufanya, hivyo akatekeleza.” Magreth alijibu lakini alijikuta akiwa kwenye himaya ya macho makali ya kamanda Amata.
“Hayo tu? Unafikiri ni ukweli anaoueleza? Ina maana hiyo meza huwa anaitumia peke yake?” Kamanda akauliza. Magreth akajikuta anashindwa kujibu swali hilo.
“Hilo hatukuuliza,” akamwambia Amata. Kasha Kamanda Amata akaomba kuonana na mtu aliyekuwa akifanya mahojiano na Chilungu, akapelekwa ofisi ya CID na kumkuta kijana mmoja mchangamfu sana aliyevali suti nadhifu kama anakwenda harusini, Magreth akamtambulisha Kamanda Amata (ACP Jaffari) kwa kijana huyo. Kasha mazungumzo yakaendelea.
“Kwa kweli afande, huyu mtuhumiwa Chilungu kaeleza hayo tu, hata hivyo kuna kitu cha ziada katika majibu yake, inaonekana ana uhusiano na watu wa karibu wa Kizota Bar pale Segerea ama mmiliki au wafanyakazi, amesema leo hii aliahidiwa kupewa kazi nyingine na mtu huyohuyo ambaye alimpa kazi ya kwanza,” Yule kijana alieleza kifupi lakini kwa mtindo ambao majibu yalijitosheleza.
“Ok, nimekuelewa, sasa nafikiri inabidi twende hapo Kizota Bar sasa hivi tukamnase mtu huyo tukishakuwa naye mkononi kazi itakuwa nyepesi,” kamanda Amata aliwaeleza.
“Sawa afande,” Yule kijana akajibu na kusimama kutoka pale kwenye kiti, akavuta motto wa meza na kutoa pingu mbili, akazitia katika mfuko wa koti, akanyanyua redio call yake, kisha wakatoka pamoja na afande Magreth na kamanda Amata (ACP Jaffari). Kwa kutumia gari ya Kamanda Amata waliondoka eneo la Tabata na kuelekea Segerea katika bar ya Kizota iliyopo katika kona ya kuingilia Segerea makaburini. Kamanda Amata akaegesha gari karibu na watu wa bodaboda. Wakashuka na kuingia katika bar hiyo, Magreth na Yule kijana CID wakaketi meza moja wakati Kamanda Amata akenda kaunta na kuagiza kinywaji pamoja na vya wenzake, wakaendelea kunywa wakati wakisubiri windo lake.
Waliendelea kusubiri kama lisaa limoja hivi, Kamanda Amata aliiona Lexus moja nyeusi ikiingia mahali hapo, ikiwa na muziki mnene kiasi kwamba ilikuwa kero kwa waliopo eneo hilo. Hakuna aliyelitilia maanani gari hilo, kijana mmoja akashuka na kuingia katika bar hiyo, alikuwa ni wa kawaida tu, motto wa mtaani, alionekana hivyo kutokana na mavazi aliyokuwa amevalia na minyororo aliyoning’iniza shingoni. Akaisogelea kaunta na kumbusu mhudumu kwa mbali, na Yule mhudumu bila hiyana huku akitabasamu akarudishia busu lile kwa mbali vilevile. Yule kijana akatoa bahasha ya kaki na kumpa Yule mhudumu, “Kama kawaida basi, mpigie halafu mtegeshee,” aliposema hayo Yule kijana akaondoka na kutoka nje ya bar ile. Kamanda Amata akagundua mchezo huo unaochezwa mahali hapo, akamuona Yule mhudumu akitoa simu yake na kubonyeza namba fulani, kwa kuwa waliondoka na simu ya Chilungu, Amata akamuonesha ishara Yule CID aipokee simu hiyo. Yule kijana kwa haraka akatoka pale mezani na kuelekea nje, akaipokea ile simu, “We vipi! Utapitwa na gari ya mshahara,” ndiyo lugha laiyotumia Yule mhudumu huku asijue anaongea na nani. Yule CID kule nje akajifanya kukohoa kwa kuwa alijua sauti yake haitofanana na ya mlengwa. “Vipi kwani tayari?” aliuliza, “Ah muda tu, nakuwekea palepale,” akamwambia, “Poa fanya hivyo nipo tu hapa nje si mbali,” Yule CID akajibu.
Muda huohuo Yule msichana akatoka na ile bahasha na kuiweka katika meza fualani pamoja na bia ya Kilimanjaro akatumia kuikandamiza isipeperuke, akaiacha na kuondoka. Wakati Kamanda akishangaa tukio hilo akamkumbuka Yule kijana aliyeleta ile bahasha, akageuka kumtazama, akakuta ile gari haipo, akabaki mdomo wazi, akashuka pale katika stuli ndefu na kuelekea nje, hakuiona hata ilikoendea. Akarudi ndani na kumuona Yule CID akiingia kutoka nje, mara hii alikuwa akiielekea ile meza iliyokuwa na bahasha, alipofika akaisogeza bia pembeni na kuinyakua bahasha, Yule mhudumu akaja mpaka pale, “Samahani kaka sio ustaarbu, kuna mteja nimemuwekea hiyo bahasha yake na bia akija atalalamika wewe kuichukua, mbona watu hamjiheshimu ee?!” Yule mhudumu alikuwa akiongea Kiswahili cha waswahili kanakwamba anakusuta. Kamanda Amata akasogea mpaka pale, na kusikiliza mzozo huo, “Kwani we unamjua mwenye bahasha hii?” Yule askari akauliza.
“Ndiyo namjua na nimempigia simu sasa hivi!” yue mhudumu akaeleza.
“Mpigie tena basi,” Yule aksri amwambia na Yule mhudumu bila kujali akachomoa simu yake na kupiga zile namba, simu ikaita mkononi mwa Yule CID. Kwa kitendo hicho Yule mhudumu akabaki hana la kusema.
“Dada mimi ni afisa wa polisi, kuanzi sasa upo chini ya ulinzi,” Yule askari akamwambia. Magreth akafika na kuchukua pingu kwa Yule CID akamvesha na kuondoka naye mpaka kawenye gari waliyokuja nayo, pamoja na malalamikop yote aliambiwa tu atajua hiyo kesi polisi.
Wakiwa ndani ya gari kamanda Amata akaichana ile bahasha na kuifungua ndani, kulikua na hundi ya shilingi million mbili na kijikaratasi kidogo kilichosomeka ‘Dr Omongwe Shabani, Magereza Segerea, zahanati, zamu ya usiku leo,’ akaingiza mkono katika kijidroo cha gari akatoa kitu kama mkebe wa kompasi lakini mwembaba wa plastiki akaufungua na kuilaza ile hundi ndani yake, akafunga vizuri, kisha akabonyeza kitufe Fulani, na kitu kama mwanga kikaonekana kikitembea ndani ya kimkebe, alipokamilisha zoezi hilo Amata akarudishia kama vilivyo na kumpa Yule CID, “Hii ni kwa ushahidi wako wa kesi.”
Kutoka kwenye kile kimkebe akafungua kwa chini na kutoa hundi nyingine ya mfano uleule akaikunja na kuitia mfukoni, alikuwa ameitoa kivuli chake ‘photocopy’.
§§§§§
Wigo mkubwa wa ukuta ambao juu yake uliwekwa vipande vya chupa ulilificha jumba la kisasa ndani yake, lango lake lililoonekana kujifungua lenyewe liliruhusu gari ya Matinya na Fasendy kupotelea ndani kasha nalo likafichwa humo. Madam S alipita taratibu na gari yake na kuelekea mbele zaidi, alipoona panamfaa akaegesha gari pembeni na kuchukua simu yake, akabonya namba Fulani ambayo iliita moja kwa moja katika ofisi za ardhi kitengo cha mipango miji, akamuulizia mtu anayemfahamu na mara moja akampata, akamtajia namba za lile lango la ile nyumba zilizokuwa zikiashiria namba ya kiwanja, akahitaji kuambiwa ni nyumba inayomilikiwa na nani au kampuni gani, kasha akasubiri jibu. Hakuchukua muda mrefu, akatumiwa meseji kuwa ni nyumba inayomilikiwa na idara ya ushuru na forodha ya serikali, akamshukuru sana huyo aliyempa jibu na kukata simu kasha akapiga namba nyingine kwa rafiki yake ambaye ni mmoja wa waajiriwa katika idara hiyo, akauliza kama anamjua mtu anayeishi katika jumba hilo, akajibiwa ni meneja wa idara hiyo kanda ya Dar es salaam, Madam S akaona kuwa mpaka hapo alikuwa amefanya kazi kubwa ambayo hakupaswa kuifanya, akarudi ofisini huku akiwa amemwambia Chiba wakutane hapo ofisini kuna kazi ya ziada.
Majira ya saa tisa walikutana ofisini kwake katikati ya mji karibu kabisa jumba la mkuu wa nchi.
Madam S akiwa kitini kwake alionekana kuchoka sana. “Bibi ustahafu sasa, utakufa kwa mawazo!” Chiba alimtania wakati akiingia ofisini kwa Madam S.
“Na we usianze maneno kama kaka yako Amata, na leo mpaka sasa yupo kimya hajanipa lolote,” Madam S alikuwa akimwambia Chiba maneno hayo huku akichukua kinywaji kwenye glass na kumpatia.
Akachukua kamera yake ndogo na kuweka picha ya Yule mwanamke mwenye kipara, “Chiba, hebu mtambue huyu mwanamke,” Madam alimwambia huku akiwa anamkabidhi ile kamera. Chiba aliichukua na kuiangalia ile picha kwa makini sana, kasha akaihamishia kwenye kompyuta yake ndogo na kasha kuiingiza kwenye mtandao wa kiusalama na kusubiri pale mtandao huo ulipomwambia loading, mara ile picha ikarudi pale kwenye kioo na nyingine kama ishirini hivi, kati ya hizo picha tisa zilioana na kumuelezea Yule mwanamke kama mwanamke hatari katika medani za kijeshi, mzaliwa wa Somalia, aliyepitisha maisha yake kwa miaka mingi katika magenge ya wahuni na waasi, alilitumikia jeshi la Somalia kwa miaka minne na kisha kutoroka ambako mpaka sasa anatafutwa, taarifa zile zilionesha mpaka hati yake ya kusafiria pamoja na alama za vidole. Chiba akamjulisha majibu hayo Madam S. kwa taarifa hizo akashtuka sana na kung’amua jambo zito la mbeleni.
“Vipi Madam, unamhisi?” Chiba akauliza.
“Yeah, Chiba, hapa kuna jambo zito lazima tuwe tayari kwa kazi ngumu, mwitw Amata tafadhali, tuifanye kazi hii kiofisi zaidi” Madam S akamwambia Chiba.
§§§§§ Matinya, Fasendy na mtu mwingine mkubwa katika idara cha ushuru wa forodha walikuwa bandarini mida ya jioni ya siku hiyo. Huko katika gati namba tano ambako meli kubwa ya LINEA MESSINA ilikuwa ikipakua makontena mengi yaliyojazwa kama viberiti, lilikuwamo kontena moja la futi arobaini mali ya kampuni ya MG investment lilikuwa tayari limeteremshwa na kuwekwa pembeni tofauti na mengine. Likafunguliwa vifungo vyake na milango yake kubaki wazi. Fasendy akaingia ndani ya kontena hilo na kupepesa macho haraka haraka, akatoka na kumfanyia Matinya ishara ya dole gumba.
Matinya akanyanyua simu yake na kupiga anapopajua yeye kutoa taarifa kuwa mzigo umefika.
“Kwa hiyo mheshimiwa!” Matinya alimwuliza Yule kibosile wa idara ya ushuru.
“Yaani hapo kajipangeni mi mnitoe milioni ishirini tu huu mzigo kesho mnauchukua na hakuna atakayewakagua njiani, hii nchi yetu bwana.” Yule mkuu wa idara akamjibu Matinya.
Baada ya mazungumzo yao wakaagana na kila mmoja akaondoka eneo hilo. Fasendy na Matinya wakaingia kwenye ila gari ya serikali na kuondoka eneo hilo.
“Fasendy, nataka ndani ya mwezi mmoja wale jamaa kule chaka wawe kamili, maana shughuli yetu lazima ifanyike miezi miwili mbele kwa ufanisi wa hali ya juu. Leo usiku tutakuwa na kikao pale Paradise Hotel Bagamoyo, nakualika uwepo ili ujue mikakati yote jinsi ilivyo,” Matinya akamwambia Fasendy.
“Hamna shaka, ukiwa na mimi amini hakuna lisilowezekana, hili ni jeshi la mtu mmoja, waulize al shabab watakwambia mimi ni nani,” Fasendy alijigamba mbele ya Matinya.

OFISI KUU T.S.A

MADAM S alikutana na vijana wake makini wawili, Kamanda Amata TSA 1, Chiba Chibila TSA 2.
Kilikuwa ni kikao cha dharula siku hiyo jioni, wakichanganya mawazo ili kupata picha kamili ya lile wanalolizungumzia.
“Kamanda Amata, nieleze umefikia wapi katika jitihada zako?” Madam S alimuuliza Amata. Baada ya kutafakari kama sekunde thelethini hivi, Kamanda Amata akafungua kinywa chake na kueleza kuanzi pale alipoanza kuhisi kitu katika kesi ya Yaumi mpaka kifo cha Chonde na kumalizia juu ya mkakati wa kumsaka muuaji na waliomtuma. Lakini habari iliyomgusa sana Madam S ni juu ya ile hundi ambayo Kamanda Amata aliitoa kivuli kuwa ameifuatilia katika benki husika na kugundua ni nani mmiliki wa kitabu hicho cha hundi, na jina alilopewa hakuweza kuamini hata kidogo, jina la mtu mkubwa serikalini, Madam S alibaki midomo wazi, hakuamini anachokisikia, alimtazama Kamanda Amata na kuamini huyo jamaa ni kiboko na kweli anastahili kuwa namba moja katika idara yao nyeti, idara isiyo na mipaka, yenye kibali cha kuua au kumlinda mtu yeyote, yenye kuzuia au kuruhusu jambo lolote litokee ili mradi azma na lengo la kazi litimie.
“Kazi nzuri Kamanda Amata,” madam S alimpongeza kwa hilo, kisha nae akaanza kuwaelezea juu ya safari yake kwa jaji Ramson na mazungumzo yao, kisha akampa Chiba kile kifaa kilichonasa sauti ya mazungumzo ya Matinya na jajai Ramson, baada ya hapo akawaelezea alivyomfatilia Matinya na Fasendy mpaka kwenye lile jumba la meneja wa idara ya ushuru na forodha kule Masaki.
“Madam, nafikiri umeona nililokuwa nakwambia, nyuma yah ii kesi kuna mpango mzito,” Kamanda Amata alililieleza jopo.
“Sasa Kamanda na Chiba kwa kuwa kazi hii inayowahusu baadhi ya vigogo wa serikali, naomba ifanyike kwa siri sana, ila itakapofikia siku ya kufanya hivyo ndipo umma wa Watanzania utakapojua uovu wa wale wanaowapigia kura ili siku nyingine wajue nani ni nani,” madam S aliwaeleza Chiba na Amata.
“Sasa Madam, mi nafikiri ili tuujue ukweli wa hili lazima tumpate Yaumi,” Chiba alieleza.
“Lakini Yaumi ananyongwa, na kwa taarifa ambayo ninayo Yaumi ananyongwa kesho mchana wa saa saba katika gereza la Ukonga na mheshimiwa ameshasaini hati yake ya kunyongwa, tutafanyaje?” Madam S aliwaeleza.
“Hapo tuna mtihani mgumu, tungejua mapema tungefanya utekeji palepale atokapo mahakamani, sasa tutafanya nini?” Chiba aliuliza kwa wasiwasi.
“Yaumi atapatikana tu, Chiba kesho tunaenda kumtoa Yaumi gerezani, jipange,” Kamanda Amata akamwambia Chiba.
“Aaaa maadam umesema wewe Kamanda, hakuna kitakachoshindikana,” Chiba aliitikia.
“Mtafanyaje kumpata?” Madam S aliuliza.
“Madam S, mi na Chiba, we tuachie hiyo kazi, ikifika kesho saa tano chukua gari yetu ile prado isogeze karibu na gereza, Yaumi kesho tunamtoa, na hiyo itaitwa ‘mpango wa ukombozi’ tutakapompata tu ni moja kwa moja shamba, tunamficha dunia isimuone mpaka ukweli utakapodhihirika” Kamanda Amata akamweleza madam S.
Madam S aliwatazama vijana hawa kwa dhamu na kutabasamu kwa kuelewa kuwa kazi inawezekana. Madam S akamuomba Chiba amuonesha Amata ile picha ya Fasendy.
Amata aliitazamaile picha kwa makini sana, “Vipi, unamjua?” Chiba aliuliza. “Hapana simjui,” Kamanda Amata alijibu. Chiba alimpa Kamanda maelezo yaliyopatikana juu ya mwanamke huyo hatari kuliko hatari yenyewe, akayasoma kwa makini sana, “Ujue kabisa ipo siku ya kupambana nae,” Chiba alimweleza Kamanda.
Baada ya kikao hicho kilichodumu kwa takribani masaa matatu, mwisho mkakati ukapangwa wa jinsi ya kumtoa Yaumi gerezani kwa mbinu ambazo hazielezeki. Jambo kubwa la kwanza ilikuwa ni kutafuta ramani ya gereza ilo ambalo limejengwa na wakoloni wa Kiingereza miaka mingi nyuma kabla ya uhuru, lakini je ramani hiyo itapatikana wapi, si ajabu hata haipo nchini. “Sasa kutafuta ramani hiyo itakuwa ni sawa na kutafuta maiti ya kumi katika kisa cha Gharama ya damu kilichoandikwa na Richard Mwambe,” Madam S akawaeleza kwa kuwatatnia, wote wakacheka na kuanza kukumbushana juu ya kisa hicho kilichovuta hisia za watu wengi duniani.
§§§§§
Kama kuna siku ambayo matinya na washirika wake walikuwa na furaha basi usiku wa siku hiyo ambayo Yaumi alihukumiwa kunyongwa. Walikutana katika hoteli ya Paradise huko Bagamoyo na kupongezana kwa hatua hiyo kubwa. Wakisherehekea kumaliza awamu ya kwanza na sasa kuanza awamu ya pili ya mkakati wao. Miongoni mwao alikuwa Gabriel Matinya mwenyewe, Fasendy (mwanamke mwenye upara), OCD Kambale, meneja wa idara ya Ushuru na forodha, mtu mmoja mwenye asili ya kiarabu aliyejulikana kwa jina moja tu la Salim, tajiri mkubwa sana kutoka Oman, pia kulikuwa na mtu mwingine mkubwa tu kicheo katika jopo la watu wa karibu na mkuu wa nchi. Vyakula viliteketea na makumi ya chupa za pombe zaaina mbalimbali kumiminiwa katika matumbo hayo yasiyo na shukrani. Pamoja na hayo kulikuwa na mazungumzo ya hapa na pale kati ya hao.
Matinya alionekana ndiyo mwenyeji zaidi wa tafrija hiyo isiyo rasmi, wakiwa wameketi katika meza zilizounganishwa kwa mtindo wa duara, walikuwa ni wao tu katika ukumbi huo mdogo ambao mlango wake umepambwa kwa maandishi yaliyosomeka VIP Lounge
Katikati ya shughuli hiyo alisimama bwana Gabriel Matinya na kuzungumza machache na wenzi wake hao.
“Napenda kuchukua nafasi hii kukushukuruni nyote kujumuika jioni hii hapa Paradise, nafikiri si wote tunafahamiana, lakini si mbaya wakati huu ukawa ni wakati muafaka wa kusalaimiana, kwanza kabisa tunae mtu wa juu kabisa ambaye ndiyo namba moja wetu katika mpango huu, yeye anaishi nje ya nchi lakini atakuja nchini hapa usiku huu kwa ajili ya kuanza rasmi mkakati wetu, tunaye namba mbili wetu ambaye ni mimi ninayeongea, namba tatu yeye tupo nae hapa,” akatulia kidogo na kumtazama bwana mkubwa mmoja aliyeketi huku mikono yake kaikutanisha juu ya tumbo kubwa lililojazwa na ufisadi uliokithiri, kisha akaendelea, “Hao niliowataja kwa namba ndiyo walioshika hatamu katika mkakati huu, zaidi yao tuna mkufunzi wetu wa mafunzo haya nyeti bi Fasendy kutoka Somalia, ndiye mkufunzi wa mafunzo yetu, hapa tuna Bwana Salim, millionea kutoka Oman, ndiye anayefadhili mkakati wetu huu na kuhakikisha lazima ufanikiwe, zaidi ya hapo tuna rafiki wa karibu Bwana Gomegwa ambaye ni meneja wa idara nyeti ambayo tunaihitaji kuitumia kwa sasa, idara ya ushuru na forodha, tukiachana na jopo hili la juu, tuna kikosi kazi ambacho kinatekeleza kila linalotakiwa ili kuhakikisha mkakati wasioujua unafikia lengo lake, hwa wako nje ya hapa na hata sasa wako kazini kuhakikisha mambo hayaharibiki. Ijapokuwa tulikwamishwa na mtu mmoja lakini kwa sasa tayari hatma yake imekamilika na hivi ninavyoongea jua la saa nne kesho litakuwa ni la mwisho kwake, na mi nitakuwa pale kushuhudia tukio hilo. Tuendelee kula na kunywa bila shaka yoyote na kazi inaendelea kama tulivyopanga,” Matinya alizingumza mengi katika hafla hiyo lakini hakutaja kabisa ni mkakati gani unaozungumziwa hapo, wala hakutaja namba moja wa mpango huo ni nani. Katika hafla hiyo kulikuwa na namba mbili tu na namba tatu pamoja na hao waliotajwa.
Wakati wa hafla hiyo Fasendy alionekana wazi kutokuwa na furaha, alizama katika lindi la fikra na mawazo, hakuna aliyejua mwanamke huyo anawaza nini, Matinya alimgutusha mara kwa mara na alipomuuliza anawaza nini, jibu lilikuwa ni ‘Napanga mkakati wa kazi,’ lakini kiukweli Fasendy alikuwa anafikiri jinsi gani rafiki yake Yaumi waliyekutana mahabusu atanyongwa kwa ajili ya kuhakikisha mkakati huo unafaulu nay eye akiwa mmoja wa watu wanaounda au kuhakikisha lengo linafikiwa, akiwa analipwa pesa nyingi tena za kigeni. Fasendy alionekana wazi kuumia kwa kitendo hicho, alifikiri kuwa kama angelijua mapema basi angeshamtorosha Yaumi na kumhifadhi mbali na watu hao au angemsaidia kwa namna moja ama nyingine kufanikisha lengo lake la kulipiza kisasi cha kifo cha mumewe, hakika ilikuwa ni mapigano makali katika nafsi yake, ‘Nitamsaidiaje Yaumi? Nimechelewa, bado masaa machache atakula kitanzi, kitanzi ambacho si haki yake,’ Fasendy alijiwazia na alikuwa akiumia tangu ndani ya moyo wake.
§§§§§
Wakati wengine walikuwa wamelala usiku huo, wengine wakisherehekea kufanikisha mipango yao, mwingine akiwa gerezani akisubiri kunyongwa, ni watu watatu ambao walikuwa hawajalala, walikuwa wakifanya kazi ya ziada kuhakikisha mmoja anapona na wengine wanaangamia.
Kamanda Amata, Chiba na Madam S walikuwa katika ofisi nyeti au ‘Shamba’ kama wanavyoiita iliyopo huko Gezaulole, ng’ambo ya bahari, pande za mbali za Kigamboni, ni moja kati yab majengo mkongwe ya wakoloni wa kiarabu, lakini lilifanywa kuwa ofisi nyeti kwa kazi za kitengo hiki muhimu katika serikali. Ukilitazama kwa nje jengo hilo ambalo ni gofu, lilikuwa halina matunzo kabisa, hakuna mtu aliyejua kama humo ndani huwa kuna watu wanashughulika na kazi mbalimbali, na ukizingatia lilikuwa mbali kidogo na makazi ya watu, hali hiyo ilisaidia kuficha siri nyingi zilizopo hapo ndani, wengi waliamini kuna mashetani yanaishi ukizingatia nyakati Fulani wanaona taa ya ndani ikiwaka na wakati mwingine ikizimwa.
“Sasa hii ni ramani ya zamani sana, si unaona jinsi ilivyochakaa,” Chiba aliwaonesha Madam S na Kamanda Amata, “Unaona hapa ni lango kuu, linatazama kaskazini, huku mbele ndiyo barabara ya Pugu, upande wa mashariki wa gereza hili kuna makaburi ya zamani sana, inasemekana walikuwa wanazika wafungwa hasa waliokuwa wakinyongwa enzi hizo, na hizi ni nyumba za staff, kusini mwa gereza kuna uwanja wa mpira, ukiwa umezungukwa na nyumba za askari, upande wa Maghalibi kuna barabara inayoelekea chuo cha maafisa wa magereza. Hili gereza lina milango mikubwa miwili ya kuingilia ndani, kuna lango kuu upande wa Kaskazini unaotumika na wafungwa pamoja na askari pia raia wanaokuja kuwatembelea ndugu zao, mlango huu upo karibu na lango kuu la kupitia magari yote yanayoingia katika eneo hilo na linalindwa na askari watata kabisa wa KM, lango la pili lipo kusini, huku linatazamana na nyumba za askari, lango hili hutumika kuingilia mahabusu kwa kuwa mahabusu iko upande huu, watuhumiwa wote wanaotoka mahakamani huifadhiwa upande huu. Gereza hili lina vilinge sita vya walinzi juu kabisa ya ukuta huu mrefu ambao umezungukwa na zao la mkonge kwa mita mbili kutoka katika ukuta,” Chiba alikuwa akiichambua ramani ya gereza hilo kwa nje, ramani iliyochorwa miaka mingi nyuma, enzi za wakoloni.
“Aisee, hapa kibarua kipo,” Madam alisema kuonesha kuwa bado alikuwa hajui nini kitafanyika katika mpango huo. Kamanda Amata aliitazama tena ramani ile kwa umakini wa hali ya juu sana, kwa jinsi ulinzi ulivyokuwa umetanda nje kadiri ya maelezo ya Chiba ilikuwa ngumu kwa wao kuingia kwa njia ya kawaida.
“Ok, Chiba, sasa hapa kitanzi kipo wapi?” Kamanda aliuliza.
“Hapa kitanzi kipo upande huu wa Kaskazini mashariki, kwenye hiki chumba kikubwa, ambapo mlango wa kuingilia ni huu,” Chiba alikuwa akionesha kwa uhakika kupitia ramani hiyo.
“Na hiki kilichopita hapa ni nini?” Madam S alimuuliza Chiba.
“Kwa maelezo yalioyoandikwa ni kuwa hili ni bomba la maji taka ambalo hutpitisha maji kutoka gerezani na kumwaga huko mchafukoge,” akawaeleza.
Ramani ile ikageuzwa upande wa pili kulikokuwa na michoro mingine kama mine hivi iliyoonesha hasa muundo ya ndani na nje ya gereza hilo.
“Hapa kwenye hii point ni ghorofa au kitu gani?” Kamanda aliuliza.
“Ndiyo, hapa kwenye chumba cha kitanzi ambacho kimejengwa kwa chini kikitanguliwa na kitu kama shimo, juu yake kumejengwa jengo lenye urefu wa ghorofa sita, unaweza kupitia kwa ndani kutoka katika chumba cha kitanzi na kuibukia katika ghorofa hilo,” Chiba aliendelea kujibu maswali ya maswahiba wenzake.
“Ok, kazi imekwisha, Mimi na Chiba tutafanya kazi hiyo, Madam utakuwa katika kikosi cha ukombozi,” kamanda Amata alikuwa keshapata wazo la nini cha kufanya ili kuweza kufikia hapo anapotaka. Waliangalia saa ya ukutani, ilikuwa tayari imetimu saa nane za usiku, wakachukua vifaa vya muhimu kwa kazi hiyo, kwa maana waliona wazi kuwa hakuna nafasi nzuri ya kuingia katika gereza hilo isipokuwa ni muda huo wa usiku ili asubuhi iwakute katika maficho ndani ya gereza hilo, walichofikiri wao ni kupata nafasi tu ya kuona kile ambacho kitatukia kwa Yaumi na kujua ni jinsi gani wataondoka nae pale endapo watafanikiwa azma hiyo. Kamanda Amata akiwa ndani ya suti yake nadhifu ya kijivu, juu yake akatupia suruali ya jeans na jacket refu jeusi kabla hajaweka ile ninja yake na kujificha sura yake. Chiba na Amata walikuwa tayari, Madam S aliwachukua katika gari yao na kuja nao pande za Ukonga...

UKONGA
ALFAJIRI
SIKU ILIYOFUATA

ALFAJIRI ya siku hiyo ilimkuta Kamanda Amata na Chiba ndani ya kona tata ya Gereza la Ukonga, katika chumba maalum cha kitanzi, juu ya chumba hicho kulijengwa kighorofa kirefu ambcho kilikuwa na mlinzi upande wa juu kabisa. Chiba na Kamanda Amata waliingia ndani ya ngome hiyo usiku wa saa tisa kwa kupitia tundu lenye ukubwa wa mdomo wa ndoo, tundu hilo linalotumika kupitisha maji machafu ya jikoni na kuyatiririsha nje ya ukuta wa ngome hiyo. Baada ya kujipenyeza kwenye njia hiyo bila kuonekana walitokea jikoni na kisha wakapita kwenye dirisha dogo la kupitishia chakula cha wafungwa na kujikuta wapo katika tundu kubwa la mlango ambalo linakuwezesha kuona eneo kubwa la ngoome hiyo kwa ndani, taa kali zilikuwa zikimulika eneo hilo kiasi kwamba kila kinachopita lazima kionekane bila kujificha.
Mpango huo ulikuwa ni mpango salama, haikutakiwa hata tone la damu liguse ardhi, hiyo ndiyo tahadhari waliyopewa na mkuu wao wa kazi, Madam S, nao walihakikisha wanaitii. Hakukuwa na njia nyingine zaidi korido ndefu inayopita pembezoni mwa stoo iliyofungwa kwa milango madhubuti ya chuma, na korido hiyo ilikuwa iking’azwa kwa mwanga mkali wa zile taa kubwa zilizofungwa juu ya ukuta na zingine kwenye nguzo za chuma zilizogeukia pande zote. Hakukuonekana mtu katika eneo hilo, hiyo ilikuwa ni hatari zaidi, kwa maana Chiba na Amata hawakujua zaidi ya taa ni kitu gani kingine kinaongeza ulinzi eneo hilo kama hakukuwa na askari anayezungukazunguka. Kwa kutumia vifaa maalumu, TSA 1 aliweza kuwasiliana na TSA 2 bila kutoa sauti, kwa kunong’ona tu, kijipande kidogo chenye waya mwembamba kilitumbukizwa sikioni mwa mhusika na kisha waya wake kufichwa kwa kuzunguka shingo ndani ya vazi la mtumiaji na huo ndio unaopokea na kurusha mawimbi, kifaa hicho kinachounganishwa na simu ya mkononi ambayo imewekwa mahali pengine ikiwa imewashwa hurusha na kupokea mawimbi ya sauti kwa kutumia Bluetooth, kina uwezo wa kunasa mawimbi kutoka umbali mrefu. Simu iliyokuwa ikiwaunganisha ilfichwa katika moja ya vichaka vilivyo nje ya eneo hilo. Madam S aliweza kunasa mawasiliano hayo akiwa maenso ya Banana, kaegesha gari yake kama wateja wengine wa klabu ya usiku waliojazana katika moja ya klabu hiyo wakivinjari na wenzi wao kwa kula na kunywa. Katika gari yake akiwa na kopo tatu za redbull alikuwa aksikiliza muziki laini sana uliokuwa ukitoka katika spika za gari hiyo.
Kamanda Amata ilibidi achukue muda wa ziada kujaribu kuona atafanya nini juu ya zile taa ili aweze kupita yeye na pamoja na Chiba, alijaribu kukagua eneo hilo walilojificha, hakuona cha maana sana zaidi ya makorokoro yaliyojazana bila mpango. Akisaidiwa na miwani inayoweza kuona gizani ‘night goggles’ Chiba aliona waya mnene uliopita eneo hilo kuelekea mahali Fulani. Akajadiliana na kamanda lakini wakaona si vyema kutumia waya huo kuondosha mwanga katika eneo hilo. Katikati ya uwanja wa gereza kulikuwa na mti mkubwa sana, wakati wakiwa katika majadiliano ya kuwa wafanye nini kuweza kupita katika eneo hilo bila kujulikana, walijaribu kuangalia vilinge vya walinzi walio jirani kuona kama wamesinzia au la, walitumia darubini yenye nguvu kwa kazi hiyo. Lakini walinzi makini, hakuna aliyeonesha kulala wala nini, wote walikuwa makini na bunduki zao SMG zilizoshiba risasi. Kamanda Amata akasikia mlio wa kunguru kutoka kwenye ule mti, akampa ishara Chiba kuwa inawezekana kutumia mbinu hiyo ya Kunguru. Daima Kunguru hakai mmoja katika mti, hukusanyana familia nzima au tungeita ukoo.
Amata akampa maelekezo machache Chiba kwa majaribio kama mbinu itafanikiwa. Akachukua short gun akachomoa magazine iliyojaa risasi za moto na kupachika nyingine iliyokuwa na risasi za mipira, kisha akalenga ule mti, huku akiwa kafunga kifaa maalum cha kuzuia sauti ya bunduki ile, akafyatua risasi kama kumi hivi juu ya ule mti, muda huohuo, kundi la kunguru lilitimka kwenye ule mti, Kamanda Amata akmpa ishara Chiba na kwa kasi wakapita kwenye le korido mpaka wakaufikia mlango walioukusudia, wakati bado wale Kunguru wakipiga makelele na kuruka huku na kule, tayari Kamanda Amata alishacheza na mlango wa chuma ulioweka nkizuizi cha kuingia chini ya ghorofa hiyo iliyo katika kona ya kaskazini mashariki mwa gereza hilo, wakaurudishia mlango nyuma yao na kuufunga wa ndani kisha wakatulia bila kufanya mjongeo wowote wakikisoma chumba hicho kiko vipi.
Chumba kilikuwa giza kabisa, lakini waliweza kuona vizuri kabisa kila kilichomo, viti vichache na mbele kabisa palikuwa na kitu kama jukwaa dogo ambapo kama ni mtu akisimama basi wote mliokaa vitini mtamuona kwa juu kidogo. Kamanda Amata akashusha pumzi na kutazama vizuri, kwa haraka haraka akajua kuwa hicho ni chumba maalumu kwa kazi ile wanayoitarajia, mbele yake kulikuwa na ngazi inayopanda juu kidogo ambako viti vile vilipangwa, na ngazi nyingine ilikuwa ikielekea chini ambako palikuwa na mlango wa mbao. Akashuka mpaka kwenye ule mlango na kuufungua kwa hadhari kubwa, naam, palikuwa na kaveranda kadogo juu yake hapakuwa na dari bali uwazi mkubwa ulioweza kuonesha juu kulikokuwa na kamba nene iliyofungwa vizuri kwa umadhubuti kabisa. ‘Hapa huponi’ Chiba alijiwazia huku akiwa anapanda ngazi zinazoelekea juu, akaingia kwenye korido Fulani na kutafuta mahali pazuri na kujificha, wakati huo aliweza kuona eneo la tukio kwa uzuri kabisa. Kama si mtaalam wa mambo ya kijasusi huwezi kumgundua Chiba kwa jinsi alivyojichanganya na vitu vingine katika eneo alilojificha, vivyo hivyo kwa Kamanda Amata ambaye naye alikuwa kajificha katika upande mwingine.
§§§§§§
Tafrija ya akina Matinya na washirika wake ilifikia tamati mishale yaa saa nane usiku, kwa ujumla mipango yote ilikuwa ipo sawa. Baada ya tafrija hiyo waalikwa waliondoka kujiandaa kwa majukumu yanayomkabili asubuhi ya siku hiyo.
Gabriel Matinya alitoka hotelini hapo majira ya saa kumi alfajiri, kwenye gari yake alikuwa pamoja na OCD Kambale na Fasendy. Moja kwa moja walifika katika jumba la Fasendy huko Oysterbay na kumuacha wakikubaliana kukutana nae jioni ya siku hiyo ikiwa tayari mzigo wao umekwishatoka bandarini, meneja wa idara ya Ushuru na forodha alikuwa tayari ameshashikishwa hundi yake ya milioni ishirini ili kufaulisha mzigo huo kwa njia zisizo rasmi.
Asubuhi hiyohiyo ilimkuta afande Marina kazini, katika gereza la Segerea. Akiwa amesimama nje huku akionekana kama mtu anayesubiria jambo Fulani, alishtuka alipoona gari ya Dr Omongwe ikimfungia breki miguuni mwake, “Afande vipi, unaota jua?” lilikuwa swali la Omongwe ambalo kwa Marina lilikuwa kama mkuki wa moto moyoni, alishindwa kujibu, ukizingatia alishaambiwa na Matinya kuwa baada ya kifo cha Chonde kitafuata kifo cha Omongwe kwani yeye ndiye aliyejua japo kwa kidogo juu ya sakata la Yaumi na pia ni mtu wa karibu sana na Yaumi. Marina hakuamini kama anayemuona mbele yake ni Omongwe au mzimu wake. “Nipo Dr, si unajua huku kwetu asubuhi ni kabaridi Fulani hivi,” alijibu, na ile gari ikaendelea mbele kwa mwendo wa polepole mpaka ilipoegeshwa mbele ya zahanati ya magereza.
Marina alinyanyua simu yake na kupiga namba Fulani, akaweka sikioni kusikiliza upande wa pili.
“Hello, beibi hivi upo siriasi na mambo yako au la?” ilikuwa sauti ya Marina kwa Matinya kupitia simu hiyo.
“Kwa nini wasema hivyo?” Matinya akauliza.
“Ulinambia kuwa baada ya kupotea namba moja atapotea namba mbili,” Marina alizungumza kwa lugha ngumu kidogo.
“Ndiyo kwani vipi?” Matinya akauliza tena.
“Huyu hapa, mzima wa afya, ina maana mpango umefeli,” Marina alimpa taarifa kisha akakata simu.
Mheshimiwa Gabriel Matinya, mtu mkubwa katika idara za usalama ndani ya wizara nyeti ya mambo ya ndani na usalama wa raia, alihisi baridi kali likipita katikati ya mwili wake na kuishia miguuni. Akiwa tayari ndani ya sare yake ya kazi, safari ya asubuhi hiyo ilikuwa ni kuelekea katika Gereza la Ukonga ambako Yaumi alikuwa kwenye orodha ya kunyongwa baada ya adhabu hiyo kusitishwa kwa miaka mingi. Matinya alishindwa kuchanganyikiwa kwa habari hiyo, akarudi kitini akatafakari kwa kina, akainua simu na kumwita Scogon, akampa ujumbe afuatilie kujua imekuwaje Dr Omongwe hajauawa wakati ilipangwa asubuhi hiyo awe marehemu. Hali ilikuwa hivyohivyo kwa Scogon, alipatwa na kigugumizi cha maamuzi, kazi ngumu. Scogon akawaweka sawa vijana wake na kuanza kufanya uchunguzi kwa mtu waliyempa kazi hiyo, ambaye hakutakiwa kuwahusisha vijana hao, majibu waliyoyapata hayakuwaridhisha, walimpata Yule aliyepewa kazi, nay eye akawaambia kama ilivyokuwa mwanzo ujumbe ulifika kwa mhusika anayehusika kwa utekelezaji, na ujumbe ulifika kwa njia ileile kama ya mwanzo. Scogon akamuamuru afuatilie na ampe jibu hilo mara moja kwa njia ya simu. Ilikuwa ni utata juu ya utata, kila mmoja alikuwa amechanganyikiwa kwa upande wake.

SAA 3:30 ASUBUHI

VIONGOZI mbalimbali walikuwa katika eneo la Gereza la Ukonga, mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, kiongozi wa juu kutoka Jeshi la wananchi, kamishna wa Magereza, mkuu wa wilaya pamoja na kiongozi wa jeshi la polisi bwana Gabriel Matinya. Kutokana na kibali cha mkuu wa nchi, viongozi hao wa juu katika idara ya usalama nchini walijumuika kushuhudia kunyongwa kwa mwanadada Yaumi. Wote walikuwa tayari ndani ya eneo husika walilotakiwa kuwapo, ni miaka mingi ilipita adhabu hiyo haikutekelezwa na taifa hili lakini siku hiyo ilikuwa itekelezwe. Pamoja na kuwa mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yamepinga adhabu hiyo kutekelezwa, bado baadhi ya mataifa huko Asia na kwingineko yalikuwa yakiendelea kunyonga kama kawaida.
Kelele zilipigwa, maandamano yalifanyika, redio zilizungumza na televisheni zilionesha mambo mbalimbali yanayopinga adhabu hiyo, wanaharakati wakisimama kwenye majukwaa na kupigia kelele adhabu hiyo kuwa ‘ifutwe’ lakini bado baadhi ya mataifa yalifumba macho yakaziba masikio na kuendelea kuning’iniza watu mpaka vitanzi vinakwisha. Lakini yapo mataifa kama yetu ya nchi zinazoendelea, yanayojali utu wa mtu, yalisikia vilio, yakasikiliza maoni na kutii sauti ya watu, kwani yaliamini kuwa sauti ya wengi ni sauti ya Mungu. Tanzania ikiwa moja ya nchi zilizoacha kabisa kutekeleza adhabu hiyo labda kama kuna sababu hasa ya kufanya hivyo lakini haikuwahi kutokea kwa kipindi kirefu sana mpaka sasa mwanadada Yaumi anapohukumiwa kwa kosa hilo analodaiwa kutenda, wakiachwa wale wakubwa ambao kila kukicha wanaifilisi nchi kwa kuiba mapesa ambayo yangenunua madawa mahospitalini na kuokoa maisha ya wengi lakini je ni vifo vingapi vinatokea kwa wizi huo? Mahakama haziwaoni, sheria zinapishana nao, amini usiamini, sheria inauzwa na haki inanunuliwa.
Dakika chache baadae katika chumba hicho Yaumi aliingizwa akiwa kafunikwa mfuko mweusi usoni ili asione kile kinachoendelea didi yake. Baada ya itifaki zinazotakiwa kufanyika, alipandishwa juu ya kile kijukwaa na kamba kubwa likatoka kwa juu, lenye kitanzi chenye uchu wa kuibana shingo ya binadamu. Askari magereza mwenye dhamana alimvika kitanzi kile shingoni mwake tayari kwa kazi hiyo. Yaumi aliyefungwa kamba mikono yake kwa nyuma, hakuwa na la kujitetea, alisimama wima akisubiri adhabu hiyo, katika miguu yake tayari alikuwa amelowa kwa hofu na woga wa kifo hicho alichokuwa ama akikisikia au kuona kwenye vitabu, lakini siku hiyo ni yeye aliyetakiwa kuandikwa magazetini na wengine wasome. Kila mtu alikuwa kimya kabisa katika chumba hicho, ilisikika sauti ya rola tu lililokuwa linaloshusha ile kamba kabla ya kupachikwa shingoni mwa binti huyo mrembo. Gabriel Matinya alikuwa ametulia katika mstari wa mbele, akiangalia kila hatua inayochukuliwa, kwa mara ya kwanza Matinya aliingiwa na huruma kwa Yaumi, alitamani kama angesema wamuache lakini hakuwa na uwezo huo tena. Mnyongaji alikwishweka kila kitu tayari kwa kazi hiyo, akasogea paembeni ili aweze kufyatua tu mtambo wake na Yaumi aning’inie katika kamba hiyo mpaka roho itakapoacha mwili, ni kitufe tu kinachofungua eneo la chini ambalo Yule aliyewekwa kitanzi hukosa pa kukanyaga na kujikuta akining’inia.
Kamanda Amata kutoka pale alipojificha aliweka tayari kiupinde chake kilichobeba kishale chenye makali huku na huku, akiwa kaminya jicho lake akilenga fundo la kamba ile huku akimwangalia Yule mnyongaji, akimsubiri aminye tu kile kitufe na yeye aitume shabaha hiyo. Wakati huo Chiba alishaweka tayari mabomu yake matatu ya machozi, tayari kuvuruga chumba hicho pindi tu Kamanda akifanya yake.
Ilikuwa ni sekunde tu ambayo matukio yote matatu yalifanyika kwa mara moja, kitufe kilipominywa tu, na kufungua na kusababisha pale alipokanyaga Yaumi kufunguka ili aning’inie na kitanzi kimalize kazi yake, ni nukta hiyo hiyo, Kamanda Amata alipofyatua ule upinde wake, kile kimshale kikapita sawia katika fundo la kitanzi lililokuwa nyuma ya shingo ya Yaumi na kukata sehemu ya kamba ambayo mara hiyo ilifunguka yote kwa kuwa haikuwa na nguvu ya kubeba ule uzito. Jopo la mashuhuda lilishuhudia Yaumi akianguka na kutumbukia kwenye kitu kama shimo huku kitanzi kile kikabakia si kitanzi tena. Kabla hawajapata kujua nini kimetukia, kila mtu akiwa katika mshangao uliojalizwa na butwaa, moshi mzito ulikitawala kile chumba na kila mtu alianza kukohoa na kupiga chafya, huku macho yakikosa nuru na kutapatapa kutafuta mlngo wa kutokea. Chiba alitua kwenye sakafgu na kukutana na Yule mnyongaji akiwa kwenye harakati za kuuendea mlango, alimpa pigo moja la judo lilompeleka chini na kumpotezea fahamu, alipogeuka upande ule alikokuwa Yaumi, hakumuona.
Mara moja Yaumi alipodondoka, alikuwa kama aliyepigwa shoti ya umeme, alijua tayari yeye ni marehemu lakini bado alijiona anahisi maumivu ya kudondoka, usoni hakuwa na lile tambara jeusi, kutahamaki akamuona mbele yake mtu kama shetani, aliyevaa dude la kutisha usoni, hakumuona sura ila alimuona akitua sakafuni kando yake, Yule mtu wa kutisha akamfungua kamba ya mikono kwa haraka ya ajabu kisha Yaumi akashuhudia Yule mtu akimpa lile pigo Yule askari. Ilikuwa kama sinema vile, akili ziliporudi kwa Yaumi, alijiinua na kuingia kwenye mlango mmoja aliouona mbele yake uko wazi, huko akakuta ngazi zinazopanda juu ya jengo lile, hakuwa na budi, Yaumi alijua ni mikasa ileile inayomuandama bado inamuandama, akaamu liwalo na liwe, wacha akajiue mwenyewe, alilivuta gauni lake alilokuwa amelivaa, akalipandisha mpaka mabegani na kuacha miguu huru, kisha kwa hatua za haraka akaanza kupanda zile ngazi kuelekea juu. Kamanda Amata, kijana nadhifu, alipoona moshi ule mzito hauna madhara kwake, alilivua lile guo alilolivaa maana lilimnyima wepesi katika utendaji wake, sekunde thelathini zilimtosha, akabaki na suti yake ya kijivu, akajiweka tai yake vizuri na dakika zilizobaki alizitumia kushuka hadi kwenye sakafu ya chini wakati wengine wakihangaika huku na kule kujinusuru na hali hiyo ya ghafla, mlangoni alikumbana na Yaumi, akapitwa palepale, kisha nay eye akageuza na kuanza kupanda ngazi akimkimbiza Yaumi huku akimuamuru kusimama.
ilipoanzia episode 1
1
DAR ES SALAAM
GEREZA LA UKONGA
KELELE za miguu za watu waliokuwa wakikimbizana huku wakipanda ngazi za jengo fulani zilisikika. Alikuwa ni mwanamke mmoja aliyevalia gauni tepe, refu lakini alilishika kwa mikono yake na kuifanya miguu yake kuwa huru, alionekana ni mwanadada aliyepitia kama si JKT basi mgambo maana alipanda ngazi kwa kukimbia huku nyuna yake akifuatiwa na kijana akiyevalia suti nadhifu ya kijivu akiwa na bastola mkononi. Mbio zile ziliendendelea huku yule kijana akisikika akisema
“Binti, simama tafadhali!” lakini yule mwanamke hakusimama aliendelea kupanda ngazi kwa kasi ileile, lakini mbio za sakafuni huishia ukingoni. Ilikuwa ni juu kabisa ya ghorofa ambako mwanamke yule alisimama akijiandaa kujirusha chini.
“Tulia hivyo hivyo tafadhali!” yule kijana alimwambia huku akiwa kamuoneshea bastola , Yule mwanmke alikuwa akitweta kama mbwa aliyekuwa akikimbizwa, aligeuka nyuma yake na kukutana macho na yule kijana.
“Nimechoka, nimechoka kuandamwa nanyi kila wakati, sioni haja ya kuishi, nimehukumiwa kifo lakini mnanitesa tu, bora nijiue mwenyewe” alifoka kwa hasira.
Akiwa bado na bastola yake mkononi, ikiwa imemuelekea Yule mwanamke, Kamanda Amata alishusha pumzi na akatulia, kwa sauti ya upole akamwambia Yule aliyekuwa akimkimbiza.
“Sikia mrembo, hapa upo kwenye mikono salama, sitaki kukudhuru, na kitendo cha kile kitanzi kukatika ni mimi niliyefanya hivyo, nakuhitaji wewe kwa shughuli za kiusalama, hakuna atakayekugusa, naitwa Kamanda Amata kutoka idara ya usalama wa Taifa kitengo kisicho na mipaka” akajitambulisha na kumuonesha kitambulisho ambacho si rahisi kwa mtu wa kawaida kukiona, mwanamke akashusha punzi na kuliachia lile gauni lake limfunike sehemu kubwa ya chini iliyokuwa wazi. Kamanda Amata alirekebisha tai yake na kuirudisha bastola mahala pake ndani ya koti. Akamsogelea yule mwanamke
“Unaitwa nani?” alimwuliza
“Yaumi” yule mwanamke alijibu kwa utulivu sana, hamu yake ya kujiua ilipotea ghafla na hamu ya kutimiza azma yake ilipata matumaini mapya, Kamanda Amata alimshika mkono na kuteremka nae ngazi za upande wa nje baada ya kusikia kuna watu wakipandisha juu kwa mgazi za ndani wakibishana kuwa mwanamke huyo lazima atakuwa juu ya jengo hilo.

ITAENDELEA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi mimi najiuliza hawa Bongo movie wapo kweli?
Kama wapo hizi stori huwa hawazioni?
Kama wanaziona mbona hawazinunui na kutengeneza movie za maana kutokana na stori kama hizi kiintelijensia?
Yaani Bongo movie wao walishazoea zile stori za kijana masikini kukataliwa na binti mzuri then mwishoni kijana anatajirika na binti anajileta

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi mimi najiuliza hawa Bongo movie wapo kweli?
Kama wapo hizi stori huwa hawazioni?
Kama wanaziona mbona hawazinunui na kutengeneza movie za maana kutokana na stori kama hizi kiintelijensia?
Yaani Bongo movie wao walishazoea zile stori za kijana masikini kukataliwa na binti mzuri then mwishoni kijana anatajirika na binti anajileta

Sent using Jamii Forums mobile app
Ili movie iendane na story hii kunahitajika bajeti ya maana sn hapa,
Nadhani hapo ndio kwenye mkwamo,(Sina hakika lkn)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi mimi najiuliza hawa Bongo movie wapo kweli?
Kama wapo hizi stori huwa hawazioni?
Kama wanaziona mbona hawazinunui na kutengeneza movie za maana kutokana na stori kama hizi kiintelijensia?
Yaani Bongo movie wao walishazoea zile stori za kijana masikini kukataliwa na binti mzuri then mwishoni kijana anatajirika na binti anajileta

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawana vifaa, hawana ushawishi, hawana connection ya kuingia sehemu nyeti Kama magerezani au polisi,kwa ufupi bado hawana uwezo wa kufanya hivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simulizi : Kitanzi Cha Mwisho

Sehemu Ya Nne (4)

Kwa kutumia ngazi za nje, Kamanda Amata alimshika mkono Yaumi na kuteremka nae kwa haraka. Alipofika mwishoni tu, ilikuwa ni kitendo bila kuchelewa, Land Cruiser Prado ilikuwa imesimama mbele yake, vyoo vyeusi, kwenye usukani kulikuwa na mwanamama mtu mzima, mlango ukafunguliwa, Yaumi akapakiwa ndani kisha Kamanda Amata akafuatia, Madam S akaitoa gari ile kwa kasi. Alizipita nyumba za maafisa wa magereza na kukunja kushoto akiuacha uwanja mkubwa wa mpira na kuteremkia katika bustani za michicha alipofika karibu na bwawa la maji machafu akapunguza mwendo, mlango wa pembeni kushoto ukafunguliwa, Chiba akajitoma ndani na gari ile ikaendelea kuchanja mbuga mpaka eneo la Kipunguni. Akachukua barabara ipitayo pembezoni mwa ofisi za mamlaka ya hali ya hewa, akatiririka nayo mpaka barabara kubwa ya Pugu na kupinda kulia kuelekea mjini. Wakiwa Tazara katika foleni ya kuelekea mjini, pembani yao ikasimama gari nyingine aina ya Land Rover 110, “Nifuateni,” ilikuwa sauti ya Madam S iliyokuwa ikiamuru, wakatia huo alikuwa tayari amekwishashuka na kuiacha gari hiyo ikiunguruma kwenye foleni. Kamanda Amata akashuka huku mkononi mwake kamkamata Yaumi na kuingia kwenye ile Land Rover pamoja na Chiba, Yule dereva wa ile Land Rover akaingia kwenye Prado, safari ikaendelea.
“Yaumi usiogope, upo kwa watu salama kabisa,” Amata alimwambia Yaumi huku akimvisha guo jeusi usoni, safari yao ikaishia ‘shamba’ huko Gezaulole katika ofisi yao nyeti iyatumika pia kuhifadhi watu kama Yaumi ili wasionekane na jamii


*Sasa endelea episode ya 24, Stori ndo kwanza inaanza...>>>>>*

EPISODE 24
MADAM S alimtazama Yaumi kwa kumkazia macho, kisha akamgeukia Kamanda Amata aliyekuwa ameketi mkabala na mwanamke huyo. Simulizi hiyo aliyoitoa kwa wanausalama hao ilitikisa moyo wa kila mmoja. Yaumi aliwatazama Madam S na Kamanda Amata kwa zamu, akashusha pumzi na kuegemea kiti alichokuwa ameketi.
“Ukapumzike Yaumi, umechoka sana, daktari wetu atakuja kukupa matibabu muda si mrefu,” Madam S alimwambia Yaumi huku akimpa ishara ya kumfuata, Yaumi akainuka kwa msaada wa Kamanda Amata, akatembea taratibu na kumfuata Madam S, huko akaoneshwa chumba chenye kila kitu, maji safi ya kuoga, nguo za kubadilisha na kila kitu. “Hapa ndipo patakuwa kwako kwa muda, upumzike vya kutosha kisha baadae utaongea na Kamanda Amata ili kujua wapi pa kuanzia katika kutatua swala lako, usiogope kuwa huru, omba na uliza unachotaka, ila simu hautoruhusiwa kupiga nje ya jengo hili,” Madam S alimwambia Yaumi kisha akamuacha na kuondoka.
Kwa Yaumi ilikuwa ni kama muujiza, hakuamini kila kinachotokea katika maisha yake, alikitazama kile chumba kilikuwa na kila kitu ndani, bafu la kisasa, nguo za kubadilisha, jokofu lililojaa vinywaji vya aina aina.
Kamanda Amata alitulia kimya akitafakari hali hiyo, Madam S aliketi mbele yake, akamtazama kijana huyu aliyeonekana wazi kuchoka kwa mambo mengi. Chiba nae aliungana nao hapo mezani, jopo hilo la watu watatu.
“Sina budi kuwapongeza kwa kazi ngumu mliyoifanya leo, hakika kwa anayejua kilichofanyika leo basi hana budi kukiri kuwa Tanzania tuko juu katika idara ya kijasusi, kama ingekuwa ni lile taifa babe la ulimwengu, lazima lingeleta makomandoo wasiopungua saba kwa kazi ambayo ni ndogo sana, lakini vijana wangu wawili mmefanya kazi nzito kwa dakika mbili tu na kuikamilisha, haijawahi kutokea na mnastahili pongezi,” Madam S aliwapongeza vijana hao wakakamavu kwa kazi hiyo ya kumuokoa Yaumi, Sasa Kamanda Amata utaongea taratibu na Yaumi ili ujue ni wapi pa kuanzia sakata hili, ili kila atakayehusishwa achukuliwe hatua.
“Madam S, hapa kwanza ni kumalizana na Yule mhudumu wa bar kule ili kutoka kwake ijulikane ni nani anafanya haya chinichini, kisha tutapanda taratibu ili kujua ukweli” Kamanda Amata alijibu.
“Lakini Kamanda una uhakika kifo cha ACP Chonde kina uhusiano na kesi ya Yaumi?” madam akauliza tena.
“Ndiyo, nina uhakika kwa sababu kwa nini auawe wakati anashughulikia kesi hiyo na si wakati mwingine,?” Amata akajibu kwa swali.
“Na kwa vyovyote katika jeshi hilohilo la polisi inawezekana kabisa kuwa kuna mtu anayetoa siri ya muenendo wa kesi kwa adui wa Yaumi ndiyo maana wanajua ni nani anafanya nini katika hili,” Chiba aliongeza maoni yake.
“Nimewaelewa makamanda wangu,” Madam S alijibu, akakohoa kidogo kusafisha koo kisha akaendelea, “Sasa nani anaanzia wapi na wapi anaanzia nani?” akauliza.
Wote wawili yaani Chiba na Amata wakajipanga sawia jinsi ya kuanza kufuatilia kesi hiyo A mpaka Z na kuhakikisha wanajua mbivu na mbichi, “Kitengo mnachofanyia kazi hakimuogopi mtu, awe waziri awe mbunge awe Rais, kama anahatarisha usalama wan chi lazima ashughulikiwe ndicho kiapo mlichoapa, sivyo?” Madam S akawauli akiwa amesimama akiwatazama kwa macho yake makali, “Ndivyo, Madam,” wakajibu kwa pamoja.
Walimuacha yaumi akiendelea kupumzika, na wao wakaondoka zao kutoka katika jumba lile, Madam S alibaki kwa kazi nyingine katika ofisi hiyo ya siri.
Saa moja tu ilimfikisha Kamanda Amata katika kituo cha polisi cha Tabata, alipofika pale na kumuulizia Yule kijana CID akaambiwa kuwa ametoka kwa majukumu ya kikazi, hivyo arudi baadae, akatii na kurudi katika gari yake. Safari ya kuelekea katika gereza la Segerea ikaanza, akiwa na mawazo mengi kichwani lakini bado akitafakari kazi ya hatari walioifanya siku ile katika gereza la Ukonga, Kamanda Amata aliona wazi kuwa mbele anakabiliana na kazi nzito kama sio kubwa. Akapita eneo la kituo cha daladala cha Segerea na kupandisha kilima kidogo kisha akakunja kulia na kuingia katika uwanja wa magereza, akaegesha gari panapotakiwa na kuteremka, japokuwa alikuta askari waliokuwa katika vikundi vikundi lakini hali hiyo haikumsumbua kichwa alijua tu ni nini wanachojadili, alivuta hatua ndefundefu na kuilekea zahanati ilikua ikimtazama mbele yake, hakuwa na haja ya kuuliza kwani maandishi makubwa yaliyosomeka ‘ZAHANATI YA MAGEREZA’ yalimuongoza kuwa hapo ndipo.
“Habari yako afande,” alimsalimia askari mmoja wa kike aliyekuwa ameketi katika kiti kilichotanguliwa na meza ndhifu ya Formica
“Nzuri, karibu nikusaidie nini?” aliitikia na kumuuliza Kamanda.
“Naweza kumuona Dr Omongwe?” akauliza.
“Ndiyo, bila shaka, nimwambie nani?”
“Mwambie, ACP Jaffary kutoka kituo cha polisi kati,” Kamanda akajibu. Yule mwanadada akamtazama kwa chati kijana huyu mwenye kifua kipana cha mazoezi kilichomfanya aonekane kuwa na siha nzuri inayovutia mrembo yoyote duniani.
Akanyanyuka kutoka kwenye kiti chake na kuingia mlango namba 3, dakika mbili tu akatoka na kumpa ishara ya kuingia, Kamanda Amata akajitoma ndani na kukutana na daktari huyo aliyekuwa akitaka kuonana nae, hakujua ni nini anataka kumwambia lakini kichwa chake tayari kilianza kupanga maswali na majibu. Akavuta kiti na kuketi akitazamana na Dr Omongwe aliyekuwa ndani ya mavazi ya magereza, shati jeupe lenye vifungo vya chuma na sketi ya rangi ya udongo iliyokolea, juu ya yote hayo alivalia koti jeupe kuonesha kuwa yeye ni mdau wa afya, kofia aina ya barret ilitulia kichwani mwake ikiwa katika mtindo nadhifu, ikiwa imeinamia kidogo upande mmoja na kuruhusu nywele zake zilizosukwa kwa mtindo wa kimasai kuning’inia na kudhihirishurembo wa mwanadada huyu.
“Karibu sana, naitwa Dr Omongwe,” alijitambulisha
“Asante sana, naitwa ACP Jaffary, kutoka kituo cha polisi kati,” kamanda Amata akajitambulisha kwa jina lake na cheo bandia kama ilivyo ada kwa watu wa kazi kama yake.
“Karibu afande nakusikiliza,” Omongwe alijiweka vizuri. Kamanda Amata akachomoa peni yake kutoka katika mfuko wa shati, akachukua kipande cha karatasi na kuiminya sehemu ya juu ile peni kama mtu anayetaka kuandika, kumbe hapana kwa kuiminya vile ni kuruhusu peni ile iweze kurekodi kila linalozungumzwa, peni ya kijasusi, yenye uwezo wa kurekodi sauti mpaka ukubwa wa GB 8 lakini pia unaweza kuitumia kwa kuandika.
“Utanisamehe afande, nina maswali kidogo napenda kujua, kama ambavyo unajua kuwa kijana wetu ACP Chonde ameuawa,” kabla Kamanda Amata hajamaliza kujibu, Dr Omongwe alimkatisha, “Sasa afande, katika hilo mimi ninahusika vipi? Mbona simjui huyo aliyeuawa,” akauliza na kutulia.
“Dr Omongwe, unanitia mashaka, kwa kuwa wewe ni mwana usalama lakini inaonekana haupo radhi kunipa ushirikianoa, kama humjui mtu huyo aliyeuawa, kwa nini uliokwenda makaburini kuzika?” swali hilo la Kamanda Amata lilionesha wazi kumpa mshtuko Dr Omongwe, akatulia na kuvuta hisia zake kuzikusanya na kuweka sawa, Kamanda akaendelea kumwambia, “Mimi kuja hapa si kwamba nimekosea, bali ninajua ninachotaka kufanya, nimekuona na hivi ninavyokwambia nimetoka kumhoji WP Magreth wa polisi Kimanga ambaye jana kuna kipindi mlikuwa pamoja pale makaburini mkiteta jambo, tunataka kutatua tatizo, lakini kwa nini unataka kutumia uongo ili kukwamisha?” Kamanda alihoji sasa kwa ukali ijapokuwa alimdanganya kidogo.
“Uhhhhhh!!!!!” Dr Omongwe alishusha pumzi huku akiitoa kofia yake na kuiweka mezani kisha akajiweka vizuri na kumkabili Amata, “Haya sema hasa hasa shida yako ni nini?” akauliza.
“Ninapenda kujua uhusiano kati yako wewe na marehemu, hilo tu basi, sisi tunamtafuta muuaji na najua wewe humjui lakini majibu yako yatatupa mwanga,” Kamanda alianzia alipoishia.
“Mimi sina uhusiano na marehemu, isipokuwa siku mbili kabla ya mwili wake kuokotwa, marehemu alikuja hapa ofisini kunihoji kama wewe ulivyofanya, alipotoka hapa basi, baadae nikasikia kuwa ameokotwa amekufa ndiyo maana nikaja kuzika,” Dr Omongwe akajibu.
“Sawa, naomba uniambie alikuja kukuhoji juu ya nini? Naomba unijibu kwa kuwa ukinificha kuna mlolongo wa wtu watakaokufa, lakini ukinijibu ukweli utakuwa umeokoa roho nyingi sana,” Kamanda alitumia lugha ya kushawishi, akamtazama Omongwe aliyeonekana kuwa na matone machache ya jasho katika pua yake. “Alikuja kunihoji juu ya mwanadada mmoja naliyekuwa hapa mahabusu lakini yuko nje kwa dhamana, anaitwa Yaumi,” Omongwe akajibu.
“Yaumi? Yaumi yupi?” Kamanda akauliza wakati akijua kabisa anamzungumzia Yaumi yupi.
“Kuna Yaumi alikuwa hapa mahabusu, alikuwa na kesi ya mauaji ya mumewe, ijapokuwa alikuwa nje kwa dhamana lakini inasemekana kuwa aliendelea na mauaji kwa watu wengine, sasa marehemu Chonde alikuja hapa magereza kutafuta ukweli kama huyo mwanamke akiwa chini ya ulinzi wa askari magereza je alikuwa anaweza kutoka nje kwenda uraiani na kufanya mauaji? Ndi cho hasa alichokuwa akihoji, akafika kwangu kwa kuwa siku inayosemekana kuwa kuna mtu aliuawa nyumbani mwake huko Kimanga, yeye alikuwa mahabusu lakini siku hiyo alikuwa anaumwa sana hivyo alilazwa hapa na mimi mwenyewe ndiye niliyemhudumia usiku wote,” Dr Omongwe alijibu kwa kirefu jibu ambalo lilimpa mwanga Kamanda Amata.
“Sikiliza Omongwe, waliomuua Chonde wanakutafuta na wewe, hivi jana ilitakiwa uuawe, unalijua hilo?” Kamanda Amata akamuuliza kisha akamtazama atalipokeaje. Dr Omongwe alitulia kimya, mawazo ya ghafula yakakigubika kichwa chake, ubaridi ukapenye kuanzia nutosini mpaka unyayoni, akamtazama Amata.
“Rudia unachosema,” Dr Omongwe akaomba huku akionekana wazi kuishiwa nguvu. Kamanda Amata akamtolea kivuli cha barua ile aliyopewa Chilungu muuaji, akampatia Omongwe naye akaisoma mara nne nne kupata uhakika.
“Mpaka sasa upo hai kwa kuwa jeshi la polisi linathamini uhai na kazi yako, limemkata muuaji na limemuweka ndani, sasa nilitaka kujua kama kunauhusiano zaidi na marehemu Chonde ili tuunganishe kwa nini wanataka kukuua na wewe, umenielewa sasa?” Kamanda alipouliza swali hilo, Omongwe alitikisa kichwa kuahiri ameelewa, lakini macho yake yalikuwa yamejawa machozi ambayo yalisubiri nukta chache tu yamwagike.
“Kwa hiyo?” akauliza.
“Kwa hiyo lile ulilomwambia Chonde basi ndilo lililomuua, na hilohilo kwa kuwa wewe unalo ndio maana wanakutafuta, tumemkamata muuaji lakini sina uhakika kama yuko peke yake, uwe na hadhari kubwa, usitembee ovyo peke yako, wala nyumbani usikae peke yako,” akiwa katika kusema hayo mara mlango ulifunguliwa bila hodi, afande Marina akaingia, “Vipi afande? Mbona hivyo bila hodi jamani?” Dr Omongwe akamuuliza, “Ah samahani, sikujua kama kuna mtu,” akajibu na kuufunga mlango nyuma yake.
“Huyu ni nani?” Amata alihoji.
“Ni afande tu ila ana tabia za umbea sana, hata siku nilikuwa na Chonde hapahapa aliingia hivyohivyo, hana lolote basi tu,” Omongwe akajibu. Akili ya Kamanda ikafanya kazi haraka, ‘Anaweza kuwa pumba kama sio mahindi’ akajiwazia mwenyewe, “Anaitwa nani?” akauliza.
“Anaitwa Marina,” Omongwe akajibu.
“Asante sana, basi mimi naomba niende nitakapokuhitaji basi nitakupigia simu, naomba tusaidiane sana katika hili,” kamanda Amata alimuomba Omongwe kisha wakabadilishana namba za simu, wakati Kamanda alipokuwa akitoka, Dr Omongwe alimuita naye akageuka, “Chonde alitoka, sikumuona tena, na wewe uwe makini tafadhali, taifa linakuhitaji,” yalikuwa maneno ya Dr Omongwe kwa Kamanda, tabasamu pana liliashiria kupokelewa ujumbe huo katika moyo wa mpelelezi huyu, akatoka na kuufunga mlango kabla ya kumuaga Yule mwanadada wa mapokezi, “Asante sana mrembo, mi nakwenda,” akavuta hatua kuondoka lakini kabla hajashuka ngazi, akasimama ghafla na kugeuka nyuma, akarudi mapokezi na kuingiza mkono mfukoni akatoa waleti yake iliyotuna kwa noti za Kitazania akatoa noti ya elfu kumi akaambatanisha na kadi yake ya kibiashara, akampatia Yule dada wa mapokezi, kwa sauti ya chinichini akamwambia, “Nitafute baadae mrembo,” kisha yeye akaendelea kondoka. Yule mwanadada, afande wa mapokezi aliipokea ile kadi na pamoja na ile pesa, labda ingekuwa kadi peke yake angeikataa lakini na elfu kumi juu, ukizingatia ni tarehe dume, akazisunda mfukoni bila kuangalia vizuri…
BAADA ya kizaazaa kilichotokea katika chumba cha kitanzi, wakuu wale wa vikosi vya ulinzi na usalama walikutana falagha kutathmini tukio hilo. Mchana huo kila mtu alikuwa hana majibu, chumba cha mkutano kilikuwa hakitoshi, maana kilionekana ni kidogo mno kwa jinsi hoja hiyo ilivyokijaza. Kamisna wa Magereza alikuwa ndiye muongeaji mkuu katika mkutano huo.
“Kwa kweli ni kitendo ambacho hakijawahi kutokea katika historia ya nchi hii, hata hapa nikifikiria, bado sipati jibu kabisa, ni nini kimetokea! Chini ya ulinzi mkali wa magereza, hawa watu wamepitia wapi kuingia? Hii ni hujuma au njama,” Kamishna aliongea kwa ukali akionekana wazi kugadhibika kwa hali hiyo.
Gabriel Matinya alikaa kwa utulivu kabisa, alionekana wazi kushangazwa kwa na hali hiyo, mara nyingi matukio kama haya ambayo yametokea kwa Yaumi, yeye alihusika kwa kutumia vijana wake, lakini lililotokea leo mbele ya macho yake alikiri moyoni kuwa kuna watu wamejipanga kwa kazi za hatari, alijuwa wazi kuwa watu waliofanya hilo hana uhusiano nao, swali likabaki kichwani mwake, ni nani na kwa nini tukio hilo limetokea. Mkuu wa majeshi alikuwa ameshika tama akitafakari hali hiyo, alikurupuka pale aliposikia njina lake likitajwa, “Da kwa kweli nikiangalia tukio hilo nakumbuka sinema inayoitwa Fifty Fifty, nafikiria kama nilikuwa naangali hiyo sinema au nimeona tukio la kweli, ule ni ugaidi, tena ugaidi wa kimataifa, sasa nani kaendesha operesheni hiyo, kwa nini, hatujui, tumekwisha, kama mfungwa anachukuliwa mbele yetu, katika mikono ya askari wa majeshi yote kiulaini namna ile, basi twendeni tukailinde Ikulu kwa batalioni tatu za jeshi,” aliongea na kisha kutikisa kichwa kwa masikitiko.
Baada ya majadiliano ya muda mrefu, askari wote waliokuwa zamu siku ile waliitwa na kufanyiwa mahojiano ya ana kwa ana, mmoja baada ya mwingine. Hakuna aliyeonesha kujua lolote katika hilo, baada ya kuwahoji kwa kina ikabidi sasa wachague jopo la askari wakateua na wachache kutoka jeshi la polisi ili kufanya uchunguzi katika mipenyo yote ya gereza taarifa itolewe kwa jopo hilo ndani ya siku tatu, utata.
“Aibu sana, inabidi vyombo vya habari visiandike habari hii, ni aibu,” alisema kamishna wakati akiingia katika gari yake tayari kwa safari ya kurudi ofisini, makao makuu ya Magereza. Gabriel Matinya alionekana wazi kuchanganyikiwa kwa uzito mkubwa kwa swala hilo, alikuwa akijiuliza nani aliyefanya tukio hilo, ina maana kuna watu wengine waliokuwa wakimuinda Yaumi? Swali gumu. Aliondoka katika eneo la gereza akifuatiwa na mkuu wa mkoa na Yule wa wilaya, wao moja kwa moja waliekea Ikulu kutoa taarifa hiyo kwa mkuu wa nchi.
“Siamini mnachoniambia, mbona ni kama riwaya za Richard Mwambe kwa jinsi lilivyo?” Mkuu wan chi alimuuliza mkuu wamkoa ambaye alikuapo kwenye tukio lile. “Hii nchi siku hizi kila kitu kinaweza kutokea, nimwamini nani katika ulinzi wan chi?” alijisemea huku akiwa ameinamia mezani. Mkuu wa mkoa alimpa wazo la kuitisha wakuu wa vyombo vya usalama nchini ili kupata suluhisho na jinsi ya kuanza uchunguzi ili kujua ni nani amehusika au kikundi gani kimehusika, kama Al-Qaeda, Boko Haram, Al-Shabab, Anti Baraka au ni kikundi gani na kwa nini.
“Haina haja mheshimiwa, achana na hilo halitasaidia, hata nikiwaita nitawaambia tu waimarishe ulinzi hapa Ikulu na kwenye idara nyeti, najua ni nani wa kumuita na anayeweza kutekeleza kazi hii kwa ufanisi,” Mkuu wan chi aliongea kwa unyonge kisha wakaagana na mkuu wa mkoa akimuahidi kuonana naye siku inayofuata. Mkuu wan chi akajiinamia mezani, hofu kuu ya usalama wa nchi anayoiongoza. Alitafakari kwa kina lakini jibu lilikuwa kitendawili, amiri jeshi mkuu alibaki akifikiria nini cha kufanya.
§§§§§
“Nimekuiteni hapa kwa jambo moja nyeti sana, ijapokuwa watu hawajui kilichotokea na kwtu tumekifanya siri, lakini sina budi kuwaambi ninyi askari wangu wa miamvuli ili muingie kazini mara moja, Yaumi hajanyongwa,” Matinya alikuwa akiwaambia vijana wake, akawatazama kwa jinsi walivyopigwa na butwaa, “Ametekwa katika hali ambayo mpaka sasa sisi wenyewe hatujui ni nani aliyefanya hilo, naomba muingie kazini mumtafute awe ndani au nje ya nchi,” Matinya akashusha pumzi na kuusikiliza ukimya uliotawala katika chumba hicho, akaendelea, “Mpango wetu ulikuwa pia Dr Omongwe afe kabla ya leo, lakini nasikitika kuwaambia kuwa bado yupo hai, inaonekana kuna tatizo hapa, nalo lifanyiwe kazi mara moja, ikiwezekana auawe,” Matinya bado alikuwa akiongea kwa taabu kidogo huku akionekana kuloa jasho mwilini, presha ilikuwa inapanda na kushuka bila mpangilio maalumu.
“Boss!” Scogon alimwita Matinya, wakatazamana, “Uwezo wetu ni mdogo sana kuweza kumtafuta Yaumi kama atakuwa ametekwa na watu wenye taaluma hiyo kwa kiwango cha juu, tunaweza tukatumia muda mwingi sana na mambo yakaharibika, we unalionaje hilo?” akauliza.
“Nimekuelewa, nafikiri itabidi tukodi mtaalamu atakayeweza kutusaidia katika kazi hili, sasa sijui tuangalie wapi, Israel, Urusi, Ureno, Somalia au wapi sijui, lakini liache nitakupa jibu usiku nikikutana na mtu wangu muhimu kwa kazi hiyo,” Matinya akamaliza na kuagana na vijana wake akiomba asisumbuliwe kwa muda kwani anahitaji kupumzika.
Scogon aliwatazama vijana wake, kikosi kazi, wote aliwaona wapo katika hari ya kazi na si vinginevyo, “Tunaingia kazini, hakikisheni mnamtafuta Yaumi kwa siri chinichini na kila jibu mnipe mara moja,” baada ya kupewa kazi hiyo wakatawanyika.
Scogon alimalizia kinywaji kilichojaa katika glass yake, akaitua glass na kuiacha mezani wakati yeye akitoka nje ya nyumba hiyo, katika ngazi za kupandishia barazani akakutana na Marina ambaye ndiyo kwanza alikuwa amefika katika nyumba hiyo, “Vipi? Mzee yupo?” Marina akamuuliza Scogon, “Yupo ila kasema asisumbuliwe,” akajibiwa. Ijapokuwa aliambiwa hivyo lakini alipitiliza mpaka katika chumba ambacho Matinya hupenda kupumzika, akasukuma mlango na kuingia ndani kisha akaufunga kwa ufunguo nyuma yake.
“Marina, afadhali umekuja dear wangu, leo njiko vibaya sana hata sijielewi nafanya nini na naacha nini” matinya alimwambia yaumi huku akimshika mkono kumvutia kitandani, akambusu, “Nipe yaliyojiri magereza,” akamwambia.
“Aaaah mpenzi, my sweetheart, mbona Omongwe hajafa ni mzima mpaka sasa, halafu leo alikuja kutembelewa na ACP Jaffary kutoka kituo cha polisi cha kati, niliwakuta wakiongea maswala haya haya hasa kifo cha Chonde,” ilikuwa ni habari nyingine iliyoleta mshtuko kwa Matinya, “ACP Jaffary,” akarudia jina hilo huku akitafakari. “Nahisi mpango huu umeshakuwa mgumu,” aliongea tena kwa upole huku akiwa kamuegemeza Marina kifuani pake. “Mpango gani mpenzi, mbona siku zote hutaki nkunambia?” Marina aliuliza, lakini Matinya alichukua muda kujibu.
“Marina, una hati ya kusafiria?” Matinya alimuuliza Marina, “Hapana sina kwani vipi?” naye aliuliza.
“Kila siku nakwambia hutaki kunielewa, nitakuacha hapa wakati mi nahamia nchi nyingine siku si nyingi,” Matinya akaeleza, “Na kwa nini uhame?” akauliza.
“Shauri yake, mwenye macho haambiwi tazama,” Matinya alimalizia maneno yake na kujizungusha upande mwingine kisha akafumba macho kuutafuta usingizi.
§§§§§
“Naomba nitajie majina ya wote unaoona wanaweza kuwa watuhumiwa katika kadhia hii ili nianze mmoja baada ya mwingine,” Kamanda Amata alimwambia Yaumi wakati wakiwa wameketi sebuleni katika ofisi nyeti huko ‘Shamba’.
“Kamanda kwanza kuna mdada anaitwa Marina ni askari wa jeshi la Magereza pale Segerea, huyu kwa vyovyote anajua kitu, maana alikuwa akinifuatilia sana gerezani na kunipa maneno ya kejeli, kuniita mi muuaji,” Yaumi alikuwa akiongea huku akisikitika sana. “Ok, Marina, na mwingine ambaye una wasiwasi naye…” Kamanda aliandika pembeni na kuendelea kuuliza.
“Kwa kweli ukiacha Yaumi, nitakuwa muongo kujua majina ya wengine, kati ya ninowahisi ni mmoja namkumbuka sana kwa sura, huyu ndiye nilimuamuru kuteremka pale Morocco,” Yaumi akajibu. “Ok, baadae mtaalamu wetu atachora picha ya huyo mtu kwa maelekezo yako ili tuitambue, haya niambie unamfahamu anaitwa Omongwe? Daktari wa jeshi la Magereza” Kamanda akauliza.
“Ndiyo, ni rafiki yangu sana, nilikuwa nae JKT, yeye alipoingia Magereza mimi nikapata mchumba na kuolewa, na alikuwa ananisaidia sana mimi kutoka nje” Yaumi akajibu. Kamanda Amata akaandika tena kwenye kijitabu chake cha kumbukumbu, akaichomoa peni yake na kuunganisha kidubwasha cha kuvaa sikioni akampa Yaumi asikilize mazungumzo yake na Omongwe. Baada ya kumaliza kusikiliza, alimuona Yaumi kama mtu aliyepigwa na shoti ya umeme, “Walitaka kumuua?” akauliza, “Kama ulivyosikia,” kamanda akajibu. “Tafadhali msaidie,” Yaumi alilalama, “Usijali, yuko katika ulinzi hawawezi kumuua,” Amata akampa moyo.
“Yaumi naomba uniambie, Uganda ulikwenda kufanya nini?” Kamanda aliendelea kuhoji kiurafiki zaidi hali mbayo ilimfanya Yaumi kujibu bila woga.
“Mume wangu kabla hajafa kuna namba aliniandikia, lakini kabla hajanifafanulia juu ya namba hizo akakata roho, kwa maana alinambi akuwa kuna jambo zito anataka kunieleza, lakini hakufanikiwa, mimi sikuwa najua juu ya namba hizo, nilizinakili pembeni, nikiwa mahabusu nikapata rafiki mmoja kiziwi anaitwa Fasendy, yeye aliachiwa baada ya kukosekana ushahidi huyu mwanadada alikuwa akija kuniletea chakula mara kadhaa, akanielekeza nyumbani kwake, siku nilipotoka kwa dhamana alinikaribisha kwake nikalala pale siku kama mbili hivi ndipo aliponambia kuwa zile namba kwa jinsi zilivyopangwa ni namba za posta pale Kampala, kwa sababu alisema namba tatu za kwanza ni zinamaanisha Uganda zilikuwa ni + 256 na iliyofuatia ilikuwa na tarakimu tano 16841 baada ya kuitafakari kwa muda huyu dada akanambia itakuwa ni namba ya sanduku la posta, na ile ya mwisho ilikuwa ni tarakimu nne 5576 akanielekeza kuwa hizo ni namba za mtaa na majengo, hivyo akaniambia mpaka ofisi gani ya posta yenye hilo sanduku kutokana na na mpangilio wa hizo namba,” Yaumi alieleza kwa ufasaha kabisa. Kamanda Amata akabaki kinywa wazi akijiuliza jinsi huyo mwanamke anavyoweza kuzichambua hizo namba kwa ufasaha kujua mpaka zinamaanisha nini na kiko wapi, akaona wazi kuwa huyo si mwanamke wa kawaida, hata yeye pamoja na kazi yake ya kikachero bado asingeweza kwa wepesi huo kujua maana ya namba hizo. “Yaumi umesema huyu dada anaitwa nani?”
“Anaitwa Fasendy, anaishi Bunguruni kwa Mnyamani nyumba namba BGN/MNI 612 B,” Yaumia akajibu.
“Ok, na pale posta Kampala ulichukua nini?” Swali linguine.
“Hakukuwa na kitu kabisa ndani ya lile sanduku,” akajibu.
“Baada ya kuona hakuna kitu ukaweka bomu, ulilipata wapi?” Kamanda akauliza huku akicheka.
“Hamna, mi nilipoona lile jamaa linang’ang’ania nikaliacha na kukimbia, ni usiku wake mi naambiwa kuwa nimeweka bomu,”
“Ok, nimeshajua, asante kwa majibu haya ya awamu ya kwanza, nahitaji kuonana na Fasendy mapema ya kesho ili nae anipe machache,” Kamanda Amata alisema hayo akiwa amenyenyuka tayari kwa kuondoka, ilikuwa ni saa mbili ya usiku….
MADAM S alimwita Kamanda Amata nyumbani kwake Masaki usiku huo kabla ya yote. Wakati Kamanda Amata akiingia katika lango kuu la nyumba hiyo ilikuwa ni muda mfupi tu tangu Madam S aingie. Kama kawaida yake, alifungua mlango wa mbele kwa namna anayojua yeye na kuingia katika sebule kubwa yenye kila kinachohitajika kuwamo. Moja kwa moja akaliendea jokofu lililopo hapo sebuleni na kutoa kinywa ji murua cha Safari Lager na kuketi kwenye sofa kubwa. Sekunde chache Madam S aliungana nae. “Kamanda! Nilikuwa nimeitwa Ikulu,” Madam S akaanza mazungumzo.
“Kuna nini tena?” akamuuliza Madam S
“Tumepewa kazi ya kumtafuta Yaumi, kwa maana ametekwa na watu wasiojulikana, mkuu wan chi ana wasiwasi na hali ya usalama kwa sasa, kama watu wanaweza kuingia gerezani pasipo kujulikana na kumteka mtu ambaye yupo katika kitanzi, yumkini basi kuivamia Ikulu!?” Madam S akacheka baada ya kusema hayo.
“Vipi ulimwambia kama tunaye?”
“Hapana, sikumwambia, ila nilimwambia tu kuwa aondoe wasiwasi kwani kila kitu kipo kwenye utaratibu,” Madam S akajibu, akanyanyua glass yake na kupiga funda moja la Kilimanjaro lager, bia ya akina mama, kisha akashusha na kuiweka mezani taratibu, “Niambie, kazi yako unaanzia wapi usiku huu, maana hatutakiwi kuwapa nafasi hawa jamaa,” akauliza.
“Sasa niko njiani kwenda Buguruni kwa Mnyamani,” kamanda akaeleza.
“Kuna nini huko?” “Katika mahojiano yangu na Yaumi, kanitajia mtu mmoja anaitwa Fasendy, anasema mwanadada huyo aliweza kumfafanilia kifungu cha tarakimu alichokuwa ameandikiwa na mumewe kabla ya kufa, sasa kwa jinsi alivyokidadavua ndio kitu kilichonivutia, natamani kuonana nae, bila shaka ana mengi ya kunisaidia,” Kamanda Amata akajibu.
Madam S alimtazama Amata, kisha akashusha kichwa na kuangalia mezani, “Amata unataka kunambia kuwa Yaumi anafahamiana na Fasendy?”
“Kwa maelezo yake, ndiyo,” Kamanda akajibu.
“Amekwambia anaishi huko Buguruni? Ok, kama ni yeye basi ni Yule mwanamke hatari ambaye Chiba alikuonesha picha yake pale ofisini jana,” Madam S akaeleza, Kamanda Amata akashtuka kidogo.
“Kwa vipi Yule atafahamiana na Yaumi? Hapana itakuwa ni mfanano wa majina tu, kwa kuwa alivyonieleza hapana si Yule,” Amata alionesha uhakika kwa kile anachokiongea.
“Ok, nenda, ukikutana naye, uje unambie anafananaje,” Madam S alimweleza Amata kisha wakaagana na kupeana mkono wa heri, Kamanda Amata akamalizia bia yake na kuondoka kwa Madam S akiahidi kuleta maelezo usiku huohuo.
Akiwa katika gari, kwa mwendo wa taratibu alikuwa akiicha barabara ya Ally Hassan Mwinyi na kukunja kushoto kuchukua ile ya Kawawa kuja Magomeni, simu yake ikaita kwa fujo, akainyanyua na kuitazama katika kioo, akaona namba tupu isiyo na jina ianawakawaka, akaiweka chini na kuendelea na safari, mara ya pili na mara ya tatu ile simu iliendelea, akaamua kuipokea.
“Hello, Jaffary, unaongea na Sina, kutoka Magereza Segerea,” ilikuwa sauti tamu ya kike iliyokuwa ikitekenya masikio ya Kamanda Amata.
“Sina, habari yako,” akajibu, moja kwa moja alijua kuwa ni Yule dada wa mapokezi katika ile zahanati ya Magereza. Aliyemwachia kadi yake ya namba za simu.
“Nimekumbuka sasa nikakupigia, uko wapi?” Sina akauliza.
“Nipo kwenye majukumu ya serikali,” Amata akajibu.
“Aiiiiii jamani, mpaka sasa, mi nilitaka uje kula huku jioni hii,” Sina alibembeleza. Kamanda Amata alijisikia ganzi kidogo kwa mwaliko huo wa ghafla, lakini afanyeje, alibaki kama mbwa aliyeona Chatu, “Ok, basi nikimaliza nitakupigia, nitakuja usijali,” kamanda alikubali.
“Asante beibi, mwaaaaa!” Sina alimaliza na kukata simu.
‘Wanawake bwana, sasa hata mtu humjui we ushamkaribisha kwako, haya nitaenda nikaone hukohuko,’ Kamanda Amata alikuwa akijiwazia alipokuja kurudisha macho barabarni alikuwa tayari amefika njia panda ya Ilala Boma, akakunja kulia kuja Buguruni.
§§§§§
“Haya sasa nataka umpigie simu Yule kijana aliyekupa ile bahasha jana uonane nae hapa, mwambie aje kwani ule mzigo Chilungu hajauchukua,” sajini Magreth alimwambia Yule mhudumu wa Kizota Bar, usiku ule walipokuwa ndio kwanza wametoka kituo cha polisi.
“Sawa, hamna tabu,” Yule mhudumu akainua simu yake na kupiga zile namba, dakika chache tu akawa kamaliza kuongea na Yule kijana kama alivyoamriwa. Sajini Magreth akaketi kwenye meza iliyopo karibu kabisa na mlango ambapo kila anayeingia alimuona, Yule mhudumu alibaki ndani ya gari hakutakiwa kushuka. Magreth alikuwa amewaweka tayri vijana wake wawili waliokuwa na bastola viunoni mwao ili kumtia nguvuni kijana huyo na kumuunganisha kwenye kesi pamoja na Chilungu.
Nusu saa baadae Yule kijana akafika pale Kizota, akaegesha gari yake kwa mbwembwe zilezile, muziki mkubwa na makelele kibao, akateremka na kuingia ndani ya wigo wa bar hiyo, moja kwa moja akaiendea kaunta. Magreth alikuwa akimwangalia tu kila afanyalo, alipomkosa anyemhitaji akachukua simu yake na kupiga ile namba huku akitoka nje, alipotoka nje ya ule mlango, Magreth alimfuata nyuma na mbele yake akakutana na wale vijana wawili, wakamzuia, “Upo chini ya ulinzi,” mmoja wao akasema, Yule kijana alishtuka na kugeuka nyuma ili akimbie, akakutana uso kwa uso na Sajini Magreth, “Huna uwezo wa kukimbia, twende kituoni, utajua huko kwa nini tumekukamata. Hakuna ujanja, kimya kimya Yule kijana alichukuliwa na kuingia katika gari aina ya Noah waliyoitumia Magreth na wale vijana wawili kufika hapo.
Breki ya kwanza ilikuwa katika kituo cha polisi Kimanga, akashushwa pamoja na Yule dada mhudumu wa Kizota, akazungushwa kaunta na kuanza kuhojiwa huku akichukuliwa maelezo. “Unamfahamu huyu dada?” aliulizwa na Magreth.
“Ndiyo namfahamu,” akajibu.
“Mara ya mwisho ulimuona wapi?” Magreth akaendelea na maswali.
“Jana, katika bar ya Kizota palepale mliponikamata,” akajibu bila kupindisha.
“Safi, sasa huyu dada anahusishwa na kesi ya mauaji yaliyokwishakutokea na yaliyopangwa kutokea, na katika kumhoji amekutaja wewe kuwa ndiye mpangaji wa mauaji hayo, kweli au si kweli?” swali hilo kutoka kwa Magreth lilimmaliza nguvu kabisa yule kijana, alibakia akitazama juu ya dari kana kwamba huko ndiko kwenye jibu la kumpa Magreth.
“Samahani,” alijibu huku akitetemeka, “Nimepanga mauaji kivipi?|” alijikaza kuuliza.
“Jana ulipokwenda pale Kizota Bar ulimpelekea nini huyu dada?” swali la Magreth lilijibu swali la Yule kijana. “Nilimpelekea bahasha,” akajibu.
“Ndani ilikuwa na nini?” akaulizwa tena.
“Sijui kilichokuwapo, mi nilikabidhiwa nami nikaileta kama ilivyo tena kufuata maelekezo ya aliyenipa bahasha hiyo,” Yule kijana alieleza kila kitu, afande Magreth alikuwa akimtazama kijana huyo na kuona wazi kuwa hajui kilichokuwamo ndani humo, aliwatazama wale askari wengine wawili mmoja alikuwa akiandika yale majibu aliyokuwa akijibu na mwingine akifuatilia kila kinachoendelea katika mahojiano hayo.
“Nimefurahi sana kwa kuwa umanijibu bila kunificha, sasa naomba unijibu swali la mwisho japokuwa ni refu kidogo, kisha nitakwambia nini kilikuwa kwenye bahasha, nambie nani alikuwa anakutuma bahasha hizo?” Magerth aliuliza swali ambalo koote alikotoka ndilo hasa alikuwa akilitaka. “Kuna jamaa anitwa Swila, ndiye aliyekuwa akinipa hizo bahasha na hata gari niliyokuwa nayo pale ni yak wake,” akajibu. “Namba zake za simu unazo?” lilikuwa swali la shauku kutoka kwa Magreth.
“Ndiyo afande,” Yule kijana akajibu na kuanza kumtajia namba hizo, Magreth akaziandika kwenye karatasi na kuzihifadhi.
“Asante sana, wewe unafaa kuwa polisi jamii, najua hakuna ulilonificha na kama lipo basi litakugharimu sana, sikiliza, sasa utalala hapa na sisi leo mpaka upelelezi utakapokamilika ndipo utaachiwa, kwa maana tunaweza kukuacha sasa halafu maisha yako yakawa hatarini, tunapomhifadhi mtu, si kwamba tunamuonea, sisi kama polisi tuna jukumu la kukulinda wewe mwananchi na mali yako, sasa kwa kesi kama hii, endapo tutakuacha sasa uende nyumbani ni hatari kwa maisha yako, huyu Swila akijua lazima atakuua, hivyo basi utakuwa hapa mpaka tutakapomkamata Swila, sisi shida yetu ni huyu Swila,” Magreth alitumia lugha ya kumfanya kijana huyu awe na amani moyoni.
“Bingo” Magreth aliwaambia wale askari waliokuwa pamoja naye, baada ya kumuweka lokapu Yule kijana ili kuisaidia polisi. Aliitazama saa yake, ilikuwa tayaru ni inakimbilia saa tano za nne za usiku. “Huyu lazima apatikane usiku huu huu,” mmoja wa wale askari alisisitiza, “Habari ndo hiyo, maana tukimpata huyu ndo hasa tutajua kwa nini walimuua ACP Chonde, huyu ana majibu yote,” walikuwa wakibadilishana mawazo usiku huo wakiwa wameketi katika kibenchi kilicho nje ya kituo hicho, sajini Magreth akiwa pamoja nao alikuwa amenyamaza kimya hachangii lolote lakini alionekana kufikiria kitu. “Nyie wanaume, hivi mnamkumbuka Yaumi?” Magreth aliwauliza wale askari wakati wakiwa pale kwenye benchi. “Si Yule aliyemuua mumewe!” mmoja alijibu, “Vipi bado yupo Uganda? Yule mwanamke Ninja Yule namkubali kwa mambo yake,” mwingine akadakia. “Amenyongwa leo asubuhi,” Magreth akawahabarisha na kuwaacha midomo wazi wale askari wenzake.
Wakiwa katika mazungumzo mara gari moja Harrier yenye rangi nyeusi ilifika na kuegeshwa mbele kidogo ya kituo hicho, ikazimwa taa. Kutoka kwenye gari hiyo akashuka kijana mmoja nadhifu, aliyevalia suruari nyeusi, shati jeupe lililofunikwa kwa koti jeusi, moja kwa moja aliingia kaunta na sajini Magreth alimfuata huku akiwa kawapa ishara wale vijana waingie pamoja nae.
“ACP Jaffary, karibu sana Kimanga,” Magreth alimkaribisha Kamanda Amata, Jaffary wa bandia.
“Ndiyo, najua kama umeniita basi kuna jambo,” Amata aliongeza.
“Yap, ndiyo, tumepata tunachokitaka,” Sajini Magreth alimueleza Kamanda Amata kila kitu walichokuwa wamekifanya mpaka kumpata Yule kijana na ile namba aliyopewa na Yule kijana. “Anaitwa Swila?” alimalizia Magreth kwa kumpa jina Kamanda Amata. “Swila,” alilirudia hilo jina mara kadhaa, “Ok, sasa inabidi atiwe nguvuni lakini mmejipanga vipi?” Kamanda akawauliza.
“Niliona nikusubiri afande, ili tuone pamoja,” Magreth alijibu.
“Ok, nipe hiyo namba, wala asipigiwe lakini muda si mrefu tutajua alipo kisha tumvamie na kumtia mikononi bila jasho ikibidi,” Kamanda Amata akatoa mawazo yake, akaichukua ile namba na kuitia katika simu yake, akairusha kwa Chiba na kumtumia sms ‘Nipe uelekea tafadhali’ kisha akakaa kusubiri. Baada ya dakika chache alipata sms nyingine kutoka kwa Chiba, ‘Ruvuma mpaka Maputo, uwanja wa ndege,’ Kamanda Amata akawaambia Magreth na wenzake na kisha wakajiandaa na wote wakaingia kwenye ile Noah na kuondoka zao.
Ruvuma mpaka Maputo ni baa ya miaka mingi sana katika eneo la njia panda Uwanja wa ndege, kandokando ya barabara iendayo Kalakata. Ni baa ambayo kila mwisho wa juma bendi mbalimbali zilipenda kupiga muziki wa nyumbani na kuwaburudisha wenyeji na wageni wa maeneo hayo.
Swila, kama anavyojulikana, kijana matata asiye na mzaha kabisa na maisha, siku hii alikuja kujivinjari pamoja na wasichana wake wawili. Imezoeleka kwa walio wengi kuwa na msichana yaani mpenzi mmoja, lakini kwa Swila haikuwa hivyo, yeye alikuwa na wapenzi wawili ambao walikuwa wakifahamiana vyema, hata wakiwa katika kuvunja amri ya sita, kitandani daima huwa wote wakimpa burudani hiyo ya dhambia kuifanya kwa mwanaume au mwanamke asiye mke au mume wako. Alikuwa ameketi kwenye kiti, mwanamke mmoja huku na mwingine kule, mezani kukiwa kumetapakaa vyupa vya pombe zote unazozijua wewe, lugha iliyokuwa inatawala mezani hapo ni ile ile ya waliovumbua pombe hizo, muziki wa nguvu ulikuwa ukiangushwa na bendi ya Msondo Ngoma, huku watu wengi wakiwa wamejiachia kwa starehe hiyo. Swila alikuwa akiponda raha, hakujua hata nini kinaendelea duniani kwa ajili yake. Mhudumu wa baa alikwenda na kumgusa begani, mara simu yake ikaita, namba hakuijua, Kaiinua akaiweka sikioni, haikuongea, akaishusha chini na kuiweka mezani. Sekunde kumi baadae ikaita tena namba ileile, akatukana tusi la nguoni na kuiweka chini, mara ikaita tena, sasa ikapokelewa, simu ile ikamuamuru atoke nje kwani alikuwa anasubiriwa, ukizingatia sauti iliyotumika ni ya mwanamke, Swila akainuka na kwaambia warembo wake wamsubiri, kisha yeye akatoka nje
SWILA alimtafuta aliyemwita kwa sekunde chache akamuona, Magreth, aliyevaa kiraia, suruali ya jeans iliyomkamata sawia na kuacha bisto zake zionekane vizuri, fulana nyepesi ya rangi nyekundu iliusitiri mwili wake mtamu kwa kuutazama kwa macho.
“Ndio msichana, sidhani kama nakufahamu,” Swila alizungumza mbele ya Magreth.
“Ni sawa hunifahamu, lakini nimepewa namba na mtu wako wa karibu sana, ana shida na anatka umsaidie,” Magreth alijibu.
“Nani? Mbona mi nina ndugu hapa mjini? Ndugu zangu ni pombe tu,” Swila akajibu kijeuri na kugeuka kuondoka zake kurudi baa.
“Swila mpenzi!” Magreth aliita. Swila akisimama hasa kwa kusikia kaitwa mpenzi, akaanza kurudi kwa mwendo uleule wa kilevi.
“We mwanamke nani kakutuma kwangu nambie, au kama huna la kusema twende ukanywe pombe,” Swila aliongea kilevi.
“Hapana, nimetumwa na mama yako,” Magreth alimwambia Swila huku akiondoka eneo lile na kusogea pembeni ambako vijana wake walikuwa wakisubiri mtu huyo akae kwenye engo nzuri, Swila akmfuata Magreth lakini hakufanikiwa kumfikia kwani alijikuta akitazamana na mdomo wa bastola, “Swila, uko chini ya ulinzi,” Swila alibaki akibabaika hajui la kufanya, mara pingu ikatua mikononi mwake akasukumiwa ndani ya gari.
§§§§§
Kamanda Amata aliridhika kwa ushirikiano aliopewa na vijana wa polisi kutoka Kimanga, “Magreth, kazi imeenda poa, nashukuru, sasa naomba msijihusishe tena katika hili ila nitakapowahitaji nitakutaarifu, ili swala litafuatiliwa moja kwa moja kutoka katika kituo ofisi maalum ya usalama ili kuumaliza mtandao huu.” Amata alimwambia Magreth huku akimpa mkono wa shukrani, “Kwa lolote nitafute,” akaongeza wakatia akigeuka kuiendea gari yake.

KITUO CHA POLISI KATI

INSPEKTA Simbeye alitulia juu ya kiti chake kama kawaida, akijitahidi kukuna tumbo lake ambalo lilikuwa likiifanya nguo yake ya kipolisi kushindwa kukutana sawasawa. Hali hii ilimfanya mzee huyu wa makamo kutumia mavazi ya nyumbani hata awapo ofisini isipokuwa siku maalum na kwa kazi maalumu. Alimkazia macho Kamanda Amata aliyekuwa ameketi mbele yake, kabla hajasema lolote akaitazama saa yake ya ukutani, ilimwambia kuwa ni saa tano za usiku.
“Yaani we kijana, mi nataka kutoka usiku sasa na wewe ndio unakuja, kuna nini? Au bibi yako Yule kakutuma? Maana ninyi hamuishiwi hoja kama Ukawa,” Simbeye alimtania Kamanda Amata.
“Ni kweli, usiku sasa hata mimi nilikuwa nataka nikalale kwa kimada, sikia mzee kuna mambo mawili, nadhani kwa vyovyote yatakusisimua nikikwambia, moja mauaji ya ACP Chonde,” Simbeye alimkazia macho Amata kwa hilo alilosikia, “Enhe na la pili,” Simbeye alitega sikio.
“La pili ni utowekaji wa Yaumi gerezani siku ya utekelezaji wa hukumu yake, najua vijana wako wanahangaika kumtafuta aliyetekeleza huo mpango, usijali waambie warudi, nimekuletea watu watatu ambao ukiwabana watakupa majibu,” Kamanda Amata aliinuka na kumpa ishara ya kumfuta, Simbeye alikiacha kiti chake, mguu kwa mguu mpaka kwenye chumba kimoja kilichofungwa kwa mlango wa vyuma, “Unawaona wale?” Kamanda Amata akauliza, Inspekta Simbeye akajibu kwa kutikisa kichwa, ndani ya mioyo yao kuna unayoyahitaji, mi nimemaliza, nitakuja kesho.
“Kamanda mbona unaongea mambo nusunusu?” Inspekta Simbeye alikmuuliza Kamnda Amata wakati alipokuwa akiondoka.
“Hao, ndio waliomuua ACP Chonde na wao ndio wanaojua mpango wa kutoroshwa kwa Yaumi,” ijapokuwa maelezo hayo yalikuwa nusu kweli na nusu si kweli, kamanda Amata aliaga na kuahidi kurudi siku inayofuata.
Akiwa ndani ya gari yake tayari kwa kuondoka alitazama ile kopi ya hundi aliyoichukua kwenye ile bahasha, ijapokuwa alikuwa na uhakika baada ya kupata majibu ya benki husika kuwa kitabu kile kinamilikiwa na nani, ilikuwa haingii akilini kwa mtu mkubwa kama huyo serikalini kuweza kufanya mambo hayo, kuwalipa wauaji na kupoteza maisha ya watu wanaotegemewa na jamii, akajiuliza kama huyo aliyeuawa, Chonde ndio pekee na Omongwe alipangwa kufuatia au kuna wengine wengi walishapoteza maisha? Hakupata jibu. ‘Chilungu ndiye muuaji, Yule kijana ni tarishi, Swila ndiye mtoa maagizo,’ akatafakari kidogo, ‘Kama ni kampuni ya mauaji basi lazima kuna mkurugenzi au meneja kabisa, sasa ni nani? Labda anayetoa hundi ni mhasibu halafu juu yake ndio kuna wadosi, wanaajiri wauaji?’ Amata akajiuliza lakini hakupata jibu. Kichwa kilimzunguka, akatazama hili na lile kwa makini akajaribu kuhusianisha kisa cha Yaumi na hawa aliowakamata kama kuna muunganiko Fulani, akapata jibu, jibu sahihi, kwenda benki kutazama akaunti ya Chilungu au kama Chilungu alitoa pesa kabla ya kifo cha Chonde aione nakala ya hundi kama muandiko na saini ni ya mtu mmoja na huyu aliyetoa hundi ya kuuawa Omongwe kisha ajue kwanini Omongwe, kwa nini Chonde wakati wao wote walikuwa wakitekeleza majukumu ya kitaifa, na huyu mdosi, mtu mkubwa anayetoa mapesa kununua roho za binadamu amfuatilie pia ili kujua, hakika Kamanda Amata alijikuta kwenya wakati mgumu, ‘Wakinijua wataniua, lakini kufanimeshazoea, nimeshakufa mara kadhaa kwa nini niogope sasa, nitawatia mkononi, nitawaumbua, na lazima nijue siri iliyopo,’ Kamanda Amata akapata nguvu mpya, kama kawaida yake damu ya mwili ikaanza kuchemka, akang’amua kuwa ili akamilishe kazi kwa ufasaha ni lazima atue Kampala, Yaumi alifuata nini Kampala? Ni swali ambalo aliona wazi kuwa jibu lake kwa vyovyote litampa mwanga mpya. Akainua simu yake akabofya namba Fulani akaweka sikioni.
“Hello Gina, umelala? Wenzako tupo kazini we unalala, motto una raha wewe,” kamanda Amata aliongea kwa sauti ya tuo.
“Ok, nambie kuna shida yoyote?” Gina alimwuliza Kamanda.
“Mbona una haraka au umelaliwa?”
“Unanianza, anilalie nani wakati we unanichunga kama kuku?” Gina alilalama
“Haya bwana, naomba niandalie safari ya watu wawili kwenda Kampala kesho tafadhali,” Kamanda alimwambia Gina.
“Vipi, kumekucha?” Gina akauliza kw kupitia simu hiyo.
“Tena na makucha yake,” Kamanda akamaliza na kuagana na Gina, akamuaga na kusubiri jibu la kazi aliyompa.
Kwa mwendo wa taratibu akaliondoa gari lake na kuchukua barabara ya Railway mpaka mnara wa saa kisha akanyoosha barabara ya Uhuru na kupotelea pande za Buguruni.
BGN/MNI 612 B, Kamanda Amata akashusha uso wake baada ya kuisoma namba hiyo na kuhakikisha ni sahihi na ile aliyopewa na Yaumi, nyumba mbovumbovu tu ambayo haikuwa na utaratibu maalum. Ilikuwa saa saba usiku lakini palionekana watu bado wakiingia na kutoka japo mmoja mmoja, ‘Dangulo’ alijiwazia Kamanda, alibaki ndani ya gari yake palepale kwenye maegesho ya klabu ya usiku, na nyumba anayoita ikiwa mbele yake kama mita mia tatu hivi, kwa kutumia darubini yake maalum aliweza kuona kila kitu hata kama ni giza, aliweza kusoma namba za nyumba hiyo zilizoandikwa kwa rangi nyeupe juu ya muimo wa mlango, watu wakiingia na kutoka. Alipojiridhisha kwa hilo akateremka na kujiweka tayari, bastola zake mbili huku na huku, akavuta hatua fupifupi kuelekea katika nyumba hiyo mbovu, akazikwea ngazi zake na kuufikia mlango, akausukuma ukasukumika, akajitoma ndani, kwenye korido ndefu alikutana na wanadada wawili ambao walikuwa wamevaa kiajabu ajabu, walivalia bikini tu na hawakuwa na vazi linguine mwilini mwao, mmoja akamfuata Kamanda na kumkaribisha, “Karibu mgeni, tena we mgeni kwelikweli, hujawahi kuonekana,” yule mwanadada alimwambia Kamnda huku akimpapasa mashavuni na kumtupia busu la shavu, akijigeuzageuza kwa namna ya kutamanisha.
“Boss wenu yupo?” Kamanda akauliza.
“Boss, ndo nani, we seme uhudumiwe nini, ila boss hapa hakuna kila mtu ana idara yake,” Yule mwanadada akajibu huku akimpulizia moshi wa sigara usoni.
“Fasendy!” akatamka.
“Uuuuuuuhhhhh, Fasendy, utamuweza wewe Yule mwanamke, una pesa wewe?” Yule mwanadada alimwuliza kwa kejeli huku akimuoneshea ishara ya pesa kwa kutumia vidole vyake.
“Pesa!? Dola, Yuro, Yen, Dinari, Shilingi, Paund, Lira au hela gani mnazungumzia, hapa kila hela inapatikana,” Kamanda alijibu kwa nyodo.
“Dolari bebi, unamtaka kwa masaa mangapi, ila ni kiziwi Yule anaongea kwa alama, lakini ukimwandikia anasoma?” aliambiwa na kupewa maelekezo kwa huduma hiyo. Kamanda Amata alisikiliza kwa makini na kujikuta hana jinsi isipokuwa ni kukubali kuwa anataka kulala na Fasendy ili ikiwezekana amuone hata akiwa hana nguo kama ni kweli ndiye Yule anayesemwa na Madam S.
“Masaa mawili yanatosha, nimepata sifa zake kutoka kwa mmoja wa rafiki zangu ambaye amashawahi kulala nae mara kadhaa,” Kamanda alijieleza, kisha akaitwa kwa ndani, akamfuata Yule mwanadada. Walifika kwenye korido ya pili ambako kulikuwa na milango mitatu, kushoto, kulia, na mbele, Yule mdada akafungua ule wa kushoto kwa jinsi ya ajabu, ukafunguka, Kamanda akaingia na kujikuta kwenye sebule ya kisasa kuliko nyumba yenyewe jinsi ilivyo kwa nje, akili ikamcheza kwa haraka, kwa nini nyumba hii ijengwe namna hiyo, aliamini kipo kitu.
“Karibu!” ilikuwa sauti ya Yule mwanadada ikimkaribisha ndani, Kamanda akaingia na kutazama zile samani zilizowekwa kwa mpangilio, meza kubwa ya kioo iliyotenganisha makochi ya upande mmoja na mwingine, kabati la maana, na luninga ya inchi 110 ilikuwa imetulia ukutani kiasi kwamba wewe unayetazama unajikuta kama ni mmoja wa wanaoonekana ndani ya kioo hicho. Akakribishwa kochi mojawapo kwa kuoneshwa ishara lakini Amata aliketi kwenye kochi linguine, Yule mwanadada akasonya.
“Fasendy!” Kamanda akatamka tena.
“Huwezi kumuona kama hujajieleza vya kutosha,” Yule mwanadada aliendelea kuweka vikwazo.
“Mwambie kaka yake na Yaumi amekuja,” Yule mwanadada akashtuka kidogo kusikia jina hilo likitamkwa. Akainua kidubwasha Fulani kama simu na kubonya vitufe Fulani kisha yeye akaondoka katika chumba hicho. Kamanda Amata, akaingiza mkono katika koti lake na kuiweka sawa bastola yake maana alijua kuwa hapo kuna shari.
§§§§§ USO wa kutisha wa Matinya ulionekana wazi usiku huo baada ya kuambiwa kuwa vibaraka wao waliokuwa wakitumwa kutekeleza mauaji wametiwa mbaroni. Lakini alijipa matumaini ya kutoweza kugundulika mpango wao huo.
“Sikia Scogon, kwani ulivyokuwa unampa hizo hundi mlionana wakati wowote?” Matinya aliuliza.
“Hapana, mimi ni profesheno boss, nilikuwa namuwekea palepale juu ya kaburi na kumpa maelekezo, hatukuwahi kuonana,” Scogon akajibu.
“Vizuri, ndio maana nilikupa ukamanda, sasa wale vijana nitajua cha kufanya, ila lazima wapotelee hukohuko lupango lazima uandaliwe mpango wauawe ijapokuwa najua kuwa hawawezi kutugusa kwa lolote,” Matinya alizungumza, akainua glass yake na kujimiminia pombe iliyobaki, “Keshokutwa lile kontena litatoka na kuondoka mara moja, wewe na Fasendy ambaye ndiye mkufunzi wa mafunzo mtafuatana nalo na mara moja mtaanzisha mafunzo kule msituni, tunamwezi mmoja tu wa kutekeleza lile tulilolipanga”. Scogon alitafakari kwa sekunde kadhaa, akajaribu kukumbuka kama kuna wakati wowote alioweza kugongana sura na Swila, hakuna, hakukumbuka chochote, kwa maana alijua kama wanakamatwa kwa kufutana, nani baada ya nani basi sasa ni zamu yake, alikumbuka jinsi alivyompa ile bahasha usiku wa manane. Makaburi ya Kinondoni, katikati aliiweka ile bahasha juu ya kaburi mojawapo na kisha kuondoka eneo lile, akatulia sehemu kusubiri kama mpango umesukika, baada ya lisaa limoja, saa tisa ya usiku, Swila alifika eneo lile, Scogon alimuona vizuri sana, mpaka alipokwenda na kuichukua ile bahasha, mission clear.
Akiwa kwenye kochi kubwa la vono, Scogon aliingiwa na kibaridi cha faraja kuwa hakuwa na mkutano wowote wa uso kwa uso na Swila. Alipokumbuka mara ya pili napo ilikuwavivyohivyo, akajihakikishia kama ni kutaja aliyewatuma basi angetaja kaburi, kama ni simu ilishateketezwa kwa moto kitambo kirefu sana, na simu ya mwito wa kwanza na ile ya mwito wa pili zilipigwa kwa namba tofauti, muelekeo tofauti, na eneo la tukio ni tofauti, kisha nayo ikateketezwa, zote zilifichwa namba. ‘Hamna kitu,’
“Sasa sikiliza, katika jeshi la polisi kituo cha kati hakuna mtu anyeitwa Jaffari na kwa cheo hicho, hivyo hapo lazima kuna mchezo tumechezewa, Bwana Gomegwa akishatoa lile kontena, hatakiwi kuishi maana atakuwa amejua kipande cha siri yetu” Matinya aliendelea kutoa maelekezo, “Ninachotaka sasa, ni ulinzi mkali kila mahali, muwekee mtu Omongwe, huyu Magreth najua mimi la kufanya yeye hawezi kuniumiza kichwa kwani yuko chini ya idara yangu,”
“Sawa boss,” Scogon alijibu. Matinya alimuaga kijana wake huyo na kuelekea chumbani ambako alimuacha afande Marina. Alipofika alimkuta amekwishalala muda mrefu, akamtazama na kusonya kisha akapunguza mavazi aliyoyavaa mwilini na kujiandaa kupanda kitandani, lakini kabla hajafanya lolote simu yake iliita, akaitazama, namba iliyokuwa ikionekana aliijua vyema, ‘Simbeye,’ alijisemea moyoni.
Gabriel Matinya alikuwa akimfahamu sana Inspekta Simbeye kwa uhodari katika kazi yake ijapokuwa alikuwa na mwili mkubwa uliojaa mafuta, aliitazama tena ile simu akajishauri kama anaweza kuipokea au la, baada ya mapambannnaaao makali nafsini mwake aliamua kuipoka simu hiyo.
“Ndiyo Inspekta!” Matinya aliitikia huku akisikiliza kwa makini.
“Nafikiri hili linakuhusu kwa namna moja au nyingine,” Simbeye aliongea kwa mtindo huo kama kawaida yake.
“Niambie Inspekta,” Matinya alitoa ombi.
“Nina watu watatu hapa chini ya ulinzi, nimewahoji vya kutosha ndiyo wanaohusika na mauji ya kijana wetu Chonde, naomba uje hapa asubuhi wewe mwenyewe utajua,” Inspekta alimaliza.
“Nimekusoma Inspekta,” Matinya alijibu na kujitupa kitandani, akashusha pumzi ndefu, mawazo yakamtawala. ‘Ananiita nikawaone watu hao au wamekwishaniweka kwenye orodha ya washukiwa? Lo kitumbua kimeingia mchanga,’ alijiwazia na kujikuta akiwa na jasho mwili mzima, Marina aliamka katikati ya usiku, na kuanza kumpapasa Matinya juu ya tumbo lake hasa zaidi chini ya kitovu, Matinya aliusukuma mkono wa Marina.
“Bebi vipi jamani, mbona siku hizi umebadilika?” Marina alilalama.
“Kuna wakati wa mapenzi na wakati wa kazi,” Matinya alijibu.
Baada ya kusema hayo akaingia kwenye shuka na kugeukia upande mwingine akimwacha Marina na maswali kichwani.
§§§§§
KAMANDA Amata alitulia tuli, sasa akiwa peke yake pale sebuleni ijapokuwa yeye mwenyewe alijua wazi kuwa sehemu kama hiyo huwezi kuwa peke yako, alitulia huku mkono wake bado ukiwa ndani ya koti lake tayari kwa lolote litakalojiri katika eneo hilo. Bado akiwa katika kutafakari ndipo alipoona sehemu Fulani ya ukuta huo ambayo ilikuwa na picha kubwa ya mwanadada wa kizungu aliyesimama kwa mtindo wa pekee tena isitoshe alikuwa kama alivyozaliwa, ‘Dlimwengu wa kibepari huu’ alijiwazia wakati ile picha ikionekana kama inageuka kupotelea kwa ndani, na ghafla msichana mrefu kiasi ilikuwa tabu kujua kama ni mnene au mwembamba kutokana na vazi alilokuwa amelivaa lililomfunika kila sehemu ya mwili wake isipokuwa macho tu. Aliketi katika kiti cha mbele yake huku akimtazama Kamanda Amata aliyekuwa pale sebuleni jinsi alivyokuwa akimshangaa mwanadada huyo.
“Karibu sana mgeni, unataka huduma ya falagha na mimi?” akauliza Fasendy.
“Hapana, nimekuja kufuata mzigo ambao shoga yako yaumi alikuwa ameuacha hapa,” Kamanda Amata alimueleza.
“Ok wewe ni nani?” Fasendy akauliza.
“Bwana wake wa pembeni, ni jana tu nilipowasiliana nye nay eye kunipa maagizo haya pamoja na namba ya nyumba hii,” Kamanda akajieleza.
“Ok, Yaumi ni rafiki yangu sana, ni kweli kuna mzigo aliuacha hapa siku nyingi nyuma kabla hayajatokea yale ya Kampala, sasa hebu nambie yuko wapi? Maana nilisikia kuwa ametekwa siku ya kunyongwa kwake,” Fasendy aliendelea kuzungumza kwa kuchanganya lugha ya alama za viziwi pamoja na maneno ambayo alitamka kwa shida kidogo na kwa mtindo wa pekee kana kwamba alikuwa ni motto anayejifunza kuongea.
“Yupo, kwa sasa tumemficha huko katika misitu ya Kazimzumbwi, na keshokutwa alfajiri ataondoka nchini kwa njia ya barabara mpaka Lusaka ambako atachukua ndege na kuelekea USA kupumzika maisha yake yote.
“Ok, nimefurahi kwa hilo, maana nilisikia kwenye vyombo vya habari juu kupotea kwake,” aliposema hayo akanyanyuka na kupita palepale kisha akarudii na mfuko wa plastiki uliokuwa na vitu kadhaa ndani yake, Kamanda akaupokea na kutoka pale alipoketi, aliupekuwa mfuko huo harakaharaka akaona nguo chache, za nje na za ndani, wallet moja ya kiume, hakukuwa na kitu kingine zaidi.
“Ni hivi tu?” akauliza.
“Ndiyo hakuna cha zaidi, msalimie sana mwambie namuombea heri katika yote lakini akiwa ametulia anitafute kwa simu” Fasendy alimwambia Kamanda wakati huo alikuwa tayari amesimama.
“Sawa zimefika, na nitahakikisha anakutafuta kabla hajaondoka, maana hata yeye anakutafuta sana,” Amata aliongeza.
“Oh, samahani, si vibaya kama ningekujua jina lako,” lilikuwa ni ombi kutoka kwa Fasendy kwenda kwa Kamanda Amata.
“Jaffari,” alijibu kwa haraka huku akimpa mkono Fasendy kwa kuagana naye. Kamanda Amata alikutana na kiganja kikavu cha mwanadada huyo na kwa harakaharaka aligundua kuwa mkono huo si bure ila unaonekana kuwa na shuruba nyingi.
Akiwa kwenye gari yake, Kamanda Amata alikuwa na mawazo lukuki juu ya shughuli hiyo inayomkabili ambayo sasa alishaona kuwa uzito wake ni mkubwa, akajiuliza sana juu ya nyumba hiyo ya Fasendy kwa jinsi ilivyo nje na ndani, akilini mwake alijua wazi kuwa lazima kuna kitu zaidi ya nyumba ya kawaida.
Breki zake zilifanya kazi na kusimamisha gari hiyo pembezoni mwa mtaa Fulani huko Kimanga, ukimya uliotawala eneo lote hilo ulimfanya kamanda Amata kuchukua tahadhali hasa wapi pa kuliacha gari lake, alizungusha huku na kule na mahali Fulani alikuta kuna kagiza kidogo maana palikuwa pamefunikwa na miembe miwili mikubwa iliyokuwa upande mmoja na mwingine wa barabara, akaegesha hapo na kuzima gari kisha akatulia kama dakika kumi hivi, hakuona dalili zozote za mtu eneo hilo zaidi ya mbwa waliokuwa wakirandaranda huku na kule. Akashuka na kuuurudishia mlango kabla ya kuufunga kwa rimoti maalum ya gari hiyo.
Kisha akiwa ameweka mikono yake katika mifuko ya koti lake upande huu na ule alitembea taratibu akipita upenuni mwa nyumba hizo, huku akimulikwa na taa za nje za majumba hayo ambayo ndani yake watu walikuwa wamelala fofofo hawajui ulimwengiu wa ulikuwa ukikabiliwa na vitu gani. Aliifikia nyumba anayoitaka, nyumba ya iliyokuwa ikikaliwa na Yaumi na bwana Kajiba kabla ya umauti wake. Alizunguka upande wa nyuma ambapo palitawaliwa na zao la matembele alitazama pande zote hakuona tatizo, kwa sekunde mbili aliukwea ukuta huo na ile ya tatu ilimkuta akitua taratibu kwenye uwa wa nyumba hiyo, akatembea kwa hatua za tahadhari mapaka kwenye mlango wan a kuuchezea kidogo tu nao ukamchekea, akaingia ndani kufuata kijikorido kifupi kabla hajafika sebuleni ambako alikukuta kupo katika hali ya usafi kana kwamba kulikuwa na mtu anayeishi katika nyumba hiyo, alirudi kinyumenyume mpaka kwenye mlango mmoja wapo ulioonekana wazi kuwa ndiyo ‘Master Bedroom,’ akauchezea vile vile na kuingia ndani kisha akajifungia, kwa kusaidiwa na mwanga mkali ila usiotawanyika mbali wa kurunzi yake ndogo mithili ya kalamu aliweza kuona hapa na pale.
Akaiendea droo ya kitanda na kupekuapekua hakuona kama kuna analolihitaji, droo zote za kabati bado hakuona kama kuna la maana kwake. Dakika tano alizitumia ndani ya ndani ya chumba hicho akipekuwa huku na kule lakini tayari sehemu zote zilikwishapekuliwa na Yaumi na wabaya wake hivyo kila kilicho cha muhimu kama si Yaumi basi wale watu walikwishakuchukua. Kamanda Amata akaona hakuna haja ya kupoteza muda katika nyumba hiyo, akavuta hatua chache kuuelekea mlango, kabla hajaufungua, akili yake ilizungumza kitu, akageuka nyuma na macho yake yakakutana na picha kubwa ukutani, picha ya kioo safi, aliweza kuiona kwa kutumia ule mwanga wa ile kurunzi, akaitilia shaka picha hiyo, akaiendea na kusimama mbele yake, mara hii alizima ile kurunzi, akatoa miwani yake maalumu ya kuweza kuona gizani akaipachika usoni mwake, naam aliweza kuona sawia, akapapasa ile picha kana kwamba anataka kuiondoa pale ilipo, katika moja ya vipepeo ambao walikuwa kwenye picha hiyo hakuwa kipepeo wa kawaida, Kamanda Amata alimgundua Yule kipepeo, kipepeo hadimu sana duniani anayepatikana katika nchi ya Tanzania pekee huko Udzungwa katika milima ya tao la Mashariki. Kati ya vipepeo wengi walioipamba picha hiyo, ni huyo tu aliyemvuti Amata, kwa wepesi wa akili na kazi yake, aligundua kuwa hakuwa kipepeo wa kawaida akmgusagusa kwa namna Fulani hivi kwa mtindo tofauti, mtindo wa tano ulikuwa ni sahihi kabisa, ile picha ikafunguka kama kajimlango kadogo na kuruhusu Kamanda Amata akutane na lock ya kielektroniki iliyofunga eneo hilo kwa ndani, ‘Bingo!’ kwa kuwa lock hiyo ilikuwa ikifunguliwa kwa namba maalumu, Kamanda Amata alikuwa na mchanganyo wa namba niyingine, tarakimu 12 ambazo si rahisi kwa binadamu wa kawaida kuzijua, akaziingiza katika kile kibompoli chenye tarakimu 9 na mara kitu kama droo ya sefu ikafunguka kwa kutokeza kwa nje taratibu. Ndani ya droo hiyo kulikuwa na makabrasha kadhaa, hakuna muda wa kuyasoma, Kamanda Amata akayanyanyua kama yalivyo na kuyaweka juu ya kitanda, akachuku karatasi kutoka mfukoni mwake na kuandika ujumbe Fulani kisha akaitumbukiza katika droo ile na kuifunga kama ilivyokuwa, akavua koti lake na kukusanyia vile vikolokolo na makabrasha Fulani na baadhi zilikuwa ni pesa taslimu akarundika yote katika koti lake na kutoka eneo hilo bila kujulikana na mtu.
§§§§§
Pambazuko la siku iliyfuata lilimkuta Matinya katika VX lake la serikali akiingia mijini kutoka nyumbani kwake, yeye hakubanwa na foleni kwani hata hao wanaoruhusu fokeni ni vijana wake, moja kwa moja alifika katika jengo ilipo ofisi yake, wizara ya mambo ya ndani ya nchi. Bila kuchelewa aliendea daftari maalum na kuweka saini akifuatiwa na wengine wa chini yake kicheo. Kisha akarudi garini.
“Twende kituo cha polisi kati mara moja,” alimuamuru dereva na safari ikaanza. Haikuwachuku muda mrefu tayari walikuwa katika kituo hicho, salamu za utii kwa mkubwa, salamu za kijeshi zilimwagika kwa Matinya amabye mkononi mwake alishika rediocall yake. Alikuwa akitembea harakaharaka mpaka kwenye ofisi ya Inspekta Simbeye, bila kugonga hodi aliingia na kumkuta mzee huyo aliyechoka kinamna Fulani.
Inspekta Simbeye alimkaribisha Matinya na kuketi naye wakiwa wanatazamana.
“Ndiyo Inspekta nimeitikia wito wako,” Matinya alianzisha mazungumzo.
“Nami nashukuru, hapa kuna vijana watatu wameletwa jana kutoka kituo cha polisi cha Tabata na Kimanga, wameletwa kwa tuhumu za kufanya mauaji ya ACP Chonde, baada ya kuwabana sana kwa kipigo kinachostahili, mmoja wao akaropoka kama si kusema kuwa pia alishiriki katika mauaji ya Bwana kajiba kule Kimanga kwa kuwa yeye huwa anakodiwa tu kwa kazi hiyo kwa malipo maalum. Kwa kuwa swala la mauaji ya Kajiba lilikuwa katika idara nyeti ya polisi ambayo inapata maelekezo kutoka kwako, ndio maana nikakuita uusikie utata huu wewe mwenyewe. Ni kweli anayosema kijana huyu au ni vinginevyo?” Simbeye akawasha mtambo maalumu wenye kunasa sauti, akazirudia sauti za mahojiano na kijana Yule, Matinya alisikia wazi yaliyokuwa yanasemwa na kijana huyo, mshtuko wa wazi ulionekana machoni mwa Matinya, akajua lol, sasa siri inafichuka, ‘Swila!’ akatamka jina hilo moyoni mwake kwa hasira.
“Inspekta Simbeye, umefanya kazi kubwa ambayo ilikuwa inatutia utata na kutunyima usingizi, tulimhukumu Yule mwanamama bila kosa!” Matinya akajifanya anasikitika lakini halikuwa sikitiko la kutoka moyoni, kisha akamtazama Simbeye, “Ok, hilo liache maadam liko chini yangu nitawapa kazi wale vijana waje kumshughulikia ili aseme na wenzake wote kisha tujue tunafanya nini,” akamwambia Inspekta Simbeye kisha akaondoka zake huku akimwagiwa saluti za kutosha.
Ndani ya ofisi yake alikuwa mara ashike hiki mara kile ilimradi tu alikosa utulivu, nafsini mwake ilikuwa ni pigo kubwa sana kwa hatua hiyo ya mtu kujitaja kuwa ameshiriki mauaji ya Kajiba, hakutegemea lakini sasa aligundua kosa alilolifanya…
*************
*******************
**********************
Kamanda Amata alitoa tabasamu pana kwa Madam S kwa kusikia kauli hiyo.
“Mi Mlokole Madam!” kamanda alitania.
“Ungekuwa we ni mlokole serikalim ingefunga hilo kanisa maana lingekuwa la wakengeufu, nenda zako bwana mi nina shughuli zangu,” Madam S alimwambia Kamanda.
Kamanda Amata alitoka ofisini kwa Madam S na kupanda pikipiki lake akielekea nuwanja wa ndege, ijapokuwa kulikuwa na foleni lakini aliweza kupenya hapa na pale na akafika mapema. Ilikuwa bado saa moja ndege iondoke, aliacha pikipiki yake na kuingia ndani, moja kwa moja akapita mpaka sehemu ya kuondokea abiria kwa kuwa daima alikuwa hakaguliwi.
“Chiba!” aliita Kamanda alipokuwa nyuma yake.
“Oh Kamanda, mtu wetu huyu hapa,” Chiba alimwambia Kamanda huku akimuonesha kwa mwanadada aliyevalia guo kubwa jeusi, lililoruhusu macho tu kuonekana.
“Ok, Chiba, kuna kazi nyingine, nataka unifanyie uchambuzi wa namba Fulani kasha unitumie haraka, ukitoka hapa nenda kwa Madam S atakuonesha,” Kamanda alitoa maelekezo, akaagana na Chiba.
“Beibi,” Kamanda aliita.
“Beibi,” Yaumi alijibu. Kamanda Amata akainuka na kumshika mkono wakaondoka na kuingia chumba kingine, wakaketi humo.
“Yaumi, tunaenda Kampala, nina uhakika ulikuwa sahihi kwenda Kampala, twende ntukaona kuna nini ili tupate jibu la kitendawili hiki, nikuulize swali?” Kamanda alimuongelesha Yaumi.
“Sema au uliza,” Yaumi akajibu kwa sauti ya chini.
“Unajua lolote katika juu ya namba hii?” akamtajiia ile namba aliyoipaya katika kile kitabu. Yaumi alitulia kimya kwa muda akiitazama ile namba,
“Tarakimu nne za mwisho nakumbuka alikuwa anapenda sana kuzitumia kwenye simu yake kuhifadhi kumbukumbu,” Yaumi alijibu. Kamanda Amata aligwaya kwa jibu hilo, alitulia kufikiri juu ya jibu hilo,
“Niambie, kivipi?” kamanda aliuliza.
“Alikuwa na simu ambayo akibofya namba hizo aliweza kurekodi ujumbe wowote autakao, lakini sikumbuki alikuwa anabonyeza vipi, kuna jinsi alikuwa akifanya,” Yaumi alijibu. Kamanda Amata akachukua simu yake na kumtumia meseji hiyo Chiba ili naye aweze kufanya lolote katika hilo. Tangazo la kuwataka abiria waingie ndegeni likasikika, kamanda Amata akamshika mkono Yaumi na wote wawili wakaingia ndegeni tayari kwa safari.
******************************
Sajini Magreth alianza kazi siku hiyohiyo katika ofisi yake mpya. Alipewa maelekezo ya kazi kuwa kila anapokwenda lazima atoe taaridfa kwa IGP ili ijulikane ni wapi alielekea. Kwa ujumla Matinya alitaka kujua nyendo za Margreth ili ajue ni wapi anaweza kuitimiza azma yake.
Ofisi mpya ilikuwa ngumu sana kwa Sajini Margerth kutokana na kazi nyingi na pia kazi ngumui, kila wakati alijikuta akiwa na kazi ngumu za kuzifanya, ijapokuwa kulikuwa na posho nyingi za hapa na pale lakini bado alikiri kuwa kazi ile ilikuwa ngumu sana. IGP Matinya alifurahi kuona uchapakazi wa Mgreth lakini bado alikuwa akimwangalia ni wakati gani ambao angeweza kumuweka katika kumi na nane zake ili amalize kazi. Matinya alidhamiria kumpoteza Magreth kutokana na kuwa alikuwa tayari anajua mambo mengi sana juu ya kesi hiyo ya Yaumi.
*****************************************
CHIBA na Madam S walikuwa bize kujaribu kufungua fumbo hilo, Chiba alijaribu kila namna ya kutengeneza zile namba ili zilete maana lakini bado ilikuwa ni ngumu, kila akizigeuza kwa mtindo huu au ule bado hazikuleta maana. Walibaki hoi, ‘Marehemu katuweza’ Chiba alijiwazia. Madam S alibaki kimya kumtazama.
“Chiba, vipi, ujanja leo umekuishia?” Madam S alimtania Chiba aliyekuwa akitembea huku na huku ndani ya ofisi hiyo, “Lakini si mwenyewe si amesema kuwa hizo tarakimu nne za mwisho ni namba za kufungulia begi la mumewe, sasa we unachohangaika ni nini?” madam S aliongeza.
“Hata kama, hilo begi liko wapi?” Chiba aliuliza huku bado akiendelea kuzunguka zunguka, “Na nakuambia nikipata maana ya namba hii kazi imekwisha,” Chiba alijitupa kwenye moja ya makochi yaliyopangwa vizuri kabisa katika ofisi hiyo, akitafakari jambo moja au mawili kwa kina.
0013205 Chiba aliendelea kuitazama namba ile huku akiendelea kujartibu kuichezea angalau impe maana fulani.
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kampala
YAPATA saa kumi jioni ndege iliyowabeba Kamanda Amata na Yaumi ilifika Kampala. Kwakuwa hawakuwa na mizigo ilikuwa ni muda mchache kutoka ndani na kuelekea barabarani, walifika na mara moja wakaingia kwenye tax,
“Protea Hotel tafadhali” Kamanda Amata alimweleza dereva wa tax na safari ikaanza, mitaa michache ilimfanya dereva afanye kazi ya ziada ili kuwawahisha wageni wake. Kutokana na ujuaji wa mji walifika bila kuchelewa, Amata akamlipa pesa Yule kijana kasha akaielekea kauntaaaaa tayari kuchukua chumba chake. Kitanda kikubwa kiliwalaki wageni hao, nao bila hiyana wakawa kama wamefika nyumbani. Kamanda Amata alikiendea kiti kilicho pembeni kabisa ya chumba hicho, kutoka kwenye jokofu akajitwalia kinywa akipendacho na kuketi kitini huku bastola zake mbili akiwa amezining’iniza kwenye mikanda maalumu aliyoivaa ndani ya koti lake.
Yaumi yeye alijitupa kitandani, na mjitupo huo ulimfanya mwili wake kujichora vizuri na kumshawishi Kamanda Amata. Kamanda alimtazama Yule mwanadada kwa tuo, kiroho kikimdunda. ‘Ushindwe shetani!’ alijisemea wakati akikunja nne kwenye kiti ambacho mbele yake kulikuwa na meza iliyokwisha wekwa mvinyo. Aliichukua kile kitabu cha kumbukumbu na kuendelea kukipekua pekua ili aone kama kuna linguine. Katika kurasa za mbele kabisa alikutana na kumbukumbu nyingine lakini hazikuwa na msaada sana, Kamanda Amata alifikiri sana juu ya nini la kufanya huko Kampala, kila nukta iliyokuwa ikipita katika saa yake alikuwa anionea uchungu. Akaamka na kumfata Yaumi pale kitandani, akamsukasuka kumuamsha maana tayari alikuwa akikoroma, Yaumi aliamka kwa tabu kidogo, jicho lake aklipeleka katika saa ya ukutani, tayari ilikuwa saa kumi na mbili kasororobo jioni.
“Sasa kuanzia muda huu utaitwa Zaina, na hati yako ya kusafiria imeandikwa jina hilo, hii hapa,” Kamanda alimjuza Yaumi jina hilo jipya na kumpa ile hati ya kusafiria iliyotengenezwa ndani ya lisaa limoja huko Dar es salaam, “Ijapokuwa hakuna anayejua ujio wetu hapa Kampala lakini lazima tuwe na tahadhari ya hali ya juu sana, hakikisha unavaa ile barakoa yako ili usijulikane,” Amata aliendelea kutoa maelekezo.
“Barakoa?” Yaumi aliuliza.
“Ndiyo, mask, yaani kukaa kote Dar hujui Kiswahili, utaivaa ili ikupe sura nyingine na sasa utavaa suruali na fulana amabzo ziyakupa urahisi wa kutembea au kukimbia inakobidi,” Kamanda akampa hivyo vitu vyote. Yaumi akaingia bafuni kujiandaa, ‘Hii ndo mitego ya Madam S, anajua kabisa mi ni lijali halagfu eti hakikisha humuwachi kila utakapokuwa nay eye awepo, sasa leo tutalalaje humu ndani,’ Amata alijiwazia huku akimtazama Yaumi aliyekuwa akiingia bafuni. Kamanda Amata alikula kwa macho, motto huyo wa kizaramu aliyeumbika vizuri, mfupi wa wastani, kibonge mwenye makalio ya haja, kifua kiichokuwa na matiti yaliyokitosha kwa ukubwa kadiri ya umbo lake. Kamanda Amata aliinua glass yake na kuimiminia mvinyo hiyo kinywani, huku akijiramba kwa ladha safi ya kinywaji hicho. Mara saa yake ikamfinya kwa mbal;I, akajua kuna ujumbe, aliinua mkono na kuiruhusu ilete ujumbe huo.
‘…Kamanda Amata, uwe na tahadhari sana, ijapokuwa hakuna anayejua juu ya safari yako lakini wapo, na uangalie sana utembeapo na huyo mrembo. Tunakutumia maana ya zile namba tunaomba uyitumie sawasawa kasha utupe majibu,’
Mara zilikuja namba tarakimu zilizokuwa na mambo tofauti, namaba ya nyumba, barabara, simu, posta nk. Ilitakiwa Kamanda atumie hizo namba ama kupiga simu au kwenda kwenye namba husika au vyovyote vile. Kamanda Amata alitikisa kichwa na wakati huo tayari Yaumi alijitokeza kutoka bafuni akiwa mwingine kabisa, jeans aliyoivaa ilimpa shepu tofauti kabisa ambayo ilimfanya Amata kukubaliana na kajiba juu ya uchaguzi wa mwanamke huyo, ‘kwa nini watu walitaka kukatisha maisha ya mrembo huyu?’ alijiwazia.
Simu ya Madam S iliita kwa fujo pale mezani ilipowekwa, ilikuwa ni kitendo cha kuogofya kidogo kwa maana muda huo tayari ilikuwa ofisi zimefungwa, akainua uso wake na kumtazama Chiba aliyekuwa akifanya kazi katika kompyuta yake.
“Chiba!” akaita.
“Niambie Madam,” Chiba akajibu.
“Pokea simu hiyo!” akamwambia, Chiba akamtazama Madam S.
“Simu yako, mi nitapokeaje?” Chiba akauliza.
“Aliyepiga anajua kabisa hii ni saa kumi na mbili jioni na hakuna mtu ofisini, ina maana anajua kuwa nipo au mahali anapopiga simu hii ananiona, siku hizi lazima tuishi kwa ujanja na umakini, pokea simu hiyo mwambie mi sipo halafu usikie anasemaje,”
Chiba kabla ya kuipokea simu ile, akafunmgua mkoba wake na kutoa kitu kama shilingi mia mbili kwa umbo na ukubwa wake, akaiinua ile simu na kwa haraka akakipachika pale pa kusikilizia, kisha akaiweka sikioni,
“Hallo!” aliita na kutulia kusikiliza sauti ya upande wa pili, hakukuwa na majibu ila alisikika mtu anayehema kwa shida, sauti za kitu kama vurugu kwa mbali, zingine zikipiga mayoe na zingine ni za vitu kama viti kuanguka. Mara kwa shida ilisikika sauti ilioongea kwa mkoromo.
“Wa .. me .. ni .. ua, nisaidie,” ile sauti ilitoka kwa tabu.
“Uko wapi na we ni nani?” Chiba aliuliza kwa haraka.
“Nipo Ki… mar…a S…uk…a!” na zaidi ya hapo haikusikika ile sauti bali kelele za watu waliosikika wakikaribia simu ile.
Chiba aliendelea kusikilizia lakini alipoona ni kelele za watu kulia, aliiweka simu ile mezani bila kukata, akashusha pumzi.
“Madam, ilikuwa simu yako? Au imepotea njia?”
“kama imepigwa hapa nafikiri ilinikusudia mimi, lakini kwa nini asipige polisi? Chiba twende, kasema ni wapi?” Madam alisisitiza, kisha akavuta motto wa meza na kutoa bastola moja, akaifunga kiwambo cha sauti na kuipachika mkobani.
“Chiba twende, mengine yatajulikana ukohuko,” madama aliongeza msisitizo, Chiba akakunja ile kompyuta na kujiweka tayari wakafunga ofisi na kuiendea gari, “Hapana Madam, ili tuwahi tutumie hii pikipiki ya Kamanda,” akisema hayo Chiba alikuwa tayari amekati juu ya pikipiki hiyo aina ya Cagiva, Madam S akakaa nyuma yake na kumshika vizuri Chiba, “Ole wako uniangushe!” madam alitoa onyo. Kisha safari ikaanza. Mwendo wa pikipiki hiyo uliwafanya hata polisi wa usalama barabarani kutahayari, kwa mwendo uleule iliwachukua dakika kumi na tano tu kuimaliza Ubingo na kuianza Kimara, walipokaribia hoteli ya Mbombeye walipishana na gari ya wagonjwa iliyopita kwa kasi kuelekea mjini.
“Simama!” Madam alimuamuru Chiba, naye akatii. Chiba akaitoa pikipiki nje ya barabara, Madam akateremka na kuitazama ile gari ya wagonjwa ikipotelea kwenye upeo wa macho yake. Akapanda tena juu ya pikipiki lile na Chiba kwa mwendo wa taratibu akaingia barabara ya vumbi na kuifuata kama anakuja mbezi, akasimama katika kikundi cha watu na kuwauliza kulikoni, ndipo wakapata habari hizo za mshtuko, ilikuwa ni jioni hiyo tukio la mauaji lilitokea katika jumba la jaji Ramson, Chiba hakusubiri habari hiyo ikamilike, akauliza ni wapi nyumba hiyo ilipo akaoneshwa mtaa wa nyuma yake, akaondoa pikipiki lake mpaka katika geti kubwa jeusi ambalo bila shaka ndilo jumba la jaji Ramson, alikaribishwa na vilio na vurugui za hapa na pale. Wakashuka na kuingia ndani ya ua wa jumba hilo, akina mama na akina baba kadhaa walikuwa wakizungumza hili na lile. Mzee mmoja wa makamo aliwakaribisha. .
“Sisi ni maafisa usalama, tuambieni nini kimetokea?” Chiba alinza mazungumzo namna hiyo huku akionesha kitambulisho bandia cha upolisi.
“Kijana hapa bwana kumetokea tukio la mauaji, kama dakika ishirini au thelathini zilizopita,” Yule mzee alijibu baada ya kujitambulisha kuwa yeye ndiye balozi wa nyumba kumi.
“Muuaji mmemuona?” lilikuwa swali la Madam S huku akipanda ngazi kuelekea mlango mkubwa wa nyumba hiyo ya kifahari.
“Hapana, mkewe alimsikia mumewe akipiga kelele ndipo alipomkimbilia na kumkuta akivuja damu huku akiongea na simu, twendeni muone,” Yule mzee alijibu huku akifuata nyuma ya Madam S na kuingia nao ndani kuangalia eneo la tukio. Damu nzito ilikuwa imetapakaa katika meza ya kulia chakula, kisha matone kiasi kuelekea meza ndogo iliyokuwa na simu TTCL, mkonga wa simu ulikuwa chini, Madam S alitazama eneo lile na kisha akatazama kile kiti ambacho mheshimiwa jaji aliketi akipata chai ya jioni, simu yake ilibaki palepale mezani, Chiba akaichukua na kuitia kwenye mfuko maalumu wa plastiki.
“Madam, tazama dirishani,” Chiba alimwambia Madam S, alipoinua uso wake alikutana na tundu lenye kipenyo cha kama milimita tano likisindikizwa na nyufa nyembamba kuzunguka tundu hilo.
“Amedunguliwa!” Madam S alimjibu Chiba huku akibaki mdomo wazi, aligundu kuwa muuaji alifanya shambulio lake kutokea nje, akijuwa wazi kuwa muda huo mlengwa wake ataketi hapo, nje ya dirisha hilo kulikuwa na jengio la ghorofa nne lakini lilikuwa halijaisha bado, lilikuwa gofu lenye manyasi na tando za buibui. Madam S akifuatiwa na Chiba walitoka nje ya nyumba hiyo na kuliendela ghorofa lile bila kusita wala kuuliza walizikwea ngazi mpaka chumba walichokusudia, hakika, kachero ni kachero tu, Madam S alisimama mkabala na Chiba kisha wote wakatazama chini na kuliona ganda la risasi moja tu iliyotosha kufanya kazi hiyo, hujuma. Kwa haraka waliteremka mpaka chini na kukutana na polisi waliokuwa wakiingia katika nyumba hiyo, Madam S kama kawaida yake hakupenda kuingiliana na polisi katika majukumu, moja kwa moja waliparamia pikipiki lao na kwenda mpaka zahanati ya jirani ambako majeruhi alifikishwa kwanza na kutafuta habari kama amekwishakufa au la, daktari wa zamu aliyekuwa bado hajaelewa kinachoendelea aliwaeleza kuwa majeruhi bado hajafa ila ana hali mbaya sana na amemrufaa kwenda hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
§§§§§

YUJO SUSHI BAR AND IZAKAYA – KAMPALA

KAMANDA Amata na Zaina (Yaumi) walikuwa wakimalizia chakula cha cha Kijapan ambacho waliamua kwenda katika mgahawa huwo unaomilikiwa na raia wa Japan japo kuonja ladha ya vyakula tofauti kama supu ya Miso na vinginevyo. Walikuwa wameketi kwa muda tu wote wakiwa hawajui nini cha kufanya. Baada ya kamanda Amata kujaribu kupiga simu zote zile ambazo alibuniwa na Chiba na kuzikosa sasa zoezi lilikuwa ni kutafuta namba za mtaa na nyumba ambazo pia zilitokana na namba hiyo.
“Umefurahia chakula?” Kamanda Amata alimuuliza yaumi.
“Mmm nimejaribu kula lakini nusu nitapike mh!” yaumi alijibu.
“Pole, ndio inabidi uonje ladha tofauti sio kila siku wali na maharage tua au ugali na ngege,” Amatab alimtania kisha wote wakacheka na kuinuka tayari kuondoka. Waliletewa bili ya chakula chao, haikuwa gharama, ilikuwa dola za Kimarekani 150 tu, akalipa na kisha akamshika yaumi mkono na kutokanae nje ya mgahawa huo.
Kwa mwendo wa taratibu walikuwa wakitembea kando kando ya barabara huku Kamanda Amata akiwa kazungusha mkono wake kiunoni mwa Yaumi na Yaumia akafanya vivyo hivyo, hakika walikuwa wapenzi wa ghafla, kila mtu aliwatazama, waliongea na kucheka huku wakisimama hapa na pale. Wakiwa katika mahaba hayo ya dharula kelele za breki za gari zilisikika nyuma yao, Kamanda Amata kwa haraka aligeuka na kumuweka Yaumi nyuma yake, kabla hajakaa sawa, aliona kitu kama jiwe kikimjia usoni, akainama kidogo upande na hapo ndipo aligundua kuwa ilikuwa ni ngumi ya mtu wa miraba mine, hakupoteza nafasi, kwa kitendo hicho Yule mtu alikuwa amemuachia mbavu kamanda zikimchekea, makonde mawili mazito yalifanikiwa kuvunja mbavu moja, hakumpa nafasi akiwa anauguloa maumivu, teke moja kaliu usoni lilimuinua jamaa huyo na kumuweka wima, kamanda Amata aligeuka nyuma hakumuona Yaumi, kachukuliwa.
“Tulia hivyo hivyo!” ilikuwa sauti ya jamaa mwingine aliyekuwa kamkamata Yaumi na kumkaba akimuweka upande wa mbele yake huku mtutu wa bastola ukiwa umetulia katika shingo ya mwanamke huyo. Kamanda Amata aliuma meno kwa hasira, “Ukivuta hatua moja tu nammaliza huyu mwanamke wako,” Yule bwana alisema wakati alipomuona Kamanda Amata akimjongelea, Amata akasimama, “Weka mikono kichwani,” akaamuriwa, kisha Yule jamaa aliyevunjika mbavu akajikongoja na kumfikia Kamanda pale alipo, pigo moja la uti wa mgongo lilimpeleka chini Kamanda, hakutaka kufika chini mzimamzima alijiwahi na kupiga magoti, Yule bwana akiwa kajishika ubavu wake alizunguka mbela ya kamanda Amata.
“Ha ha ha ha ha, mchezo umekwisha,” aliongea kwa gadhabu Yule bwana mkono wake bado ukiwa ubavuni. Kutokana na hasira alizokuwa nazo yuloe jamaa baada ya kuvunjwa mbavu moja alivuta teke moja kali ili kumpiga Amata kwa mbele, kosa, kosa kubwa. Kamanda Amata aliudaka mguu na kuuzungusha kwa nguvu zake zote, Yule bwana alipiga yowe kali la maumivu, mifupa ya mguu wake ailiachana, akajibwaga chini, wakatihuo tayari Kamanda Amata alikiwishaichomoa bastola yake na kulenga shabaha makini, alipofyatua alifumua bega la Yule jamaa aliyemshika Yaumi, Yule jamaa akmwachia Yaumi na kuanguka upande wa pili naye akiugulia kwa maumivu. Ile gari ikawashwa na kuanza kugeuzwa, Kamanda Amata hakutaka kuruhusu hilo litokee aligeuka na kuiona ile gari ikiingia barabarani kwa kasi, aliinua bastola yake na kuituliza juu ya mkono wake wa kushoto, alipovuta trigger haikumpa jibu la uongo, ile gari ilipasuka kioo cha nyuma na kuyumba kisha aikagonga nguzo ya taa.
Watu walianza kuja eneo lile, Kamanda Amata akakimbia na kumuinua Yaumi aliyekuwa chini akijaribu kujiinua, akamsika mkono na kuvuka nae barabara kisha akapotelea kenye chochoro za maghorofa yaliyojipanga ng’ambo hiyo ya barabara. Wakajibanza kwenye moja ya kona chochoro hizo wakitazama kinachoendelea.
“Pole Kamanda,” Yaumi alinong’ona.
“Pole wewe, mimi haya ndiyo maisha yangu,” Kamanda alijibu, mara simu katika kibanda cha simu ya jamii ikaanza kuita kwa fujo. Kamanda Amata na yaumi wakatazamana. Haikuwa hali ya kawaida kwa simu hizi kuita, mara nyingi hutumika kwa kupiga tu lakini hii ilikuwa inaita bila kukata, Kamanda Amata alishusha pumzi, akachomoa bastola yake na kuifunga kiwambo cha sauti, “Unajua kutumia hii siyo?” alimuuliza Yaumi.
“”Ndiyo, najua!” yaumi alijibu.
“Safi, haya shika hii, nilinde naenda kusikiliza simu hiyo,” Kamanda Amata akampa bastola Yaumi kisha yeye akaisogelea ile simu kwa hadhari kubwa. Akaipokea, hakuongea chochote bali aliiweka sikioni tu, aliinua mkono wake wenye simu na kubofya vitufe kadhaa kisha akaiweka karibu kabisa na simu ile.
“…Tumekwishajua kuwa upo hapa Kampala, na jambo ulilolifanya leo dakika tano zilizopita utalilipa kwa damu yako, hujui unachokitafuta lakini sisi ndiyo tunaojua unachokitafuta na tayari tuko mbioni kukipata kabla yako, hapo ulipo nakuona wewe pamoja na huyo mwanamke uliyenaye, muda wowote naweza kukuangamiza kwa risasi moja tu kama nilivyommaliza mwingine huko Tanzania lisaa limoja lililopita…”
Kabla Kamanda Amata hajauliza chochote ile simu ikakatika, akaitazama na kuiacha kama ilivyo, hakuirudisha katika kitako chake bali aliiacha ikining’inia. Akatoka na kukiacha kile kibanda akaingia tena pale gizani na kumuta Yaumi yupo makini, akamshika mkono na kuondoka nae akifuata kauchochoro hako kalikokuwa katikati ya maghorofa hayo, akatokea upande wa pili, tax nyingi zilikuwa mahali pale lakini hakuhitaji kukodi hata moja, alitembea kwa hadhari kubwa huku yaumi akiwa pembeni yake.
“Vipi Kamanda? Nani alipiga simu?” yaumi aliuliza.
“Simjui, kabla sijamuuliza alikwishakata simu, lakini kasema anatuona na anatufuatilia, nina uhakika na hilo,” Kamanda alijibu. Walitembea mwendo kama wa mita mia tano hivi, nyuma yao Kamanda Amata aligundua kuna mtu anayewafuatilia akija kwa umakini sana akijipitisha kwenye viambaza vya nyumba ili hasionekane nao lakini hakujua kama tayari walimuona. Mbele kidogo kulikuwa watu waliokuwa wakitoka na kuingia katika ukumbi Fulani, Kamanda Amata akamvuta Yaumi na kujichanganya nao huku akimtazama Yule mtu kama anakuja au la, hakumuona, akatazama vizuri hakumuona tena, akapita mpaka mlango wa chooni akaingia na kumuacha Yaumi kaunta, akasubiri kama dakika mbili hakuna mtu, akatoka na kumpa ishara yaumi kisha wakatoke upande wa pili wa jengo hilo na kuingia kwenye tax.
“Airpot tafadhali,” Amata alimuamuru dereva naye akatii na kuiondoa gari hiyo. Walipoyaacha makazi ya wenye pesa na kuanza kuingia katika viunga vya mji Kamanda Amata alimuamuru dereva asimame, akamlipa ujira wake kisha yeye na yaumi wakaingia mitaani, huku kwetu gtungeita uswazi. Walitafuta nyumba ya kufikia wageni na wakapata moja ya kienyeji zaidi, wakapata chumba, wakajifungia ndani, harufu ya mashuka yaliyokuwa yametumika bila kufuliwa ziliwatesa wawili hao lakini hawakuwa na jinsi.
“Zaina,” Kamanda aliita kwa upole, baada ya Yaumi kuitika kwa jina lake la bandia Amata aliendelea, “Tupo hatarini sana, inaonekana adui wetu ana mtandao mkubwa sana hadi kujua kama tupo hapa Kampala, naomba nikuulize swali, unakumbuka mara ya mwisho kuja na mumeo Kampala mlifikia wapi au kwa nani?”
Swali hilo lilimfanya Yaumi atafakari kwa kina, alibaki kimya, kisha akainua uso wake na kumtazama Amata.
“Kwa kweli nakumbuka tulikuja miaka kama mine nyuma, mume wangu alikuja kumtembelea rafiki yake ambaye ni mfanyabiashara mwenzake, walikuwa marafiki sana hata wakati mwingine walikuwa wakibadilishana biashara zao, sikumbuki nyumbani kwake, lakini ni mfanyabiashara anayejulikana sana, anamiliki mabasi ya abiria ya kwenda nje na ndani ya Uganda,” Yaumi alijaribu kueleza anachokikumbuka.
“Ok, sasa unakumbuka hiyo kampuni inaitwaje? Nafikiri huyu bwana anweza kuwa funguo wa kile tunachokihitaji,” Kamanda alipata wazo hilo kwa haraka.
“Yeah kweli Kamanda, sasa sijui kama nitakumbuka lile jina la ile kampuni,” Yaumi alionesha mashaka. “Usijali, hapa haina haja ya kulala, nahisi hatari mbaya katika hili jambo, tuondoke,” kamanda Amata aliamua kuondoka na Yaumi kurudi mjini, moja kwa moja walifika kituo kikuu cha mabasi cha jiji la kampala, mabasi mengi yalikuwa yakiingia na mengine kutoka usiku huo, Kamanda Amata alitulia tuli katika meza ya mama mmoja aliyekuwa akiuza chai na matoke kituoni hapo. Kamanda Amata aliagiza kikombe cha chain a kunywa taratibu huku kaupepo mwanana kakiipendezesha hali ya hewa, ilikuwa tayari saa nne usiku.
“Kampuni hiyo ilikuwa inaleta mabasi Tanzania?” Kamanda alimuuliza Yaumi.
“Hapan ilikuwa hailet mabasi Tanzania bali ilikuwa inaunda mabodi yake pale Quality Group kabla hayajaanza kazi, na hiyo yote ilikuwa ikisimamiwa na Kajiba,” Yaumi alijibu. Kamanda Amata alitikisa kichwa chake kuashiria kuelewa jambo.
“Ok, swali la mwisho kabla hatujaingia kazini, unaweza kukumb uka chochote juu ya briefcase ndogo nyekundu?” Kamanda alihoji.
Yaumi alijikuta akishtuka kidogo, pale akakumbuka kitu juu ya briefcase ndogo nyekundu, akamtazama Amata usoni, hakuna alichoongea, alionesha dalili zote kuwa kuna jambo amelikumbuka.
§§§§§
“Umefanya kazi nzuri sana mwanamke,” sauti nzito ya Matinya ililitekenya sikio la Fasendy, aliyekuwa ameketi kwenye sofa kubwa huku begi lake la mbao lilikuwa pembeni limeegemea ukuta.
“Haikuwa kazi ngumu kama nilivyotegemea, ilikuwa kama kumsukuma mlevi tu,” Fasendy alijibu huku akiinua glass yake iliyojaa kinywaji.
“Sawa sasa Yule tayari, bado huyu mwingine wa idara ya Ushuru na forodha, tunachotakiwa ni kupoteza kila anayejua juu ya hili ambaye hayupo kati yetu, yaani tuliyemjuza kwa sababu atufanikishie jambo tu, huyu roho yake naitaka kesho mara tu akikamilisha kusini kabrasha zetu za kutoa mzigo, afe kwa ajali mbaya,” Matinya alisisitiza.
“Sawa, usiwe na shaka, hizo unazonipa ni kazi ndogo sana kama kumuua mende kwa kumkanyaga mara moja tu.” Fasendy alijibu tena kwa ujeuri.
Fasendy alikuwa amekutana na bwana Gabriel Matinya jioni ya siku hiyo katika nyumba yake ya falagha iliyopon huko Temeke, akimpongeza baada ya kazi tamu ya kuondoa roho ya Jaji Ramson kwa kumdungua jioni ya siku hiyo nyumbani kwake mara tu alipokuwa amerejea kutoka kazini na kuketi kwa chai ya jioni mezani kwake. Hakufanya makosa, alitekeleza lile alilotumwa, na bunduki yake anayoipenda sana katika kazi hiyo ya udunguaji AK 47, sasa anabadilishiwa zoezi, anatakiwa kumuua bwana Gomegwa, meneja wa idara ya ushuru na forodha mara tu amalizapo kusaini kabrash a za kutoa kontena lao pale bandarini.
“Fasendy, kuna mtu mmoja amekwishaingia katika mchezo huu na huyu mtu ni hatari sana, hatari kuliko hatari yenyewe.”…..
“Nani huyo hatari kuliko hatari yenyewe? Nimepambana na hatari kuliko hiyo unayoizungumzia, nina uwezo wa kumdhibiti kama ninavyomdhibiti chawa kwa kidole change,” Fasendy alitamba.
“Mh! Fasendy, huyo jamaa ni hatari, Tanzania inamtegemea sana kwa kazi ngumu za hatari na utata, na hakuna kazi aliyoshindwa mpaka akaitwa TSA yaani Tanzania Secret Agency namba 1, na sasa tayari yuko Kampala kwa sakata hili, sikutaka kabisa huyu bwana aingie katika hili lakini sijui siri imevuja wapi…!” Matinya alionekana wazi kuchanganyikiwa.
“Ok, nimekuelewa, sidhani kama huyu meneja wa Idara ana madhara sana, unaweza kutuma vijana wako wakammaliza, mimi nikamfungie kazi huyo wa Kampala,” Fasendy alitoa wazo.
“Uko sahihi, kule Kampala tayari tulishaweka watu sawa kumshughulikia lakini taarifa zilizonijia hivi punde ni kuiwa kawatoroka na kawaachia majeraha makubwa, mmoja keshauawa, sasa hapo ujue kitaalamu huyu jamaa keshakuwa mbogo na hatujui kajificha wapi, je ni haraka gani waweza kuitumia kufika Kampala kabla ya alfajiri?” Matinya aliongea kwa wasiwasi.
“Usijali, mimi ndio Fasendy, Comando wa kike, Somali Land wenyewe wanajua nkazi yangu, Al shabab wenyewe hapa wanakaa chini, naweza kukuhakikishi nitakuwa Kampala kabla ya saa kumi alfajiri na kazi ya kummaliza huyo bwege itanichukua lisaa limoja tu pindi nikanyagapo ardhi ya Museven,” Fasendy aliongea huku akijipigapiga kifuani kuonesha ugangwe.
Fasendy na Matinya waligonga cheers na Fasendy akajimiminia kinywaji chote kisha akainua kibegi chake ambacho ndani yake kuna Yule mwana mkiwa AK 47 na vikorokoro vingine.
“Count on me!” Fasendy alimwambia Matinya kisha akaiacha ile nyumba na kupotelea kusikojulikana. ‘Kama kuna mtu ananipa matumaini kwa sasa ni Fasendy,’ Matinya alijiwazia kisha akajiinua na kuingia chumbani alikomuacha Marina akikoroma.
§§§§§
Madam S na Chiba walisimama bila kuwa na neno lolote, wakiwatazama wauguzi wa chumba cha wagonjwa mahututi wakilivuta shuka jeupe na kuufunika mwili wa Jaji Ramson ambaye alikata roho dakika chache tu zilizopita, hakuongea kitu chochote na Madam S zaidi ya kumtazama kwa macho yake maangavu. Haikuwa kawaida kwa Madam S kuangusha chozi lakini hapa alijikuta tayari chozi lake limefika sakafuni, Jaji Ramson hakuwepo tena, Jaji kijana aliymhukumu Yaumi kunyongwa takribani wiki tatu tu zilizopita. Chiba alimvuta pembeni Madam S na taratibu akatoka nae nje.
“Madam, unafikiri hili linahusiana na kisa cha Yaumi?” Chiba aliuliza.
“Asilimia mia, nina uhakika, toa hiyo simu kwanza iwashe tuangalie kilichopo,” Madam S alimwambia Chiba. Wakiwa wameketi katika moja ya vibanda vya kupumzikia Chiba aliiwasha ile simu na kuperuzi mawili matatu, meseji moja tu ilikuwa inbox, akampa Madam S aisome.
‘…kwa nini tubishane wakati kazi ulishaimaliza? Hundi tuliyokupa inatosha kwa kazi uliyofanya, na ukileta kujua utajutia uamuzi wako…’
“Kwa vyovyote kazi hiyo ni ya kumhukumu Yaumi, umeona sasa?” madam S alimwambia Chiba.
“Sasa Madam, tuitafute hiyo hundi tuziunganishe na zingine tufananishe mwandiko na saini iliyopo tuone kama vinaona maana zile mbili za Chilungu zimefanana, sasa tuone nah ii nayo ikiwa sawa na zile, tayari hatuna la kuuliza,” Chiba alitoa wazo, wote wakasimama na kuondoka eneo hilo.
Chiba alimuacha Madam S nyumbani kwake kisha yeye kuendelea na kazi ya kuitafuta hiyo hundi, alirudi nyumbani kwa marehemu usiku huohuo.

TUREJEE KAMPALA

“Nakumbuka baada ya marehemu mume wangu kurudi na ile briefcase nyekundu nyumbani na mimi kushindwa kuifungua, aliivinja kisha akatahayari sana na kile alichokiona ndani ya briefcase hiyo, usiku huo alikesha akisoma makaratasi mengi yaliyobanwa pamoja, na asubuhi nilimuona akiwa hana raha kama awali, alitoka na kununua briefcase nyingine kama ile ile akaweka baadhi ya nyaraka hizo, akanituma niende benki kuituma, sasa nakumbuka ile briefcase niliituma kwenda Uganda, kwa huyo rafiki yake, nakumbuka sana, sikumbuki ile anwani lakini nakumbuka nilituma hiyo briefcase,” yaumi alieleza kwa kirefu.
“Safi sana, sasa unaweza kukumbuka lini uliipeleka hiyo briefcase posta na ni posta gani pale Dar es salaam?” kamanda Amata aliuliza, wakati huo tayari walikuwa wameliacha lile benchi la chain a kujivuta pembeni kuliko na vurugu nyingi za vijana wanaogombania mizigo ya wasafiri usiku huo.
“Nakumbuka, ilikuwa ni miezi mitatu ilopita, nilitumia ofisi ya posta mpya pale Azikiwe, kama unakumbuka siku ile kulipokuwa na maandamano ya vyama vya upinzani na kusababisha ile barabara kufungwa,” yaumi alijibu.
“Ok nakumbuka tarehe, sawa, sasa saa moja inatutosha kujua ni wapi ulituma mzigo,” Kamanda Amata alimwambia Yaumi, lakini alimshauri kutafuta mahala salama kujificha japo kwa dakika sitini tu ambazo watakuwa wanasubiri jibu. Kamanda Amata alimpigia simu Gina ili awasiliane na mkuu wa posta usiku huo na ikiwezekane apate taarifa juu ya mzigo huo usiku huohuo.
Yaumi akiwa na Amata waliachana kila mmoja akichukua njia yake ili kuwapoteza kama kuna wanaowafuatilia. Katika kituo hicho cha mabasi kulikuwa na nyumba nyingi za kulala wageni, Yaumi alichagua mojawapo na kwenda kuchukua chumba, kisha Kamanda Amata akafuata, akiwa anatembea kwa tahadhari kubwa sana, aliiendea ile nyumba ya wageni na kuingia kisha akaketi katika viti vya mapokezi, hakuingia chumbani, aliketi mahala hapo akitazama televisheni kubwa iliyofungwa hapo mapokezi, wafanyakazi hawakuwa na tatizo walimuacha apumzike. Mkononi mwake alikuwa ameshika jacket la ngozi ambalo lilifunika bastola iliyoshikwa kwa mkono wa kuume. Kwa ujumla walijipanga, Yaumi alikuwa na bastola nyingine kutoka kwa Kamanda Amata, akiwa anafuata maelekezo sahihi anayopewa na Kamanda huyo.
Yaumi aliingia chumbani na kutulia tuli bila kuwasha taa yoyote mle ndani, aliketi kitandani na bastola mkononi tayari kwa lolote, alishukuru sana kwa kupitia mafunzo ya JKT mara alipomaliza shule miaka mingi nyuma, na sasa anaona mafunzo hayo yanavyomsaidia, alitazama kidubwasha alichopewa na Amata na kuambiwa kikipiga alam tu, ajue kuwa Kamanda matatani.
Saa moja ilitosha kwa Gina kukamilisha kazi hiyo kama alivyoamuriwa na bosi wake, alipata tafutishi zote alizoagizwa juu ya ule mzigo, tarehe uliotumwa, kwa nani, alinakiri kila kilichotakiwa na alipohakikisha kuwa amekamilisha alitoka katika ofisi hizo usiku huo wa saa tano ikiwa ni karibu na saa sita, moja kwa moja akaingia katika gari yake na kuketi nyuma ya usukani, jambo la kwanza kabla ya yote alituma kwa njia ya meseji ujumbe ulea na kuufuta katika simu yake na kishapo akachana ile karatasi katika vipande vidogovidogo na kuimwaga kwa nje, akawasha gari na kugeuza, akaingiza barabarani kama anaelekea posta ya zamani kwa mwendo wa wastani.
Palepale alipoketi Kamanda Amata alijikuta ameketi na mtu mwingine aliyevalia pama kubwa na fulana nyeusi, hakuonesha dalili yoyote ya kuwa na ubaya na Amata, mara simu ya Kamanda ikaita kuashiria kuna ujumbe umeingia muda huo, akaingiza mkono wa kushoto mfukoni kuitoa ile simu.
“Nilikuwa naisubiri hiyohiyo!” sauti ya Yule mtu ikamfikia Kamanda Amata, wakatazamana, kwa kuwa pale mapokezi palikuwa na watu mbalimbali wawili hawa hawakutaka kuonesha uadui. Kamanda Amata aliendelea kumkazia macho kijana huyo aliyejiamini, “Lete simu!” aliendelea kumuamuru Amata huku akimsukasuka kwa mkono wake.
“Unataka nini kwenye simu yangu?” Amata akauliza.
“Mi nataka simu, sikutaki wewe,” Yule jamaa bado alikuwa akimhimiza Kamanda. Mara mlango wa kuingia vyumbani ukafunguka, Yaumi akatokea alipotazamana tu na Kamanda alielewa kuwa tayari Kamanda wake yuko katika mtihani, Yaumi aliketi katika viti vinavyotazamana na na vile vya upande alioketi Kamanda Amata, wakawa wakitazamana, Kamanda Amata akampa ishara ya macho Yaumi kuwa atangulie nje, nae akafanya hivyo, haikuchukua muda Yule bwana aliyekuwa aking’ang’ania simu alitulia tuli, Kamanda Amata akamuegemeza vizuri katika kile kiti, bastola ya Kamanda iliyokuwa imefutikwa ndani ya koti lake, kisha yeye akainuka na kutoka mpaka nje, akamshika mkono Yaumi na kupotelea gizani. Wakiwa katika moja ya vichochoro vya eneo hilo, aliichukua simu yake na kuusoma ujumbe ule,

ITAENDELEA

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom