Asante kwa ufafanuzi ila nitakuwa na maswali machache -"USTAARABU" ni nini? "TABIA MBAYA" ni nini"
Umesema "Watu wa Kariakoo" walikuwa "wastaarabu" kabla ya watu wa "bara" kuwavamia huko "uswahilini" kulikokuwa na "ustaarabu"! Ina maana watu wa bara hawakuwa na "ustaarabu" na ndiyo maana walipochanganyika na watu wa "Kariakoo" ikatokea "tabia mbaya"?
Nitakuambieni kwanini "uswahili" unadharaulika.
Ukiangalia mentality ya watu wa Pwani, hasa DSM utaona wana kijitabia cha kudharau watu wa bara. Na kigezo chao kikuu ni kujifanya wanajua kukunja chapati, kunywa kahawa na kucheza bao wakiwa wamekunja miguu kwenye mikeka! Hili sijatunga mimi.Aliwahi kusema Ukiwaona Ditopile Mzuzuri ( R.I.P) kwamba watu wa bara washamba wakuja hawajui kukunja chapati! Hivyo haya siyo maneno yangu bali ya watu wa Pwani. Sitaki kuamini hivyo ndivyo vigezo vya USTAARABU!
Kitu kingine, utaona kwamba watu wa Bara wamekuwa wanadharauliwa sana na hawa "waswahili" kwa kisingizio ati wabara hawana "ustaarabu" na ndio maana nauliza "ustaarabu ni nini? Wabara walikuwa na haki kuja DSM na kwingineko kwani ni Watanzania. Kwamba wameenea kila kona ya DSM siyo kosa lao. Wenyeji wa DSM wanajiita "wenyeji" ukiwachunguza, hawakuzaliwa DSM.
Hoja yako ya wazungu kuja na kugawa matabaka - Uzunguni, Uhindini na Uswahilini - Ukichunguza utaona kuwa tabaka ziliwekwa kufuata "race" au rangi - USWAHILI siyo race! UAFRIKA ndio race.Jiulize kwanini kusiwe "Uafrikani" kukawa "uswahilini"? Food for thought!Characterists za uswahilini ni nini? Kila mtu anakimbilia kukaa uzunguni, uhindini lakini hakuna anayekimbilia kukaa "uswahilini" badala yake kila mtu "anatafuta kukwepa uswahilini".
Niachie hapo.Nitarudi ikibidi. Tusichakachue mada ya Boss on Mashangingi.