Wanaume hupenda wanawake wagumu kupatikana?

Wanaume hupenda wanawake wagumu kupatikana?

ShesRise_1

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2025
Posts
21,722
Reaction score
50,265
Mara nyingi humu JF nimeona wanaume ndio wanaoandika sana mada zinazohusu wanawake, na wakati mwingine inafika hatua unaona kama kuna complaints nyingi kuhusu wanawake.

Leo nataka kuuliza jambo kwa wanaume na wanawake pia karibuni tujadili kwa heshima na uhalisia 👇

Mara nyingi nimekuwa nikisikia kwamba:

Mwanaume hapendi mwanamke ambaye yupo too available anapomhitaji. Mfano, mwanaume akikuhitaji na wewe unapatikana bila excuses, kuna wanaosema mwanaume anaweza kuona kama wewe ni too easy au hata cheap

Sasa swali langu ni:
Ni kweli mwanaume anaona mwanamke wa namna hiyo hafai au ni assumption tu ya mitaani? Au kweli mnataka ile chase game yaani kidogo mkimbizane kama jogoo na kuku?
Kipengele A vs B:

A: Unapenda mtu anayekuelewa ukimuhitaji, on time yupo.

B: Au unapenda ule wa kumbembeleza kidogo, mpaka drama kidogo ndiyo anakubali? 😜
Na je, ni kweli kwamba mwanamke akiwa too available kwa mwanaume wake, inaweza kumfanya amchoke au amdharau?

Pia nimewahi kusoma sehemu mtu akisema:

“Ukitaka mwanaume akudharau, muombe sex wewe wa kwanza. Sasa hapa nauliza, ni kweli wanaume hampendi kuombwa? Na kama ukiombwa, unamchukuliaje mpenzi wako unamdharau au ni mitazamo tu ya watu? Na kwa wadada pia. Unaogopa kuomba attention/affection kwa mwanaume wako?

Kama ndio, why? Tuambiane ukweli bila kujificha. Wanaumeeeeee, igweeeeeeeee 🔥💬

ShesRise_1 😎
 
mimi siwezi kufukuzia demu mdamrefu, naamini kama yeye ananikubali hawezi kunizungusha bali atanifanyia urahisi kumpata. akionyesha kutokueleweka naachana nae kabisa....

kuna drama kiogo unaona kweli ni drama ila si ana ku ignore hizo ni nzuri
Hapa tunazungumzia ambao tayali ni couple sio mitongozano
 
Mara nyingi nimekuwa nikisikia kwamba:
Mwanaume hapendi mwanamke ambaye yupo too available anapomhitaji. Mfano, mwanaume akikuhitaji na wewe unapatikana bila excuses, kuna wanaosema mwanaume anaweza kuona kama wewe ni too easy au hata cheap
hivi vitu ni kama sanaa, hakuna kanuni moja kwa wanaume wote, anachokipenda "John" sicho anachokipenda "Michael", and vice-versa.

Na kinachopendwa na "Mohammed" sio kwamba ndo kitapendwa na "Nasib" au "Amir", and vice-versa.

Wengine hawapendi kuzungushwa, wanataka jibu chap chap (availability, immediate response)

Wengine wapo tayari kuzungushwa zungushwa, kusubiri (ku-play a long game, cat and mouse games.)

Na je, ni kweli kwamba mwanamke akiwa too available kwa mwanaume wake, inaweza kumfanya amchoke au amdharau?
Pia nimewahi kusoma sehemu mtu akisema:
“Ukitaka mwanaume akudharau, muombe sex wewe wa kwanza. Sasa hapa nauliza, ni kweli wanaume hampendi kuombwa? Na kama ukiombwa, unamchukuliaje mpenzi wako unamdharau au ni mitazamo tu ya watu?
Kama mizuka imepanda, wewe omba tu, don't hold yourself back. Better be real.
 
Nyoshaaa hii imekaa kimchongo
Unapenda kuombwa nini
Ni nini kinachoombwa mpka umbatize Jina muombaji kua OMBA OMBA?
Ukiwa unaomba vitu kama vocha, hela ya pedi, au nauli ya boda boda, wewe ni ombaomba, una ufukara uliopitiliza..!!

Hivi ni vitu vya msingi ambavyo mwanamke anayejitambua anapaswa kuwa navyo standby.

Huwa tunachoka zaidi pale meseji inapoingia "Baby i miss you" halafu inaishia na "...nina kashida ka elfu tano."

Obviously unaona kabisa hapo upo na tapeli la mapenzi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom