Riwaya: Asia digital

mzaramo

JF-Expert Member
Sep 4, 2006
6,371
5,183
*****SEHEMU YA KWANZA*****

NA.GEORGE IRON MOSENYA


. . Joto lililokuwa katika chumba kikubwa cha ‘internet café’ liliwafanya wateja wajipepee kwa kutumia makablasha kadhaa waliyoingia nayo ama kuyakuta katika chumba kile.
. . Joto lile lilikuwa kero kwa kila mteja mle ndani, lakini kwa mtu mmoja tu nd’o lilikuwa sherehe.
. . Alikuwa ameyaona mawindo sahihi kabisa.
. . Mawindo ambayo yangepewa ushirikiano mkubwa na lile joto.
. . Mkabala na mahali alipokuwa amekaa alitazamana na kijana wa makamo ambaye afya na mavazi yake pekee yaliidhinisha uwezo wa yeye kuwa ameegesha gari nzuri nje ya jingo lile na mfukoni hakukosa noti kadhaa zenye uzito wa kuitwa pesa. Jasho lilikuwa likimtiririka na alikuwa amejikita katika kujipangusa kwa kutumia leso yake.

. . Kabla umeme haujakatika kijana huyu alifanya siri na kuchungulia mapaja meupe ya binti huyu ambaye hakuteswa na joto lile bali ilikuwa sherehe. Wakati kijana huyu akidhani kuwa alichofanya kilikuwa siri sana…jicho kali na la kitapeli la binti yule liliweza kushuhudia matamanio ya kijana yule.
Sasa umeme ulikuwa umekatika, joto limetawala binti akaamua kuitumia nafasi.
. . “Atanijua mimi nd’o Asia.” Alijisemea wakati akifungua baadhi ya vishikizo vya blauzi yake. Alifanya hivi huku akkizuga kuwa anateswa sana na lile joto.
. . Maziwa yake ambayo pia yalikuwa meupe pee yalionyesha mchirizi ambao asilimia kubwa ya wanaume wakiutazama hutamani kuona na kinachoendelea chini.
. . Asia hakuachia uhondo wote, alimuacha yule kijana katika mtihani wa matamanio.
. . Kwa jicho lililofuzu kulaghai wanaume aliweza kuiona suruali ya kitambaa ya yule kijana ikitoka katika kutepeta na kukakamaa.
. . Akafanya tabasamu la kusanifu, akijifanya anaitazama simu yake.
Kijana wa watu hakujua kama anachezewa akili.
. . “Kashajileta pumbavu zake.” Aliendelea kufanya tathmini.
Mara akaitupa karata ya mauaji ambayo aliamini kwa namna yoyote lazima yule mwanaume atajiingiza katika himaya yake.
. . Asia kwa kutumia vidole vyake vyenye kucha bandia alibofya simu yake iliyokuwa katika mkoba.
Ikaanza kuita akaichomoa.
. .“Hellow……..mwenzangu….yaani najaribu kucheki Bro Smith, Skype umeme nao huko umekatika, nimemcheki kwenye simu, dah network ya Germany sijui vipi. Mbona yamenishuka mwenzako.” Asia aliongea kwa sauti nyororo inayobembeleza na bila shaka ilikuwa inatangaza maisha bora anayoishi kwani alikuwa katika kudeka.
. . Kimya kikatanda kama anayesikilizia kitu fulani kutoka upande wa pili. Kisha akafanya cheko, cheko lililoyaruhusu maziwa yake kifuani kucheza kidogo, akafanya kuiegemea simu akayarekebisha. Jicho lake kama kawaida likamchungulia muhusika wake.
. . Muhusika alikuwa amesahau kujipepea, alikuwa anatokwa jasho na alikuwa katika kushangaa.
. .“ “Mi nataka kuondoka hapa, maana hakuna jipya, ..” akaweka kimya tena. Kisha akaendelea.
. .“ “Naenda Msasani sahivi, lakini shoga mwenzio si unicheke kabisa mapema….sina gari hapa najishaua tu….maza kaenda nalo Mwanza, na mimi kuendesha ka Lexus kake sitaki.”
Akaweka nukta tena.
. .“ “Mh…atoke wapi wa kunichukua wewe……naenda zangu kupanda daladala mie. Nitafanyaje sasa………baadaye basi Shosti.” Alimaliza maongezi akaufunga mkoba wake baada ya kuwa ameweka simu ndani yake.
. .“Akasimama, akapiga hatua kadhaa, taratibu huku akiruhusu nyamanyama zilizovimbiana kwa nyuma na kumfanya apendeze zikitikisika kwa fujo. Yote haya yalitokea ili fulani aweze kuona.
. .“Macho hayana pazia, mikono ikamwenda kinywani, akakunja kunja sharubu zake, kisha mkono mmoja ukamponyoka na kuifikia suruali yake, akauingiza ndani na kusawazisha mambo.
. .“Macho ya Asia hayakukosea kumsoma, alikuwa ametamanika.
Kijana akasimama, akajifanya kunung’unika kutokana na huduma mbovu walizopata, hakukumbuka kudai pesa zake.
Akapiga hatua kubwa akamfikia Asia.
. .“ “Vipi dada na wewe wamekuchosha nini? Watu gani hawa yaani umeme umekatika hawawashi jenereta. Aaaargh.” Alilalamika.
Asia akajichekesha kisha akasonya.
. .“ “It’s boring…..yaani dah basi tu….but it sucks….” Akatema maneno, Kiswahili kwa mbali ung’eng’e mwingi.
Wakaendelea na mada ya kuwalalamikia watoa huduma hizo. Hadi wakaufikia ukumbi ule wa kuoneshana nani ni nani.
Ilikuwa sehemu ya kuegeshea magari.
. .“ “Kwani dada unaelekea wapi.” Kijana ambaye alikuwa hajajitambulisha jina akauliza.
. .“ “Msasani, ngoja nikapate kero nyingine ya kugombania magari. We unaenda pande zipi au safari yetu moja?” aliuliza Asia huku akijua nini kinafuata.
. .“ “Mimi nafika Namanga hapo. Kuna watu naenda kuonana nao hivi mara moja. Dah hizi kazi hizi.” Alilalamika katika namna ya kujifagilia njia.
. .“ “Poa kumbe gari moja twende ukanisaidie kuwania siti.”
Jamaa kusikia vile akajikoholesha kisha akamwonyesha Asia kwa kutumia kidole cha shahada, gari aina ya Noah nyeupe ikiwa imetulia ikimsubiri mmiliki.
. .“ “Mwenzangu heri yako…poa kaka siku nyingine lakini hapa sirudi tena aisee.” Alisema Asia huku akiondoka.
. .“ “Twende nikusindikize kidogo bwana..” alisihi yule kijana.
Asia akajifanya kufikiri kidogo kisha akauliza swali la kijinga.
“Hamna mahali unapita maana mimi nina haraka kweli.”
. .“ “Naenda moja kwa moja.”
Asia akakubali, wakaongozana garini.
. .“Safari ya kuelekea Msasani.

. .“Ndani ya gari maongezi ya hapa na pale yaliendelea….Asia kwa kutumia simu yake akafanya jambo jingine lililompelekea kujikuta anahamishiwa rasmi katika timu nzima ya digitali.
Akaandika ujumbe baada ya dakika moja simu yake ikaita.
“Mh…sorry..simu yangu inatatizo la speaker I hope sitakuboa nikitumia loud.” Asia alisema huku akiyafinya macho yake katika namba ya kumhangaisha mwanaume dhaifu.
“Aaah…hata usijali ongea tu….” Alijibu.
Asia akapokea simu akaiweka katika spika kubwa.
. .“ “Ehe nambie….” Akaanzisha maongezi.
. .“ “Peter kanipigia mwenzangu…..”
. . “Anataka nini?”
. . “Asia jamani…msamehe mwenzako …..kabembeleza sana ujue….” . . Sauti kutoka upande wa pili ikasihi.”
. . “Jackline, nakuheshimu sana…nakuomba kwa heshima ya urafiki wetu…usinambie lolote kuhusu huyo tapeli wa mapenzi, Jack umekuwa shahidi wa ujinga alionifanyia Peter….umeshuhudia uchafu wake wote…leo hii unamwombea msamaha…Jack kweli umenichoka kiasi hicho, amekulipa huyo Peter umwombee msamaha……ok Jack labda niseme neno moja tu….ulifurahia alichonifanyia sivyo…..Mbarikiwe sana “ Akamaliza huku analia, akaikata simu, uso ukiwa mwekundu, ngozi yake ya rangi ya chungwa ikikosa ustahimilivu na kuchafuliwa na machozi…kilikuwa kilio haswa. Asia alikuwa analia.
. . Kijana aliyekuwa anaendesha gari ambaye mwanzoni alikuwa amemtamani Asia alijikuta akipagawa, mara akaiegesha gari pembeni.
Vioo vyeusi tii…nani atajua kinachoendelea ndani. Nd’o uzuri wa tinted
. . Akaanza kumbembeleza Asia.
. . Akamsihi sana asilie, Asia akawa analia huku anawalaani wanaume wote.
. . Alimlaani Peter hadi yule kijana naye akamsaidia katika kumlaani.
. . “Mpendwe vipi nyie wanaume …mnataka roho zetu…mnataka tufe nd’o mjue kuwa mlipendwa au? Yaani mtalaaniwa nasema atalaaniwa huyo Peter, kwa chozi hili linalonitoka mimi Asia…Peter alitaka nini mimi nikamnyima, pesa zangu za kutumia chuo, pesa za kujaza gari mafuta zote nimempa mimi. Alitaka nini sasa, nimepigwa na dadiii mimi mamii akanichukia, kaka zangu wamenipiga makofi mimi. Kisa Peter, Peter….aah…” Asia aliendelea kulaani maneno yaliyomsulubu yule kijana.
. . Akiwa hajui cha kufanya Asia akiwa analia alimlalia, alimlalia kifuani, zile chuchu alizoziona kwa kuibia kule ‘internet café’ sasa zilikuwa zimemlalia zikimchoma katika namna ya kuleta hamasa, kucha za bandia za Asia zikalifinyafinya shingo lenye afya la yule kijana.
Pumzi za kupishana ndani na nje zikawa zinatesa katika sikio la yule kijana.
. . Sasa alianza kupagawa. Huyu Asia alikuwa anajibembeleza ama.
Akawa katika sintofahamu. Nani atampa jibu?
. . Asia akalisikia paja lake likiguswa na kitu ambacho hakikuwepo hapo awali. Hakushtuka
. . Akafanya tabasamu jepesi kisha akamzomea yule jamaa.
Hicho kitu kilivimba kutoka katika suruali nyepesi.
. . “Bwege linawahi kweli kupata hamu hili.” Asia alikebehi kimya kimya.
. . Hamu zikamzidi yule kijana, mara naye akakumbatia, mara akakumbatia kwa nguvu zaidi. Mara akaanza kunena katika lugha za maajabu zisizojulikana kitaifa wala kimataifa.
. . Mikono yake ilikuwa ikitalii katika mzigo wa titi mbili ndogo za Asia.
. . Afadhali yeye alikuwa ananena kilugha.
. . Asia alikuwa hoi kama aliyezirai.
Jamaa akajua kuwa Asia kakolea.
. . Laiti kama angejua kuwa Asia anatumia mbinu ya kidigitali, basi ni heri angebaki katika dunia ya analojia aliyokuwa anaishi awali.
. . “Baby…..Baby…..unaniua mweenzio….unaniaaa…..pliiz stop…..”
. . “Am sore bebi…am sore vere sore….me you know…” Jamaa akajaribu kiingereza asichokijua, Asia akataka kupitiwa na kicheko.
Akajikaza. Alikuwa kazini.
. . Mkono wa jamaa ukapenya katika mapaja…..Asia akajua jamaa anataka kumpima kina cha kisima na kutazama kama kina maji ama ni kikavu.
. . “Bwege asije akanichafua bure..akavuka mipaka…..”
Asia digitali akacheza kidigitali, alishagundua kuwa jamaa ni mwepesi sana.
. . Ulimi mkali kama ule wa kinyonga, ulimi ambao ulishausema uongo hadi uongo ukauzoea ukazama katika sikio la yule jamaa.
. . “Uwiiiiiii….ooooohhh yeees..” jamaa akaganda kama roboti, mkono haukwenda mbele wala kurudi nyuma.
. . Akazidi kunena kwa lugha zake zisizokuwa za kiroho.
. . Asia akagundua kuwa amefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Akafanya tekniki ya mwisho.
. . Akajibandua katika mwili wa jamaa….akaanza kujifuta midomo, na kujifanya anaona aibu……jamaa kaduwaa tu hajui digitali inakwenda vipi. Analojia ilikuwa imemwathiri.
. . Jamaa akawa na aibu za kweli, suruali ilikuwa wima sana. Akajitazama, shughuli ikaja je airekebishe ama aiache ilivyo…
Asia akajifanya haoni chochote, naye akajifanya kuzidiwa na hali.

. . “Yaani sijui tu what to say…but siwezi kujicontrol mwenzio” Asia alivunja kimya, huku akionekana dhahiri kuwa tayari amekolea.
. . “Sasa tunafanyaje jamani?” aliuliza kibwege yule mwanaume.
. . “Mi siwezi yaani sijui tu unanisaidiaje……” alizidi kulalamika.
Mwanaume akawasha gari, akaiondoa kwa mwendo wa kawaida.
Akafika Kinondoni, Chichi Hotel.
. . Hapo hakuna aliyekuwa anakumbuka kuwa alisema anaenda Msasani wala namanga.
. . Asia alikuwa anaifahamu fika ile hoteli lakini akazuga kuuliza.
. . “Vipi hapa nd’o kwenu?”
. . “Hapana hii ni hoteli baby wangu. Vipi tunaweza kuingia.”
. . “Yaani dah..sawa tu kwa kuwa siwezi kujicontrol. Lakini hapa hapana my dear…pako wazi sana siwezi” Alilalamika kinafiki.
. . “Sasa twende wapi jamani.”
. . “Popote hata Magomeni lakini hapa hapana, hizi hoteli kubwa kubwa Dady anawewza kunifumania.” Alidanganya. Uongo ukakubaliwa.
. . Gari ikageuza kurudi magomeni.
Baada ya dakika kadhaa walikuwa katika chumba katika nyumba ya kulala wageni ya bei ya kawaida. Asia alikuwa ana maana kubwa ya kuchagua sehemu kama ile.
. . “Baby kwani unaitwa nani?”
. . “Mimi naitwa Jumanne, niite J fo na Juma tu inatosha.”
. . “Ooh J fo nd’o zuri zaidi.”
. . Walipotulia kidogo Asia alichukua simu yake, kama kawaida alituma ujumbe kwa umakini mkubwa.
. . Kisha vikafuata vitendo.
. . Jumanne akiwa anaona aibu bado, mara Asia akamrukia akamfungua kishikizo kimoja, mkono mwingine ukalifikia sikio, kidole cha kati kikapenya katia sikio la kuume, mapigo ya moyo ya Jumanne yakaongezeka mwendo, shati likatoka, mara mkono laini wa Asia ukapenya katika suruali ya Juma, akaanza kujichekesha.
Asia akaongeza utundu, mara anapapasa huku mara kule.
. . Jumanne hoi.
. . Hatimaye Juma akawa laini kabisa, akapaparika akamminya Asia chuchu yake ngumu, Asia akatokwa na mlio wa ajabu wa kimahaba, Juma akapagawa zaidi.
. . Asia akajiviringisha mithili ya samaki nguva, kinguo chake kifupi kikapanda juu kidogo.
. . Shanga kadhaa katika kiuno chake.
. . Kama shambulizi basi hili lilikuwa la kimataifa.
Juma likuwa mlevi katika jambo hili.
. . Juma na shanga?? Hakuambiwa kitu na mtu.
. . Akamrukia Asia, akakirushia mbali kigauni chake.
. . Juma ana kwa ana na bikini nyeupe, jicho la Asia likiwa katika mlegeo wa ajabu kama linalotaka kufumba.
. . “Juma mi natakaaa.” Akalia Asia.
. . Juma akatoa kibukta kilichobaki mwilini.
. . Kama Juma alidhani ni ujanja kwa mwanaume kutangulia kuvua nguo, basi huo ni ujinga katika mfumo wa digitali aliokuwa anautumia Asia, labda kwa wana analojia wenzake huo nd’o ulikuwa ujanja.
Asia akamtazama Juma anavyokuja kwa kasi, akamuwahi palepale kabla hajakifikia kitanda, akamwangusha chini, mkono mmoja ukaifikia himaya ulimi ukazama sikioni……
. . Juma akalegea kama mlenda Asia akaligundua hilo.
Mdigitali akafumbua macho akakutana na kitu alichokuwa anakisaka kuanzia ‘internet café’.
. . Funguo. Zilikuwa funguo mchanganyiko.
. . Asia akamgalagaza Juma, hatimaye wakaifikia ile meza mbovu iliyokuwa chumbani.
. . Meza ikapinduliwa na Asia huku akilia kimahaba.
. . Funguo zikamwagika chini.
. . Juma hakujua lolote, mkono wa Asia ulikuwa unamsulubisha.
Sasa kikafuata kitendo cha maajabu kikiwa katika mfumo wa Digitali.
Asia akamruhusu yule jamaa kumwingia sasa.
Lengo likiwa safari ya maajabu.
. . Jumanne akafika kwa kasi zote, akatulizwa kidogo kisha akaruhusiwa.
. . Kwa papara akaleta staili ya kibaba na mama.
Asia digitali sio mjinga, yaani umweke kibaba na mama ili umwangalie usoni anavyofanya maigizo? Hata haiwezekani.
Lakini cha ajabu alikibali bila kinyongo.
. . Akalala chali, bwana mapapara akamvamia.
Vigaye vikampa raha Asia, kila mara jamaa alivyomsogelea kwa fujo naye alizidi kusogea nyuma. Si kwamba mikito ilikuwa inamzidia Asia alikuwa anafanya jambo ambalo kwa kuhadithiwa tu huwezi kuelewa we muanalojia unatakiwa ufanyiwe uumbuke nd’o utajua.

. . Wakati Asia akifanya yake pale chumbani, nje ya chumba mwanadada Janeth ama kwa jina la kazi ‘profesa maji ya shingo’ alikuwa bize akijipitisha hapa na pale akijifanya kuna jambo anatafuta.
Uzuri wa gesti za hadhi ya kawaida hakuna wa kukuuliza.
. . Kilio feki cha Asia kilimpa amani moyoni kwani ule muda ulikuwa umewadia.
Akajiweka mbali akawa anahesabu dakika.
. . “Kwa ninavyomjua Asia hapo ni viuno sita tu mambo tayari.” Janeth alijisemea huku akisoma ramani.
. . Mara akausikia mlango wa chumba cha Asia ukiguswaguswa.
. . “Tayari mambo...” Jameth alijisemea, akaiweka simu yake mfukoni.
Akatembea upesi upesi akaufikia mlango wa Asia akainama, akatoka na kitu.
. . Laiti kama ungebahatika kumuona wala usingeweza kudhani kuwa alikuwa amechukua funguo tayari. Funguo ambayo ilikuwa inasukumwa na mgongo wa Asia kila ambapo Juma alikuwa anakipampu.
. . Juma alikuwa katika dunia ya analojia, wenzake walikuwa kazini kidigitali.
. . Baada ya dakika kadhaa mwanadada Janeth akiwa katika mataa ya magomeni alikuwa anatafuta mahali pa kuwashia redio ndani ya gari la Juma, ajiliwaze huku akiyangoja mataa yaweze kumruhusu ajiondokee zake na kwenda anapojua mwenyewe. Leseni ilimruhusu kujitapa kwa raha zake.

. . Wakati Janeth akiwa anakula kiyoyozi. Asia alikuwa analia, alikuwa analia sana.
. . Juma alikuwa anambembeleza.
. . “Nipo katika siku za hatari…halafu tumefanya bila kinga….then sijui kuhusu afya yako..” alilalamika.
Juma alikiri kosa lakini baadaye akasema jambo la kushangaza.
. . “Asia usijali mimi ukipata mimba nitalea mtoto..nakupenda kutoka moyoni. Nakupenda sana.” Asia aliyapokea maneno yale kama igizo endelevu.
. . Akajifanya yamemfariji.
. . Juma akajiona yeye ni mshindi.
. . Wakaoga pamoja.
. . Wakati wa kuagana pale chumbani, mwanaume akafuta aibu. Akampatia nauli shilingi elfu hamsini.
Asia akaipokea kwa heshima zote. Moyoni akimcheka Juma kwani hakujua kama anahamishiwa digitali kilazima.

. . Hatimaye ukafika wakati wa kujipekua kama gari huwa inahifadhiwa mfukoni ama kwenye pochi.
. . Juma alipagawa, hapakuwa na gari lolote linalofanana na la kwake pale nje.
. . Alihaha na kutaka kuwauliza watu. Lakini akakumbana na maneno.
. . “Park at owners risk.” Akaishiwa nguvu. Asia naye akajifanya amepagawa lakini kupagawa kwa Asia kulikuwa katika namna ya kidigitali.
. . Asia alipiga mayowe, sio mayowe ya kuita watu hapana. Hayo ni ya kianalojia.
Asia alipiga mayowe ya kumita dereva taksi.
Alipofika akamweleza huku amepaniki. Hakumweleza juu ya gari kuibiwa, hapana akamuuliza swali jingine.
. . “Kutoka hapa hadi Tandika bei gani.”
. . “Elfu ishirini nakupeleka.”
. . Asia hakujibu kitu, akaingia garini na kufunga milango.
Juma akabaki kuhaha peke yake.
Asia digitali, akatambaa na kutoweka upesi kidigitali.
. . “Chezea Asia wewe.” Alipokuwa katika taksi alikutana na ujumbe huo. Ujumbe kutoka kwa Janeth Profesa maji ya shingo.
. . Asia akafanya tabasamu hafifu.
. . Uhakika wa kula na kutesa viwanja kwa mwezi mzima ulikuwepo.

. . . . . . . . . . . . *****
 
KISA CHA PILI


. . Juma akiwa katika kitanda hospitalini akiwa hoi kiafya analetewa taarifa ya kusikitisha lakini inayotia matumaini kidogo.
. . Gari lilikuwa limepatikana. Taarifa haikuishia hapo.
Gari lilikuwa ni sawa na kopo.
Tairi zote tano hadi ya spea, usukani, viti, taa, na redio havikuwepo tena.
Ilichekesha kuiita gari.
. . Jumanne akazimia tena.


. . Wakati Jumanne akiwa katika mashindano ya kuzimia na kuzinduka huku akifikiria maisha mapya bila kuwa na gari.
. . Wasichana watatu wenye maumbo ya tofauti lakini wakishabihiana rangi walikuwa katika meza mojawapo ya baa isiyokuwa maarufu sana katikaji ya jiji.
. . Walikuwa wameichafua meza kwa vinywaji mbalimbali huku nyama ya mbuzi ikiwafanyia tabasamu la dhihaka.
Walikuwa wameishughulikia na sasa ilikuwa imewakinai.
. . “Kwa hiyo hiyo laki mbili ya viti wanatoa lini.” Asia aliuliza baada ya kumeza funda la bia baria aina ya Kilimanjaro.
. . “Kesho jioni.” Mdada mnene kuliko wote aliyeathiriwa na utumiaji wa vipodozi vikali alijibu.
. . “Na yule bwege aliyechukua tairi mpya nd’o kasema anatuma kwa Mpesa au.”
. . “Kama kawaida yake.” Sasa alijibu Janeth.
. . “Kuhusu redio?” swali jingine kutoka kwa Asia.
. . “Ipo nyumbani kwao Messi”
. . Asia alimgeuzia macho yule dada aliyeathiriwa na vipodozi vikali.
. . “Husna Hakikisha huingii tamaa ukaiuza maana hukawii.” Asia alimwambia yule dada ambaye walimzoea kwa jina la Messi kutokana na mambo yake mengi.
. . Husna akatabasamu kisha akasema, “Nina dili jingine murua, redio kitu gani?” Husna alisema. Asia akapaliwa na donge la bia.
. . “Dili gani?” aliuliza kwa shauku.
Husna badala ya kutoa jibu, alizama katika mkoba akatoka na ‘business card’. Akamkabidhi Asia.
. . “Ya nini hii we Mmanyema.” Aliuliza.
. . “Chukua namba hizo.”
. . Asia hakuuliza swali, akaichukua namba.
. . “Nimekutana naye maeneo ya benki. Sho me me what u can do.”
. . Asia ahakujibu kitu. Alielewa Husna anamaanisha nini.
Janeth alikuwa amejikita katika kuzishambulia nyama huku Salome akiwa anafuatisha mashairi ya wimbo wa taarabu uliokuwa unapigwa katika baa hiyo.
Mavuno kwa siku hiyo yalikuwa mazuri sana.

. . . . . . . . . . *****

. . DENISS KAZINYINGI alikuwa amejikita katika kutazama filamu ya kusisimua nyumbani kwake, mara uliingia ujumbe katika simu yake ya mkononi. Simu ilikuwa katika kiti kilichokuwa mbali naye.
. . “Neema….nipatie hiyo simu” alitoa amri.
Mtoto wake wa kike akaifuata na kumpatia.
Akaitazama namba iliyotuma ujumbe. Ilikuwa mpya.
Akaufungua ule ujumbe.
. . Kabla hajaanza kuusoma mara ikaingia simu.
Nayo ilikuwa namba mpya.
Akaipokea kwa utulivu wa hali ya juu.
. . “Halow…..Deniss Kazinyingi hapa.” Alijitambulisha kwa ujivuni wa hali ya juu.
. . “Samahani…aah shkamoo anko….sorry aaah nimekosea namba pliiz, nilikuwa namtumia mdogo wangu pesa nimetuma kwako.” Sauti ililibembeleza sikio la Dennis, hakika ilikuwa sauti ya kike isiyohitaji aina yoyote ya nakshi kuipendezesha.

. . “Pesa? Saa ngapi?”
. . “Sasa hivi, yaani muda si mrefu kaka yangu.”
. . “Ok ngoja nitazame nitakupigia.”
. . Simu ikakatwa, ujumbe uliokuwa unafunguka ulikuwa ujumbe unaoonyesha pesa imeingia.
. . Kutoka katika namba ile ile iliyompigia.
. . Shilingi laki mbili na nusu. Deniss akastaajabu kidogo, hakuingiwa na roho yoyote ya tamaa. Alikuwa ni mtu ambaye pesa kama ile si chochote kwake.
. . Akanyanyua simu yake akaipiga namba iliyompigia awali ikilalamika kukosea kutuma pesa.
. . “Wewe nd’o Asia?”
. . “Ni mimi kaka nisaidie tafadhali.”
. . “Nipe dakika moja tafadhali.”
. . Simu ikakatwa tena. Kama alivyoahidi baada ya dakika moja alikuwa ametuma pesa kurudi kwa mmiliki.

. . “Game limeanza…..” ilikuwa sauti ya Asia akijisemea mwenyewe huku akimtazama Husna ambaye alikuwa amelala tayari.
. . Asia alijipongeza kwa karata ya pata potea aliyoweza kuicheza japo alikuwa na hofu ya kuibiwa ama kudhulumiwa kiasi hicho cha pesa.
. . Asia alikosea kutuma pesa maksudi, mwanzoni alitaka kutuma meseji na kujifanya kuwa amekosea namba, mbinu hiyo akaiona ya kianalojia sana.
. . Akataka kupiga na kujifanya amepiga bahati mbaya akaiona mbinu hiyo pia batili. Akaamua kuitumia mbinu ambayo matapeli wachache wanaweza kuitumia.
. . Akatuma kiasi hicho cha pesa.
. . Sasa pesa ilikuwa imerudi.
. . Asia akamshukuru Mungu wake, kisha akachukua simu yake akazipiga namba za Dennis, bila shaka jambo hilo hata Deniss alilingojea.
. . Nd’o maana akajitoa nje ya nyumba na kwenda katika bustani yake ndogo kuingoja simu ile.
. . “Ubarikiwe kaka yangu, yaani ubarikiwe sana, ni watu wachache sana wenye moyo kama wako, utaongezewa mara mia ya ulichonifanyia. . . Ujue ni ngumu sana kwa mtu ambaye hamfahamiani, ama kweli umenipa nafasi nyingine ya kuamini kuwa duniani bado kuna watu wana utu…..naomba nisizungumze mengi asante sana kaka yangu.” Alitiririka Asia, maneno kuntu lakini sauti mahaba,
. . “Usijali Asia, mambo madogo hayo nadhani huu ni mwanzo wa urafiki wetu, utajuaje maana ya Mungu mengi.’ Deniss alirusha kete yake.
. . “Haya Deniss mi nikutakie usiku mwema.”
. . “Haya asante japo hata sijajua unaishi wapi.”
. . “Mimi nipo Dar, sema ni mzaliwa wa Mwanza na mara kwa mara huwa nasafiri hapa na pale. Lakini kwa kifupi nipo Dar.” Alijibu.
. . “Ok mimi nipo Dar pia lakini nyumbani Maswa Shinyanga huko..ona sasa kumbe mimi na wewe wa kanda ya ziwa.”
. . Asia akatoa cheko la kisasa, cheko linalotangaza huba.
Walizungumza mengi. Usiku huu ukapita.
. . Asia akiwa hajamuuliza Deniss anafanya kazi gani. Hakutaka kupaparuka alitaka kushambulia taratibu lakini kwa umakini sana.

. . Siku iliyofuata, Asia akategemea kuwa Deniss atamuanza. Haikuwa hivyo.
. . Asia akajihisi kuchanganyikiwa kwani aliona dalili za kuupoteza ushindi zikimsogelea, na hakuwa tayari kukubali kushindwa ilhali alimuhakikishia Husna kuwa baada ya siku nne mambo yatakuwa sawa.
. . Asia akaamua kucheza pata potea nyingine.
Binti huyu aliyeemrejesha Jumanne kutoka katika kutembelea makalio mpaka kurejea mtaani kwa kutumia miguu, sasa alikuwa akicheza na namba nyingine asiyoifahamu.
. . Dennis. Anachokumbuka ni kwamba aliambiwa Deniss hana njaa na anaonekana ana pesa za kutosha.
. . Asia akisikia pesa, basi kuchanganyikiwa ni halali yake. Hakuna alichopenda kama pesa.

. . Asia akarusha kombora jingine.
. . Akaingia katika simu yake kitu cha kwanza akaandika ujumbe kisha akauhifadhi. Kitendo kilichofua akamtumia Deniss pesa kiasi cha elfu sitini za kitanzania. Kisha upesi akatuma ule ujumbe.
. . “Habari. Naomba upokee kiasi hicho kama shukrani zzangu za dhati kwa ukarimu ulionifanyia jana. Wewe ni wa ajabu sana. Ubarikiwe. Ninapotea hewani kwa dakika kadhaa naingia katika ndege naruka hapo Kampala mara moja. Nadhani kesho kutwa nitakuwa Dar. Take care.”
Kisha akazima simu yake.
. . Hakuna aliyeshirikishwa wakati mambo haya yanaendelea.

. . Deniss aliupokea ujumbe na pesa zile na kweli alivyojaribu kupiga namba haikuwa inapatikana.
. . Akaghafirika, hakutaka kushukuriwa kwa namna ile.
Alituma ujumbe lakini haukupokelewa na baadaye ulirejesha majibu kuwa haukufanikiwa kumfikia muhusika.
. . Deniss alikuwa katika mshangao wa hali ya juu, ujasiri wa Asia ulimshangaza. Hatimaye akapatwa na kile kitu ambacho Asia alikuwa anakijenga kwa kutumia gharama hizo.
. . Deniss akatamani kumuona huyu mwanadada ambaye kiuhalisia anaonyesha kuwa ni mjasiriamali haswaa.
Ni hicho Asia alikuwa anakihitaji.
. . Deniss na pesa zake zote alikuwa hajawahi kuipanda ndege, leo hii anatamkiwa na mtu kuwa ‘eti naruka hapo Kampala mara moja’.
Ni mtu wa aina gani huyu?
. . Akatamani kuiona sura ya Asia.

. . Baada ya siku mbili.
. . Asia alikuwa anapatikana tena.
. . Sauti ya ujivuni na majigambo ya Deniss haukuwepo tena kama awali, daraja alilokuwepo akamuweka na Asia hapo hapo.
. . Hata kumwambia kuhusua kuonana alikuwa anatetemeka. Lakini baada ya kumweleza Asia, alipata jibu jepesi lakini linalokera.
. . “Ngoja nicheki na ratiba zangu basi.”

. . Deniss alingoja kwa masaa mawili hatimaye akapokea ujumbe kutoka kwa Asia.
. . “Kesho saa moja hivi. Nitakuwa na kikao maeneo ya Hotel Valentine Kariakoo, na nitaimaliza siku katika hoteli hiyo kwani kuna mgeni wangu amefikia hapo. Karibu kama utaweza” Deniss akavuta pumzi. Akairudiua tena meseji ile. Hakika ilikuwa imetumwa na mwanamke jasiri sana, ambaye kukutana na watu ni jambo la kawaida sana.

. . Asia aliutuma ujumbe ule baada ya kufanya tathmini ya kina. Hakuhitaji kumchelewesha Deniss iwapo atajiweka machinjioni mapema.
. . Baada ya ujumbe ule alijitoa muhanga tena, akachukua chumba katika hoteli ile ambayo ina hadhi ya kuitwa hoteli. Hakuwa na kikao chochote bali alikua katika mawindo.
. . Alikuwa radhi kutumia pesa nyingi lakini mwisho wa siku apate nyingi zaidi, si kwa kuua mtu bali kuutumia mwili wake katika namna ya digitali.
. . Na katika dili hili hakutaka kuwashirikisha shoga zake wengine, hata Husna alitakiwa kungojea majibu tu.
. . SIKU ya siku ikafika, Asia kwa uvaaji wake hakika usingeweka tofauti yao na mfanyakazi yeyote katika benki ya dunia ama ikulu.

. . Siku iliyofuata majira ya saa moja jioni, Deniss alikuwa bize kubadili nguo, mara avae jeans.
. . “Ah hapa ataniona muhuni.”
Mara avae suti.
. . “Ah hapa nitaonekana mshamba sana….usiku huu na hili lisuti.”
Mara avae hiki mara kile.
. . Hatimaye akajituliza katika vazi la Jeans lakini juu akitua shati la mikono mirefu lililomkaa haswa.
. . Akaiendea gari yake na kuitia moto.
. . Safari ya kwenda kuonana na Asia.
. . Mtoto wa mjini.
. . Laiti kama angejua mtu anayekwenda kuonana naye.
Ni aheri angejishughulisha na mambo mengine na kuyapa kisogo hayo aliyojikita nayo.

. . . . . . . . . . ****

. . Gari liliegeshwa katika maegesho ya magari kwa kulipia.
Deniss kabla ya kushuka katika gari lake, alichukua manukato makali na kujipulizia tena kisha akajitazama katika kioo.
. . Alikuwa ametakata.
Akatabasamu peke yake, ndevu zilizounda mfano wa ‘O’ kidevuni zikachanua. Akazidi kuvutia kumtazama.
Kwa utulivu na umakini wa hali ya juu akashusha mguu mmoja chini kisha ukafuata na ule wa pili.
. . Akabofya kitufe katika rimoti iliyobeba funguo za gari.
Yakatoka makelele kidogo yasiyokera masikioni.
Kisha akaanza kunyata akaufikia mlango, walinzi wakamkaribisha kwa macho, kisha wafanyakazi wa kike wakamlaki kwa bashasha.
. . Alifanania na mfalme.

. . Alipofika mapokezi alifuata maelekezo aliyopewa na Asia.
Simu ikapigwa katika chumba alichokuwa Asia.
. . “Samahani dada kuna mgeni wako hapa.” Sauti ya muhudumu ikatambaa.
. . Kimya kikatanda kisha akaitoa simu sikioni na kuuliza, “Unaitwa nani? Na je ulikuwa na miadi naye?” muhudumu alimuuliza deniss.
. . “Yah..nilikuwa na miadi naye…..naitwa Deniss..mwambie tuli…” kabla hajamalizia ngonjera zake muhudumu alikuwa amerejesha simu sikioni. Akatoa majibu.
. . “Nenda chumba namba 18…” alimweleza Deniss.
Japokuwa hakusema neno, Deniss alionyesha macho ya kuonyesha kuhitaji kuelekezwa zaidi. Muhudumu akaling’amua hilo.
Akamwita muhudumu mwingine akampa zoezi la kumpeleka Deniss kwa Asia.
. . Chumba namba kumi na nane.

. . Deniss akaugonga mlango. Zikapita kama dakika tatu.
. . “Ingia…” sauti kutoka ndani ikajibu.
Deniss akakishusha kitasa akaingia.
. . Marashi yake yakasahaulika yalikuwa yananukiaje hapo awali.
Akakutana na marashi makali ya kisasa zaidi yakinukia kutoka ndani.
Akapiga hatua mbili, akakutana na mwanadada akiwa amejikita katika kompyuta mpakato (laptop) yake.
Alitumia dakika nyingine moja, akanyanyua kichwa. Akafanya tabasamu mwanana. Vishimo vikajichora katika mashavu yake.
. . “Hi Denny!!” sauti nyembamba kama inayojilazimisha kutoka lakini yenye kuliwaza na kusahaulisha kama kuna shida duniani ilitoka katika kinywa cha Asia.
. . Deniss akakodoa macho hakuwahi kuitwa kwa maringo namna hiyo hata mkewe a ndoa hakuwahi kumtolea sauti inayoliwaza namna ile.
. . “Hi!!” hatimaye alijibu.
. . “Karibu…karibu kitandani maana humu naona kuna kiti kimoja tu. Pole lakini next time nakukaribisha kwangu.” Alijieleza Asia.
Deniss akaketi.
. . Alichokosea ni kujionyesha kuwa mapema sana ameshangazwa na urembo wa Asia. Binti huyu alipata wasaa wa kumsoma.
Kosa kubwa sana wanalofanya wanaume wengi katika mfumo wa analojia.
. . Maongezi yakaendelea kidogo, asia akaitazama saa yake. Ilikuwa inakaribia saa mbili usiku.
Akaitwaa simu ya mezani. Akabofya namba kadhaa.
. . “Nahitaji mtu wa jikoni tafadhali.”
Simu ikakatwa.
Baada ya dakika tano. Hodi ikasikika.
Kwa mara ya kwanza Asia akasimama, kwenda kuufungua mlango ili muhudumu aweze kuingia.
. . Zilikuwa ni hatua sita tu lakini kila hatua haikutakiwa kuchezewa.
Kinguo kifupi alichovaa kiliruhusu michirizi ya utamu kuonekana nyuma ya goti, wepesi wake ukaruhusu mitikisiko ya kawaida na nyongeza ya mitikisiko ya kichina, mgongo nao haukuwa nyuma.
Asia alikuwa kifaa cha nguvu.
Akaufungua mlango. Muhudumu akaingia.
. . “Msikilize huyu kaka.” Asia alitoa amri kwa muhudumu.
Deniss akaanza kujiuma uma.
. . “Chipsi kuku….” Akaropoka.
. . “Mimi niletee mchemsho wa kuku.” Asia akauendea mkoba akaamua kulipa mapema. Akatoa kwa maksudi burungutu kubwa kiasi la pesa alizokuwa amezikomba katika akaunti yake.
Deniss akaziona.
. . “Mtoto hana njaa huyu.” Akabashiri.

Muhudumu alipoondoka, Deniss na Asia wakaendelea na stori za hapa na pale.
. . Mara simu ya Asia ikaita.
Akaitoa, akausoma ujumbe.
. . “Mh msichana mrembo kama wewe unatumia Nokia Obama ya tochi?” Deniss alitania.
. . Asia akafanya mfano wa tabasamu.
. . “Hebu simu yako…” akamuomba.
Deniss akamkabidhi, ilikuwa ni iPhone5.
. . “Umenunua bei gani hii?”
. . “Milioni moja na ushee.” Alijinadi Deniss.
Asia akatikisa kichwa kwa masikitiko.
. . “Deniss…..unajua kuwa kuna viwanja vinauzwa kijijini hiyo pesa uliyonunulia simu. Mimi niliyenunua kiwanja ambacho hakifutiki kabisa, na wewe uliyenunua simu nani amewekeza? Shtuka Deniss sisi ni vijana tunatakiwa kuwa na mawazo ya miaka kadhaa mbele sio kuwaza leo tu, chimbia pesa zako chini Deniss chimbia pesa kizazi chako kizikute, mwanao hataikuta hiyo sijui funifuni faivu sijui nini…simu uliyozungumza na mimi ndo hii je? Ulibaini tofauti?” asia alizungumza kwa hekima zote. Maneno kuntu kama kawaida yake. . . . . Yakamchoma Deniss akaanza kujichekesha kisha akajaribu kujibu hoja.
. . Asia alikisubiri kipengele hiki.
. . “Lakini Asia, huwezi jua mimi nimenunua kiwanja na bado nimenunua na simu, kama pesa ipo na inabaki nd’o ninunue viwanja tuuu.” Alijibu kwa kulalamika.
Asia akapata alichokuwa amehitaji.
. . “Kumbe bwege ana pesa chafu eeh…” alimuwazia huku akimtazama usoni.
Jicho la Asia likamwathiri kisaiokolojia Deniss lakini hakuweza kuanza.
Simu mfululizo zikawa zinaingia katika simu ya Asia.
Kila simu ilikuwa ya kibiashara.
. . Hakika Asia alikuwa namba nyingine. Deniss alikiri.

Majira ya saa tano usiku Deniss aliaga kuwa anaondoka.
Asia akamsindikiza mpaka mapokezi, wakaagana.
. . Deniss akatoweka bila kufanya lolote na Asia, alikiri kimoyomoyo kuwa alimuogopa sana binti yule mjasiriamali.

. . Siku iliyofuata mawasiliano yaliendelea kama kawaida.
Baada ya kutumia pesa nyingi kujaribu kumuweka sawa Deniss sasa Asia akaamua kulipua bomu lake.
Deniss akiwa anamuamini sana Asia kama rafiki wa karibu tena mshauri mzuri.
Ikafikia siku ambayo kamwe haitasahaulika katika kumbukumbu za Deniss.
 
KISA CHA 3


. . Simu kutoka kwa Asia ilimkurupua kutoka katika kiti cha ofisi yake.
. . “Asia ametoka Msumbiji?” alijiuliza.
. . “Nambie.”
. . “Ukwapi Denny.”
. . “Ofisini vipi umerudi bongo?”
. . “Yeah nimerejea. Upo bize sana nahitaji kukuona.”
. . “Hapana sio bize sana.”
. . “Nipo huku Royal Temeke..kule pa siku ile.”
. . Dennis akaelewa akaingia garini akaelekea alipokuwa Asia.
Akamkuta chumbani akiwa mnyonge sana.
. . Tofauti kabisa na siku nyingine.
Vazi lake jepesi la kitambaa laini liliyaruhusu yale mapaja yaliyompagawisha Jumanne na hatimaye kulizwa gari yalikuwa nje.
. . Alikuwa amejilaza kihasara hasara haswaa.
Deniss alipoingia. Asia hakushtuka akajiweka vyema kitandani huku akijifanya kujisitiri mapaja yake.
. . Deniss alitegemea Asia atasema jambo lolote, hakusema.
Akamsogelea pale kitandani.
Akamgusa.
. . “Asia…we Asia.”
. . Asia hakugeuka, Deniss akaamua kumgeuza.
Lahaula. Asia likuwa ameuchafua uso wake kwa machozi.
. . Mrembo alikuwa analia.
Kilio cha kimya kimya.
. . “Asia….kuna nini…nani Asia kakufanya hivi.” Deniss akataharuki.
. . “Niache Denny, niliumbiwa shida hizi. Niache tu.” Alizungumza huku analia.
. . Deniss hakukubali kumwacha. Akazidi kuuliza.
Ndipo Asia alipohamia digitali na kuendelea kucheza na akili ya Denny.
. . “Denny, mume wangu…mume wangu ananinyanyasa sana, mie wa kuwa naamua kulala hotelini kisa kitanda cha nyumbani kichungu.”
. . “Asia umeolewa?”
. . “Ndio. Lakini ni bure…bure kabisa Denny.”
. . “Nini kwani?”
. . “Ubunge wake ananiletea mimi hadi nyumbani….ubunge wake unanifanya mimi mtumwa. Ameona hiyo haitoshi kisa dini inaruhusu kaniongezea mke wa pili.” Asia alisikitisha na kama angekuwa muigizaji, wengi wangekuwa wanalia akiigiza vipande kama hivi.
. . Denny akahamaki, “kumbe Asia mke wa kigogo, ndo maana ana pesa huyu mtoto……dah…..watu wengine hawapendi shobo hata siku moja hajanambia.”
Denny akajaribu kumsihi sana asilie, Asia akazidi kulia.
. . “Denny asante kwa kuja katika maisha yangu, japokuwa ni karibia mwezi mmoja tu tangu tufahamiane nimejifunza mengi kwako. Na ukiwa kama rafiki mwema nimeamua kukuzawadia kitu kama utakuwa tayari.”
. . “Asante Asia hata mimi nafurahi kuwa rafiki yako. Nitafurahi kupata zawadi kutoka kwako” Denny alijibu huku mawazo yake yakiwaza ngono tu.
. . “Zawadi zipo za aina mbili, zote nitakupa.” Alisema Asia kisha akasita, “Zawadi ya kwanza itakuwa ni swali, na zawadi ya pili itaanza kabla ya zawadi ya kwanza.” Aliongea Asia huku akiwa ameremba sauti yake.
. . “Denny….nimeamua kujitolea pesa yangu milioni thelathini kwa ajili yako.”
. . “Kivipi?” aliuliza Denny.
. . “Nilikwambia huwa kamwe sinunui magari ya bei ghari wala simu. Nilikwambiaje?”
. . “Unachimbia chini..” alimalizia Denny.
. . “Ok..unapafahamu Bahari Beach..”
. . “Napafahamu kwa wazito kule….”
. . “Nataka nawe uwe mzito lakini kwa kujibu swali langu.”
. . “Niulize tu Asia.”
. . “Nitatoa katika akaunti yangu pesa taslimu milioni thelathini….nawe utatakiwa kufanya kitu kidogo tu milioni kumi….ifike milioni arobaini.”
. . “Ehee.”
. . “Kisha nakununulia kiwanja kikubwa pande zile, na ukionyesha uhai katika kujenga nitachota pesa nyingine nitakusaidia ujenzi….pesa inafukiwa chini mpenzi wangu….sio katika iPhone sijui nini” Asia alisema kwa maringo, walau aliweza kutabasamu.
. . “Nakufanyia haya yote kwa ukarimu ulionionesha kabla na baada ya kujuana.”
. . “Nilisema sihitaji jibu kwa sasa maana patakuwa na mjadala mrefu, kwa kuwa umezikubali zawadi zote, Denny ipokee zawadi yangu hii ya pili…”
. . Asia alimrukia Denny akamkumbatia, akajivika uso usiokuwa na soni hata kidogo. Akamnong’oneza Denny, “Ukiamua kuniona mimi Malaya sawa Denny lakini naomba niwe wazi…..Denny unanitesa…unanitesa Denny….”
. . Kijana hakukumbuka kama anayo pete ya ndoa, hakukumbuka kama anao watoto nyumbani.
. . Denny akachukua mkondo wa wanaume wengi, kuwa watumwa wa ngoni linapokuja suala la ana kwa ana na msichana.
Akamkumbatia Asia.
. . Ulikuwa mchezo wa dakika zisizopungua hamsini, sakafu ilihangaishwa, kitanda kiliteseka, bafu nalo liliona kilichotokea.
Deniss hakuwahi kufanyiwa manjonjo hayo na mkewe wa ndoa.
Walipotoka bafuni. Deniss akakumbuka kujibu swali.
. . “Nipo tayari kwa zawadi ya kwanza, nami nitakupa zawadi pia mpenzi.”
. . “Ok siku ukiipata hiyo pesa utanambia…” Asia akauliza swali la mitego.
. . “Sio kuipata ipo tayari..yaani siku ukiwa na nafasi tu my dear.” Deniss akajileta kwenye kumi na nane. Asia akachekelea maana hakuna mchezo alioupenda kama mchezo ndani ya kumi na nane.
. . “Basi tufanye kesho kutwa maana kesho nakimbia Mbeya…..narudi keshokutwa mchana…” alidanganya Asia ili aweze kujipanga kuchuma baada ya kupanda mwezi mzima.

. . DENISS aliondoka kurejea nyumbani akiwa na furaha ya aina yake. Hakuwa na moyo wowote wa majuto juu ya kitendo chake cha kufanya mapenzi na Asia wakati yu katika ndoa.
Alikuwa akiwaza kuwa ameweza kumzunguka mbunge fulani na kulala na mkewe. Nafasi ya kipekee kabisa.
. . Jambo jingine lililompagawisha ni uamuzi wa kushangaza wa Asia wa kumnunulia kiwanja na ikiwezekana kumsaidia katika ujenzi.
. . “Wabunge wetu wana pesa hawa pumbavu zao…” alitokwa na kauli hiyo Deniss huku akiwa makini na barabara.
. . Akiwa katika kumuwazia Asia mara ukaingia ujumbe katika simu yake, akasubiri alipoyafikia mataa ya kuzuia magari, akaichukua simu.
Alikuwa ni Asia ametuma ujumbe.
. . “I have never been fucked like this. Thanx.”
. . Ujumbe ule mfupi, Deniss aliurudia mara mbilimbili, hakuamini hizo sifa alikuwa anapewa yeye.
. . Alikuwa amefanikiwa kumteka Asia kwa penzi la muda mfupi tu.
. . “Hapa huyu mbunge asahau kabisa kama ana mke. Na mimi ndo sitoki hapa.” Aliongea kwa sauti ya juu, tabasamu likiutawala vyema uso wake.

. . Deniss alitamani sana kuendelea kuwa na ujumbe ule katika simu yake, lakini tatizo alikuwa na mke. Akalazimika kuufuta huku moyo ukimuuma.

. . . . . . . . . . ****. . . . . .

. . HATIMAYE baada ya mwezi mzima wa kutengana na rafiki zake, Asia alihitisha kikao cha dharula. Japo awali alitaka kuyamaliza mambo haya kimya kimya, lakini akajikuta harakati zake akimuhitaji mtoto wa kikurya Janeth, na wenzake wawili akiwemo Messi ambaye ni mtaalamu wa mipango.
. . “Jamani nimekuwa kimya mwezi mzima, najua mmechonga sana ooh Asia anaringa, sijui nini……hayaaishi midomoni nyie watoto kama Janeth ulivyokuwa mpana kama magagulo ya wasomali sikuezi.” Akazungumza Asia kwa nyodo, kimya kikatanda kisha kama wameambizana akaanza kucheka Janeth, Messi ambaye jina lake halisi ni Husna akafuatia, mara Asia, mwishowe meza nzima wakawa wanacheka.
. . “Imetosha sasa.” Aliwakatisha Asia.
. . “Nimeleta kazi mezani.” Alisita akagida maji kisha akaendelea, . . . . “Messi unamkumbuka jamaa uliyekutana naye benki mwezi ule.”
. . “Jamaa gani?” Husna akauliza.
. . “Yule ambaye ulinipa namba ya simu.”
. . “Eeeh nimemkumbuka vipi kwani?”
. . “Mambo yameiva ni sisi tu kupakua.” Asia aliwashirikisha wote kwa pamoja.
. . Akawasikiliza anasema nini.
Akausikiliza ushauri wa Husna, haukuwa ushauri mzuri sana, ushauri wa kumuibia Deniss kadi ya benki na kwenda kuvuta pesa.
. . “Hapana Messi hiyo mbaya…mi nataka ile ya kisasa mbona hiyo imekaa kinjaa njaa sana. Kama tunachuna mwanachuo banaaa.” Aligoma Asia.
. . Janeth alikuwa kama hawasikilizi vile, lakini aliponyan yua kinywa na kusema neno mambo yakaonekana kua sawa. Akakubaliana na Janeth.

. . Wakaagana huku wakiisubiri siku ya siku.
Milioni kumi.
. . Hazikuwa pesa ndogo. Isitoshe Asia hakuwa ametumia zaidi ya laki tano katika kufanikisha hili.

. . . . . . . . SIKU IKAWADIA.

. . ASIA alikuwa ameikalia vyema gari aina ya Harrier, alikuwa anaikanyaga vyema kana kwamba ni ya kwake.
. . Ndani ya gari aikuwa yeye na Deniss, siku hiyo Asia aligoma kutumia gari ya Deniss alihitaji naye kumuendesha.
“Mapenzi ya kihindi haya…” alijisemea Deniss wakati akikubaliana na Asia.
. . “Au umechukia baby.” Asia alibembeleza kiwiziwizi.
. . “Hamna jamani mbona sawa tu…” alijibu Deniss.
Sasa alikuwa katika gari la Asia, ilikuwa ni saa sita mchana.
. . “Tuanzie kwangu ama kwako.” Asia aliuliza ka kuridhika akia anaikanyaga gari kwa umakini.
. . “Mh. Kwani we unachukua wapi?”
. . “Standard chattered Posta kule.” Alijibu Asia.
. . “Mimi Crdb yoyote tu…lakini huwa napendelea ya kule mtaa wa Lumumba. Hakuna foleni na uhakika wa pesa ndefu upo.”
. . “Pesa ndefu? Kwako pesa ndefu ni ipi? Hao CRDB walioshindwa kunipa ki milioni hamsini kwa wakati unasema wanatoa pesa ndefu? Benki za kibongo ushenzi tu…walinifanya nionekane mwongo mbele za watu ” alijibu Asia ka kuonyesha kukereka.
. . Deniss, kimya aliogopa kujibu kitu maana kwake pesa ndefu alihesabia hiyo milioni kumi, kumbe mwenzake aliwahi kukosa ki-milioni hamsini.
. . Ipi pesa ndefu sasa?.
. . Deniss hakujua kama mfumo wa digitali hauhitaji kupandisha antenna juu ili kuondoa chenga chenga. Hakujua kama ni kuseti kidogo tu king’amuzi na mambo yanaenda sawa.
Deniss naye alikuwa analojia.

. . Wakalifikia ghorofa kubwa ambalo chini kuna benki ya Standard chattered…….
. . “Tushuke basi si unajua kuna kukabwa……’ Asia akamsihi Deniss. Wakashuka.
. . Ðeniss aliposhuka, asia akamfuata na kumnong’oneza kwa tahadhari.
. . “Jiweke mbali kidogo si unajua tena wavimba macho, nisije nikatolewa magazetini nikaivunja ndoa.” Maneno yale yakamtia wivu mkali Deniss, Asia alihitaji sana hali ile.
. . Akazama ndani ya benki Asia, akamwacha Deniss amekaa mbali kabisa akiwa hana habari na yule binti.
Asia akajaza karatasi kadha wa kadha.
. . Deniss akiwa amezubaa katika gazeti mara ukaingia ujumbe.
. . “Njoo unisaidie.’ Mtumaji alikuwa Asia. Deniss akaangaza huku na kule akamwona, akasimama na kumfuata.
. . “Nisaidie kujaza” Asia alisema kwa sauti ya kimahaba.
Deniss akaanza kujaza.
. . “Nitolee 45 kabisa. Nimekumbuka nina safari juma lijalo.” Asia alimpa maelekezo Dennis, Deniss akajaza milioni arobaini na tano kutoa.
. . Asia akachukua ile karatasi akaenda dirishani.
Akafanya tukio la sekunde kadhaa.
Akabadili karatasi.
Akamkabidhi yule dada aliyekuwa dirishani.
Akamkabidhi na pesa kiasi cha shilingi elfu hamsini.
Alikuwa anaweka katika akaunti ya Janeth.
Aliporudishiwa ‘paying slip’ akafungua koba lake kwa mbwembwe akaweka ndani.
. . Akatoa karatasi nyingine tena akamkabidhi yule muhudumu.
Akaweka elfu thelathini katika akaunti ya Husna.
. . Nayo kama ile ya awali akatia karatasi katika koba lake.
Mchezo ulienda kama alivyotaka.
Akasogea pembeni akazugazuga kisha akaondoka.
. . “Twende zetu afisa.” Alimshtua Deniss.
Wakatokomea.

. . Walipoifikia zamu ya Deniss kutoa pesa ikazuka ile dhana ya wanaume wengi kupenda sifa mbele ya msichana hasahasa akiwa mrembo. Sifa hizi za kijinga huwatokea wanaume wengi puani, yaani hupenda kujionyesha kuwa wana pesa nyingi, kujidai kuwa hawajali hata pesa zao zikitumika hovyo.
. . Lakini mwisho wa siku akilala kitandani anasema. NINGEJUA.
Pepo hilo likamkaba Deniss pia.
Akataka kujiweka daraja moja na Asia.
. . “Na mimi njoo unisaidie.” Alijifanya kudeka.
Asia ambaye katika filamu hii ni mke wa mbunge, akarembua jicho. Kisha akachukua kalamu.
Alipofikia kiwango cha kutoa.
. . “Nitolee kumi na tano kuna jambo nataka kufanya na hiyo tano.”
Asia akacheka kidogo kisha akamjazia, moyoni akafurahia dau kupanda.
Deniss akapanga foleni, baada ya nusu saa akarejea akia na bahasha yenye chapa ‘CRDB BANK’
. . Ujazo wake ulikuwa wa kulidhisha.
Asia akarukwa na mate mdomoni, lakini kama alivyoanza taratibu alitaka kumaliza hivyohivyo.
Wakaondoka.
. . “Yaani pesa bwana hicho hapo kimilioni kumi na tano eti….duuh.” alisema Asia huku akiingalia ile bahasha kwa dharau kiasi.
Deniss hakujibu.

. . Akiwa anaendesha mara simu ikaita.
Akaegesha gari pembeni kidogo. Akapokea.
Ilikuwa simu ya kuigiza kutoka kwa mmiliki wa kiwanja ambacho walikuwa wanaenda kununua.
. . “Wakati mwingine nachukia kufanya biashara na wabongo.”
. . “Kuna nini?”
. . “Eti hadi saa kumi na mbili, sijui kuna mambo gani gani aaargh. https://jamii.app/JFUserGuide” alighafirika.
. . Deniss akaanza kushusha chini kihulka. Alifanya vile kama anafanya kwa mpenzi wake wa siku nyingi.
. . “Baby…nahitaji kupumzika pliiz…..we have to go somewhere..we unadhani sasa hivi saa nane hadi ifike saa kumi na mbili ni leo…”
Kauli hiyo ikamfurahisha Denny, akaikumbuka ile siku alipoonja tunda la mke wa mbunge.
. . Kama alivyotaka Asia baada ya saa zima walikuwa ndani ya chumba wakila raha.
. . Deniss kichwani akiamini kuwa ndani ya kile chumba kuna milioni hamsiniAsia ndiye aliyeijua hesabu sahihi.
Asia Digitali akachezesha kiuno kwa umakini huku akicheza na muda, alimpa Deniss kitu roho inapenda akamzidishia makusudi viuno ili afikie lengo.
. . Lengo la kumchosha.
. . Kweli akachoka mwishowe akalala.
Asia naye akazuga kulala.
Akamshtua Denis saa kumi na mbili na nusu.
Walikuwa wamechelewa.
Wakajiandaa upesi wakatoweka.
Asia akiwa ameukamata usukani.
Wakapita hapa na pale.
. . Foleni ikawa kikwazo Asia akaamua kupitia njia za panya, ni huku walipokutana na dhahama.
Wakakutana na gari nyingine, hakuna aliyetaka kumpisha mwenzake.
Kigiza kile kila mmoja akammulika mwenzake.
. . Asia akaghafilika. Deniss akagundua hilo.
. . Ama kwa hakika ukitaka mwanaume apigane basi mdharau mbele ya msichana.
. . Deniss akashuka mbiombio kuwakabili wale walioziba njia.
Asia naye akashuka.
. . Akakutana na kimya cha hatari.
. . Mara akazolewa mtama. Akatua chini kama mzigo alipojaribu kupiga kelele alikutana na mdomo wa bunduki.
. . Kidogo Asia acheke kwa jinsi Deniss alivyokuwa anatetemeka lakini akaumbuka kuwa alikuwa katika kuigiza filamu.
. . Hakutakiwa kucheka, akaendelea kulia.
Mmoja kati ya watekaji akaiendea gari. Badala ya kupekua akaiwasha. . . Ikaunguruma kisha ikageuzwa na kupotea.
Deniss alikuwa amejikojolea tayari.
. . Watekaji walificha nyuso zao.
Wawili walikuwa wanaume. Mmoja mwanamke.
. . “Ole wako usimame.” Alipewa onyo Deniss aliyekuwa amelala chini.
. . Asia kitambo alikuwa amejifanya kuzimia. Alikuwa ametulia tuli.
Baada ya dakika kumi eneo lile lisilokuwa na nji za magari walikuwepo watu wawili, Asia na Deniss.
. . Deniss alikuwa amepagawa.
Alijaribu kumwamsha Asia, hakuamka. Akamtikisa lakini hali ikawa vile vile.
. . Deniss akaamua kujijali kwanza yeye, Asia baadaye, akatimua mbio kali.
Kuna kichwa kilikuwa kimejibanza mahali kikisubiri jambo hilo litokee.
. . “Amka wewe bwege kasepa.” Sauti tulivu ya Janeth maji ya shingo.
Asia akainuka, akasahau viatu, pekupeku akajikongoja.
Wakaikuta taksi inawasubiri.
. . Wakatokomea.
. . “Janeth wewe mbayaaaa.” Asia alimsifu mkurya yule.

. . Wakati Deniss anachanja mbuga kuitafuta barabara aweze kupata daladala ya kumrudisha nyumbani.
Asia alikuwa anasikilizia ladha mbaya ya vidonge vya majira alivyotoka kunywa muda mfupi baada ya kuzinduka kutoka katika kuzimia feki.
. . “Bwege asije akawa amenitia mimba mtoto wa Razak mie.” Asia alibetua midomo na kuyasema hayo.
. . Janeth hakuweza kumsikia alikuwa amejikita katika kutafuta ni namna gani simu aliyoikamata mkononi aina ya iPhone inafunguliwa aweze kutoa kadi ya Deniss na kuweka yak wake.
. . “Mh Janeth ushajimilikisha mtoto weee.”
. . “Si nilikwambiaga nataka iPhone si ndo hii au? Watanikomaje?” alijibu bila wasiwasi kana kwamba ni yeye aliyefanikisha Deniss kujiingiza mkenge.
. . Asia hakuwa na neno, na roho ya kwanini hakubarikiwa nayo.

. . . . . . . . . . ****

. . Milioni kumi na tano mezani.
Wale wanaume walioambatana na Janeth kwa ajili ya kuwateka akina . . Asia na kuondoka na gari, hawakutambua kama dili lilikua kubwa kiasi kile.
. . Walipewa shilingi laki mbili wagawane.
. . Habari yao ikaishia hapo.
Mashujaa watatu wa kike walikuwa wanazikodolea macho pesa zile ambazo baada ya kuguswa na yule dada wa benki aliyemkabidhi Deniss basi hazikuwa zimeguswa tena.
. . “Milioni kumi na tano hizo” Asia aliuvunja ukimya.
. . “Hapa sasa tunatakiwa kumiliki gari yetu…..” Husna alidakia.
. . “Na nyumba kubwa ya kupanga….” Aliongezea Janeth.
. . “Mh…mna mahesabu nyie wadada……” Asia alichombeza kisha akacheka kidogo.
. . Akamtazama Janeth kisha akamtazama Husna. Akafumba macho kidogo, akawafikiria jinsi walivyokuwa wa muhimu kwake wakati anaingia jijini Dar es salaam.
. . Hakuwa na hili wala lile, japo walimwingiza katika biashara ya uchangudoa ambayo Mwanza alifanyishwa bila malipo.
. . Hakika, hakuwa analipwa, kila mwanaume alijipitia kwa kumpa ahadi kedekede za kumtoa kimaisha.
. . Asia alikuwa ni msanii wa maigizo anayechipukia.
Kwa kuligundua hilo kila mdau wa mambo ya sanaa aliyesikiliza kilio cha Asia aliahidi kumkutanisha na wasanii wakubwa na wanaofahamika Tanzania.
. . Huyu aliwambia ana namba ya JB, huyu akadai Johari wamesoma naye, mara mwingine akadai kuwa kama Kanumba asingekufa basi walikuwa wanakaribia kufanya naye filamu.
. . Asia akadanganyika, akatekenywa akatekenyeka.
. . Mwisho wakamvua vinguo vyake vya kishamba na kufanya yao kisha sanaa ya maigizo inaishia hapo. Wale wanaojuana na JB anakutana nao wakipiga debe katika magari ya kwenda Buhongwa na Nyegezi, na wale waliosoma na Johari anakutana nao vijiweni wakivuta bangi.
Alikuwa amedanganywa.
 
KISA CHA 4

Jambo hili lilimtesa sana.
. . Aliyafanya yote haya ya kuipigania sanaa ya maigizo na kuamini kuwa itamtoa kwa sababu akimtazama mama yake mzazi alikuwa hajiwezi kiuchumi na kama hiyo haitoshi alikuwa mgonjwa wa mara kwa mara.
. . Asia muhitimu wa darasa la saba katika shule ya msingi Nyegezi, kisha hakupata bahati ya kuchaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza. Akapiga konde kuwa sanaa itamwokoa yeye na mama yake.
Sanaa ikamfanya kuwa changudoa wa mkopo, asiyelipwa zaidi ya kupewa ahadi kedekede.
. . Mwishowe ahadi hazitimizwi na mwili unatumika.
Wasanii wa maigizo wapo Dar….Asia akaamua kutoroka na kukimbilia Dar.
. . Ni huku alipokutana na mshikemshike wa kuitamani pepo kisha ufufukie Mwanza.
Jasho, hofu, wasiwasi, mateso na chuki nichukie. Vyote vikawa vyake. . . Mara leo kikundi hiki cha sanaa, kesho kile mara leo alale kwa msanii huyu mchanga mara kesho afukuzwe.
. . Hatimaye akakutana na Janeth. Walikutana katika kikundi kimoja cha sanaa, Janeth alikuwa amemsindikiza rafiki yake.
. . Wakajikuta katika mazungumzo na Asia.
. . Mwishowe akaenda kulala kwa Janeth siku hiyo.
. . Huu ukawa mwisho wa sanaa ya maigizo, hatimaye wakaingia katika sanaa ya mapenzi ya wiziwizi. Ni huku alipomkuta Husna Messi.
Asia alikuwa na faida mbili katika tasnia hii, kwanza alikuwa ameuona mfumo wa analojia unavyotesa, na hakika ulimtesa sana Mwanza. Maongezi mengi kisha mwili wake unatumiwa.
. . Akaamua kuubadilisha, ni yeye alitakiwa kuongea na kutenda sana kisha achume pesa. Hakuwa na haja na mwili wa mwanaume.
. . Pili alikuwa muigizaji mbunifu. Hili lilimsaidia kuwa tofauti na wenzake. Alikuwa ni mwepesi wa kuunda maneno, mwepesi wa kutokwa machozi na mwepesi kujifanya hamu zimempanda amesisimka na anataka huduma.
. . Asia akawa Asia digitali.
. . Akakiri kimya kimya kuwa wawili hawa walikuwa msaada mkubwa sana kwake, japo si kihalali.
. . “Mimi nahitaji milioni nne tu….nimtumie mama nyumbani.” Hatimaye Asia alisema neno baada ya kuwa amefumbua macho.
Hakuna aliyepinga.

. . “Halafu Asia….hebu ngoja nikiri kwamba wewe ni mtaalamu. Naomba unisaidie jambo moja. N ahitaji pesa ya mafuta ya gari letu.” Husna alizungumza.
. . “Kivipi?”
. . “Kuna kitoto changu kimoja huko Mwanza kina pesa pesa ni kianafunzi pale SAUT…..nahitaji kwenda kuchuma.”
Asia akacheka sana na kujisikia fahari kukubalika namna ile.
. . “Kwa hiyo hapo unataka nini labda Messi.”
. . “Kadi yake ya benki niweze kuchomoa walau milioni hata mbili tu mi inanitosha.”
. . Asia akapiga kimya muda mrefu kidogo, kisha akazinduka.
. . “Huyo mwepesi, dozi yake hata buku tano haifiki na anatoa utakacho.” Alijibu.
. . “Kivipi?”
. . “Ngoja nikaifanyie majaribio hiyo njia yako kwa yule K-Matelefoni halafu nitakuambia cha kufanya.” Aliufunga mjadala Asia, Husna akangoja majibu.
. . Pesa ikahesabiwa Asia akachukua milioni tano, nne ya kutuma nyumbani na moja ya kuhifadhi katika amana yake.
Milioni kumi ikatulia kwa mdada wa kikurya, mrembo usoni katili moyoni. Janeth. Kila mmoja alimuamini.
. . Biashara bora kupita zote tangu wahamie digitali.
Wale wa analojia waliendelea kutanua mapaja kwa shilingi elfu tano kwa mshindo.

. . . . . . . . . . . . ****

. . KELVIN aliiona siku hii kuwa ya kipekee sana kwake.
Tangu afumaniwe na Asia akiwa na msichana mwingine hakutegemea kama binti huyu anaweza kumtafuta kwenye simu tena.
. . Mara ya mwisho walionana mtaa wa Agrey jijini Dar.
Asia alimsalimia Kelvin kijuu juu na hakutaka kumsikiliza zaidi maana ubaya aliomfanyia Mwanza, licha ya Asia kumpenda haukuwa wa kusameheka.
. . Mara ya pili Asia alimuna Kelvin katika luninga, alikuwa akilinadi duka lake la simu.
. . Hakuwa Kelvin tena bali K-matelefoni.
. . Asia akapuuzia.

. . Sasa Asia si yule wa analojia tena. Yu katika digitali na anataka kukutana na Kelvin.
. . Lengo si mapenzi bali mapenzi ya kidigitali.
Kelvin akashtuka sana kumsikia Asia.
. . Licha ya kwamba siku nyingi sana zilipita, lakini Kelvin aliikumbuka ile kadha ya kiuno cha Asia katika kitanda cha futi yoyote ile, na hata miguno yake sakafuni pia ilimkumbusha mbali.
. . Akatamanika.
. . Asia akanung’unika katika simu kisha akamkumbusha Kelvin kuwa siku hiyo ilikuwa tarehe kumi na nne, siku ya wapendanao.
Kelvin akashtuka kwa furaha, kumbe Asia bado anampenda.
“Mtoto nilimkuna vizuri hawezi kunisahau yule. Nilijua tu atarukaruka kwa mahanithi wa hapa mjini kisha atarejea kwangu.” K alikitapa kwa rafiki zake.
. . “Vipi kuhusu Amina sasa akigundua.” Aliulizwa.
. . “Amina ni Amina na Asia anabaki kuwa Asia, nilipotoka na Asia ni mbali jamani niacheni.” Kelvin alikuwa amepagawa.
. . Hatimaye wakapanga kuwa pamoja na Asia siku hiyo ya wapendanao.
. . “Lakini uelewe kuwa nafanya kwa kuwa nakupenda na nilikupenda sana, kwa sasa nina mchumba tunafanya kuiba usije ukanogewa.” Asia alimtumia ujumbe wa kumremba Kelvin.
. . Kijana akaingia katika mtego.
Sasa tatu usiku. Asia alikuwa yu na kanga moja pekee katika kikubwa cha kifahari katika hoteli yenye hadhi ya juu.
Kelvin mapapara alikuwa anahaha, mara amtekenye mara vidole visafiri katika masikio.
. . Kelvin alijaribu kuonyesha ujanja ambao kwa Asia yalikuwa marudio tu.
. . “Ngoja nikaoge kwanza mpenzi wangu, mimi ni wako jamani. Haraka ya nini.” Asia akachombeza kisha akazama bafuni, akarejea baada ya dakika chache.
. . “Na wewe kaoge.” Asia alimwambia K.
Kosa alilolifanya K ni kukubali kwenda kuoga.
. . Asia upesi akazama katika mkoba wake akaibuka na unga unga unaofanana na rangi ya matiti yake.
. . Akajipaka katika matiti yote, akaufunga mkoba na kumngojea Kelvin.
. . Mwanaume akarejea huku akiona aibu kwa jinsi taulo ilivyonyanyuka maeneo fulani, Asia akamcheka.
K akamvamia.
. . Asia akahamia katika maigizo. Akajirejesha digitali.
Kama K alidhani amekutana na Asia muanalojia ambaye alikuwa akikubali kila kitu huku akitoa vilio vya mahaba vya hisia, basi alikuwa anajidanganya.
. . “Baby…suck my breast….” Alilalamika Asia huku akiyakamata vyema ‘manyonyo’ yake.
. . K akamrukia kama bwege vile au kama ndama anavyorukia maziwa ya mama yake.
. . Akaanza kuyanyonya kwa ustadi mkubwa.
Tatizo la kitandani ni moja. Yaani hata kitu utakachokilamba kikiwa kichungu, hakuna namna itakubidi umeze tu.
. . Ukitema mpenzi atajishtukia kuwa umemuona mchafu.
Wangapi wanalamba masikio machafu, wanajikausha na kumeza?
Wangapi wanakosea njia badala ya kulamba matiti wanalifikia kwapa. Nao wanajikausha.
. . Na ni wangapi wakikuta chumvi imezidi ukali kunako wanameza hivyo hivyo.
. . Kwani chumvi kitu gani??
. . K- matelefoni naye akawa kama wanaume wenzake. AKAMEZA…..
. . Mara mwendo wa kunyonya ukapungua.
. . Akaanza kuongea lugha zisizoeleweka.
Mara akatulia na kuanza kukoroma.
Asia akamsukuma pembeni.
Akasonya kisha akauendea mkoba tena.
Akarejea na vijiko viwili vya kulia chakula.
Akavikamata ipasavyo.
Akaingia kazini.

. . Asia akamsogelea Kelvin, akafumba macho yake kisha akaomba mbinu hiyo aliyofunzwa usukumani iweze kufanya kazi.
Mbinu ambayo hutumiwa na wanafunzi wenye imani hiyo kufanya wizi ama kugundua siri kadhaa. Kwa wale wataalmu wa afya njia hii kwa usasa wanaaita ‘haipotenaizesheni’ hutumika hasahasa jeshini, mjeshi hata afiche siri vipi, mbele ya haipotenaizesheni hana ujanja.
(Sifundishi zaidi ya hapa maana watu hawakawii kuifanyia kazi na kuwasumbua wenzao mitaani)
Asia akagonganisha vijiko mara mbili katika sikio na Kelvin upande wa kulia, kisha akafanya hivyo katika sikio la kushoto.
Kisha ukafuata utendaji.
. . “Kelvin…Kelvin..” Asia akaita japo kwa uoga.
Maajabu, Kelvin akiwa amefumba macho aliitika japo kizembezembe.
. . “Mama yako anaitwa nani?”
. . “Mama yangu anaitwa Monica.” Alijibu kama mtoto mdogo.
. . “Unaishi wapi?”
. . “Naishi huko Temekeee Mokoroshini.”
. . Asia akataka kucheka. Akajikaza, yale yalikuwa maajabu makubwa.
. . “Una akaunti benki?”
. . “Ndio ninayo akaunti.”
. . “Wapi na wapi Kelvin?”
. . “NBC, CRDB, na AZANIA.”
. . “Wapi kuna pesa nyingi?”
. . “CRDB kuna milioni nane.” Alijibu, Asia akafanya tabasamu.
. . “Kadi ya CRDB ipo wapi?”
. . “Kwenye suruali, mfuko wa nyuma kuna wallet ipo humo katikati.”
. . “Namba za siri unazikumbuka?”
. . “Ndio..”
. . “Ni zipi?”
. . “6798”
. . Asia hakuwa na swali la ziada.
. . Akafuata suruali. Kama yule bwege pale kitandani alivyotoa melekezo, naye akayafuata.
. . “Mh…imani hizi??” alijisemea Asia wakati anakumbana na kadi ya benki. Ilikuwa mahali palipotajwa.
. . Asia akaikwapua ile kadi na kuzamisha katika mkoba wake.
Kisha akaibuka na mtandio, akakitanda kichwa chake.
Kama vile anaigiza filamu ya mapigano huku yeye akiwa kinara akapiga hatua kadhaa akatoka nje.
. . Uhakika wa usingizi kwa masaa zaidi ya matano kwa ‘doromee’ aliyomeza Kelvin katika matiti ya Asia ulimpa jeuri msichana yule.
. . Akaufunga mlango.
Akachikichia mtaani. Huku na huko akakutana na ‘ATM’ ya CRDB….akaingia ndani.
. . Akabofya kama alivyoelekezwa na jamaa aliyepo usingizini.
Mashine ikaunguruma.
. . Ule uboreshaji wa kuweza kutoa hadi shilingi milioni moja kwa siku katika ATM ulikuwa faida kwa ASIA akachomoa milioni moja.
Alipoitazama saa yake zilikuwa zimebakia dakika kumi saa sita usiku iweze kutimia, hii ilimaanisha kuwa ile inakuwa siku nyingine.
Asia akzuga zuga hapa na pale, ikatimia saa sita akazama tena katika . . ATM akachomoa milioni moja nyingine.
Akazisweka kibindoni milioni mbili ndani ya muda mfupi tu..na hapo alikuwa hajaugawa mwili wake.
. . Baada ya zoezi kukamilika, msichana yule aliyejitanda baibui, alirejea katika chumba chake akamkuta Kelvin ametlia vilevile. Akairejesha kadi ya benki na kujirusha kitandani kama vile hakuna lililotokea.
. . Akapitiwa na usingizi hadi alipoisikia mikono nikimpapasa majira ya saa kumi.
. . Akajifanya kusisimka.
. . Akampa kile alichotaka yule bwana K matelefoni.
Asubuhi, supu ya maana ikaagizwa wakanywa kujipooza na uchovu.
Asia akiigiza kuchoka kuliko K matelefoni.
. . Wakati wa kuagana bwana Kelvin akamzawadia Asia nauli shilingi elfu hamsini.
. . Asia akashukuru.
. . Wakaagana.

. . Maskini K Matelefoni aliishia kupewa picha ya mtu amejiziba sura.
. . “Kamtafute huyu ndiye ulimpa kadi akakutolee pesa.” Benki walitoa tamko hilo hawakuwa na la kumsaidia kwa namna nyingine.
Hata ‘RB’ aliyochukua pia alitakiwa kumtafuta mwizi wake mwenyewe.
Wazo la kwamba alilishwa vitu na kuchezewa kamchezo zikamfanya asimuwaze Asia kama muhusika wake.naume asiyekuwa makini.
. . Mbinu ile ambayo ilifanya kazi ipasavyo. Husna alipewa majibu naye akafunga safari kuelekea mjini Mwanza.
. . Kwenda kumchuna mwanaume wake kidigitali.

****

. . . . . . . . . . ASIA DIGITALI ATIA TIMU VYUONI.

. . Baada ya kuzipanda ngazi ndefu za ghorofa mbili, kijasho chembamba kilikuwa kinamtoka, alizamisha mkono wake katika mkoba akatoka na kitambaa cha kujifutia jasho. Akajipangisa kidogo.
Kwa kutumia simu yake ya mkononi akajitazama jinsi alivyokuwa amependeza.
. . “Kumbe ukiwa na gari unakuwa na weupe mzuri hivi.” Alijisemea Asia, kisha akapiga hatua kadhaa hadi akaufikia mlango wa ofisi ambayo alikuwa anaihitaji katika chuo kikuu cha Dar es salaam.
. . “Department of Business Administration” palisomeka hivyo mlangoni.
. . Asia akavuta kumbukumbu ya mambo ya msingi ya kuzungumza akiwa katika ofisi ile.
. . Sauti yake nyororo iliyobeba kiingereza cha kuombea maji lakini kinachofanana na huenda kuzidi lafudhi ya mzungu kilimbeba.
Asia akaugonga mlango, akaruhusiwa kuingia. Akapiga hatua kadhaa akauruhusu uso wake kutabasamu. Lile tabasamu linalowakosha wanaume wengi.
. . Akaruhusiwa kuketi.
. . Ndani ya ofisi hiyo alikuwemo muhusika mmoja ambaye aliweka mambo yake kando baada ya ujio wa Asia.
. . “Karibu sana.”
. . “Asante sana kaka, aah samahani sijui nd’o Mr. Lucas?” aliuliza kwa utafiti kiasi.
. . “Yeah ni mimi. Umeagizwa kwangu.”
. . “Offcoz nimekuja kwako, na ninashukuru kuwa sijapotea….walionielekeza hawajakose kabisa maelekezo yao.” Alijieleza kwa furaha Asia.
. . “Karibu sana.”
. . “Aaah labda niende moja kwa moja kwenye point yangu ya msingi. Ni kwamba naitwa Halima…na hii ni business card yangu unaweza kuipitia kwa kifupi, aah mimi kuna msaada ama kuna jambo nalihitaji sana kutoka kwako.”
. . “Jambo gani dada.” Alihoji kwa utulivu Lucas.
. . “Wewe ni mkufunzi katika chuo hiki, hasa hasa katika masomo ya biashara. Nahitaji uwe mwalimu wangu katika topiki kadha wa kadha….kwa kifupi nimeishia kidato cha sita, kuna mambo kadha wa kadha katika biashara yangu yanaanza kunizidia. Si unajua tena mambo ya kukimbia shule, sasa kama hautajali tunaweza kufanya hivyo.
Muda wa kurejea shuleni sina kiukweli. Nahitaji tu kujua mambo kadhaa ndo maana nimekufata wewe moja kwa moja.” Alimaliza kuzungumza Asia huku funguo ya gari ikicheza katika kidole chake.
Bwana Lucas akatulia kwa muda kama anayefanya tafakari.
. . “Basi nadhani kwa kuwa nina kadi yako basi nitakupigia tutapanga, maana suala hilo lipo nje ya ajira yangu.” Alijibu huku akionyesha macho yanayompa tumaini Asia ambaye alijitambulisha kama Halima.
. . “Ok basi hamna shaka nitaingojea simu yako kwa hamu kubwa. Utakuwa msaada mkubwa sana kwangu, ujue mambo ya final accounts sijui manini nini yananiumiza sana.” Alimaliza Asia huku akionyesha kuwa anajua vitu kadhaa.
. . “Usijali mambo yote yatakuwa poa.”

. . Waliagana, Asia akaondoka akiwa ametimiza azma moja ya kupata miadi kutoka kwa bwana Lucas.
Hiyo ilikuwa hatua kubwa sana……

. . Asia aliondoka huku tabasamu likiishi katika midomo yake.
Alikuwa na haki ya kutabasamu maana kwa kiasi kikubwa alikuwa amefanikiwa katika malengo yake. Lengo la kuanza kuichota akili ya mkufunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam, bwana Lucas.
Asia alizama katika gari alilokujanalo. Akatia moto, akaondoka zake.

. . Baada ya masaa kadhaa alikuwa chumbani, alikuwa akijiuliza maswali iwapo ni kweli alichoambiwa kitafanya kazi ama la.
Asia akanyanyua simu yake akapiga namba fulani.
. . “Nakuja hapo sasa hivi.” Alizungumza.
Kisha akabadili nguo, akatoka nje.
Asia alijivuta hatua kadhaa, akatazama kushoto na kulia akaliona gari.
Akapunga mkono wakamwona, gari likasogea upande wake.
. . Gari ikaegeshwa, wakashuka wanawake watatu.
. . “Mambo Asia…..”
. . “Poa wadada karibuni….”
. . Asia aliwakaribisha wakachukua nafasi wakaketi, ilikuwa mara yao ya pili kuonana.
. . Walianza kuongea wakianzia walipoishia, akina mama hao walikuwa na shida ya kumkomoa mwanamke ambaye alikuwa akijitamba hasahasa baada ya kufunga ndoa na mwanaume ambaye alikuwa hawara wa mmoja kati ya wanawake wale.
. . Shida yao kubwa ilikuwa kumkomoa mama yule, kumfunza ajue kwamba mume wake si lolote si chochote.
. . Wakaelekezwa kwa Asia.
. . Aliyeusuka mchezo huu na kumuunganisha Asia na wanawake hawa alikuwa ni yuleyule mtaalamu wa mipango ya nje na ya ndani.
Husna Messi.
. . Sasa Asia alikuwa amechukua tenda hii na aliamini ataitendea haki.
Siku hii ilikuwa ya kupewa pesa ya awali ya malipo kwa ajili ya kuendelea na kazi hii.
Laki nne zikawekwa mezani, Asia hakuzihesabu akazikita katika pochi yake.
. . “Kwa hiyo tutegemee lini..” mama yule aliyekuwa na uchungu kupita wote aliuliza.
. . “Nampika kwa sasa, nitakupa taarifa ya maendeleo. Lakini hautazidi mwezi mmoja.” Alijibu kiuhakika Asia.
. . “Umeonana naye tayari?”
. . “Yeah si ndo anaitwa Lucas, amepanda hewani na ana mwili wa mazoezi.” Alijibu Asia. Hakika alikuwa anamzungumzia yuleyule Lucas. Mkufunzi wa chuo kikuu.

. . Mazungumzo yakamalizika. Akasimama na kuondoka zake.

. . Kitendo cha kuchukua pesa za watu kilimfanya Asia awaze mara mbilimbili atafanya nini kumkomoa yule bwana ili aweze kuaminiwa zaidi na wale wanawake waliompa kazi ile.
Asia akaijiwa na wazo, akatuma ujumbe kwa mtu aliyemfahamu yeye.
Majibu yaliyokuja yakamfanya atabasamu.
Kisha akalala, akiwa ameingiza pesa nyingi.

. . . . . . . . . . ****

. . Siku iliyofuata kama alivyotarajia, majira ya jioni. Asia akapokea simu. Ilikuwa namba mpya.
. . “Halow Halima…..Lucas hapa.”
. . “Lucas yupi, samahani.” Aliuliza maksudi Asia.
. . “Yule wa jana chuo…”
. . “oooh habari bwana mkubwa…nambie.”
. . “Leo jioni tunaweza kuonana kwa ile ishu?”
. . “Bila shaka tutafanya hivyo….mi nakusikiliza wewe.”

. . Mazungumzo yakaenda sawia, hatimaye wakakubaliana kukutana katika hoteli mojawapo katikati ya jiji.
Asia alikuwa anaifahamu.

. . Baada ya kukata simu ile Asia alipiga simu kwa bwana aliyemtumia ujumbe usiku uliopita.
. . Akazungumza naye, akamuelekeza wapi alipo wakenda kuonana.
Hayakuwa mazungumzo ya muda mrefu. Wakaachana baada ya Asia kukabidhiwa kifuko kidogo.
. . Akamkabidhi noti kadhaa bwana yule.

****
 
Back
Top Bottom