Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,926
- 6,575
Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imemfutia uanachama wa Chama hicho leo Agosti 26, 2026 aliyekuwa Makamu wa Rais, Dkt. Emmannuel Nchimbi ambaye alitangaza kujiuzulu nafasi hiyo na kustaafu siasa jana Agosti, 25, 2026.
Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro leo Agosti 26, 2026 akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba.
Dkt. Migiro ameeleza kuwa uamuzi huo umefikiwa mara baada ya kukaliwa kwa vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya chama hicho ambavyo vilijadili suala la maadili ya Dkt. Nchimbi na vikaazimia kwa pamoja kumfuta uanachama mwanachama huyo.
Soma Pia: Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ajiuzulu