Mwanamke SHANGINGI...............

Mwanamke SHANGINGI...............

Ana tatizo gani?
Hivi kuconform ni sifa ehhhh?

sijui kama tumeelewana

binadamu hujifunza best kwa vitendo
na zaidi kwa makosa.....
na umri wa 13 -19 ambao ndo unaitwa foolish age
na wengine wanasema mpaka 25......
ni umri wa mtu kujitafuta
ndo maana kuna wengi wanajaribu sigara,bangi na still
ukubwani ukija kuambiwa yule shule alivuta bangi huamini....
wengine pombe saana but mwisho hanywi kabisa...
waswahili husema 'ujana maji ya moto'

bila kufanya hivyo.ina athari saana ukubwani......
 
Tunawaita fuata upepo au vichwa panzi

Yeahhh. Kina "fulani alifanya ndio maana na mimi nikaenda, fulani akaenda ndo na mi nkaenda". Mbaya zaidi hata watu wazima wapo wa aina hii.
 
sometimes unasikia...'mashangingi wa bunge' mfano....
au mashangingi wa NEC ccm au CHADEMA...HAPO JEE??????
Hawa inawezekana pamoja na sifa nyengine zilizokwishatajwa (baadhi zao-umbo kubwa, watu wa madili ya pesa rahisi ikiwemo uchunaji mabuzi na ubazazi, kuvaa ghali na kujipamba kupindukia) bungeni huwa wapashaji na wapayukaji wakubwa sana. Hawatumii hoja za nguvu bali mipasho na husikiliza zaidi sauti zao wenyewe kuliko za wengine.

Kwa kudandia mada hapa hapa, kuna sehemu imesemwa "ukimwita ma.laya anahamaki lakini ukimwita shangingi anavimba kichwa". Ni suala la lugha tu, sawa na yule anayerusha vichwa ukimuliza "mkeo hajambo?" na kukenua umulizapo "vipi wife mzima?"; au anayefurahia kuitwa ba.sha lakini akahamaki kuitwa sho.ga. Kwa ufupi, sifa moja ya ushangingi ni hiyo ya um.alaya hata kama hili la mwisho linawakwaza.
 
Hawa inawezekana pamoja na sifa nyengine zilizokwishatajwa (baadhi zao-umbo kubwa, watu wa madili ya pesa rahisi ikiwemo uchunaji mabuzi na ubazazi, kuvaa ghali na kujipamba kupindukia) bungeni huwa wapashaji na wapayukaji wakubwa sana. Hawatumii hoja za nguvu bali mipasho na husikiliza zaidi sauti zao wenyewe kuliko za wengine.

Kwa kudandia mada hapa hapa, kuna sehemu imesemwa "ukimwita ma.laya anahamaki lakini ukimwita shangingi anavimba kichwa". Ni suala la lugha tu, sawa na yule anayerusha vichwa ukimuliza "mkeo hajambo?" na kukenua umulizapo "vipi wife mzima?"; au anayefurahia kuitwa ba.sha lakini akahamaki kuitwa sho.ga. Kwa ufupi, sifa moja ya ushangingi ni hiyo ya um.alaya hata kama hili la mwisho linawakwaza.

umezungumza kitu cha maana mno
ni rahisi hata mwanamke kujiita 'shangingi'
hata kama sio shangingi......this is very interesting........
 
Nilikuwa Tanga miaka ya hivi karibuni tumekaa sehemu sehemu basi wakapita madada walikuwa wanne wamevaa kiajabu ajabu na pia walikuwa wamejisiliba kupita kiasi. Basi dada mmoja katika kundi letu akasema, "Angalia wale makunyuu." mie nilikuwa sijawahi kulisikia hili neno nikauliza makunyuu ndio maana yake nini? Basi yule dada akajibu Kunyuu ni juu ya Shangingi au kwa maneno mengine Shangingi haoni ndani kwa Kunyuu.... mie nikabaki kushangaa shangaa tu.
 
Embu tutaje mifano ili wengine tuelewe, kati ya Gea Habibu, Zamaradi, Dina, Dida, etc nani ni kubwa la 'maadui' a.k.a shangingi apo.
 
Ni kawaida katika mazungumzo kusikia watu wakisema..
'nimepata bonge la 'shangingi'
au mke wa fulani 'shangingi la kufa mtu'
au mitaa ya sinza kuna 'mashangingi ya ukwel'....

na hata wanawake utasikia 'wifi yangu fulani 'shangingi' hasa..
na kadhalika...........

sasa hapa nauliza usahihi wa neno shangingi ni upi?
na mwanamke 'shangingi' ni yupi???

je mwanamke mwembamba anaweza kuwa shangingi??????

au mwanamke mfupi ????

mwanamke mpole sana kama mlokole ??????

je wanawake wanene na wenye maumbo makubwa automatically ni mashangingi????

msichana teenager anaweza kuwa shangingi???

ushangingi nini hasa?umbo au tabia?
tabia zipi?????????

je unaweza kusema natafuta shangingi la kufa mtu????lol

au kumwambia mkeo ..nataka uwe shangingi hivi '??????lol

tazama.. mfano wa magari.....magari mashangingi ni ma land cruiser na ma nissan
yote aghali makubwa na yanatumia pesa nyingi ku ya maintain....
huwezi kuita corola shangingi...lol

Happy New Year The Boss

Mi mashangingi ninayoyajua ni yale magari ya waheshimiwa wabunge na mawaziri
 
Hao wageni wa kutoka bara wamekuja na maendeleo wakiwaacha wenyeji waswahili wakicheza bao na kusomesha watoto wao madrasa.hao watoto kubaki kulakulala na kukosa kipato then wanaanza udokozi wauze vitu ili nao waishi kama wageni kutoka bara!!!
mateja yote ni born hiahia die hiahia
,

Nadhani hujui Historia ya Waswahili, Mimi baba yangu ni mmoja wa Waswahili walosoma kiukweli kweli kabla ile dhana yao ya kanisa haijakuja, Kumbuka hii njama ilikuja baadae baada ya kuona Waswahili wakisoma WATAWAFUNIKA kwa hiyo wakahakikisha wanawadumaza na kila alietaka kusoma lazima awe mgalatia.

NA kwa kukupa mifano midogo tu uliza Philemon Sarungi jina lake kamili lilikuwa nani? Kigoma MAlima na wengine wengi ambao sitaki kuwataja ambao wengi wao walikuwa Waswahili, lakini ilibidi wabadili dini na MAJINA kwa kutaka kusoma ! hizo zilikuwa njama ! Lakini tulistuka ambapo ilikuwa too late!

Na ukisema kuhusu maendeleo ya watu wa Pwani, hivi hukumbuki nyerere ALITAIFISHA MALI NYINGI ZA WASWAHILI? mie baba yangu alikuwa na nyumba nyingi sana maeneo ya KAriakoo ilibidi auze nyumba zake kwa kuogopa kutaifishwa na nyerere ! na hivo tu kuna na wazee wengi wa kiswahili walifanya hivi, na kuwaacha masikini.

Mmetoka kwenu huko kwa kupewa kazi ardhi , na matokeo yake mnahakikisha mnawadhulumu ardhi WASWAHILI ili mkae na mnawatupa mbaaali halafu leo mnasema mna maendelao ya DHULMA?

Leo unaongelea eti wabara wana maendeleo, nani kasema labda huko kwenu ! NAdhani unakutana na Waswahili WALOCHANGANYA! Waswahili TULOENDELA TUPO ! lakini yanini KUJIONESHA ?

So tafadhali acheni kuwabeza Waswahili.
 
haya ni makubwa yenye uzito mdogo,sasa haya yote yanatokea wapi mpendwa wangu ilhali nilishakuomba samahan,au ina maana mm ndio mtu wa kwanza kulitumia neno uswahili au uswahilini au waswahili kwa maana niliyomaanisha,mbona hata mm ni swahili speaker which makes me kuwa mswahili pia.Tafsiri yako ya uswahilini si kama niliyomaanisha mim,uswahilin yangu ni ile ya kulee kote kuleee kwa wanakosutana na matarumbeta kuleee ambako mtu akila nyama kila siku ni tajiri kulee wanakojibizana kwa maneno ya kanga.Kila siku watu hapa wanawa-refer wasichana wa kutoka uswazi niliyomaanisha mim kuwa ni kuku wa kienyeji,au hujasikia,mbona huwashambulii..Pia sijakutusi ww mwenyewe ndo umeamua kutafsiri kuwa unatusiwa.Vile vile kinakushangaza nini hadi useme huku uswahilin tunafata nin wkt nina haki yakuweka makazi ktk sehemu yoyote niitakayo tanzania,kwanza hata majumba mazuri huko Dar ni sisi wakuja kutoka bara hao wenyewe wametuuzia viwanja ili wapate pesa za kucheza watoto na kuongeza idadi ya wake huku watoto wao wakiishia kuwa vibaka na mateja.Dar imejengwa na wakuja na watoto wa wenyeji ndio wanaongoza kwa ukibaka na uteja na uhuni.
hii ni coment yangu ya mwisho hapa naona hali si shwari na mie safari za dhoruba na mawimbi siziwezi.
nalog off.

Acha uongo ! Dar ilikuwa na maendeleo makubwa sana kabla nyerere na fitna zake za kutaifisha mali za Waswahili.

HAya nakubali, na JE KWANINI MNAJIJAZA DAR ES SALAAM, ? imekuwa desturi sasa hivi kila ajae DAR hataki kurudi kijijini ! nowonder magufuli juzi alisema asoweza kulipa nauli arudi kijijini ! nadhani alikuwa anawaambia ndugu zake WANAONG'ANGA'ANIA DAR! japo simuungi mkono kwa kauli yake hii ya kejeli!
 
Shangingi ni neno la kimasai.
Kwa sababu wana age set system, shangingi ni mwanamke kwenye thirties au 40s akipata mjukuu huwa wanaitwo kokoo. i.e bibi au mwanamke mzee.

Kwa wanaume ni baada ya morani huwa "Seuri".... baadae "Laibon".
Seuri ni kama shanginki kwa kiumri.

Kwa kuwa maanti huwa wanaongeza weight in their 40s na kuchukua taswira ya makalio na umbo nene kiaina fulani, basi waswahili tukaanza kuwaita mashangingi.. from maasais.
Kwa mfano, Shyrose, Michelle Obama,.....

kwa hiyo, hao ni mashangingi?
 
Hii inanikumbusha 'uswahili'.

Utasikia mtu anasema 'mi sina mambo ya kiswahili kama hayo'.

Sasa 'uswahili' ni nini? Na kinyume cha 'uswahili' ni nini?

Manake unakuta mtu anakaa 'uswahilini' halafu eti anajidai 'hana mambo ya kiswahili'. Hapa naibua hoja nyingine. 'Uswahilini' ndiyo wapi? Na huko 'uswahilini' kukoje? Na kinyume cha 'uswahilini' ndo 'uzunguni'?

Kama kinyume cha 'uswahilini' ni 'uzunguni' je, ni sahihi kusema kinyume cha 'uswahili' ni 'uzungu'?

Hayo yote ya hapo juu mimi kwa mtazamo wangu, watu hupenda kuwabeza waswahili hata bila kujua maana ya Waswahili au Uswahili.

NAweza kusema labda kutokana na maisha ambayo waswahili wamekuwa wakiishi tokea enzi za mababu ambazo walikuwa na MILA NA DESTURI zao !

Nadhani walipokuja wazungu kukatokea matabaka ya aina tofauti na utakuta eneo la dar ndio kama hivo liligawanywa sehemu tofauti kutokana na watu waliokuwa wakiishi maeneno hayo , nilikuwa nikisikia nilipokuwa mdogo " uzunguni ", uhindini na uswahilini.

Lakini ikumbukwe kuwa huko uswahili kulikuwa na watu WASTAARABU wakiishi (Kariakoo) ambapo walikuwa wastaarabu sana ! baadae maeneno hayo YAKAVAMIWA na watu wa aina tofauti ! na baadae mila na desturi zikachanganyika na tabia mbaya zikajitokeza huko! lakini kwa sababu kulishazoeleka ni uswahilini basi watu tena hawaangalii nini maana ya Uswahili wanasema tu just kukejeli watu wa Pwani !

Nadhani nimefafanua kiasi. Ninavoelewa mimi
 
195883_111163985630694_100002112798449_105141_2361756_n.jpg


Shangingi huyu hapoo Ashura Shangingi | Facebook
 
Hayo yote ya hapo juu mimi kwa mtazamo wangu, watu hupenda kuwabeza waswahili hata bila kujua maana ya Waswahili au Uswahili.

NAweza kusema labda kutokana na maisha ambayo waswahili wamekuwa wakiishi tokea enzi za mababu ambazo walikuwa na MILA NA DESTURI zao !

Nadhani walipokuja wazungu kukatokea matabaka ya aina tofauti na utakuta eneo la dar ndio kama hivo liligawanywa sehemu tofauti kutokana na watu waliokuwa wakiishi maeneno hayo , nilikuwa nikisikia nilipokuwa mdogo " uzunguni ", uhindini na uswahilini.

Lakini ikumbukwe kuwa huko uswahili kulikuwa na watu WASTAARABU wakiishi (Kariakoo) ambapo walikuwa wastaarabu sana ! baadae maeneno hayo YAKAVAMIWA na watu wa aina tofauti ! na baadae mila na desturi zikachanganyika na tabia mbaya zikajitokeza huko! lakini kwa sababu kulishazoeleka ni uswahilini basi watu tena hawaangalii nini maana ya Uswahili wanasema tu just kukejeli watu wa Pwani !

Nadhani nimefafanua kiasi. Ninavoelewa mimi

Asante kwa ufafanuzi ila nitakuwa na maswali machache -"USTAARABU" ni nini? "TABIA MBAYA" ni nini"

Umesema "Watu wa Kariakoo" walikuwa "wastaarabu" kabla ya watu wa "bara" kuwavamia huko "uswahilini" kulikokuwa na "ustaarabu"! Ina maana watu wa bara hawakuwa na "ustaarabu" na ndiyo maana walipochanganyika na watu wa "Kariakoo" ikatokea "tabia mbaya"?

Nitakuambieni kwanini "uswahili" unadharaulika.

Ukiangalia mentality ya watu wa Pwani, hasa DSM utaona wana kijitabia cha kudharau watu wa bara. Na kigezo chao kikuu ni kujifanya wanajua kukunja chapati, kunywa kahawa na kucheza bao wakiwa wamekunja miguu kwenye mikeka! Hili sijatunga mimi.Aliwahi kusema Ukiwaona Ditopile Mzuzuri ( R.I.P) kwamba watu wa bara washamba wakuja hawajui kukunja chapati! Hivyo haya siyo maneno yangu bali ya watu wa Pwani. Sitaki kuamini hivyo ndivyo vigezo vya USTAARABU!

Kitu kingine, utaona kwamba watu wa Bara wamekuwa wanadharauliwa sana na hawa "waswahili" kwa kisingizio ati wabara hawana "ustaarabu" na ndio maana nauliza "ustaarabu ni nini? Wabara walikuwa na haki kuja DSM na kwingineko kwani ni Watanzania. Kwamba wameenea kila kona ya DSM siyo kosa lao. Wenyeji wa DSM wanajiita "wenyeji" ukiwachunguza, hawakuzaliwa DSM.
Hoja yako ya wazungu kuja na kugawa matabaka - Uzunguni, Uhindini na Uswahilini - Ukichunguza utaona kuwa tabaka ziliwekwa kufuata "race" au rangi - USWAHILI siyo race! UAFRIKA ndio race.Jiulize kwanini kusiwe "Uafrikani" kukawa "uswahilini"? Food for thought!Characterists za uswahilini ni nini? Kila mtu anakimbilia kukaa uzunguni, uhindini lakini hakuna anayekimbilia kukaa "uswahilini" badala yake kila mtu "anatafuta kukwepa uswahilini".

Niachie hapo.Nitarudi ikibidi. Tusichakachue mada ya Boss on Mashangingi.
 
Back
Top Bottom